Saturday, 28 April 2012Baada ya kukaa pamoja kwa miaka saba na kufanya kila kitu kuanzia chumbani hadi bustanini na kupata watoto si haba eti Brad na Angelina ndiyo wametangaza uchumba! Wenye nazo kweli wana vituko. Hakuna kilichovuita blogu hii kama pete ya uchumba yenye thamani ya dola 500,000. Wenzetu wanazo lakini hawana uwezo wa kupata vitu tulivyopata bila hata kutumia senti tano kama ndoa na watoto wenye kuzaliwa ndani ya ndoa. Wao wana pesa sisi hatuna. Sisi tuna amani wao hawana. Maana wangekuwa na amani na kuaminiana isingewachukua miaka yote hiyo kuridhishana kuwa wanapaswa kuwa mme na mke. Kweli wahenga walisema kuwa pesa na ukwasi haviwezi kununua amani, upendo na ridhiko la moyo. Usishangae wawili katika ndoa kutoka kwenye ubavu wa mbwa wakicheka ilhali matajiri wakitoka kwenye hekalu na kasri wakilia hata kununiana. Binadamu ni nini hadi awe mtumwa wa vitu sifa vyeo ukwasi na kujilisha pepo?


No comments: