Ingawa tumesikitishwa na kifo cha Steven Kanumba, kuna haja ya
kuuangalia ukweli kama ulivyo. Pamoja na kupewa heshima kubwa kuliko
hata aliyostahiki kutokana na wakati wa kifo chake, sasa basi turejeeni
kwenye mambo muhimu. Tumefanikiwa kuuonyesha ulimwengu kipaumbele chetu
hasa kujali sana usanii kuliko uchapakazi. Najua wengi hawatapenda
mawazo haya. Ukweli ni kwamba nimeshangaa kuona Kanumba akishabikiwa na
viongozi kuliko hata marehemu makamu wa rais Omar Juma. Kunani? Je hii
ni sawa? Sikuona rais, kwa wakati tofauti na mkewe, na vigogo wengine
wakimiminika kwenda kwenye msiba wa Omar Juma kwa spidi kama hii. Hakika
Tanzania ni nchi ya wasanii.
Bwana alitoa Bwana amechukua. Maisha yanaendelea. Turejee kwenye kupambana na ufisadi, usanii, uvivu na urongo basi. Au siyo?
4 comments:
Kifo cha Kanumba kimeniachia fundisho na hasa kwa wanasiasa wetu wapenda sifa na watafuata umaarufu wa kisiasa. Nilikuwa nasubiri Kanumba afikishwe kwenye nyumba yake ya milele halafu niandike a short article. Muda ukiniruhusu nitafanya hivyo karibuni.
Mkuu, article niyoahidi hapo juu imeshaiva naimeshaingia hewani ndani ya www.malkiory.com. Kazi kwako! kuiperuz.
http://www.malkiory.com/?p=2467
Inasikitisha. Ni kikombe cha babu cha mwaka huu
Post a Comment