Monday, 18 June 2012

Afukuzwa kazi kwa kunyonyesha hadharani


Kwa wanaojua faida za kunyonyesha na umuhimu wake kimila na kiafya watashangaa kusoma habari hii ambapo mama mmoja nchini Marekani amefukuzwa kazi kwa kusa la kunyonyesha hadharani. Inashangaza na kusikitisha kuona watoto na akina mama wakifanyiwa unyama na unyanyasaji huu ambao ni kinyume cha haki za binadamu. Je dunia inakwenda wapi inapofumbia macho haki za msingi na kutetea haki zisizo za msingi kama ushoga na usagaji? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

nanukuu "Je dunia inakwenda wapi inapofumbia macho haki za msingi na kutetea haki zisizo za msingi kama ushoga na usagaji?" Mwisho wa nukuu. Nilipoanza tu kusoma nikabaki mdomo wazi na nikataka kusema kama hii nukuuu. Hakuna chakula bora kwa mtoto kama maziwa ya mama na tena yanaepusha magonjwa mengi sana....inauma na kusikitisha...