Saturday, 30 June 2012

Hatimaye mapinduzi ya Misri yakamilika!Habari za kuapishwa kwa rais mpya wa Misri aliyechaguliwa kidemokrasia Mohammed Mursi ni njema kwa wapenda amani na demokrasia. Kwa namna moja au nyingine kuapishwa kwa Mursi kunaashiria kuanza ngwe ya mwisho ya kukamilika kwa mapinduzi ya umma ya Misri yaliyomuondoa Hosni Mubarak madarakani baada ya kukaa muda mrefu. Hata hivyo kuna maswali yanayoendelea kuwasumbua wachambuzi wa mambo. Je Mursi atatimiza ahadi zake mojawapo kuwa rais wa wote bila kujali itikadi za dini na vyama? Je Mursi atajitenga na chama chake cha Muslim Brotherhood na sera zake za kihafidhina au ataamua kupuuzia ahadi zake? Ni mapema. Wakati utaamua maana hakuna awezaye kuuzuia. Kila la heri Mapinduzi Matakatifu ya Misri ambayo yanapaswa kuwa mfano na kichocheo cha kuondoa ufisadi na udhalimu kusini mwa Sahara.

No comments: