Tuesday, 24 April 2012

Je wajua wabia katika serikali ya Kikwete?

Image Detail


Ingawa rais Jakaya Kikwete aliwahi kukanusha kuwa serikali yake si ya ubia, ukweli ni kwamba ni ya ubia. Ukiangalia tangu iingie madarakani, imekuwa ikiteseka na wabia ambao kwa sasa wameanza kuwa donda ndugu kwa Kikwete. Mfano, chukulia hawa mawaziri wanaopaswa kuachia ngazi na wasifanye hivyo, kama si wabia ni nani? 
Kwa ufupi wabia katika serikali ya Kikwete ni:
Familia ya rais mstaafu Benjamin Mkapa ambaye aliidhinisha wizi wa pesa ya EPA iliyotumika kumuingiza Kikwete madarakani.
Familia ya rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye alimuibua Kikwete
Familia ya katibu mkuu wa CCM mstaafu Yusuf Makamba,
Mawaziri William Ngeleja, Ezekiel Maige, Makongoro Mahanga, Mary Nagu, Emanuel Nchimbi, William Lukuvi, Mustapha Mkulo, Adam Malima,Sophia Simba, Celina Kombani, Hawa Ghasia na George Mkuchika.
Pia wamo makatibu wa wizara kama vile Ladislaus Komba, David Jairo, na wengine wenye kashfa kubwa kubwa wasitimliwe.
Yumo pia Paulo Noni, Edward Lowassa na Rostam Aziz. Kuna na wafanyabiashara wengine ambao tukipata taarifa zao tutawarusha hewani.

No comments: