Saturday, 28 April 2012

Mjue Osama bin Laden wa kizungu


  • Al'Qa...  Adolf Hit...Caligula

Andre Behring Brevik ni kijana mdogo wa  Norway lakini mhafidhina, katili, bazazi na mjinga. Brevik amekuwa maarufu kutokana na kuwaua watu wapatao 69 wengi wakiwa vijana waliokuwa kwenye kambi kwenye kisiwa cha Utoya tarehe 22 Julai 2011.  Muuaji huyu hajutii wala kuona kama alichofanya ni kosa. Kwetu sisi, kutokana na kasumba alizolishwa kupitia michezo ya runinga, hana tofauti na gaidi Osama bin Laden. Hawa wawili wanafanana kutokana na ukweli kuwa wote ni watetezi wa dini na imani zao kwa kutumia maangamizi bila kuangalia hata upande wa pili.Wawili hawa wana sifa zinazofanana. Licha ya wote kuzaliwa kwenye familia zenye uwezo, wanachukia watu wasio wa dini zao. Wote hawajui historia za kile wanachokitetea kuwa ni matokeo ya dhuluma, ukoloni na ukandamizaji wa watu wengine. Wakati Osama aliwachukia wasio waislamu, Brevik anawachukia Waislamu na Wasoshalisti. Wote pamoja na bangi zao, hawakufanikiwa. Je Brevik angekuwa mwarabu vyombo vya magharibi vingesita kumuita gaidi tena mfuasi wa Al Qaeda? Wawili hawa hawana tofauti na wawili wengine waliotangulia yaani Adolf Hitler na Gaius Carigula.

No comments: