Wednesday, 6 June 2012

Barrick, Mkapa na matunda ya uhujumu na udhalimu


Taarifa zilizopo ni kwamba kampuni ya kuchimba madini ya Barrick imeichangia NGO ya rais mstaafu Benjamin William Mkapa kiasi cha dola 500,000. Kwa viwango vya nchi maskini hii si pesa kidogo. Kwa wanaojua jinsi Mkapa alivyouza na kugawa mali zetu hasa madini, watajiuliza nini cha mno baina ya Mkapa na Barrick zaidi ya kulipa fadhili?
Juu pichani  rais Jakaya Kikwete akimpongeza makamu mwenyekiti wa Barrick ,Deo Mwanyika (sijui kama ana uhusiano na Johnson Mwanyika mwanasheria mkuu wa zamani fisadi) huku marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Mkapa wakiangali.

No comments: