Thursday, 14 June 2012

Je wajua kuwa King Leopold ni wa kwanza kufanya mauaji ya halaiki?

Image Detail
Leo nimemkumbuka jambazi na mwanaharamu aliyeitwa mfalme Leopold II (1835-1909) wa wabelgiji ambaye ni binadamu wa kwanza kufanya mauji ya kimbari nchini DRC. Mwanaharamu huyu aliyepata malezi mabaya kiasi cha kuoa hata asiweze kufanya tendo la ndoa kwa mkewe, aliua zaidi ya wacongoman 15,000,000 akitaka kutimiza tamaa yake ya madaraka na utajiri. Wengi huwa hawajui kuwa jambazi huyu ndiye alifyatua tufe la mauaji ya kimbari na halaiki kwa muda wote aliokalia DRC. Sura yake hata mavazi yake yanaonyesha ukatili usio kifani. Huyu pamoja na majambazi wengine kama Dk. David Livingstone, Fredrick Lugard, Cecil Rhodes,Mungo Park, Henry Morton Stanley, Christopher Columbus, Fransico d'Almeida,  Lord Kitchner aliyefika kwa kuiteka na kuikalia Sudan akitumia fuvu la binadamu mwafrika kama kidau cha wino na wengine ndiyo waliotusababisha haya masahibu ya umaskini tunayokumbana nayo. Wakati mwingine tunahitaji kujua historia yetu ili tujikomboe. Je ni wangapi wanalijua hili wakati kwa ujinga wao waliwaita majina watoto wao kwa kumbukumbu ya watesi wao?

1 comment:

Jaribu said...

Watu ambao ni "sexually frustrated" huwa wanakua makatili. Wanafikiri uanaume ni kuwa na gari kubwa, bunduki kubwa au kuua watu bila mpango. Nakumbuka kisa cha mzungu mmoja alimvamia mwanamama kutaka kumbaka, aliposhindwa kutimiza lengo lake akamuua huyo mwanamke kwa ghadhabu.