Tuesday, 17 April 2012

Kikwete alivyowaacha hoi waandishi wa habari UghaibuniWengi wanachukia tabia ya rais Jakaya Kikwete kupenda raha na utoro kazini. Pia anapenda sana matumizi ya hovyo kiasi cha kutunisha deni la nje la Tanzania. Kimsingi, hakuna kikwazo cha maendeleo yawe ya kijamii au kiuchumi Tanzania kama Kikwete ambaye amejiruhusu kuitwa Vasco da Gama ukiachia mbali kuunda serikali kubwa ya kishikaji na kifisadi. Hebu jiulize kwa mfano. Wale mawaziri waliotuhumiwa kughushi vyeti vya shahada wamefanywa nini? Unawakumbuka? Tukukumbushe. Mawaziri waliotuhumiwa kughushi vyeti vya taaluma ni Matayo Matayo, Mary Nagu, Makongoro Mahanga, Emanuel Nchimbi na William Lukuvi. Hata meya wa jiji la Dar es salaam Didas Massaburi yumo ukiachia mbali tuhuma za ufisadi wa kutisha wa kampuni ya UDA.
Angalia Kikwete anavyoendelea kuharibu pesa ya umma kwa kumlipa pesa ya ustaafu swahiba yake Edward Lowassa waziri mkuu aliyeachia ngazi kutokana na kashfa ya Richmond iliyoliacha taifa mahali pabaya huku wananchi wakikabiliwa na mgao na ulanguzi wa umeme. 
Kikwete ameamua kwa makusudi mazima kutumia cheo chake kulipana fadhila kwa kuunda mikoa mipya huku akiwapa ukuu wa mikoa watu waliokataliwa na wapiga kura kama Mwantumu Mahiza, Joel Bendera na  mabalozi Deodorus s Kamala, Matilda Buriani na Philip Marmo. Kikwete ameunda wilaya mpya zaidi ya kumi na mikoa mipya minne. Kwa uchumi gani kama siyo kutumia urais kuwapa ulaji washikaji zake?
Ukija kwa wakuu wa wilaya wasio na sifa zaidi ya ushikaji ndiyo usiseme.  Wakati tukitafuta chanzo cha umaskini wetu tunapaswa kumkaba shati Kikwete na genge lake.

No comments: