Saturday, 9 June 2012

Msiba wa Makani ni wa taifa si wa CHADEMA


  1.  
    Buriani Bob Nyanga Makani. Kifo chako ni pigo kwa taifa hasa wapenda haki na demokrasia.  Msiba wa Makani ni wa taifa zima ikizingatiwa kuwa alitoa mchango mkubwa kwa taifa kutokana na nyadhifa alizowahi kushika . Makani anakumbukwa kwa changamoto alizotoa kwa Chama Cha Mapinduzi baada ya kuona kinapoteza mwelekeo. Makani aliwahi kuwa naibu gavana mkuu wa Benki Kuu (BoT) ambako bila shaka ndiko alipokutana na kufahamiana vyema na mzee  Edwin Mtei mwanzilishi wa CHADEMA.Pumzika mahali pema peponi Bob Mohamed Nyanga Makani.

No comments: