How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Friday 4 May 2012
Angalia wanaojua maana ya PhD za heshima hawazitumii kama vile walisomea
Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga alirejea nchini mwake akitokea Marekani alikopewa shahada ya heshima ya Udaktari na chuo kikuu cha Florida Agricultural and Mechanical University huko Tallahase. Kutokana na ukio hilo, gazeti la The Daily Nation la Kenya lilipambwa na kichwa cha habari hiki "Applause as 'Dr Odinga' returns. Au shangwe ujio wa 'daktari Odinga'. Wametumia neno daktari kwa uangalifu kwa kuliwekea alama za kufunga na kufungua usemi wakijua kuwa udaktari wa kupewa hata kama ni wa heshima si heshima kuutumia kama baadhi ya viongozi wa Tanzania wanavyofanya hasa rais Jakaya Kikwete. Wanaojua maana ya shahada za heshima wanashangaa sana hasa ikizingatiwa kuwa marehemu baba wa Taifa alikuwa miongoni mwa viongozi waliotunukiwa shahada nyingi za heshima kutoka na mchango wake katika kufikiri kidunia. Hivyo ingekuwa vizuri wanaomshauri rais Kikwete kumwambia aachane na kutambia udaktari wa heshima. Maana hata marais wenzake kama vile Mwai Kibaki, Yoweri Museveni na Paul Kagame wanazo shahada hizi tena nyingi lakini hawajinasibishi nazo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Kwetu TZ hadi kichefuchefu. Utasoma na kusikia MWENYEKITI, MHESHIMIWA,RAIS Dr....
Post a Comment