Tuesday, 17 April 2012

Rais wetu ni wa hovyo kweli kweli

Rais Jakaya Kikwete akishuhuduia mkewe akisalimiana na kocha wa zamani wa timu ya taifa Maxio Maximo.  Rais na kocha wapi na wapi jamani?
Katika pita pita yangu kwenye vyombo vya habari nchini, sikuona mahali ilipo taarifa ya rais Jakaya Kikwete aliyeko nchini Brazil ukiachia mbali makala moja toka Sao Paolo iliyoandikwa kwenye Mjengwa Blog ambako picha hii imetoka. Habari inaongelea upuuzi mtupu eti jinsi ya kuwa na timu nzuri ya taifa. Hiyo si kazi ya rais ni kazi ya waziri wa michezo hata vilabu vya michezo. Kwanini rais asifute wizara ya michezo akaiweka chini ya ofisi yake ili angalau tujue rais wetu ni rais na waziri wa michezo?
Ukisoma ile makala ambayo bila shaka Anna Nkinda aliyeiandika ameandamana na rais, unapata kichefuchefu.
Nilichojifunza ni kwamba rais wetu hana jipya wala la maana la kuandikwa na vyombo vya habari. Maana nijuavyo, rais wa nchi ni alama ya nchi. Popote awapo lazima umma wa wananchi ujue anachofanya na yuko katika hali gani. Kuna uwezekano kuwa rais yuko Brazil akifanya mambo ya hovyo kama hiyo picha juu inavyoonyesha. Nadhani ndiyo maana magazeti ya Tanzania  hayana muda wa kufuatilia kuandika anachofanya rais. Sasa inashangaza hata hao waandishi wa habari wanaolipwa na kuandamana na rais wanafanya kazi gani kama hawana hata habari za kutuma nyumbani? Kwa maana hiyo huu ni ushahidi kuwa rais wetu ni wa hovyo kweli kweli.

1 comment:

Miss K. said...

hahahah hii ni kiboko! Raisi anaenda Brazil kukutana na kocha wa zamani wa taifa.Na hao waandishi aliowatanguliza kwenda kumpokea wote ni mafisadi kama yeye. Hii haikuwa ziara ya kiserikali ila ni yake kama kawaida yake ya kufanya vacation za haopa na pale. Nadhani ilikuwa ni nadhiri yake kuwa akiwa raisi atatembela nchi zote duniani. Hapo mtaona tu kocha mpya wa taifa analetwa kutoka Brazil.Huu ufujaji wa pesa za wananchi utaisha lini?