Tuesday, 17 April 2012

Mawaziri matatani kwa kununua ndege mbovu ya rais


President Paul Biya of Cameroon, and his wife Chantal
Rais Paul Biya na mkewe ChantalImage Detail
Heri marais wa kiafrika wawe na ndege kama hizi ili kupunguza gharama na utapeli
Mawaziri wawili nchini Kameruni wamejikuta matatani baada ya kugundulika kuwa ndege waliyonunua kwa ajili ya rais wa nchi hiyo aina ya Albatross kumbe ni ya zamani ingawa wao walisema ilikuwa mpya. Ndege hiyo yenye thamani ya dola 31,000,000 ililazimika kutua ghafla kwenye safari yake ya kwanza ya uzinduzi huku ikiwa imempakiza rais Paul Biya na mkewe Chantal. Waliotiwa nguvuni ni Marafa Hamidou Yaya ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani na Chief Ephraim Inoni a aliyekuwa waziri mkuu wa zamani. Ingawa rais Biya anasifika kwa uhovyo wake, angalaua amewakamata mafisadi wenzake tofauti na Tanzania ambapo si ajabu hata huu mdege wetu wa rais nao ni mkangafu kama ule wa Kameruni. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

No comments: