How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday, 21 May 2012

Huu ni utajiri, mapenzi au kichaa?


Comstock

Wazungu wana mapenzi makubwa kwa wanyama kiasi cha waswahili kama sisi kuwa na wasi wasi-kulikoni? Hivi karibuni mjini Vienna Austria ulifunguliwa mgahawa unaoruhusu wateja kuja na mapaka yao kupata chochote watakacho huku mapaka yakiruhusia kurandaranda yatakako. Mwenye mgahawa huu anasema mgahawa wake umeanza kuvutia watu wengi. Najiuliza ingekuwa Afrika hali ingekuwaje? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

3 comments:

Jaribu said...

Upweke huo, si unajua huku kila mtu na lake. Hata mimi enzi za zamani nilikuwa na paka, mpaka nilivyogundua niko allergic.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Pole sana kaka. Nashukuru nina vitegemezi vyangu na bi mkubwa. Nawashaurini muoe kuondoa balaa hili. Sioni mantiki ya kulisha jinyama wakati unaweza kuishi na mwenza wako. Andaeni utaratibu wa kuwa na asasi ya kuwakutanisheni watanzania mlioko nje ambao hamjaoa ili lau muweze kupata wenzi. Ni ushauri tu.

Jaribu said...

Ni jambo zuri hilo. Lakini hiyo ilikuwa miaka 25 iliyopita. Nishaoa mara mbili na sasa nina watoto wawili. Enzi hizo Watanzania hapa Texas walikua wakuhesabia; lakini siku hizi wengi tu.