How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Wednesday, 18 April 2012

Familia ya Mkapa kwenye kashfa nyingine

 Anna Mkapa bingwa wa kuchuma asipopanda aliyeiachia ikulu yetu uchafu wa ajabu unaoendelezwa na Salma Kikwete.
Hivi karibuni mdhibiti na  mkaguzi mkuu wa fedha za serikali (CAG) alitoa taarifa ya ukaguzi wa fedha za serikali na kugundua madudu mengi mojawapo yakiwa kashfa ya wizi wa mabilioni ya shilingi uliofanywa na familia ya rais mstaafu Benjamin Mkapa. CAG ameonyesha wasiwasi mkubwa kwa uamuzi wa CHC wa kufuta madeni mengi ya iliyokuwa kampuni ya Simu 2000. Kampuni hiyo iliundwa na kuongozwa na familia ya Mama Anna Mkapa, kwa ajili ya kuuza zilizokuwa mali za Shirika la Posta na Simu. Kuna habari kwamba familia hiyo ilijitwalia mali kadhaa zenye thamani ya mabilioni ya shilingi. Miongoni mwa majengo yaliyouzwa ni maghorofa yaliyopo Ilala.
Kwa wanaokumbuka Anna Mkapa alivyomchafua mumewe kwa kumfundisha wizi hawashangai. Huenda kuna mengi ambayo bado hayajulikani. Nani mara hii kasahau jinsi kaka zake Anna walivyopewa uuzaji wa iliyokuwa benki ya biashara (NBC) wakishilikiana na kampuni ya kijambazi ya Net Solution Group ya Afrika Kusini?
Nani mara hii kasahau wizi ulioasisiwa na Anna wa kuunda NGO na kujitajirisha kupitia mgongo wa ikulu unaoendelezwa na Salma Kikwete?
Nani mara hii kasahau ujambazi wa wazi wa Mkapa, familia yake, marafiki na vivyele wake uliohusisha kujitwalia mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira? Je ni siku gani wezi hawa wenye madaraka watafikishwa mbele ya haki kabla ya kuonja mauti?

1 comment:

Anonymous said...

Na bado mengi yatatokea na wataumbuliwa sana tu! Nakumbuka ule "mfuko" alioanzisha kuwasaidia wanawake wasiojiweza ilikuwa danganya toto. Kwani alikuwa anawasaidia walikuwa wanajiweza tu. Ule mfuko uliwapeleka watu maarufu kwenda kusoma kama vile akina Hoyce Temu na mdogo wake. Mfuko ulikuwa ni wa manufaa yao tu. Na huko Moshi mdogo wake ni yaleyale tu wana majengo kibao na mahospitali binafsi wanayomiliki.