Tuesday, 24 April 2012

Uanasiasa, Ufisi na uchangudoa

Image DetailImage DetailImage DetailJulius Ma...funny pic...
  • Image DetailImage Detail

Kwa wanaokumbuka jinsi kijana Julius Malema (31) aliyekuwa rais wa Umoja wa Vijana wa ANC, alivyotumiwa na Jacob Zuma kumfurusha madarakani rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, wameshagaa sana kusikia kuwa Zuma na Malema wameishakuwa maadui kiasi cha Zuma kumtimua Malema ambaye alimtumia kuingia madarakani. Wanasiasa, kama vyangudoa, ingawa si wote, hupenda kutumiana. Kama fisi wako tayari kuvamia kila mfupa wakijua mwisho wa siku wataula ingawa si mifupa yote inatafunika. Na wachumia tumbo kama Malema, kama nepi, hupenda kutumiwa. Jana Malema alikuwa mwiba kwa Mbeki ambaye hakutaka kuchafua heshima yake kubishana na kijana juha kama Malema. Sasa Malema amegeuzia domo lake kwa Zuma kiasi cha kumuita dikteta kama alivyomuita Mbeki. Je kutimuliwa kwa Malema toka ANC ni mwanzo wa mwisho wake au mwanzo wa mwisho wa Zuma? Kwa wale waliozoea kutumiwa wajifunze toka kwa Malema na Zuma ua Raila Odinga na Mwai Kibaki kama hawakujifunza kwa Edward Lowassa na Kikwete Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA

No comments: