Habari tulizopokea toka kwa ripota wetu toka Dodoma ni kwamba Tanzania imeanza kukomaa ambapo mawaziri nane wameachia ngazi baada ya wabunge kuwatolea uvivu. Ingawa habari hii hajathibitika toka serikalini, wanaotajwa ni Omar Nundu (Uchukuzi), William Ngeleja (Nishati na Madini) , Dk. Haji Mponda (Afya), Jumanne Maghembe ( Kilimo Chakula na Ushurika) ,
George Mkuchika (Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Cyril Chami (Viwanda na Biashara), Mustafa Mkulo (Fedha) na Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii). Pamoja na kuendelea kufuatilia habari hii, ukweli ni kwamba bado hatujapata uthibitisho toka serikali. Kwa mfano, waziri Mkullo yuko nje ya nchi. Hivyo kuingizwa kwenye kundi la kujiuzulu bila ya yeye kuwepo bado kunafanya habari hii kuendelea kuwa tetesi ingawa kila penye moshi shurti kuwa na moto. Je wahusika wamevujisha habari hii ili kupima upepo? Ukweli kamili utajulikana kadri tunavyoendelea kufuatilia.
No comments:
Post a Comment