Sunday, 15 April 2012

Mutharika, kurithishana na maburungutu ya dola


UROHO NA UNAFIKI WA MARAIS WETU
                                                           


Hii hapa chini ni nyumba ya Mutharika huko kwao Ndata.Image Detail


Habari zilizoripotiwa na gazeti la Nyasa Times  ni kwamba mabegi na masanduku yaliyojaa pesa yalikutwa kwenye chumba cha rais wa zamani wa Malawi, marehemu Bingu wa Mutharika. Habari zinaendelea kusema kuwa pesa hiyo  ilikamatwa na polisi baada ya kugundua kuwa ndugu wa marehemu walikuwa wakipanga kuihamisha pamoja na mali nyingine za serikali. Ni aibu kiasi gani. kwanza kwa rais kuficha pesa uvunguni mwa kitanda tena kwenye karne ya 21? 
Ni aibu kiasi gani kitendo hiki kinapotendwa na rais tena msomi aliyebobea katika uchumi? Je huyu rais alikuwa ameelimika kweli? Je ni watawala wangapi wa kiafrika ni aina ya Mutharika? Je wanajifunza nini ingawa uwezo wao wa kujifunza siku zote ni mdogo? Muhimu ni kuwaambia wazi kuwa kila mficha maradhi kilio kitamfichua kama ilivyotokea kwa Mutharika. Ajabu wakati rais akilalia mamilioni ya dola na kwacha, mamilioni ya watu wasio na hatia wanakufa kwa magonjwa yanayotibika! Je namna hii kuna haja ya kuwa na rais ambaye kimsingi ni mwizi anayeitwa mheshimiwa? Kama rais wa nchi maskini kama Malawi isiyo na raslimali za kutosha anakutwa na mamilioni ya dola uvunguni mwa kitanda hao marais wa nchi zenye raslimali nyingi kama DRC na Tanzania wanalilia mabilioni kiasi gani? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

No comments: