Thursday, 7 June 2012

Pata shahada ya Uzamili kwenye kulima bangi

Hapa Kanada kumekuwapo na  vituko vingi. Kwa mfano kwenye jimbo nililoishi zamani la New Foundland and Labrador ilikuwa mtu akikamatwa anavuta bangi alitozwa faini ya dola 50. Sasa mambo yameongezeka baada ya bwana mmoja kuamua kufundisha watu jinsi ya kulima bangi kisheria. Wahitimu watapata shahada ya uzamili  (Masters) kwenye masuala ya bangi. Hivyo, usishangae siku moja kusikia mtanzania mwenzako akiitwa Daktari kama wengi wapendavyo kuitwa hata kwa shahada za heshima baada ya kupata PhD in Cannabis sativa processing or growing even smoking. Nawaza. Hivi wazo kama hili lingetolewa na Mbongo au Muafghanistan ingwekuwaje zaidi ya FBI kumweka kwenye orodha ya watu hatari. Ila kwa vile mwenye kuja na wazo hili ni mzungu, usishangae likapata wapenzi na mabwana usalama wakanyamaza.  Bila shaka wauza bwimbwi wataipenda shahada hii itakayotolewa hapa Kanada.  Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

2 comments:

Anonymous said...

Kwa nini usichukue hiyo Shahada na wewe upo karibu huko sisi itabidi mambo ya visa ni taabu kwetu
wewe ni raiya hapo unaweza ukaipata kwa urahisi sana au?

NN Mhango said...

Bahati mbaya nshasoma mambo mengine. Isitoshe sihitaji shahada ya bangi. Laiti ningekuwa kiongozi wa CCM huenda ningeichangamkia ili niitwe Dk kama wanavyopenda kuitwa.