Sunday, 22 April 2012

Makanisa ya kweli yanaweza kujengwa kwa pesa chafu?


Hakuna ubishi kuwa siku hizi makanisa, maduka hata madangulo yanaanza kukosa mpaka ingawa si yote. Hebu fikiria. Kanisa linalojengwa kwa pesa, kwa mfano, ya EPA linakidhi matakwa ya kiroho? Jikumbusheni uhovyo wa serikali iliyotokana na pesa chafu kama hiyo. Usijeshangaa kukuta siku moja makanisa kama haya yakifanya kazi ya kubariki pesa ya ujambazi hata kuwasaidia wakwepa kodi kama siyo kusimamiwa au kutumiwa na wauza mihadarati. Hakuna kilichotusikitisha kama kusikia mafisadi wanaochangia makanisa wakidai eti wanachangisha pesa ya kumtafuta Yeus. Yesu hawezi kutafutwa kwa pesa chafu inayotokana na kuangamiza watu wa Mungu.  Je makanisa ya namna hili yana tofauti na maduka-kanisa ya akina Getrude Rwakatare, Silvester Gamanywa, Zakaria Kakobe, Adam Lusekelo na matapeli wengine wa kidini? 
Inashangaza kuona waziri mkuu aliyefurushwa kwa kashfa ya Richmond Edward Lowassa anavyoshabikia na kushabikiwa na makanisa kuyachangia ili kuendeleza shughuli zake ambazo kimsingi hazina tofauti na biashara. Je makani kama haya yana roho mtakatifu au roho mtakakitu? 

No comments: