Sunday, 17 June 2012

Israel yaonyesha walivyo wabaguzi hasa kwa weusi


Taarifa kuwa mamlaka za Israel zimewaondoa kwa nguvu wakimbizi toka Sudan ya Kusini zinasikitisha licha ya kuonyesha tabia na sura halisi ya taifa hili la kizayuni. Kwa unafiki Israel ilikuwa ikiwakaribisha wakimbizi toka Sudan hasa wadarfur ili kuonyesha kuwa inawajali kuliko waislamu wenzao wa Kaskazini mwa Sudan ambao ndiyo wenye madaraka. Inashangaza kuona inavyowavungia virago wasudan wa kusini baada ya kuwatumia wadarfur. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Inasikitisha kwa kweli.....

Anonymous said...

duh!!! kazi kweli kweli yaani hawa ngozi nyeupe kila kukichA wanapiga bomba mswaili kwa pingu.wengine wanaozea majera ya ulaya bila hata kua na hatia. jela za sweden,norway,holland,ubelgiji,uk nk

Jaribu said...

Tuwalaumu viongozi wetu ndio wanasababisha yote haya kwa kuvuruga nchi zetu mpaka tunazishindwa inabidi tukimbie. Hata nchi za weusi kama Afrika Kusini hawataki wageni wengine. Hamna anayampenda maskini, hata akiwa ndugu.

Nchi kama Marekani ni watu weupe kidogo kama WaMexicani na Walatini wengine ndio wanasumbuliwa. Huku ukiwa mweusi unakwenda kimya kimya tu, labda Watanzania wenzako wakuchongee. Kuna rafiki yangu mmoja mCameroon alikuwa kwenye basi bila makaratasi, walivyoingia jamaa wa Uhamiaji akajifanya ana usingizi mzito. Wakamuacha lakini Wamexican kwenye basi wakashushwa wakati wengine ni raia wa Marekani. Go figure!

Anonymous said...

Nakumbusha Wa israil wanabagua mtu yoyote Asiyekuwa katika dini yao na sio mtu mweusi au mweupe.

Kwani wa falasha kutoka Ethiopia walikuwa na rangi gani?
si walituwa ndege nzima kutoka ethiopia kwenda israil au huna kumbukumbu hizo.
hao hawana rangi hata uwe mweupe kama karatasi

NN Mhango said...

Kama utakumbuka vizuri ni kwamba hao mafalasha wanabaguliwa nchini humo hata treatment yao ni tofauti kabisa na waisrail weupe so to speak.

Anonymous said...

Nakumbusha Wa israil wanabagua mtu yoyote Asiyekuwa katika dini yao na sio mtu mweusi au mweupe.

Umeisoma hii ukafahamu au? so to speak.