Thursday, 19 April 2012

Pongezi John Mnyika kutumbua jipu la Salma Kikwete

Image DetailImage DetailImage Detail


Blogu hii imekuwa ikifichua uoza mbali mbali unaofanywa na wake wa wakubwa. Ilifikia kipindi nikaonekana kama nina chuki binafsi na mama Salma Kikwete. Hii ilitokana na kushupalia uchafu anaofanya kwa kutumia NGO yake ya WAMA ambayo mimi huiita MAWAWA yaani Maulaji ya Wake za Wakubwa. Kimsingi, uanzishwaji wa NGO za wake wa wakubwa hasa marais wanapoingia madarakani ni aina mpya ya ufisadi unaopaswa kupigwa vita kwa nguvu zote. Alianza Anna Mkapa (Mama Tamaa) na sasa anaendeleza Salma Kikwete. Kinachofanyika ni kujitafutia utajiri kwa njia haramu kwa kutumia ikulu.
 Mnyika akiaririwa na vyombo vya habari akisema, “Mheshimiwa Spika naitaka serikali itoe tamko hapa kuwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na mke wa rais itakuwa ya kwanza kuchunguzwa na kuwajibishwa kutokana na kuwa ilihusika katika kipindi cha uchaguzi mwaka 2010 kwa kufanya kampeni.” 
Sambamba na kumpongeza Mnyika, nawapongeza wabunge wote hasa Deo Filikunjombe (CCM), Ludewa, Tundu Lissu (CHADEMA) Singida Mashariki na  Zitto Kabwe (CHADEMA) Kigoma Kaskazini na wengine wote walioshupalia upanya na umchwa unaoendeshwa na mawaziri wetu. Kimsingi, kwa shinikizo na azimio lao tutajua mbivu na mbichi za Jakaya Kikwete na Mizengo Pinda. Haya shime msikate tamaa wala kulegeza kamba tunaweza kulichinja joka lililowashinda CCM kulichuna ngozi.
kuna haja ya kuwapa shime wabunge wa CCM kuachana na kutumika kama mihuri ya ufisadi. Kama rais atawapuuzia waachane na CCM. Maana wanavyo vyama mbadala kuhamia na kufanya kile kilichofanywa na Wakenya, Wamalawi na Wazambia walipovipiga buti vyama vyao tawala.

POAC deputy chairman, Mr Deo Filikunjombe

No comments: