Friday, 20 April 2012

Wabunge wanapaswa kumuondoa spika kabla ya waziri mkuu na mapanya

 

Hakuna ubishi kuwa spika wa Bunge Anna Makinda ni changuo la mafisadi. Ushahidi ni kushindwa kujibu tuhuma hizi ziliporushwa na spika wa zamani Samuel Sitta baada ya kuenguliwa na kusimikwa Makinda. Kwa kutojibu Makinda alithibitisha ukweli wa tuhuma dhidi yake.
Makinda amekuwa kikwazo kwa heshima na uhuru wa bunge. Rejea alivyomzuia mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema alipodai kuwa waziri mkuu Mizengwe Pinda ni muongo. Si hilo tu, amekuwa akiliburuza bunge kutokana na kutokuwa na taaluma ya sheria. Karibu mabunge yote ya Afrika Mashariki isipokuwa la Tanzania, yanaendeshwa na maspika wenye taaluma ya sheria.
Ukiachia hilo, Makinda amekuwa mtu wa jazba na kiburi kiasi cha kujiona ni bora kuliko bunge. Sasa kwa kuzuia Zitto Kabwe alilete hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu, kwa mara ya pili Makinda amethibitisha alivyo kibaraka wa waziri mkuu na mhimili mzima wa utawala. Kisheria mihimili mitatu ya dola yaani Utawala, Bunge na Mahakama havipaswi kuingiliana au kuzidiana mamlaka katika utendaji wake. Huu ndiyo msingi wa kwanza wa utawala bora.
Je kwanini wabunge wasimwajibishe Spika ambaye ameonyesha wazi kuwa mtetezi wa uoza, ukale na ufisadi?

No comments: