Saturday, 21 April 2012

Tahariri kwachafuka tena wanataka kieleweke


Umati wa watu kwenye viwanja vya Taharir mjini Cairo unaoandamana kushinikiza utawala wa kijeshi uachie ngaziuachie ngazi.
Wamisri wameamka tena na kurejea uwanja wa Taharir kudai serikali ya kijeshi ambayo wanaiona kama mwendelezo wa serikali ya Hosni Mubarak iondoke madarakani ili kukamilisha mapinduzi matakatifu ya umma. Inashangaza kuona wenzetu wanathubutu tena si mara moja wala mbili. Je watanzania tunaoteseka kuliko hata hao wamisri ambao wana maisha ya uhakika ikilinganishwa na yetu tulirogwa na nani? Je ni lini tutaamka na kufikiri kama watu na taifa kwa maslahi ya vizazi vijavyo? Je tumepata somo gani toka Misri? Wenzetu wana huduma kama umeme, maji,simu hata afya za uhakika kuliko sisi lakini bado wanaingia mitaani kutaka maisha bora zaidi. Sisi tumekuwa watu wa kupokea taarifa za maangamizi ambapo mabilioni  shilingi yanavujwa au kuibiwa kila uchao nasi tunaangalia tu. Hatuna umeme wa uhakika pamoja na kuwa na vyanzo vingi vya umeme. Hatuna huduma za afya za maana. Makampuni ya nishati na mawasiliano yanatulangua na kutuibia kama vile hatuna akili wala macho. Wakubwa wanazidi kuchuuza na kugawana nchi yetu. Wanatanua wao na vizazi vyao wakati sisi tukiendelea kuteketea. Je ni lini tutaacha kuwa punda wa kubeba mizigo ya watawala? Inauma sana. Lazima tuanze kuhiari kujikomboa toka mikononi mwa genge la watu wachache. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

No comments: