Sunday, 29 April 2012

Ni wakati muafaka kumm-empeach hata kum-recall Kikwete


  • Image DetailKutokana na madudu ambayo yametendwa na serikli ya rais Jakaya Kikwete kwa miaka sita ambayo amekuwa madarakani, kuna haja ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye hata kumrecall. Bahati mbaya CCM ni chama cha Mafisadi. Bila hivyo, walipaswa kum-recall Kikwete kama ilivyotokea Afrika Kusini kwa Thabo Mbeki ambaye licha ya uchapakazi wake aliondolewa tena kwa chuki binafsi za uroho wa madaraka. Pia huwezi kumlinganisha Kikwete na Mbeki ambaye alisifika kwa weledi na uwajibikaji.  Kikwete amethibitisha kuwa mzigo kwa taifa. Ni rais dhaifu asiyeweza kufanya lolote hadi asukumwe. Rejea alivyoshindwa kuwatimua mawaziri wake waliotuhumiwa kughushi vyeti vya kitaaluma. Rejea alivyoshindwa kumtimua waziri mkuu na mshirika wake mkuu Edward Lowassa hadi bunge lilipofanya hivyo. Je hii inatokana na ukweli kuwa Kikwete anashiriki karibu katika kila upotevu wa pesa tajwa au woga? Je rais wa namna hii anapaswa kuvumiliwa huku lawama wakitupiwa wasaidizi wake wakati tatizo kuu ni yeye? Je Kikwete ataendelea kuwadanganya watanzania hadi kipindi chake kiishe? Wabunge wa CCM na wa upinzani wanaoliona tatizo bila kupindisha ukweli wapaswa kuendelea kushinikiza Kikwete awajibishwe na watu wake. Hakika ni wakati muafaka kumfurusha Kikwete na siyo kumpa fursa ya kuwatoa sadaka wenzake. Lao ni moja.

No comments: