Saturday, 2 June 2012

Rais anapoangusha kilio kama kichanga!


Baada ya kupatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha, rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak alijikuta akibubujikwa na macho kama kichanga alipopelekwa kwa helkopta kwenye gereza la Tora alimozoea kuwaweka wabaya wake. Kweli hujafa hujaumbika. Mubarak aliyefikia kujiona kama yeye ndiyo Misri na Misri ni yeye, katika umri wake wa miaka 84, hakuamini kuwa angefia gerezani. Maisha ndivyo yalivyo, ukishangaa ya Musa utaona ya Filauni na ukishangaa ya Charles Taylor unaona ya Mubarak. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: