Sunday, 22 April 2012

Ridhiwan jibu tuhuma zako badala ya kujificha nyuma ya Millya


Kwa waliosoma au kusikia shutuma za mtoto wa rais Jakaya Kikwete, Richiwan dhidi ya aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha wameshangaa sana. Wanashangaa Ridhiwan anapata wapi jeuri ya kumshambulia Millya huku yeye akikabiliwa shutuma lukuki za kujitajirisha kupitia mgongoni mwa rais. Wanashangaa jinsi ambavyo Ridhiwan anaongea kwa mamlaka kutokana na kuwa mtoto wa rais. Hii si nchi ya kifalme au ya utawala wa ukoo kama ilivyokuwa Libya, Malawi na Misri au ilivyo Uganda. Inashangaza kwa mtu ambaye anasemekana amesomea sheria kutoona mbali na kuuona ukweli kuwa utawala wa baba yake una mwisho tena usio mwema kutokana na madudu unaoendelea kufanya. Ajabu hata Kikwete mwenyewe anaridhika na uchafu huu. Je vijana wa Tanzania wataendelea kujiruhusu kutumiwa kama dodoki na watu fulani wachafu na wenye tamaa wanaotumia madaraka kama mali ya ukoo? Hivi kati ya Ridhiwan na Millya fisadi au mtoto wa fisadi ni nani?

No comments: