Sunday, 29 April 2012

Elimu inapokuwa chanzo cha ujinga!


  1. Elimu ya Tanzania na Education for ignorance! Kweli hawa nao ni wasomi au makapi?    Hilo ni bango mojawapo kati ya yale yaliyobebwa na wanaoitwa wasomi wa vyuo Tanzania! Inasikitisha licha ya kukera. Je hawa ni wasomi kweli au waganganjaa wanaoweza kutumiwa na fisadi yoyote awe mtu au chama kufikia malengo yake. Usomi maana yake ni uasi siyo ukondoo, ukuku wala upunda. Yaani hawa hawajui tatizo la CCM siyo wale wanaokihama bali walioking'ang'ania na ufisadi wake? Hivi kweli gamba ni yupi kati ya wale waliojazana CCM na wale wanaochoshwa na ufisadi na kuhama chama? Hawa wanafunzi wanamdanganya nani? Kwanini wasiseme wanaganga njaa? Ajabu makapi haya  yanapoanza kubwagwa na kuchomwa moto yanaanza kulalama! Acheni kutumia matumbo hata masabauri kufikiri. Tumieni vichwa vyenu vizuri.

No comments: