Monday, 30 April 2012

Ndoa ya CHADEMA na Sabodo si mtihani tosha kwa upinzani?Hakuna ubishi kuwa ndoa ya anayeitwa mfanyabiashara maarufu kwa jina la Mustafa Sabodo pichani imeshika kasi. Kwa wanaojua jamaa zetu hawa walivyoletwa na kuchuma, anahofia usafi wa huyu jamaa anayesifika kutumia jina la marehem Mwalimu Julius Nyerere kujinufaisha. Anajiita mpenzi wa Mwalimu ambaye wakati wa uhai wake hata hivyo hatukuwahi kumsikia. Je hii ni janja ya wahindi kuanza kutafuta pa kushika baada ya kuona CCM ikiyoyoma? Je kama wameitosa CCM iliyowalea na kuwakumbatia hadi wengine kuzawadiwa ubunge, CHADEMA ni nani wasiifanyie  hivyo? Je nao falsafa yao ni ya 'Sina adui au rafiki wa kudumu bali maslahi'? Mwanzoni Sabodo aliahidi kuwapa CHADEMA jengo lake la Mwenge. Ghafla amepiga U-turn na kusema eti atawajengea ofisi. Tusije tukaruka mkojo tukaishia kukalia manonihino. Kusema ndoa ya Sabodo na CHADEMA inabindi iangaliwe isijekuwa mtego wa CCM kumtuma kada wake kuwachafua. Kama Sabodo anaipenda CHADEMA anangoja nini CCM? Kimsingi anataka kuweka vyama vyote mfukoni mwake.
Sabodo alikaririwa akisema, “Kwa kweli nimefurahi sana kunialika kwenye mkutano wenu, nimeshawahi kuisaidia CCM, lakini hawajawahi kunishukuru kama mlivyofanya ninyi.”
Je hii ni sababu yenye mashiko kumfanya aipende CHADEMA hivyo au anaandaa pa kushika baada ya CCM kujiishia?

No comments: