Wednesday, 6 June 2012

Wamarekani kwa vituko, mama akamatwa kwa kushangilia


Shannon Cooper is arrested after cheering for her daughter at her graduation (WPDE News)Shanon Cooper amejikuta matatani baada ya kumshangilia binti yake aliyekuwa akimaliza darasa la 12. Wamarekani hawakosi vituko. Mama kwa furaha ya mzazi hasa katika nchi ambapo weusi wachache humaliza shule, alijikuta amejawa na furaha kiasi cha kushangilia kwa nguvu na kufanya akamatwe! Ingekuwa Bongo sijui ingekuwaje hasa ikizingatiwa kuwa misikiti na vibanda vya muziki hupiga kelele kiasi cha kuwanyima hata watu usingizi? Je hii imemtokea kwa vile ni mswahili au ni ustaarabu uchwara wa jamaa zetu? Maana inashangaza kuona nchi inatoa haki hata kwa wasagaji na mashoga lakini inamnyima mtu haki ya kufurahi kama ilivyotokea kwa Cooper. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: