Wednesday, 27 June 2012

Madaktari sikilizeni wimbo huu, wanasiasa kama wahubiri

Wanasiasa, sawa na wahubiri wapenda pesa wa kisasa, si watu wa kuamini. Hawana uaminifu zaidi ya sanaa. Mgomo wa madaktari ulipoanza mwezi Aprili rais Jakaya Kikwete aliwaita madaktari ikulu na kuongea nao akiwakirimu kila vinono vya ikulu. Walifanya kosa kubwa kumuamini wasijue alikuwa na 'elimu' kuwatenza kama asemavyo Shari Martin kwenye wimbo huu. Ondoa neno wanadamu au wahubiri utaona nimaanishacho. Dk Steven Ulimboka angejua haya kabla huenda angeepuka balaa lililomkuta ambalo kimsingi ni aibu ya Kikwete. Alaaniwe mtu yule aliyemtesa na kumdhalilisha Dk Ulimboka. Alichofanyiwa Ulimboka, kimsingi, ni aibu kwa rais, watanzania, madaktari, wagonjwa na serikali kwa ujumla. Kwani hakileti jibu zaidi ya kuzidisha tatizo. Alaaniwe mtu yule awahadaye wenzake ukiachia mbali kuwatesa.

No comments: