Saturday, 28 April 2012

Nini fundisho la mbunge kunusurika kichapo?


Taarifa zilizotufikia ni kwamba mbunge wa Geita Donald Kevin Max alinusurika kichapo baada ya kumtetea diwani fisadi wa kata ya Nkome. Wananchi walichukizwa na kitendo hiki kiasi cha kuamua kumpa kisago mbunge. Je tukio hili la kuondokewa woga kwa wananchi linatabiri na kutufundisha nini? Bila shaka wenye nchi yao wamechoka kugeuzwa shamba la bibi kana kwamba wao ni mataahira. Wahusika tieni akilini mambo yanaanza kubadilika na hakuna kisichobadilika. Walatini husema,Omnia mutantur nos et mutamur in illis yaani kila jambo hubadilika hivyo nasi tubadilike. Ubabaishaji, usanii na kulindana havina nafasi tena katika jamii ya sasa inayoanza kujitambua na kujikomboa.

No comments: