- Leo ilikuwa siku ambapo sayari ya Zuhura au Venus imepita kati ya dunia ya jua. Kwa mashabiki wa astrophysics kama mimi ilikuwa ni siku ya kukumbuka. Kitendo kama hiki kitatokea tena mwaka 2117 ambapo wengi watu watakuwa historia kama vile walioona tendo hili karne iliyopita walivyo historia. Wataalamu wengi hutumia tukio hili kufanya mambo mengi kisayansi kama vile kutumia mnurulisho unaopatikana pale kupima urefu baina ya dunia na jua, kujua aina za gazi zilizomo kwenye maumbo mengine angani na kadhali.
No comments:
Post a Comment