Tuesday, 26 June 2012

Huu ni ulimbukeni, ushamba au usafi?


Mke wa rais, Salma Kikwete akimwagilia maji mti alipotembelea kituo cha kulea watoto cha SOS jijini Dar Es Salaam. Kinachogomba ni huyu mama kuwekewa mkeka kusimamia ili kumwagilia maji. Inashangaza viongozi wetu na wake zao wanavyoogopa udongo ilhali wametokea huko. Na isitoshe utajiri wanaochuma toka kwetu unatokana na udongo huu huu. Je huu ni mfano gani kwa vijana wetu kuhusu kupenda udongo na kufanya kazi za mikono? Ajabu huyu ni mke wa mtu anayejigamba kutetea sera yake ya Kilimo Kwanza. Hapa ni Kilimo Kwanza au Usafi Kwanza? Hivi nani anawashauri watawala wa namna hii ambao wnaishi kwenye Alinacha na dunia feki? Kwanini hawakujifunza kwa watawala walioonja chungu ya kuishi kwa kujidanganya kama Muamar Gaddafii ambaye hakuwa akijua kuwa walibya walikuwa wakimchukia hadi kumuu kwa kipigo kama mwizi? Nisaidieni jamani.
1 comment:

Anonymous said...

Mke wa Rais Kapendeza Kweli picha ipo safii kabisa.