Saturday, 28 April 2012

Mheshimwa anapoangua kilioWengi wameshangaa ni kwanini mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alilia aliposikia kuwa ameshinda kesi ya kupinga ubunge wake iliyiokuwa ikimkabili. Tunadhani alilia kuonyesha ambavyo hakuwa na imani na mahakama zetu hasa kutokana na jinai iliyotendeka Arusha ambapo mtu aliyedaiwa kukashifiwa alishinda hata bila kufika mahakamani. Hii ni kinyume na sheria ya kashfa. Kitu kingine ni kwamba kwa majaji hawa wa kupeana na kulipana fadhila, yeyote angelia. Bwana Lissu hongera kwa kuvuka kikwazo hasa ikizingatiwa kuwa wewe ni mwiba kwa magamba na mafisadi. Alluta Continua.

No comments: