Monday, 23 April 2012

Watawala wetu ni vipofu na wanyanyasajiUkiangalia hivyo picha vizuri unashangaa kitendo cha anayejiita kiongozi wa watu kukaa huku akiongea kwa raha mstarehe wakati mwenzake amesimama bila sababu ya msingi. Je mabodigadi si watu kiasi cha kutenzwa kama mashine zisizo na uhai? Kwa mfano, nini mantiki ya mtu kusimama wakati watu wote wamekaa? Je huo ndiyo ulinzi au udhalilishaji? Maana hakuna tishio kwa usalama wa rais iwapo waliohudhuria kikao hicho wamesachiwa na kupitia taratibu zote za kiusalama kabla ya kuingia kwenye jengo. Je huu siyo ufalme wa kizamani unaowageuza watu wake kuwa punda? Je ni kosa la nani na hii hadi lini?

No comments: