The Chant of Savant

Wednesday 27 January 2010

Tatizo ni Zanzibar si Maalim Seif

MAKALA ya Absalom Kibanda kuhusu mustakabali wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla haiwezi kupita bila kujadiliwa.

Naomba niungane na Kibanda na kutofautiana naye kimtazamo.

Kwanza nakubaliana na Kibanda kuwa tatizo ni Zanzibar si Maalim Seif ingawa naye ni sehemu ya tatizo. Kabla ya Seif kuja na madai ya kuahirishwa uchaguzi na kumuongezea muda Rais wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, Amani Abeid Karume, Seif alikuwa akivutia na kuonewa huruma kutokana na kuibiwa ushindi kama ambavyo mara zote amedai.

Katika makala tajwa Kibanda anaonekana kutekwa na hoja za Maalim Seif Sharrif Hamad, hasa woga. Ni kweli Zanzibar imepitia kwenye mikiki na mikwaruzano mingi kabla na baada ya uhuru.

Kwa vile tumeishaainisha kiini cha haya yote kuwa ni wizi wa kura na uchaguzi usio huru na wa haki, tunapaswa kutafuta majibu yanayokubalika kisheria na kuingia akilini kimantiki.

Kwa vile wote tumeishatambua umuhimu wa amani ya Zanzibar kama ngazi ya amani ya taifa, hakuna haja ya kugwaya kutafuta jibu hata kama ni kidonge kichungu.

Ingawa Kibanda ameridhia kuchezewa kwa katiba na kusogezwa mbele uchaguzi, kuna mambo ya msingi yamempiga chenga. Kwa mfano, anaridhia kusogezwa mbele uchaguzi. Hili haliingii akilini hata kama lina nia njema kwa nchi. Kwanini tusifanye yafuatayo:

Iundwe tume huru ya uchaguzi ambayo itaundwa na vyama vyote vya siasa na asasi za kiraia kama inavyopaswa kuwa kwenye uchaguzi wa vyama vingi.

Bado tuna muda wa kutosha wa kufumua na kusuka upya tume ya uchaguzi itakayoundwa na kukubaliwa na pande husika.

Pili, uchaguzi uendelee kama kawaida. Tofauti, usimamiwe na waangalizi huru wa kimataifa.

Kama kweli CUF wamekuwa wakiibiwa ushindi, hawana haja ya kugwaya kuingia kwenye uchaguzi. Maana wapiga kura wao bado wapo na kinachogomba ni mfumo.

Tatu, turekebisha mazingira ya kampeni ambapo vyombo vya habari vya umma kama radio na runinga zitoe airtime sawa kwa vyama vyote vitakavyoshirika uchaguzi.

Hivyo basi, hoja iwe kuweka mazingira ya uchaguzi huru na haki na si kuchezea katiba.

Kama kweli CUF wana imani na rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, kwanini wasitumie fursa hii kuingia kwenye uchaguzi?

Na kama kweli CUF ilikuwa ikishinda na kuibiwa kura na ushindi kama ambavyo CUF wamekuwa wakidai, sasa wanaogopa nini wakati huu wanapoaminiana na Karume kiasi cha kumuona kama ndiye muarobaini wa kuivusha Zanzibar?

Nne, kwa vile makubaliano ya Karume na Seif ni kwa ajili ya wananchi wote wa Tanzania na si Zanzibar pekee kama inavyoanza kuaminishwa, lazima yaliyojadiliwa na Karume na Seif faraghani yawekwe wazi ili umma ujue.

Maana ni juu yake, si wawili hawa. Hawa ni viongozi tu wanaoweza kutoweka lakini umma siku zote utakuwapo. Kuna haja ya kuangalia mbali.

Tano, muafaka utokane na kuangalia sheria na kukubali hoja za upande mwingine badala ya ‘one man show’ inayoendelea.

Sita, suluhu itafutwe kwa kushirikisha vyama viwili vinavyokinzana badala ya watu wawili binafsi.

Leo maalim Seif na CUF watakuja na madai ya kubadilisha katiba ili kukidhi mahitaji yao, tutakubali. Kesho kikiundwa chama kingine cha siasa au hata CCM ikajikuta ilipo CUF, nao watakuja na wazo kama hili. Tutachezea katiba mara ngapi? Hakuna haja ya kujifunza mchezo mchafu hata kama nia ni nzuri.

Hatuna haja ya kuvunja katiba.

Ingawa huu ni mtego na mtihani wa aina yake kwa CCM na taifa kwa ujumla, CCM itapaswa kuwa makini na kusimamia ukweli. Iji-commit kwenye badiliko hili hata kama maana yake ni kuinyima ulaji.

Hii itasaidia kuisafisha CCM kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki na mshindi wa kweli atapewa ushindi wake.

Hakuna ubishi. Kuna hisia kuwa kuna hoja fichi ya Uzanzibari dhidi ya Muungano. Hii imesimikwa na matamshi ya Seif hivi karibuni kuwa Bara hawapaswi kuongelea mambo ya Zanzibar.

Hili haliwezekani na haliingii akilini. Kwanini tumekuwa wote kwenye mazonge yote haya kwa muda wote wa zaidi ya miaka 40 halafu leo tunaenguliwa kana kwamba hatuna haki kwenye masuala ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya nchi moja ya Tanzania?

Ingawa Kibanda amekubaliana na msimamo wa wanachama wa CUF kuhusiana na suala zima ambalo hawalijui undani wake zaidi ya kupewa matumaini kuwa linalenga kuleta amani ya Zanzibar, kuna haja ya kuambiwa kilichomo kwenye makubaliano husika.

Kitendo cha Kibanda kukubaliana na hoja ya kuchezea katiba ikiwa ndiyo njia ya kutibu majeraha ya Zanzibar hakitoi jibu la tatizo lenyewe. Hatuwezi kuacha kufanya uchaguzi eti kwa kuogopa vurugu. Kinachopaswa kufanyika ni kutatua tatizo na si matokeo ya tatizo.

Kibanda anasema: “Ni jambo la kusikitisha kwamba wanazuoni ambao wameingia kwa kujua au kutojua katika kundi la wachambuzi wanaomshambulia na kumsuta Maalim Seif, kwa sababu tu ya kushindwa kwao kutambua au kwa sababu ya kusahau kwao kwamba Zanzibar haijapata kufanya uchaguzi huru na wa haki katika chaguzi tatu za vyama vingi za mwaka 1995, 2000 na 2005.”

Hii hoja haina mashiko. Maalim Seif ‘anashambuliwa’ na kukosolewa kutokana na alivyoleta na kutetea hoja yake ambayo si ya kidemokrasia, hasa pale anaposhinikiza lake liwe asijue kuwa kama anavyosimamia masilahi ya chama chake, na wapinzani wake wanasimamia masilahi na sera za chama chao ambacho kwa bahati mbaya ni tawala.

Hapa suluhu inaweza kufikiwa si kwa kushinikiza, kutishana, kuenguana au kuitana majina ya ajabu kama kidudumtu au wasioitakia Zanzibar mema bali kufuata sheria na kuona mbali.

Tatizo kama nilivyobainisha hapo juu kuwa ni kutokuwapo uchaguzi huru, basi tutafute namna ya kuwa na uchaguzi huru lakini si kumuongezea muda Karume au kusogeza mbele uchaguzi. Kama walitaka hivyo, kwanini wamengoja hadi saa za majeruhi kama kweli hakuna namna?

Leo Karume ameishatamka wazi wazi kuwa hataki kuongezewa muda. Je, atakapojipiga mtama ilhai kilichokubaliwa baina yake na Maalim Seif bado ni siri ya wawili hakijulikani, Kibanda na wenye mawazo kama yake hawaoni kuwa ataeleweka kama alikuwa akichezea akili zetu kwa kujifanya hataki kuongezewa muda wakati ukweli ni vinginevyo? Je, hii haitamjengea kutoaminika mbele ya umma litakapokuja suala zima la kuandaa mazingira ya uchaguzi huru?

Kuna hili la serikali ya umoja wa kitaifa. Nadhani Tanzania hatujafikia huko, zaidi ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na mazingira muafaka kwa uchaguzi huru.

Uzoefu unaonyesha kuwa serikali za umoja wa kitaifa si jibu la matatizo bali mafuta kwenye moto wa matatizo. Kenya na Zimbabwe ziliridhia kuundwa kwa serikali za umoja wa kitaifa.

Jiulize mwananchi wa kawaida amefaidika nini zaidi ya wahusika kutumia muda mwingi na rasilimali kulumbana wakishindania ukuu? Niliwahi kuliandikia hili kwenye jarida la The African Executive Magazine Nairobi Aprili 30, 2009 chini ya kichwa cha ‘Power sharing deals; Africa ’s anathema.’

Kwa sasa Wakenya hata Wazimbabwe wanajuta kwanini walikaribisha jinamizi hili.

Maana wahusika hawana muda wa kuwatumikia zaidi ya kuwatumia kutafuta madaraka. Tanzania haiwezi kwenda huko.

Huwezi kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa upande mmoja wa nchi huku upande mwingine ukiendeshwa na serikali ya chama kilichoshindwa. Lazima kutakuwa na mgongano mkubwa katika utekelezaji. Hili ni rahisi kuliona. Halihitaji uwe na PhD kwenye political science.

Hata hivyo Kibanda ameshindwa kuibua kitu kingine muhimu-muungano wetu unahitaji marekebisho ili kuepuka kuendelea kuwepo mazingira ya wizi wa kura na vitu kama hivyo.

Hakuna ubishi. Muungano wetu ni wa kale na unaendeshwa kikale tofauti na mazingira ya sasa. Ingawa CUF hawaweki wazi madai yao-wangetaka yaendelee kuwa - kuna shaka.

Kuna hisia za kuona kama Zanzibar imedumazwa na Bara.

Hili unaweza kulipata kwenye maneno ya Maalim Seif aliposema anataka Zanzibar iwe Hong Kong ya Afrika Mashariki. Hii si ndoto nzuri. Hapa tatizo si muungano, bali serikali zisizo na visheni na mipango mizuri hasa kupambana na ufisadi na ubunifu.

Nafasi haitoshi. Kibanda na Seif wanaweza kuwa na hoja. Kinachowaangusha ni kuangalia matokeo badala ya mzizi wa tatizo. Yote yanawezekana. Lakini suluhu itokanayo na kuvunja katiba si suluhu kitu na haitufai kama taifa. Ieleweke. Tatizo ni Zanzibar si Maalim Seif, ingawa naye ni sehemu ya tatizo.
Chanzo: Tanzania Daima Januari 27, 2010.

Hili la Msekwa ni aina nyingine ya ufisadi


SAKATA la Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Pius Msekwa, kudaiwa takriban shilingi 7,000,000 alizokopa ubalozini Uingereza, limetufumbua macho.

Msekwa alikopa pesa tajwa ili aweze kumtibia mwanae aitwaye Julius aliyeugua ghafla akiwa njiani kwenda Paris Ufaransa akiwa ni mfanyakazi wa ubalozi.

Ukichukulia na kugundulika kuwa watoto wengi wa vigogo wa chama na serikali wamejazana Benki Kuu (BoT) tena wengine kwa kuingia na vyeti vya kughushi, hili linazidisha shaka.

Hebu fikiria, Msekwa huyu huyu alikuwa Spika wa Bunge kwa miaka nenda rudi kabla ya kuteuliwa Makamu Mwenyekiti wa CCM. Zidi kufikiri. Msekwa huyu huyu mwanaye anafanya kazi ubalozini.

Bado hajaridhika na neema zote hizi anazokamua kwenye nchi. Msekwa huyu huyu anakopa pesa ubalozini. Mwisho wa yote anaacha kulipa? Je, huu si ufisadi na ubinafsi wa kutisha? Je, ni wangapi kama Msekwa madudu yao hayajajulikana?

Ingawa huu mara nyingine huchukuliwa kama umbea, utakuta kuna ukweli hasa kuhusiana na watawala wetu kujipendelea wao na familia zao.

Nenda pale Ikulu. Alipoingia Benjamin Mkapa tulianza kusikia baadhi ya majina yakitajwa. Kwa sasa hatujui wapo kina nani. Ila uhakika ni kwamba kuna watoto wa vigogo ama wa chama au serikali.

Je, balozi zetu zina watoto wangapi wa watu kama kina Msekwa? Je, wamepelekwa kule kwa vile wana sifa au ni kwa vile wazazi wao ni vigogo?

Hivi karibuni nchini Kenya kuligunduliwa kitu cha kutisha ambapo mabalozi na baadhi ya wafanyakazi ni ndugu wa vigogo. Walitajwa mabalozi Dk. Wenwa Akinyi (USA) dada yake Waziri Mkuu, Raila Odinga; Bi Catherine Muigai Mwangi (Jamhuri ya Ireland) ambaye ni dadake Waziri wa Afya, Bi Beth Mugo, ambaye pia aliwahi kuwa mkurugenzi wa tume ya mawasiliano wa Kenya Airways.

Bi Mishi Masika Mwatsahu ambaye muda wake kuwa balozi nchini Pakstan umerefushwa ni dadake Waziri wa Uchukuzi, Chirau Ali Mwakwere.

Wakati huo huo mwakilishi wa kudumu wa UNESCO, Dk. Mary Khimulu, ni dadake Waziri wa Ushirika, Joseph Nyagah. Huyu aliteuliwa mara ya kwanza wakati kaka yake alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.

Profesa Sospeter Machage (Urusi) ni pacha wa Waziri Wilfred Machage. Kabla ya kuteuliwa alikuwa akiendesha hospitali binafsi kwenye mji mdogo wa Kilgoris.

Mwingine ni Elkanah Odembo (Ufaransa) ambaye shemeji yake ni Chief Whip wa serikali, Jakoyo Midiwo.

Kwa vile sura za ufisadi barani Afrika zinafanana, kuna haja ya Watanzania kuanza kuchunguza mabalozi wetu nje hata wafanyakazi wa ubalozi nje kujua kuna kina “Msekwa, Sons & daughters” wangapi.

Hapa tunaongelea balozi zetu nje. Bado kuna sehemu nyingine nyeti kama uhamiaji, bandari, wizarani, mbuga za wanyama na sehemu nyingine zenye vipato vikubwa.

Hapa bado hujamulika makampuni binafsi ya vigogo yanayofanya shughuli za kibiashara na serikali hiyo hiyo wanayotumikia. Rejea sakata la miraba ya uwindaji na kumilikiwa na mawaziri na wazito wengine serikalini au washirika, wake na marafiki zao.

Rejea kashfa inayozidi kusukumizwa chini ya busati ya wizi wa mapato pale Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo ambapo wizi umehamishiwa Machinga Complex.

Je, kwa mtaji huu nchi haijawa mali ya vigogo wanaotuaminisha kinadharia kuwa ni yetu wakati kivitendo ni yao?

Je, pesa aliyokaa nayo Msekwa kwa muda aliokaa nayo ingekuwa benki ingezalisha faida kiasi gani? Je ni wangapi wamekopa pesa kubwa kuliko hii kwa miaka mingi kama ilivyobainika kwenye ufisadi wa CIS hadi leo hawajalipa wala kuchukuliwa hatua?

Je ni wangapi wamepeleka watoto, marafiki hata ndugu zao kusoma nje kwa pesa za umma ambao hatuwajui kwa vile wanalindana serikalini?

Kwa nchi za Magharibi zinazotupa misaada, kitendo cha Msekwa kilitosha kumwajibisha na chama chake kuingia tafrani kwenye uchaguzi ujao. Lakini kwa vile Tanzania ni shamba la bibi la mafisadi, hakuna anayeliona hivi.


Achia hili la Msekwa, Mawaziri na wabunge waliotuhumiwa kughushi vyeti vya taaluma wamechukuliwa hatua gani zaidi ya kuendelea kupeta wakati ni matapeli wa kawaida tu? Je, rais hata umma unaowavumilia wahalifu kama hawa si wa wahalifu na mafisadi pia?

Leo watu kama Profesa Mwesiga Baregu wananyimwa ajira wakati kuna matapeli walioghushi wako kwenye nyadhifa za juu wakilipwa vinono kwa ujuzi wasio kuwa nao!

Kama kuna maafa yanayoikumba Tanzania si mengine ni haya. Maana hawa wanalipwa pesa nyingi na kutumiwa na wezi wanaoitwa wawekezaji kwa kujua hawajui lolote kiasi cha taifa letu kuendelea kuwa maskini wakati lina raslimali nyingi.

Mawaziri vihiyo au walioko madarakani kwa udugu ndio chanzo cha mikataba michafu kama ya TRL, IPTL na mingine inayolisumbua taifa. Nani atamwajibisha nani kwa mfano mtu anayeshutumiwa kutenda kosa ni shemeji au kaka hata dada wa anayepaswa kumwajibisha?
Chanzo: Tanzania Daima Januari 27, 2010.

Kilimo First au ulaji wa magabacholi kwanza?

“The zebra needs not pronounce on its zebritude. It simply stripes!” Kwamba pundamilia hapaswi kuonyesha upundamilia wake bali milia (mistari) Kwaku Sakyi-Addo Wole Soyinka, gwiji la fasihi naye anasema: “A tiger does not shout its tigritude, it acts.” Yaani duma hapigi kelele kuhusu uduma wake bali hutenda. Kumbuka huyu jamaa tumesoma chuo kimoja huko Maiduguri.

Nilikutana na mistari hiyo hapo juu nilipokuwa nikitafakari baadhi ya sera mpya za sasa yaani Kilimo First na utabiri wa mauti.

Mzee mzima nilikuwa kizani. Kabla ya magabacholi waliooiweka kaya mfukoni kuanza kuparurana sikuwa najua kilichokuwa kikiendelea kuhusiana na usanii wa kilimo first! Hapa ijulikane. Kilimo first ni tofauti na kilimo kwanza ya jamaa.

Eti wanasema ni msaada toka kwa serikali ya India. Msaada msahadaa? Kwa nini itulazimishe kutumia wahindi wezi kama si wizi? Mbona wajep wakitoa msaada hatuoni wajep kuja kusimamia msaada?

Je wajua: bila hawa magabacholi-nyemelezi kutaka kutoana roho huku wakiwaanika wabungwe uchi tusingejua ukweli? Si wewe si mimi tuliokuwa tukijua! Kumbe kilimo first ni sanaa tupu na ulaji wa magabacholi na mawaziili? Niulize kwanini?

Yako wapi matrekta zaidi ya kusikia vita ya kunguru ambayo ni neema kwa panzi wa Tanzia? Nani hajui kuwa lile dili la matrekta 1,000 lenye thamani ya madafu 50,000,000,000 limeanza kujulikana kuwa ni la makuadi wenye madaraka na magabacholi fisadi papa kama alivyosema mzee wa Nkuu na Nronga?

Sijui kama jamaa zangu wa Kimbushi, Nkwarungo, Kyarie, Kalali, Namikupa, nakapanya na Goweko wanajua hili. Sasa nawajulisha mchana kweupe; mwaliwa kama hamjui jueni mwaliwa ati!

Matrekta 1,000 ni kitu gani? Jembe la kukokotwa na mbuzi linatushinda tunadandia matrekta!

Mmefungwa kamba, kama mbuzi, mmeingia mkenge tena kichwa kichwa! Muambiwe mara ngapi kuwa adui yenu ni nyinyi wenyewe na ujinga na woga wenu ndiyo mtaji wa mafisadi hawa?

Jiulizeni. Nani awezaye kilimo usawa huu wa ubangaizaji, umachinga, ufisi, ufisadi, ubinafsi, ubinafsishaji na ukuushaji? Kwa nini wasiseme wazi umachinga, ufisadi na ubangaizaji kwanza? Hakuna haja ya kuona aibu kusema wakati unatenda hivyo.

Watu wanakwenda kwenye sinema za semina na wakiwashwa washwa na warsha wanarejea na mipesa tena bila kutoa jasho. Nani awekeze kwenye jembe? Mie naenda zangu Ngurdoto kwenye sinema elekezi narejea na minoti.

Kuna bomba mpya nimetoa hapa. Wasiojua maana ya ukuushaji nawasaidia. Ni ile hali ya mkuu wa kijiwe kumtumia Bi Mkubwa wake kutengeneza fweza kwa kuwatumieni wake zenu na mabinti yenu chini ya mradi sawa na wa bi mkubwa wangu wa MAWAWAWA.

Pia ni ile hali ya vitegemezi vyake kusimikwa kwenye ulaji mbali mbali iwe chamani au lisirikalini. Upo hapo mwanawakwa? Shauri yako!

Wenzenu wamewageuza mitaji nyie bado hamstuki! Ajabu kila siku mnaotea Kanani wakati mwendo uonyeshavyo mtaishia Sudan tena Darfur. Kalagabaho uuwiiii! Nilizeje muelewe kuwa mmekwisha wajameni? Anayedhani mie mbea ajiulize: tangu lini paka akamjali panya kama hamna namna? Na kwanini sasa tena wakati wa lala salama.

Huko nyuma walikuwa wapi na wanafanya nini zaidi ya kuhomola wakati nyinyi dhiki zikizidi kuwaponyoa mmoja baada ya mwingine? Mla mla leo kesho kala’ni?

Tuzidi kujidodosa. Hivi kweli katika karne hii ya ishirini na mosi nani anataka kulima iwapo hata maksai wakilazimishwa hugoma na kulia kama binadamu? Nani anataka trekta wakati hata baiskeli hana?

Mpe uone kama hatauza mataili ili kununua lau nyama ukiachia mbali kupeleka mtoto sekondari hata kuongeza kidosho kingine kutokana na bi mkubwa wake kuharibiwa na shida mlizotengeneza. Unadhani hawa ni wapumbavu kama mnavyowachukulia?

Tuseme ukweli hata kama unauma na kutusuta. Inataka roho ya mwendawazimu kuaminisha na kuaminishwa kuwa kitu kama hiki kinawezekana kwenye kaya ya wamachinga na mafisadi. Inataka wendawazimu acha roho yake kuamini ubangaizaji katika kila nyanja unaweza kuwavusha wachovu na walevi wa kaya hii.

Kwa nini kuvushwa na jembe ziliposhindwa almasi, dhahabu, chuma, tanzanite na madude mengine ya thamani? Kwanini msiyatoe kama mikopo kwa wafa na ngwamba lau waweze kutanua kama nyinyi?

Afadhali hizo bilioni mngewapa mawaziri wajengee mahekalu kama ya boss wa Bunch of Thieves (BoT) au yule mwenzie wa zamani wa shirika la migao ya umeme.

Juzi jamaa yangu mmoja alitoa mpya. Kwanza ieleweke. Jamaa mwenyewe fyatu kama Sofiii. Hivyo akisema jambo si vizuri kulipa uzito. Anavuta ndumu si mchezo!

Unajua alizozaje? Eti anasema ukiona hivi ujue mtaji wa kusakia ulaji kwenye uchafuzi wa uchaguzi mkuu wa kaya unatafutwa hivyo? Yeye bila hata woga anasema hii ni EPA nyingine ya mahepe!

Hayo tuyaache. Wanuka njaa na uchovu watajijua kama wataingia huu mkenge mbichi. Mie simo mwanawakwa!

Juzi nilisika watu wakipiga kelele kuwa wazee tung’atuke kwenye kijiwe. Hawa jamaa wapuuzi kweli. Eti wanasema tuwapishe vijana! Hebo huu ni ubaguzi. Kwa nini jamaa yenu mliyemchagua kuwa ni kijana amefanya nini cha mno ukimlinganisha na wazee kama Alhaj Ali?

Hata ukimlinganisha na mzee Moi Kibaki mzee wa Kikikuyu ana nafuu. Hazururi hovyo mzee wa watu wala mkewe ingawa ni mbabe hana MAWAWAWA kama huyu wenu.

Balaa lote hili lilianzishwa na bwana mazingaombwe mwenyewe alipotaka kuwafunga kamba na kuwatumia vijana asijue naye ni mzee. Yeye ana ujana gani? Hivi kweli kijana wa miaka 60 ni mzee au mzee wa miaka 60 ni kijana?

Tukiacha uvivu wa kufikiri, tutajua kuwa tatizo letu si uzee wala ujana bali uroho, roho mbaya, ufisadi na upofu uliojaa ubinafsi wa kupindukia. Tatizo letu ni mfumo mbovu usiorekebishwa siku nenda rudi.

Kwanza nani anataka kuitwa mzee usawa huu ambapo ukistaafu lazima ung’ang’anie mjini maana shamba kunatisha kwa ukapa na ukosefu wa usalama? Hujaona kila anayestaafu anaishia Bongo badala ya kwenda kwao Namikupa na Likawage kwa jamaa yangu Kimdunge Mwehu?

Ukiona vipi unaanzisha kampuni ya bi mkubwa anakwenda pale Ubung’o au Machinga Comp anafanya vitu vyake siku zinayeya. Lakini siyo kufikiri kulima ati!

Hata ndugu zangu wa Zaainzibaa wanafikiria kuwa Hong Kong kama alivyowahadaa jamaa wa Madevu aliyepata kichaa cha Karumekenge. Hong Kong hawalimi ati. Kilimo ni mambo ya kizamani sana. Hii ni karne ya sayansi na teke linalokuijia. Kilimo tuliwaachia akina Adam na Eva ambao nao walikiona noma wakaamua kuvamia mti wa kati kati ya bustani.

Ila jamaa zangu nao wajue. Hong Kong haiji kwa kuvunja katiba na kuhadaiana kama nionavyo sasa ambapo ndoa ya mkeka inazidi kupanda chati huku jamaa zangu wakiingia mkenge kichwa kichwa!

Nani atahangaika na kilimo iwapo biashara kama vile ya bangi, uchuuzi, udokozi na jinai nyingine inalipa haraka? Mie nimeamua kuanzisha dhehebu langu la dini ili kuepuka kilimo. Mke wangu naye ameanzisha kampuni ya kukusanya ushuru na Ngo ya kupigania haki za wanawake.

Tukikusanya pamoja mambo yanakwenda ati ukiachia mbali zile ninazoponyoa kwenye kijiwe.

Hakuna atakayejiingiza kwenye kifo cha jembe wakati kupiga soga maofisini kunalipa. Kama wapo basi ni wale ambao hawana pa kwenda wala kamba za kuifungia jamii na kusavaivu.

Naona jamaa wanakuja kuhutubia kuhusu kilimo first. Acha nijikate nifikiri jinsi ya kuwatoa takrima hawa wanaokuja kunibamiza mkenge. Salamu kwa Pio Msekua. Bwana we lipa njuluku za watu na ueleze kitegemezi chako kilivyopata ulaji kwenye ubalozi.
Chanzo: Tanzania Daima Januari 27, 2010.

Friday 22 January 2010

Mkuchika asituchonganishe na jeshi


HATUA ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika kufungia gazeti la KuliKoni kwa siku 90 inalenga kuchonganisha jeshi na wananchi.

Mkuchika anasema gazeti limetenda “kosa” la kuandika taarifa za kuvuja kwa mitihani ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kwanza, huu ni uonevu na hatua inayolenga kupoka haki ya binadamu ya kujieleza, kutoa na kupokea habari bila kizuizi. Waziri anazima sauti ya wasio na sauti.

Pili, kumekuwa na tuhuma za kughushi vyeti vya taaluma nchini. Wanajeshi hawajawahi kuhusishwa kwenye tuhuma hizi. Tatizo la ufisadi wa kitaaluma linazidi kukua sawa na ufisadi mwingine.

Mawaziri wapatao watano na wabunge kadhaa wana vyeti vya kughushi. Hili kwa sasa si kosa kwa kuwa limetendwa na wateule. Si rais wala bunge wamewawajibisha watuhumiwa; hata kuwakaripia.

Hii ndiyo maana kitendo cha gazeti la KuliKoni kufichua uoza kama huu kimejibiwa kwa kulifungia badala ya kulipa nishani. Limegusa ambako wakubwa wasingependa paguswe. Bali naamini hata jeshi haliungi mkono uamuzi wa waziri.

Askari wengi wangependa ufanyike uchunguzi ili waliotenda kosa wakipatikana waadhibiwe. Kwani, siyo jeshi lote linalohusika na mitihani; utungaji wala usimamiaji.

Hivyo hatua ya Mkuchika inatuelekeza kuona kuwa watawala wanataka kulibinafsisha jeshi kwa kulijengea sifa chafu. Hata haya madudu yanayoitwa kampuni ya dhahabu ya Meremeta na ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi serikalini, ambamo jeshi letu limehusishwa, tayari yanajulikana kuwa ulikuwa mradi wa watawala na jeshi lilitumiwa kama pazia.

Hivyo, kama kuna mashaka katika kilichochapishwa na gazeti, basi ulihitajika uchunguzi kama alivyopendekeza mhariri wa gazeti husika ili ukweli ujulikane.

Tusisitize. Kwa jeshi lenye kufanana na watu linaolinda na kutumikia, inapotokea taarifa kuhusu kashfa au uvunjaji wa sheria au kanuni, haliwezi kuogopa kuandikwa au kutendewa sawa na Watanzania wengine.

Kitu gani Mkuchika anaweza kusema hakiwezekani kutendwa na jeshi? Mara ngapi wanajeshi wamewapiga polisi? Mara ngapi wamewapiga wananchi, tena mkoani Dar es Salaam?

Kila uchafu wa aina hiyo unapotokea, utawala wa jeshi unachukua hatua ya kuchunguza na hata hatimaye kuadhibu wahusika. Kwa nini kunakuwa na uchunguzi? Ni kwa kuwa makosa au uchafu haukutendwa na jeshi zima.

Kwa hiyo, kama kuna wizi wa mitihani haliwezi kuwa kosa la askari wote. Haliwezi pia kuwa kosa la kwanza ndani ya JWTZ. Lazima wawe wachache wanaoweza kugundulika kwa njia ya uchunguzi.

Waziri anakinga nini?

Kinachoweza kujadiliwa hapa ni, kama hakuna tatizo kwanini “wahusika” wanakataa kuunda tume na kukubali taarifa ya tume iwe wazi tena neno kwa neno?


Je, waliokataa uchunguzi ni jeshi au serikali ambayo inaonekana ililichukulia hili kwa hasira na ukosefu wa busara kwa faida zake kisiasa? Hatua hii nayo inalenga kuwatisha wananchi na kujenga hofu kwa jeshi lao.

Kimsingi, kufanya kama serikali ilivyofanya, licha ya kuficha ukweli, imelifedhehesha jeshi letu na kuua ukweli.

Kwingine Afrika ambako kila kitu juu ya jeshi ni siri, “usalama wa taifa” umezaa “uhasama wa taifa.” Tanzania tusifikishwe huko. Bado tunaliheshimu na kulithamini jeshi letu.

Waziri atumie busara badala ya hasira. Asijenge imani ya kila kitu jeshini kinakwenda vizuri na hakuna kinachoweza kukosewa. Tafadhali Kapteni George Mkuchika usituchonganishe na jeshi. Lifungulie gazeti la KuliKoni haraka na utafute sababu nyingine.

Chanzo: MwanaHALISI Januari 20,2010.

Thursday 21 January 2010

Forgery in Africa's Military

Kulikoni, one of Tanzania’s Swahili Weekly has been banned for 90 days. Why? It exposed an examination fraud in Tanzania People’s Defence Force (TPDF)! The story Kulikoni published alleged that the process of setting and sitting for exams in the army provides easy chances for officers who are not qualified.

In its issue number 812 of November 27th, 2009, the paper further alleged that TPDF exams of 25th May, 2009 in Dar es Salaam, Ruvuma, Tabora, Arusha, Mwanza and Zanzibar centers were leaked out and that Ruvuma and Tabora were the leading culprits.Remember, Tanzania is also dogged by exam forgery allegations involving ministers and Members of Parliament. Were Tanzania soberly against this abomination, this would be welcome in order to act decisively against this alarming criminality. But nay!

With regards to this surging purge against press freedom and accountability, the minister for Information, Culture and Sports, Capt. George Mkuchika, argues: “The country's army holds respect across Africa, because it has been tested in different circumstances, including fighting in a war against the Idi Amin regime in Uganda. TPDF is also among peace keeping forces in United Nations and African Union units.” What nonsense!

In trying to get away with it, the minister adds: “The editor could not substantiate his claims in the story after he was formally asked by the registrar of newspapers. Kulikoni editor refused to provide evidence but instead asked TPDF to form a committee that would look into the matter and the newspaper would publish (in verbatim) the committee's report (as it is for everybody to see).”

How can we believe this conflicting hoo-ha from the minister? Did the editor fail to substantiate his story or the government and the army refused to take in the method proposed by the editor? Good enough, the minister himself is an army captain. Even if the editor would furnish all water-tight evidence, would it help with this frozen thinking given that what he reported is against the ‘sacred’ army? He was in a straight jacket and the verdict is vexatious.

You can’t say that the army is highly respected compared to the Wananchi simply because it fought wars or participates in the UN peace keeping force. It does so as its duty and it is enabled by the taxpayers to do the same.Everybody in the country has the share in whatever achievement the nation makes. Therefore, the country must hold respect for all of its citizenry regardless of their trade.

What’s more, the minister argues that the said paper breached the National Security Act of 1970 and the Newspaper Act of 1976, "which prohibits publication of seditious stories that might cause unrest within the army. Was the story seditious or informative? Should we keep quiet if the army embezzled public money for fear that they can wreck havoc on us! If this is the practice, aren’t we hijacked by the said armies in Africa? Aren’t we under military regimes acting behind the curtains?

What dismays and discombobulates is the fact that the army officer demanded that the editor disclose his source under the pretext of substantiation! Nowhere in a democratic country on earth, is the media duty-bound to disclose its source. It is totally against ethics and rule of law.

The effecting of this ban shall make Tanzania to join other dictatorial regimes in Africa that curtail press freedom. The army is a sacred cow and 'untouchably' noble and the authorities can not keep their cool when they are touched. Everybody is rubbed the wrong way in our continent especially when catawampus steal from us in broad daylight thanks to being protected by corrupt armies.

Befuddled as we are, should we show them what a daughter of Ares did to Hallirhothios when justice failed her? How can we fail short of thinking doing that if at all what we evidence is nothing but their naked self interests in the name of leadership? The armies we wrongly thought are spending our tax to guard us are there for a kit and caboodle of corrupt rulers.

Now that bloom appears to be off the rose as far as rule of law is concerned, it is time we face it head on. Though in many countries people care about the luge than the legislature, this issue of favouring the armies even when they contraband the law, must awake us. Fear of armies does not help any of us except rulers and their cronies. We need to stamp out all those thieves who cling to power and accumulate dubious wealth. Though many people were killed in Guinea last year, their message is still crystal clear. And this can act as an early wake up call. To know how their voices added up, refer to how the tyrant in that country wanted to victimize his aide who decided to shoot him as a result.

We’re talking of one incident in one country where the army is alleged to have allowed its members to openly forge. Remember. Almost all armies in Africa are enjoying illegal privileges such as getting bigger hidden budgets than other dockets, traveling free and what not. This sums it up that albeit claiming that Africa is democracy, it still is under military rule.

To evince this, I will cite an example from my own country where military officers dominate some positions such as Regional and District commissioners. Most of our RCs and DCs are soldiers whereas the multiparty constitution stipulates that no military personnel or civil servant should serve in political capacity for the fear of favouritism.

It’s no wonder thus to find that police people and military personnel have strong ties with the ruling party. And this is why in Tanzania; two bodies are: the army and the ruling party. This marriage of hoity toitty plus military is the great barrier for hoi polloi in Africa to forge ahead.
Source: The African Executive Magazine Jan. 20, 2010.

Tuesday 19 January 2010

Maalim Seif, usimkwaze Karume

HAKUNA ubishi. Katibu Mkuu na mtu mwenye ushawishi mkubwa katika Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad, anazidi kujichanganya na kutaka kuuchanganya umma.

Alikaririwa hivi karibuni akitaka Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, Amani Abeid Karume, aongezewe muda wa kukaa madarakani siku tatu baada ya yeye kusema hana mpango wa kukiuka katiba kuongeza muda mwingine juu ya ule uliotajwa na katiba.

Alikaririwa akisema: “Baada ya kutafakari, mimi binafsi naungana na wale wanaotoa wito wa kuchukuliwa hatua ya kusogezwa mbele kidogo uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka huu.

Aongezewe kipindi cha kati ya mwaka mmoja au miaka miwili, ili kutoa nafasi kwa Rais Karume kukamilisha kazi njema aliyoianza.”

Huyu bwana anatuchanganya licha ya kujichanganya. Hajui kuwa Karume hakuwa akifanya kazi yake bali ya wananchi. Kwanza aambiwe wazi. Hakuna kazi ya Karume. Pili, aelewe Karume hakusomea hiyo ‘kazi’, hivyo kazi hiyo inaweza kumaliziwa na mtu yeyote. Nani kamwambia Zanzibar itapata rais mwenye kufanya kazi mbaya na si njema?

Je, huku ni kuishiwa kisiasa na kimkakati kiasi cha mtu aliyegombea urais mara nyingi tu na kushindwa kuamua kujipiga mtama?

Demokrasia gani isiyoheshimu katiba? Kama seif, kama Augustine Mrema ameishiwa udhu wa kugombea baada ya kushindwa mara nyingi na kuamua kuacha basi awaachie wengine wenye udhu waongoze.

Hivi Seif bado hujui kuwa kuvunja katiba kwa namna yoyote ni kosa la uhaini? Je, haya ndiyo matunda ya makubaliano ya faragha ambayo yanaanza kuonyesha masilahi binafsi kuliko umma?

Kumbe wanachama wa CUF waliotaka kumtia adabu baada ya kutangaza walichoona kama usaliti hawakukosea? Je, hii ndiyo sababu ya kufanya makubaliano kwa niaba ya chama kuwa siri na mali ya Maalim Seif na Karume? Je, Serikali ya Muungano itajipinga na kukubali usaliti huu wa mchana?

Je, Seif hajui kuwa Karume anajua katiba ya chama na nchi yake kiasi cha kusema wazi hataki kuongezewa muda?

Hakika hii ni usanii (political gimmicks). Maalim anahitaji msaada hata kama kaahidiwa vinono haviwezi kuja kwa kuvunja katiba. Je, hapa nani anataka kumtumia nani kati ya Karume na Seif?

Kwanini Seif hakujiuliza swali moja kuu na muhimu kama kweli anatetea masilahi ya umma na si yake binafsi. Kwanini Karume ametambua haki ya mshikamano wa Wazanzibari baada ya kumaliza muda wake kama ni kweli?

Kwanini muafaka unaoihusu jamii-hasa vyama vikubwa viwili hasimu vya siasa na pande mbili za nchi na si watu wawili- ufanyike kwa usiri mkubwa kama hakuna namna kama Seif anavyoanza kubainisha huku akiwa ameachwa peke yake baada ya mwenzie kutamka wazi hataki hicho Maalim anachoona kama ni nusra ya Zanzibar.

Je, Serikali ya Muungano itakubali kudhalilishwa wazi wazi kwa kuonyeshwa kama haina mamlaka na sehemu moja ya nchi ukiachia mbali kushindwa kutatua matatizo ya Zanzibar ?

Inabidi Maalim akumbushwe kuwa Karume hawezi kuukata mkono ambao umemlisha kwa miaka kumi, yaani Serikali ya Muungano. Hata akiwa mwizi wa fadhila akafanya hivyo, anajua madhara yake kutokana na nguvu na namna ya kufanya mambo ya serikali hii.

Kwanini Maalim anataka kutumia makubaliano ya mdomo tena ya watu binafsi kuvuruga katiba mbili, yaani ya Muungano na ya Zanzibar?

Je, ameshauriana na wanasheria wake au amekurupuka asijue hili haliwezekani? Je, huu ni mwanzo wa mwisho wa Maalim baada ya kuonyesha wazi kuwa hawezi kukivusha chama? Swali moja litamuandama Maalim hata Karume. Kwanini muafaka baina ya Karume na Hamad na si CCM na CUF kama kweli una nguvu kisheria? Maelezo?

Mbali na ufafanuzi wa hivi karibuni -ulioonyesha kuwa pigo kwa CUF- wa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, hakuna kauli rasmi kutoka CCM.

Rais Kikwete hajazungumzia hili kwa kinaganaga na kwa namna inayostahili kama mkuu wa chama na serikali. Je, hakushirikishwa? Kama hakushirikishwa ni kwanini?

Kama alishiriki anagwaya nini wakati katiba aliyoapa kuilinda inataka kuvunjwa? Kama anashiriki na hataki kuhusishwa, je, anajua mambo yatakavyoharibika mbele ya safari au hajui-ajenda ya siri - kuvunja katiba tena wakati wa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu?

Kwanini Maalim amegeuka ghafla hata bila kuchelea aliyowahi kusimamia na kusema huku nyuma ukiachia mbali kuwaacha wanachama na wafuasi wake hoi? Kuna nini nyuma ya pazia?

Je, ule uvumi kuwa Maalim anadhani anaweza kuchukua dola hivyo kuhitajika na Karume kumlinda unaanza kuwa ukweli? Je, Karume alisema hataki kipindi kingine kama geresha bwege akijua kuwa msukumo wa CUF utaifanya CCM isalimu amri?

Hivi Maalim anadhani hatujui kuwa siku zote amedai ushindi wake uliibiwa na Karume huyo huyo na CCM? Hili swali ndilo linalowasumbua CUF. Ushindi wao umerejeshwa lini?

Je, unataka kurejeshwa kwa makubaliano ya siri ambayo kisheria hayawezi kuleta maana wala kutekelezwa? Kwanini Maalim amekuwa akimlaumu Karume baba kuwa alifanya makubaliano ya Muungano kwa mdomo na sasa anarudia yeye?

Kwanini muafaka nje ya CCM kama hakuna namna? Jiulize tena. Kwanini kwa usiri mkubwa na bila kutarajia hivi? Wengi wanajiuliza. Na kwanini saa chache kabla ya uchaguzi na kwa faida ya nani kama siyo Uzanzibari kutangulizwa mbele ya Utanzania? Je, watafanikiwa?

Kitu kingine kama si ubinafsi ambacho Maalim alipaswa kujiuliza ni haki za wale walioathirika kwenye sakata hili.

Kwanini baada ya miaka tisa ya Karume kuwa madarakani? Je, hapa haki za wale waliopoteza maisha, mali na kugeuzwa vilema kwanini hazikuzingatiwa kama hakuna namna?

Wapo wanaoota wakisema serikali ya mseto yaja. Kwa katiba gani na sera ipi? Ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hiki. Hizi ni ndoto za mchana na bahati nzuri CCM wameishalitolea jibu hili.

Rejea ufafanuzi wa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, hivi karibuni: “Watu wanatakiwa kuelewa kuwa hakuna muafaka wowote wa kudumu ulioafikiwa baina ya vyama hivyo, bali kilichotokea ni CUF kumtambua Rais Karume tu na hakuna makubaliano mengine. Kutokana na uamuzi huo, CUF inaweza ikapata nafasi mbili za uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi.”

Maalim, usimkwaze Karume. Kaishasema wazi hataki kuongeza muda. Hata CCM haina mpango huo. Kama makubaliano yanalazimisha hivyo, jaribu njia nyingine ambayo haikudhalilishi wala kuvunja katiba. Kwanini ulazimike kulamba matapishi yako?
Chanzo: Tanzania Daima Januari 20, 2010.

Tafdhali rais, tangaza mali zako

MARA ya mwisho ikiwa ni ya tano kumtaka Rais Jakaya Kikwete kutangaza mali zake ilikuwa ni kwenye gazeti hili Agosti 12, 2009.

Kwa hiyo, hii ni mara yangu ya sita kumtaka Kikwete atangaze mali zake, ukiachia mbali kumkumbushia pia kurejesha nyumba za umma alizoahidi kurejesha lakini asifanye hivyo.

Nina sababu kuu mbili

Mosi, ingawa ameshindwa kutekeleza ahadi zake zote alizotoa kwenye kampeni za 2005, anaweza kutimiza moja-kutangaza mali zake na za mkewe ambaye ni mwenyekiti wa NGO inayoingiza mabilioni ya shilingi ya WAMA.

Pili, ni baada ya kuona waziri wake mkuu Mizengo Pinda kukiuka mizengwe yote na kuamua kuweka hadharani ‘utajiri’ wake (kama kweli hakuna alichoficha. Nasema hivi kutokana na uzoefu na udhaifu wa sheria husika ukiachia mbali usanii).

Jambo hili licha ya kumuongezea heshima, ni suto kwa wale ambao hadi sasa hawataki kuweka wazi utajiri wao. Pia Pinda ametoa changamoto kwa rais ambaye ndiye bosi wake.

Amefanya kitu kilichomshinda bosi wake. Hili linahitaji ithibati na ujasiri wa hali ya juu. Maana kwa tawala zetu za kujuana, kufanya hivi kunaweza kumponza mhusika huko tuendako.

Ingawa watu wenye ufisadi wa kimawazo wamemuona Pinda kama hajafanya kitu chochote, kuna haja ya kumpongeza na kumpa moyo kuwa kazi aliyofanya si haba. Imewashinda wengi akiwamo bosi wake. Laiti wangemuuliza ni kwanini hakutaja za mkewe, kiasi fulani ingeingia akilini.

Kitu kingine kinachovutia kuhusiana na tukio hili la kupigiwa mfano, ni ile hali ha Pinda kuwa maskini kwa viwango vya wakwasi wetu. Huyu amejionyesha asivyo pale kutafuta mali bali kutumikia umma. Kwa vile tunataka watu waadilifu wasio na ulafi na ufichi, tuweke nukta hapa ili hapo baadaye atufae.

Hili likitokea, hata hivyo, litamjenga kisiasa hasa katika nchi ambamo watu waadilifu ni tone la mkojo baharini.

Wakati Rais wa Urusi, Dimitry Medvedev, alipotangaza azima yake ya kuweka wazi utajiri na mapato ya familia yake, ikiwa ni kuthibitisha dhamira yake safi ya kupambana na ufisadi, nilidhani Kikwete angefuatia. Lakini wapi? Kwanini? Ajuaye ni Kikwete mwenyewe.

Juzi juzi serikali ya Rwanda ilipowatimua watu kazi kutokana na kutotangaza mali zao, nilidhani Kikwete angetangaza mali zake.

Bila kutangaza mali kama sheria itakavyo, Kikwete ataendelea kuvutia mashambulizi mengi kuwa ni muhimili wa ufisadi licha ya yeye kuwa ni fisadi.

Pia atawapa kichwa wasaidizi wake mafisadi. Hawatatangaza mali zao. Maana jogoo aliwafundisha vifaranga kunya ndani. Kikwete ni kama baba. Hawezi kuzuia watoto kutokunywa iwapo yeye analewa tena chakari.

Kuna wanaoona kuwa Kikwete anaogopa kutaja mali zake kutokana na kutokuwa na maelezo ya jinsi zilivyopatikana hasa ikichukuliwa kuwa alipotuhumiwa kwenye list of shame hakujitetea wala kutoa maelezo.

Hii maana yake ni kwamba kilichodaiwa na Dk. Wilbroad Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA kule Mwembe Yanga ni kweli tupu.

Je, kwanini Kikwete hataki kutaja mali zake? Je, alineemeka kwa namna yoyote na dili za awamu ya pili na tatu? Je, ni miongoni mwa waliopewa mgawo hata wa nyumba za umma zinazosemekana ziligawiwa kwa vigogo wa wakati ule ambapo naye alikuwa waziri na mjumbe wa baraza la mawaziri lililopitisha wizi huu?

Kuepuka kumzushia rais, tungemtaka atangaze mali zake na kutoa majibu ya baadhi ya maswali muhimu kama kipato chake na cha mkewe hasa ikichukuliwa kuwa kwa kuanzisha NGO kama ya Anna Mkapa aliyemchafua mumewe, anafanya biashara ikulu.

Hata hili la NGO nimeishaliandikia sana. Kwanini ianzishwe baada ya kuingia madarakani na kuona madudu ya EOTF? Tulioko nje tunaiona EOTF kama madudu. Kwa walio ndani ni ulaji wa dezo tena mkubwa.

Kikwete, kwa kukaa madarakani miaka mitano bila kutangaza mali zake, ilipaswa lichkuliwe kama kosa kubwa ambalo lingetosha kutorejea tena.

Maana hatujui aliingia na mali kiasi gani na kutoka na kiasi gani. Kwa maana nyingine ni kwamba amejenga mazingira yenye utata kuhusiana na uadilifu na uwezo wa kuongoza kwa mifano.

Iwapo Benjamin Mkapa aliingia na kutangaza mali zake lakini akatoka bila kutangaza anachukuliwa kama fisadi, inakuwaje kwa Kikwete na mkewe ambao hawakutaja wakati wakiingia? Na sasa wamebakiza miezi michache kuondoka.

Ingawa wanaosema Kikwete hapaswi kuongezewa muda wanaonekana kumchukia, mambo mengine Kikwete ajilaumu mwenyewe.

Huwezi kuhimiza watu watii sheria wakati wewe na familia yako mnaivunja wakati mlipaswa kuwa kioo kwa walio chini yenu.

Kama ni uongozi, huu ni mfano mzuri wa utawala mbovu usioheshimu sheria wala kanuni. Kama kutangaza mali imekuwa mbinde, je, itakapokuja kuitolea maelezo si tutakesha?

Ingawa Kikwete amekuwa akipuuzia miito mbali mbali kumtaka atangaze mali zake, ajue kitu kimoja. Watanzania wa sasa si wa jana. Wanaweza kumbwaga kwenye uchaguzi, kama uchaguzi utakuwa wa haki kama ilivyotokea nchi jirani ya Kenya.

Watu wamechoka na uongozi fisadi na fichi. Wanataka watu watakaowavusha toka kwenye bahari hii ya ubabaishaji na ufisadi. Na hakika hawa si wengine bali watakaoonyesha sura zao halisi kama alivyofanya Pinda.

Ingawa wapambe wa Kikwete wanajitahidi kutuhadaa kuwa ametenda mema, hakuna baya kama kuficha mali zako huku ukiwa msimamizi wa mali za umma.

Ingawa wanajipa moyo kuwa atashinda tena kwa kishindo kama ilivyotabiriwa na wapiga ramli na makuadi, mambo yanaweza kubadilika asiamini macho yake.

Maana imekuwa too much. Ameshindwa kutupeleka Kanani alipotuahidi. Anaweza kusingizia mtikisiko wa uchumi duniani ingawa si kweli zaidi ya matumizi mabovu na usimamizi mbovu, je, hata hili la kutangaza mali nalo limemshinda?

Sasa kama ameshindwa suala dogo lakini nyeti kama hili la kuthibitisha uadilifu wake, atatufaa kwa lipi huko tuendako ambapo ufisadi unazidi kupanda chati?

Tafadhali bwana rais, tuondolee kupiga ramli. Tangaza mali zako na za mkeo kabla ya kumaliza muhula huu.
Chanzo: Tanzania Daima Januari 20,2010.

Mie mali sitangazi ng'o

JUZI nilitaka kupasuka. Nilitaka kupasuka baada ya kusoma magazetini kuwa kumbe waziri mkubwa wa Jamhuri ya Mgongano ya Kaya, Mizengwe Pita alitangaza mali zake hadharani.

Huyu jamaa hajui anatuponza wengine hata kama hatumo kwenye lisirikali lake? Laiti angejua baada ya kutia guu kijiweni swali la kwanza litakuwa ni lini nitatangaza mali zangu!

Bwana mkubwa uwe unaomba ushauri wetu hata kama hatumo kwenye lisirikali wala chama chako. Hayo ni ya wakubwa tuyaache. Tutayamaliza tujuavyo.

Sasa Pita kapindua hata wakubwa zake kama sisi akaamua kutangaza mali bila mizengwe. Kweli mzee mzima nitanusurika? Juzi kuna mshauri wangu alitaka niige mfano wa waziri mkubwa. Sikumuelewa.

Kwanza waziri mkubwa mwenyewe si wangu ni wa linchi. Mie ni kiongozi wa kijiwe bwana. Niliamua kujitetea kwa mshauri wangu huyu anayejitia ni mzalendo.

Baada ya kurejea nyumbani nilimfikishia salamu za kijiwe hasa kutaka nitangaze mali zangu. Kumbe naye alishazinyaka kwenye runinga yetu. Hivyo ulikuwa ni msiba kwetu hasa ikizingatiwa kuwa mwaka huu nina uchaguzi kijiweni na walevi wanajua madudu na sanaa zangu zote.

Swali la kwanza ilikuwa ni kumuuliza Bi mkubwa tufanyeje. Alijibu kuwa tufiche baadhi ya mali zetu kama vile mikufu yake, viatu vya bei mbaya na kadhalika. Niliona ni jambo zuri. Tatizo lilikuwa ni je waliokwisha kumuona na vipuri kama hivyo nisipotangaza si watauliza? Jibu? Alibaki kutoa mimamcho!

Wakati mimi nikihangaika na jinsi ya kuepuka kikombe hiki, najiuliza. Naye jamaa yangu nonihino wa juu kule atafanya nini iwapo walio chini wameamua kufanya kweli yarabi? Ajabu tunajua kuwa Shortie wake chini ya MAWAWA ameishatengeneza mabilioni kama si matrilioni. Sijui atakuja na kamba gani msanii huyu toba?

Jamaa inaonekana kuna uhasama kwenye usalama wa taifa. Inakuwaje jamaa aweke vitu vyote wazi wakati huu mbaya? Je utabiri wa shehe Ubwabwa unaanza kumgeukia jamaa au wale wazee wazima wenye hekima kama mlima wameanza kufanya vitu vyao. Pamoja na kwamba nami nimeoza, nangoja kuona jamaa atalitatua hili kwa kamba gani au sanaa tuseme.

Je naye atafanya kama alivyoshauri mke wangu-kuficha ukweli na kuwaongopea walevi wake au ataamua kuendelea kula pini kama mimi?

Tunituni alijifaragua akatangaza wakati wa kuukwaa. Lakini wakati wa kuutema sikusikia cha mali wala hali zaidi ya kutimka kama kibaka baada ya kuwa amechafuka mbele nyuma. Je jamaa yangu hapa atatembeza sanaa gani ili niige mfano ninusurike bila kuadhirika?

Naona ataagiza Shehe Ubwabwa atabiri kuwa akitangaza mali zake atakufa ghafla. Siku hizi kufa ghafla ni sera ati. Hivyo si bora kutangaza mali kabla ya uchaguzi wezi waliotamalaki kuteka mabasi wanaweza kwenda kumuibia jamaa hata kumdhuru na kaya ikawa kwenye mtafaruku.

Kwa vile wanakaya wengi ni waumini wazuri wa ushirikina na udaku, huenda wataingia mkenge kwa mara nyingine na jamaa aponyoke msalabani saa tatu kabla ya kusulubiwa. Kama atawapata katika hili nitaamini kuwa jamaa hawa kweli mataahira. Mie simo. Mie janja bwana. Naendelea kukamua wakati wao wakikamuana.

Jana nilipita kwenye baa moja jina siri kubwa kwa usalama wa taifa kama kuchonga peni dhidi ya ndata wanapoiba miexaminations. Nilisikia jamaa akisema ana usongo na jamaa. Anasema asipotaja jumla ya nyumba zake hasa zile ndogo, jamaa atajinyonga mbele ya listeitihausi.

Mwingine nilimsikia kwa masikio yangu mwenyewe akisema kama jamaa hatatangaza mali, yeye atazitangaza mali za jamaa azijuazo.

Jamaa ingawa ni mlevi alikuwa na pwenti. Unajua alisemaje? Alisema hakuna haja ya sisi wakubwa kudanganya kwa sababu mali zetu zinajulikana. Kwa kusema hivyo nilisikia kiroho kikininyatuka. Maana huyu jamaa alinitisha.

Kama wanajua mali zetu si anaweza kutuvua nguo kichaa huyu tena hadharani?

Kumbe walevi wanajua mengi sema wanajifanya mabwege tu. maana mwenzie alisema tena kwa uhakika kuwa anaijua miradi mikubwa mikubwa ya bi mkubwa kule kusini! Mwenzenu kusikia hivi nilisikia haja ndogo ikianza kunibeep.

Vyoo vyenyewe vya kulipia na siku hiyo sikuwa nimetembea na kashi zaidi ya ATM mashine iliyonusurika kuchanywa na waziri nonihino alipomuuliza mlinzi fulani: unajua mimi ni nani? Jamaa mmoja alisikika akijibu: “Fisadi wa kawaida kisiasa aliyependelewa.”

Basi bwana, nikiwa naanza kuloa kwa jasho, nilingoja jamaa amalize nijue kama anajua habari za kijiwe changu. Maana baa ile iko karibu na kijiwe chetu. Akiwa anajiandaa kusema si mlevi mwingine aliingilia kati. Alisema: “Sisi hatutaki kutangaza mali tu bali kueleza hiyo mali ilivyopatikana wakati sisi tunakufa bila hata tone la mali.” Du! Kumbe walevi wanajua siasa kuliko wanasiasa.

Mara nilimsikia mlevi mmoja akisema: “Nangoja kusikia waziri wa uwekezaji na uchukuaji na kadhalika akitangaza utajiri wake. Maana kila siku humuona mwanae akiendesha Hummer anapokuja mtaani kumchukua changudoa jirani. Hubadilisha magari kama nguo. Je, huyu ataweka mambo hadharani madudu kama haya?”

“We unasema huo mgari na kubadilisha magari kama tai. Mbona huongelei yule kitegemezi wa vidudu aliyehonga wapiga kura wa kamati ya nonihono kumchagua tena kwa kukata madafu 35,000 kila kichwa? Hawa jamaa wanatufanya sisi wapuuzi siyo? Wanarithisha ulaji kwa watoto wao je watoto wetu wale wapi? Baya zaidi wanasema kaya ni yetu sote wakati wamejibinafsishia wao na walamba viatu wao!”

Kicheko.

Mwingine alisema. “Natamani mzee wa Vijipesa au Daktari Iddiliishia kwa Rashid naye atangaze tujue kama atatangaza akaunti yake ya Londoni.” Mwenzie anamkosoa na kusema: “Sema Landani siyo Londoni bwana we.”

Nikiwa najiandaa kuondoka, mlevi mmoja alitoa mpya! Alisema. “Nijuavyo sera za sanaa na mibangaizo ya kaya hii, jamaa atatufunga kamba na kusema ameruhusu wa Kupinda atangaze vitu vyake ili yeye afanye hivyo baada ya uchaguzi. Baada ya hapo, imetoka lala salama. Mmeliwa wajameni. Jamaa ana roho ya chuma hatangazi kitu na akifanya hivyo sanaa tupu.” Mwenzie aliingilia ghafla.

Nkiwa najiandaa kusikia bomu jingine si mlevi mmoja mwenye lafudhi ya Kiha alikuja na mpya. Alisema. “Mugaboye, mie nashaangaaa.

Umesikia yale ya Zaainzibaaa. Eti yule Mugabo wa madevu anataaka uchaguzi uhairishwe atimize dili lake la kutumiana na Karumekenge wa Migebuka! Karabaye mugaboye! Hizi ni ngorane gusa ye.”

Hili limenikera hadi natamani nimlambe mtu bakora. Eti kule Zaainzibaa yule jamaa wa Madevu aliyejigeuza nyumba ndogo ya Karumekenge anasema tusifanye chaguzi? Is he sick or what? Akasome katiba aache uvivu wa kufikiri.

Kwa vile haja ndogo iliendelea kunibana, niliamua kukitoa nikiwaza jamaa yangu, kama mimi atafanyaje?

Tangazeni mali zenu muumbuke. Hata mkigoma, mtaumbuka tu kama Madevu na Karumekenge wanavyoumbuka na kuhaha kutuweka sawa wasiweze.

Mie simo ila nyinyi mmo tu tangaza au tangaziwa tujue nani afaa na nani amechemsha. Hapa kuna haja ya kupigana vibuti kama alivyosema Matewo wa Kareishi. Jamaa amezidiwa na hana sera wala sura.

Lo! Kumbe nami nahusika! Naona jamaa wa tume ya maadili wanakuja kuulizia utajiri na madili yangu. Acha niishie.
Chanzo: Tanzania Daima Januari 20,2010.

Thursday 14 January 2010

Kawawa, hatukuenzi, tunakusanifu tu

Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na marehemu mzee Rashid Kawawa.



Ni wengi wamejitahidi kuelezea walivyomjua marehemu Rashid Kawawa mmojawapo wa viongozi waadamizi na waasisi wa vuguvugu la kupigania uhuru wa Tanzani na rafiki na mshirika wa karibu wa nguli baba wa taifa marehemu Mwalimu Julius Nyerere.

Ukijikumbusha vilio na mayowe na machozi ya mamba kwenye msiba wake hivi karibuni, unaweza kuona ukweli wa kichwa cha habari hapo juu-unafiki unafiki unafiki mtupu!
Ni kitu kimoja kilikosekana katika onyesho hili-nyimbo zilizotungwa tayari kuomboleza kifo chake.

Kama Mwalimu Nyerere, Kawawa alikuwa mkiwa na mwenye sononeko litokanalo na kushuhudia mema yake yote yakiporomoshwa hasa baada ya kuingia awamu ya tatu na ya nne ambazo zinasifika kupanua ufa uliowekwa na utawala wa awamu ya pili chini ya dhana mbovu ya ruksa ambayo kimsingi ndiyo msingi wa ufisadi na kuvunjika kwa maadili tunavyolalamikia. Rejea kuvunjwa kwa Azimio la Arusha chini ya utawala huu na kuundwa ujambazi wa Zanzibar.

Leo huu si mjadala wetu. Tunataka kubainisha kuwa machozi yaliyomwagwa kwa ajili ya Kawawa ni ya mamba na sifa alizopewa ni za unafiki. Wengi wa waliomwelezea Mzee Kawawa, walimwelezea kama mtu msafi aliyechapa kazi na kufuata maadili. Je wao wanachapa kazi na kufuata maadili kama yeye au madili na soga?

Kawawa na mwenzake Nyerere waliweka miundo mbinu kwa taifa kisiasa hata kijiografia. Je hawa wanaowanafiki na kuwasifia wanafanya nini zaidi ya kubomoa vitu hivi? Muulize Benjamin Mkapa. Wakati akina Kawawa walianzisha NBC yeye aliiuza tena kwa bei ya kichaa!

Muulize Jakaya Kikwete rais wa sasa, akina Kawawa walichunguzana na kutimuana kama ilivyotokea kwa Marehemu Oscar Kambona na wengine. Leo tunalindana! Rejea kushindwa kuwawajibisha watuhumiwa wa ufisadi na kughushi waliojazana kwenye ofisi za umma.
Je namna hii twanaweza kumuenzi au kumheshimu Kawawa zaidi ya kumuona kama mzee mshamba ambaye hakujua kutumia madaraka yeye, familia yake na marafiki zake? Huwezi kumuenzi mtume Mohammad (SAW) kwa kula nyama ya nguruwe au Yesu Kristo kwa kupenda utajiri wakati wao kwao hivi vitu vilikuwa haramu na zahama.

Leo kila mtu atajifanya anamuenzi na kumjua Kawawa kwa vile ameishatoweka. Ukweli ni kwamba hawampendi bali kumtumia tu. Hii imenikumbusha mhindi mmoja tapeli ambaye amekuwa akimtumia baba wa taifa bila kustukiwa. Ni juzi juzi amejinasa pale alipodai taasisi yake inaongozwa na watu fisadi wakati fisadi ni yeye.

Kawawa alisifika hadi kuitwa simba wa vita. Bahati mbaya hawa wanaojifanya kumjua na kumuenzi si chochote bali wasaliti ambao ni panya kwenye ligi ya kumtafuna simba wa vita Kawawa ambaye vita yake ilikuwa kumkomboa mtanzania.

Huwezi kuridhia mikataba mibovu inayosababisha kuibiwa raslimali walizolinda na kutunza akina Kawawa ukamheshimu Kawawa. Huwezi kuuza viwanda na mashirika waliyoyaanzisha akina Kawawa ukawaheshimu hadi kuwaenzi zaidi ya kuwatumia kwa sababu binafsi kisiasa. Huwezi kuingia madarakani kwa pesa chafu za EPA tofauti na wao walioingia kwa uchapakazi na uzalendo wa kupigiwa mfano ukawaenzi mashujaa hawa. Huwezi kutawala kwa ushikaji na usanii ukawaenzi mashujaa hawa. Yote katika yote, huwezi kukataliwa nao ukaja kuukwaa baada ya wao kuondoka ukajifisifu unawajua na kuwaenzi. Huenda neno kuenzi lina maana nyingine tofauti na tuijuayo. Kama ni hivyo sadakta.

Kawawa na wenzake waliongoza nchi. Hawakuiacha ijiendee au kutawaliwa na mafisadi nyuma ya pazia. Walijenga, kuheshimu, kutekeleza na kutegemea miiko na misingi ya uongozi siyo watabiri, mafisadi na mitandao. Walevi na wazinzi hawawezi kusafisha makaburi ya watakatifu. Wakifanya hivyo jua basi ni kufuru sawa na watawala wa sasa kuwaenzi waasisi wa taifa hili wanaloliuza kwa hongo ya upuuzi mdogo mdogo.

Hatuna uchungu na taifa hili kwa sababu hatukulivujia jasho wala kulihangaikia zaidi ya kulipoka kwa njia zao za kifisadi na jinai na kulikabidhi kwa mabwana zetu.
Tungemuenzi Kawawa tungepambana na ufisadi badala ya kuupamba kwa mbinu hizi na zile. Tungemuenzi Kawawa tungechukia rushwa, utukufu, kupenda anasa na sifa tusizo hata stahili. Tungemuenzi Kawawa tungeheshimu maadili ya uongozi aliyoanzisha na si madili kama ilivyo.

Kawawa alisifika kwa kukataa posho za vikao visivyokuwa na faida zaidi ya kuwa vigwena vya ulaji.

Kawawa aliwahi kuua simba waliowasumbua wanakijiji wenzake. Sisi tumefuga majini yanayowasumbua watu wetu. Bila majini haya hakifanyiki kitu hata kiwe kidogo namna gani.

Wao waliwekeza kwenye utu na watu. Sisi tumewekeza kwenye vitu na wawekezaji na mafisadi wetu. Wao waliishi kwa ajili ya kesho. Sisi tunaishi kwa ajili ya le oleo bila kujua kuna kesho-vipofu na majuha.waliasisi ujamaa na kujitegemea. Sisi tumeasisi uhujumu (uhujumaa), kujimegea na utegemezi. Waliasisi Tanzania ambayo tumeigeuza Tanzia.

Walijenga taifa tunalouza na kubomoa. Waliongoza kwa mifano safi . Tunaongoza kwa mifano michafu. Rejea EPA, Richmond , CIS, ANBEN, Tanpower na uchafu mwingine. Wala maskini hawakujilimbikizia mali za wizi kama sisi. Rejea ukwapuzi wa Kiwira na pesa zitokanazo na hongo na NGO za wake na washirika zetu. Hawakuwarithisha madaraka watoto wao kama sisi. Hawakuwa na wenyeviti wa chipukizi wala wa umoja wa vijana waliotoka viunoni mwao kama sisi.

Wakati kina Kawawa walikonda na kupandwa presha kuikomboa nchi hii, sisi tunaotesha viriba tumbo na kutononoka tukiifuja na kuangamiza. Wao walikuwa chachu sisi dumuzi wa maendeleo. Hawakufuga mafisadi-rejea kutaifisha mali za mabwenyenye na makabaila. Sisi tunagawana nyumba za umma na kufadhiliwa na maadui hao hao. Je hapa twaweza kujinakidi kuwa tunafanana na kuwaenzi akina Kawawa?

Panya hawawezi kumuenzi simba wagugunaye ngozi yake. Ni nani ana udhu na roho ya kumuenzi Kawawa miongoni mwetu. Nionyeshe mmoja nitakuonyesha panya elfu. Heri ya kutawaliwa na simba mmoja kuliko panya mia. Pumzika mahali pema kwa salama mzee wetu Rashid Mfaume Kawawa aka Simba wa Vita aka Charles Chaplin wa Tanzania na mkono wa kuume na mwanafunzi mtiifu aliyefuzu wa Mwalimu Nyerere.

Nenda kamwambie Mwalimu kuwa nchi yake sasa haipo tena bali jina. Hakika hatukuenzi Kawawa bali kukutumia na kukusanifu tu.
Chanzo: MwanaHALISI Januari 14,2009.

Wednesday 13 January 2010

Afghanistan's Lesson for Africa

Afghan parliament in session


Many African countries have unnecessary bigger governments made of cronies of their nugatory rulers. Aloof personal greedy and carbuncular constitutions, many parliaments are but rubber stamps when it comes to keep rulers on tenterhooks. This coupled with inducements (like being appointed in boards of various government firms) makes it difficult to connect the dots as far as mega corruption is concerned.

Afghanistan, a war-torn country, has made an indelible mark on democracy. Its parliament unanimously turned down 17 out of President Hamid Karzai’s 24 nominees for his cabinet. Instead of seeing a conga-line of MPs supporting the president’s choice, the world witnessed the rejection of Afghanistan president’s sacred cows! What a precedent for Africa to ape!

This reminds me of what happened in Britain in 1642 when the parliament under Oliver Cromwell toppled King Charles whom they later hanged after he tried to usurp power as opposed to Magna Carta. This is a breakthrough for struggling Afghanistan compared to Africa that is hijacked by dictators, thieves and their stooges. Parliaments in Niger, Senegal and Uganda were used to amend the constitutions in order to let their dictators remain in power. In Zimbabwe, the tyrant is still in power thanks to the support by parliament.

In the Gambia, Libya, Algeria, Tunisia, Egypt, Ethiopia, Eritrea and other countries the situation is the same. Parliaments are used as napkins by rulers to clean their mess at the peril of hoi polloi.

"I think, unfortunately, that the criterion used was either ethnicity or bribery or money," MP Fawzia Kufi said, in remarks quoted by AP news agency.

To the contrary, in Tanzania’s cabinet, there are five ministers and many MPs alleged to have forged their degrees not to mention many more that are alleged to be nominated just because they are closer to the president. Other countless are alleged to have big hand in various thievish privatization scandals dogging this country. Being the cronies or ‘sacred cows’ of the president, the alleged forgers are still in office though illegally. The Tanzania parliament has nothing it can do to show them the door thanks to the ruse propaganda instigated against it after it heroically ousted Edward Lowassa, a former corrupt prime minister. This move has verily cost the speaker of the house who narrowly survived being expelled from the ruling Party- Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Many African rulers appoint their ministers not by merit but by connection. Some are appointed just because they contributed generously in enhancing the big men to bribe voters and police to ascend to power. Some helped them to rig elections especially those manning internal and security dockets. Some share ethnicity with the big men. Some know their dirty linens so as to act as consgliori. Some bribe them. Refer to how Amin appointed former Ugandan minister for foreign affairs Princess Elizabeth Christobel Edith Bagaaya Akiiki. This lady however declined to obey Amin’s evil advances.

Another source of bad and huge governments is party solidarity. Ruling parties use their mandate to form a bad government thanks to being able to control the houses full of their members and cronies they sponsored in the elections. Also in many African countries, the relatives of rulers are propelled to the parliaments in order to man and convince others to back them. In Tanzania, the president has the power to appoint ten MPs. What are these for if not to back the strong man?

This is why, for example, in Kenya, many post-election warlords are still in the cabinet not to mention thieves and those that plundered DRC in neighbouring Uganda. This is why names of the first families and their cronies feature high in government and political circles in Africa.

The killer bait that turns MPs into fish, sheep even sycophants is the provision in many African constitutions that empowers president to appoint his ministers from the MPs. This, if anything, has enabled African presidents to hijack and enslave MPs despite representing the citizenry directly.

Division of power is clear that nobody should serve two organs of the state at a go.But in Africa this is not espoused to. Instead, the presidents are like Kings even demigods with more discretion to abuse the country as pleased.

In some countries, ruling parties have even introduced party gangs in women, youths, elders and parents they use to hoodwink and mobilize the citizenry to back the same. These gangs are allocated some illegal positions in government and party ranks as a tip to remain loyal to the leaders of their parties. In Tanzania, the ruling CCM party has turned youths into zombies that can swallow any nonsensical stuff from politburo and politicos at any time and manner. Sheepish and bullish as they’re, they fully participate in rigging elections and brainwashing rural dwellers whose know-how is next to never thanks to be starved in all spheres of life.

This coupled by MPs looking for employment from the chief executive has ruined democracy in Africa. Instead of representing the voters the said MPs represent the president so as to entice him to appoint them ministers or members of the boards of parastatals.

This is why many bad and sabotaging laws are enacted thanks to the support from MPs. This is why it is difficult to impeach African rulers even to question some of their bad decisions. They have all cards in their hands. To make things smoother, African governments give MPs big salaries and many emoluments so as to make them easily forget the people they say they represent.

Going back to Afghanistan, is it the love of afghan MPs to their country or their constitution that made it possible for them to squarely reject president’s choice? We need to dig deeper so that we can use the same formula to tame our Thieves-in-Chief.

Indeed, though perceived as a failed as it seems, Afghanistan still has something to teach Africa. Can African MPs ape Afghan MPs?
Source : The African Executive Magazine Jan. 13, 2010.

Tuesday 12 January 2010

Je kuna mpango wa kukolimba wapinzani wa Kikwete?





Katika nchi zinazotawaliwa na serikali dhalimu na chafu, watawala hukaa madarakani kwa muda mrefu wakitumia mbinu chafu mbali mbali. Vitisho, wizi wa kura, hongo, wizi na hata ulaghai hutumiwa sana katika kufikia malengo yao ya kukaa madarakani kinyume cha utashi wa watawaliwa.

Katika kufanikisha hili, vikundi vya kijamii kama vile vijana, wanawake, matajiri, matapeli, waandishi wa habari hata wana taaluma hutumika. Kadhalika vikundi vya kidini hutumika. Hii ikichangiwa na ujinga, uroho, umaskini na tamaa za wahusika, watawala-wenye pesa na madaraka-huvutia kila wachumia tumbo.

Hivi karibuni vikundi uchwara vya kidini vimejiingiza kwenye siasa chafu vikiwaunga mkono watawala ili vipate lau makombo ya ufisadi. Rejea maandamano yaliyokuwa yameandaliwa na viongozi wa kidini wa mitaani kutaka kupinga wale wanaomkosoa rais. Kutokana na ujinga na umaskini kiakili wahusika hawakujua kuwa kumpinga au kumkosoa rais ni haki ya kidemokrasia!

Hivi karibuni mtu aliyejipachika utabiri katika Afrika mashariki na kati, shehe Yahya Hussein alikuja na mpya. Alitabiri kuwa atakayesimama kumpinga rais Jakaya Kikwete kwenye uchaguzi ujao atakufa ghafla! Hii inatisha na ni jinai. Amejuaje iwapo kisayansi hata kiimani binadamu hakujaliwa kujua ya kesho? Je huyu jamaa anatumiwa kutisha au kupeleka ujumbe kuwa atakayejitokeza ndani ya CCM kama ambavyo hali inaonyesha atashughulikiwa kama alivyofanyiwa katibu wa zamani wa CCM Horace Kolimba? Je hili likitokea jeshi la polisi litaacha kumshughulikia mhusika kwa vile anamtetea rais? Je ametumwa na rais kuwatisha wale anaoona wanaanza kutaka asipewe nafasi ya kugombea awamu nyingine? Je huu si uhuni?

Kutojua sheria wakati mwingine huleta ushujaa wa kipumbavu. Inakuwaje mtu mzima kiumri atabirie watu vifo asijue ikitokea anawajibika yeye kisheria?

Kinachoonyesha kuna namna, ni ile hali ya shehe Yahya kumfagilia Kikwete kiasi cha kudai atashinda kwa kishindo wakati hata kampeni za uchaguzi hazijaanza kisheria. Je kwanini shehe Yahya amesema hivi tena kwa kujiamini kama hakuna njama hii chafu? Je hii si taarifa kuwa tutake tusitake tumchague tusimchague lazima Kikwete, kwa mbinu ajuazo, ashinde hata kama hana sifa?

“Natabiri kuwa Kikwete ndiye Rais mpya wa mwaka 2010 na atakayempinga katika chama chake atakufa ghafla. Natabiri ushindi wa Rais Kikwete mwakani utaleta serikali ya mseto Tanzania Bara na Tanzania Visiwani," alisema Shehe Yahya.

Bahati mbaya sana, taifa letu limegeuka la washirikina na mataahira wanaoweza kulishwa kila uchafu. Ni juzi juzi tumeona kwenye vyombo vya habari mchungaji wa kujipachika Getrude Rwakatare akionyesha “mchawi’ aliyekuwa na mfupa wa binadamu bila wahusika kuchukuliwa hatua! Inakuwaje karne ya 21 tunaruhusu upuuzi kama huu? Kwanini hatujifunzi kutokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaliyoasisiwa na kuchochewa na waganga njaa na wachungaji uchwara kama hawa? Ingekuwa si hivyo wachumia tumbo hawa wangeona aibu na kuogopa kusema upuuzi wao. Kwa wanaokumbuka kilichompata shehe Yahya alipokuwa mkuu wa kitendo cha masuala ya kidini Bakwata chini ya marehemu shehe mkuu Hemed Jumaa, atakumbuka alivyotimuliwa bila hata yeye kutabiri hili lingemtokea. Tulimuona akilialia kwenye vyombo vya habari akiwafokea waliomuuliza ni kwanini hakuweza kutabiri hili.

Inakuwa hatari sana pale watawala wanapotegemea na kuamini watu kama hawa ambao kimsingi hawana utaalamu wowote bali utapeli na uganga njaa. Hebu jionee mwenyewe uganga njaa na utapeli ulipo kupita nukuu hii ya shehe Yahya: "Kwa hiyo Kikwete alirithi urais huu kutoka kwa Nyerere. Ngoja awamu ijayo, mwachie Mkapa, kauli hiyo bado haijafutwa kwani mirathi kutoka kwa mwalimu ni ya awamu mbili.’

Hivi ni mtanzania gani hajui kuwa Nyerere alimkataa Kikwete kutokana na kukodisha ndege kwenda kuchukua fomu Dodoma bila kueleza yeye na mwenzake Edward Lowassa walipokuwa wamepata hiyo pesa? Nani hafahamu kuwa Nyerere alimwambia Kikwete kuwa hana ukomavu kisiasa na aliokuwa ameshikamana nao wameoza ukiachia mbali kutokuwa na sera wala udhu wa kuwa rais? Shehe Yahya asitufanye wote wapumbavu tusio na kumbukumbu wala kujua historia ya jana.

Huyu mshirikina inapaswa aambiwe na kuonywa kuacha kuutukanisha uislam (kwa kuutumia kupiga ramli) ukiachia mbali kutaka kumtumia marehemu baba wa taifa kuhalalisha utapeli wake. Asimtumie kwa vile hawezi kujibu ameisha kufa. Hii ni kashfa kwa Nyerere kusema aliridhia ufisadi. Nyerere hakuwa kipofu, juha hata mjinga kiasi cha anachotaka kuonyesha huyu anayeitwa shehe.

Kuonyesha ni kwa jinsi gani anavyotapa tapa anataka kupindisha ukweli kuwa aliyerithi madaraka toka kwa Nyerere ni Kikwete badala ya Ali Hassan Mwinyi!

Shehe Yahya anazidi kuonyesha ujuha wake pale anaposema: "Natabiri kuwa kutatokea maandamano makubwa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa pande zote za vyama vya upinzani na CCM kuhusu wizi wa kura,"

Haiwezekani rais ashinde kwa kishindo halafu wabunge wake wasipewe kura sambamba naye ili kumrahisishia kutawala. Huu ni uganga njaa wa hali ya juu.

Angalia ukihiyo mwingine: "Zanzibar, CUF imeshinda, wewe ukiona mtu anamkaribisha mshindani wake nyumbani basi ameshindwa," alisema Shehe Yahya.

Maskini mtabiri wetu hajui kuwa kilichotokea Zanzibar hakilengi anakoelekea kutokana na CCM kuweka wazi kuwa hawana sera ya serikali za mseto! Kwanza si kweli kuwa CUF imeshinda. Ingeshinda mwenyekiti wake prof. Ibrahim Lipumba asingesema kumtambua rais wa baraza la mapinduzi, Amani Karume ni kamari ya kisiasa (political risk).

Zanzibar hakuna ushindi kwa CUF zaidi ya kutaka kutumiana na kuzidiana ujanja ambapo mmoja anadhani anaweza kumlewesha mwenzake wakaingia kwenye uchaguzi halali akashinda asijue mwenzie anampigia mahesabu ya kujenga mshikamano haramu wa kizanzibari ili aweze kugombea ngwe nyingine kinyume cha katiba! Utabiri , uganga na siasa wapi na wapi?

Kuna haja kwa wapinzani wa nje na ndani ya CCM kutafuta haki mahakamani kwa kufungua kesi ya kutaka shehe Yahya aeleze alipopata habari hizi chafu na mpango mzima ili kuzuia watu kukolimbwa na hatimaye kuja kuambiwa ilitabiriwa.

Kuna haja ya kumshauri Kikwete kuachana na kutumiwa na waganga njaa hata kama ni kwa kumpa matumaini yasiyokuwepo. Umefika wakati wa kuliondoa taifa kwenye ushirikina na ufisadi wa kiimani na kiakili.

Je kuna mpango wa kuwatisha au kuwakolimba wanaompinga Kikwete?

Lazima watanzania wajue. Kama kuna mtu atakayesimama kumpinga Kikwete na akafa tujue ameuawa kama alivyobainisha shehe Yahya. Na hili likitokea mtu wa kwanza kuwajibishwa awe shehe Yahya. Kwani inaelekea anajua mpango huu mchafu. Ndiyo maana haogopi kusema hadharani. Mkutano wake na vyombo vya habari ni ushahidi tosha wa hili mahakamani.
Chanzo: Tanzania Daima Jan. 13, 2010.

Mpayukaji aanza maandalizi ya uchaguzi

Ndugu wapendwa sana wanakijiwe na jamii kwa ujumla,

Huu ni mwaka wa uchaguzi wa kijiwe chetu kitukufu. Hivyo, kama mgombea mtarajiwa, nimesimamisha au kupunguza kuzurura ili kuwa karibu na kijiwe tayari kukibamiza mkenge. Hivyo, leo niko kijiweni tele kama pishi la mchele.

Najua wachovu wengi walionichagua kwa kupenda sura yangu wameishanichoka. Wanasema: wanataka sera siyo sura. Hata wale waliosema mie chaguo la Mungu wameishastukiwa nao kustuka. Wameniruka futi mia!

Tufuatane katika kikao cha leo uone ninavyosulubiwa na kujinasua kabla ya siku ya tatu-uchaguzi.

Namuona mpambe wangu na mropokaji mkuu Mgosi Machungi almaarufu Joe Makambale ametulizana pale akitabasamu baada ya kunideku nikitia timu.

Pia yupo mwezeshaji mkuu gabacholi Kanji almaarufu Roast Tamu. Eddie Ewassa au Mkwapuzi Mbwa Mwitu yupo pia. Kadhalika yupo msomi Mkata tamaa almaarufu Daktari (Lakini si wa kughushi).

Timu leo imekamilika. Namuona Mpemba almaarufu Madevu na mzee Maneno almaarufu Kimdunge Mwehu bila kumsahau mzee Kidevu almaarufu Mtoboa siri.

Naona msomi anaingia akiwa anaimba wimbo wake wa kizungu. Ukiona msomi kaimba ng’eng’e jua mambo si mambo. Huko mbele sijui kama salama.

Anaendelea kujiimbia:

By the rivers of Babylon , there we sat down
ye-eah we wept, when we remembered Zion.

When the wicked
carried us away in captivity
required from us a song

Aaaaa aaaaaaa!

Now how shall we sing the lord's song in a strange land
Let the words of our mouth and the meditations of our heart
be acceptable in thy sight here tonight
Let the words of our mouth and the meditation of our hearts
be acceptable in thy sight here tonight
nnnnnnh nnnnnnh!

By the rivers of Babylon , there we sat down
ye-eah we wept, when we remembered Zion.

By the rivers of Babylon (dark tears of Babylon )
there we sat down (You got to sing a song)
ye-eah we wept, (Sing a song of love)
when we remember Zion . (Yeah yeah yeah yeah yeah)
By the rivers of Babylon (Rough bits of Babylon )
there we sat down (You hear the people cry)
ye-eah we wept, (They need that ???)
When we remember Zion . (Ooh, have the power)

Naanza kujitetea baada ya msomi kuacha kuimba. “Nani kakumbusha farao rafiki yangu?”

Msomi anajibu haraka: “Mwizi, msanii na jambazi yeyote hata awe na sura nzuri hana tofauti na farao. Period.”

Kijiwe kimepigwa na butwaa hasa ikizingatiwa si wote ung’eng’e unapanda.

Machungi anajifanya hii si kitu. Anaanza kwa kunikaribisha kwenye kijiwe. Anasema: Mheshimiwa Mpayukaji. Ingawa ni siku nyingi hatijakutia machoni kutokana na shughui za ujenzi wa kijiwe, keibu kwenye kijiwe chako.” Anabwia kahawa yake huku akijichekesha kama changu na kuendelea: “ Kwanza tipe habai za bi nkubwa ambaye juzi tilimuona kwenye uninga akikufanyia vitu vyake.”

Naweka chini kikombe changu cha tangawizi na kukohoa na kusema: “Mabwana na mabibi, ni furaha iliyoje kuona kijiwe chetu kimeshikamana na kina amani. Sina maneno kuwashukuruni mnavyoelewa mzigo nilio nao kwa ajili yenu.”

Kabla ya kuendelea, lazima niwataarifuni. Tuna mgeni kijiweni. Naye si Mwingine ni bi Sofii Fyatu almaarufu Lioness. Anasifika kwa kubwia ugolo, kuvuta ganja na kupayuka hakuna mchezo!

Kabla ya kuendelea bi Sofii anatia guu kilingeni. Anasema: “Mzee na kiongozi wetu. Hapa tuna ugogoro. Kuna watu wanamuonea wivu Ewassa kwa vile ni kidume cha shoka.”

Kabla ya kuendelea Mpemba anaingilia. “Weye mama tumia lugha ya kistaaarabu ati. Nani waona si kidume weye au kwa vile siye si mumeo?” Jaribu utupe uone kama lugha haitabadirika.”

Mara Mgosi Machungi anadandia kuokoa jahazi. “Jamani, tiwe na adabu. Kia mtu ni kidume cha shoka kwa nkewe bwana. Naomba Sofiii usiseme hivyo tena. Tinaweza kupandwa na hasia tikafanya kitu mbaya hapa.”

Anapokea sigara kali toka kwa Sofii na kuendelea. “Leo tinataka tipange mikakati ya uchaguzi na sio habai za vidume na upuuzi mwingine kama huu.”

Kachokoza nyuki! Mipawa anatia timu bila hata kutoa taarifa. “Hapa hakuna cha kupanga mikakati ya uchaguzi bali ya kumuengua mwenyekiti (yaani mimi).” Ananiangalia kwa jicho la chuki na dharau na kuendelea. “Mwenyekiti amekuwa akizurura muda wote. Mara yuko Nairobi kwa wakora, mara Uganda kwa akina SSebo mara huku mara kule.”

Hapumui. Anaendelea. “Baya zaidi anatumia pesa ya kijiwe na mkewe kwenye haya matanuzi utadhani tulimchagua huyo shorty wake!”

Napandwa na hasira na kutia timu. “Mipawa nakuheshimu. Usirudie kumuita lazizi wangu shorty. Huoni alivyopendeza na kuchana siku hizi?”

Mwe! Nimelikoroga! Msomi anaingilia bila hata kungoja nimpambe bi mkubwa. Anasema: “Mzee kubali umechemsha sana hata kama wapambe zako akina Makambale Mgosi hawaoni.

Huwezi kukiibia kijiwe ukatumia pesa vibaya halafu ukaanza kutufundisha jinsi ya kukueleza matatizo yetu. Mie napendekeza usiruhusiwe hata kugombea mwakani. Maana wewe ni hovyo. Umeacha kijiwe kiendeshwe na akina Mbwa Mwitu na Kanji na Mgosi ilhali sisi hatutendewi haki. Kijiwe kinakabiliwa na ombwe la uongozi.”

Anajiweka vizuri kwenye benchi na kuendelea. “Kwenye kampeni ulituahidi maisha ya raha kwa kutoa kashata na kahawa bure kwa wote tusistuke kumbe wote ni wewe na wapambe zako na shorty wako!’

Anapiga chafya mara mbili na kuendelea. “Ulituhadaa kwa sura yako nzuri wakati ule. Sasa huna sura wala sera. Umenenepeana kama guruwe kwa pesa ya kijiwe. Huyo mkeo ndiyo usiseme. Yaani hata pesa ya mkorogo atumia ya kijiwe!”

Mzee uzalendo unanishinda. Naamua kuamka na kukabiliana naye nisijue daktari wangu alinishauri nipumzike. Nilianguka nikazimika kwa dakika kama mbili hivi kabla ya kuokotwa na wapambe wangu na kuniondoa kwa aibu.

Ukiondoa wapambe wangu, naona wajumbe wote wanatikisa vichwa kuunga mkono yaliyosemwa na msomi.

Wakati wakinizoa zoa msomi anaendela kuzoza. “M tu mwenye keshajiishia! Mwaka huu tunataka matendo si maneno matamu na usanii wa kijinga. Sisi si wajinga tena na tumechoka na kutumiwa kama nepi.

Nasema wazi ingawa wapambe zako wanasema kukukosoa ni kukuchukia-hufai ndugu yangu kitoe uache watu wenye uwezo wafanye vitu vyao. Tumekuchoka tumekuchoka tumekuchoka hakuna mfano.”

Baada ya kumwangiwa maji na kupata nafuu nakaa nikiwa nimejiinamia.

Kabla ya kuendelea kusiliba, Mpemba anaingilia. “Ami usemayo kweli. Lakiini kuna namna ya kuyaongelea ati.”

Hangoji Mpemba amalizie. “Hakuna cha namna wala nini jamaa hafai hata ujumbe wa nyumba kumi achia mbali ukuu wa kijiwe!’

“Loo!” Anatia guu mzee Maneno. “Kwanza Mpayukaji omba radhi sheitwan apite. Pili Msomi hujakosea ingawa umekosea. Tatizo la wengi wetu ni kujifanya wanajua hata kama hakuna wanalojua; kujifanya wanaweza hata kama hakuna waliwezalo. Kusema ukweli mkuu tunakushika faini. Toa tangawizi na kashata ili kikao kiendelee.”

Kwa nyonde nyonde namnong’oneza Kanji anifadhili kuwanunulia walevi tangawizi. Naona nyuso zinaanza kufurahi.

Msomi anasema. “Mie sinywi tangawizi yako. Ni hongo. Mie si panya bwana.” Anaamka na kujikata kislesi!

Nabaki nimepigwa butwaa. Lakini hanitishi huyu. Nitamwambia shehe ubwabwa atabiri kuwa atayakenichukia na kutishia kitumbua changu lazima adedi ghafla. Shauri yenu.

Hayo tuyaache. Vipi mlinionaje juzi nikiwa nimejinoma na Drogba? Eti wapuuzi wanasema nilipaswa kuwa waziri wa michezo kwa sababu mambo yangu ya mchezo mchezo. Hawajui huu ni wakati wa kuwabamiza mkenge vijana na wapenda michezo! Mie hata kwenye misiba naponyoka na kwenda kucheki mechi.

Kabla ya kusahau, nilipewa mwaliko kwenye harusi ya my friend Zuma alipojiponyolea kimwana cha tano. Mie haya siyawezi. Nafanya kwa siri.

Bado mwaliko toka kwa kijogoo mwenzako Mswati wakati wa Umhlanga atakapoponyoa kitu cha 15. Duh mila au uchangupaka mtupu? Tuyaache. Nyumba na ukuu vinaficha mengi na mengine.

Guys I am serious. Mark my words.

Acha nami nikitotoe kabla ndata hawajanifungulia kesi ya uchochezi ingawa ni ukweli!
Chanzo: Tanzania Daima Januari 13, 2006.

Ujumbe wa rais nje uwekwe wazi

Rais Jakaya Kikwete na mkewe Salma wakibembea nchini Jamaica.

WATANZANIA wengi wanajiuliza: Kwanini siku hizi rais anapokwenda ziarani nje ya nchi ujumbe wake hauwekwi wazi?

Je, kunakuwa na watu – mfano wanafamilia, marafiki, washirika hata mafisadi – ambao asingependa wajulikane au wasiostahili lakini bado wanafaidi kodi ya umma?

Kinafichwa nini kama hakuna namna ya ufisadi au ufujaji pesa ya walipa kodi maskini?

Kisa cha mwisho kutokea ni cha safari ya juzi nchini Jamaica ambapo tulionyeshwa picha ya rais na gazeti la serikali akipanda ndege kwenda Jamaica na baadaye picha akiwa anafika uwanja wa ndege wa Manley, mjini Kingston .

Hapa ndipo tulijua kuwa kumbe aliandamana na mkewe. Zaidi ya hapo hakuna anayejua idadi na majina ya watu alioandamana nao rais. Kwanini tufichwe wakati wanatumia kodi zetu kwenda kutumbua huko?

Hata ukiangalia kinachompeleka huko ni kutuwakilisha ingawa mara nyingi hatuhitaji hili kwa kuzingatia hali yetu mbaya kifedha.

Kipindi fulani yalitokea malalamiko kuwa rais anatumia pesa nyingi kutalii ughaibuni. Wapambe wake walijibu kuwa huenda kule kuomba ingawa hawakutwambia katika ombaomba hii amewahi kupata kiasi gani kikilinganishwa na alichotumia kufanya hivyo.

Inashangaza kwa rais wa nchi inayowategemea wahisani kwenye bajeti – kwa aslimia 40 – kurukaruka na kutumia mabilioni ya shilingi bila kuangalia hili.

Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye utegemezi mkubwa kwa wafadhili na inayoshika namba ya juu kwa rais wake kufanya ziara ugenini.

Katika bejeti ya mwaka wa fedha wa 2009/10 (Julai-Juni), aslimia 11.4 ya bajeti yake au $831,000,000 ilitolewa moja kwa moja na nchi 14 wafadhili.

Kwanini hili halimsumbui rais kama kweli anadhamiria kutuletea maisha bora kama alivyoahidi, ingawa hali ilivyo hakuna kitu kama hicho.

Gazeti la The Economist la 7 Mei , lilihoji mantiki ya Kikwete kutumia muda mwingi nje akihangaikia matatizo ya nje huku akiyapuuzia yale ya ndani hasa uchumi na ufisadi.

Kwanini rais au washauri wake hawataki kuliona hili? Je, nchi inaweza kuendelea kwa kutegemea sera za nje tu bila kuwa na sera madhubuti za ndani?

Je, uchumi wetu unaweza kukuzwa na misaada na biashara tu bila kuwa na uwajibikaji na nidhamu ya matumizi?

Kama ziara za rais zinalipa zaidi ya kuwa utalii binafs, mbona hatuwaoni akina Mwai Kibaki (Kenya), Yoweri Museveni (Uganda) hata Komredi Almando Guebuza (Msumbiji) wakikesha kwenye ndege lakini uchumi wa nchi zao ni imara kuliko wetu?

Turejee kwenye usiri wa wanaoandamana na rais. Licha ya majina ya wanaondamana na rais kuwa nadra kutangazwa, mke wa rais naye anaonekana kushabikia aina hii ya utalii.

Kwani kwenye ziara nyingi hupenda kuandamana na mumewe bila wote wawili kujali kuwa kufanya hivyo ni kumuongezea mzigo mlipa kodi huku wakizidisha mateso kwa watu wa kawaida.

Kama anapenda sana kutanua si ampe uwaziri kama alivyofanya imla wa Uganda ili awe na uhalali wa kuandamana na rais kila aendeapo ughaibuni? Mbona hatumuoni mikoani na rais ingawa rais hufanya ziara za mikoani kwa nadra?

Hebu fikiri, kwa mfano, kwenye ziara zisizo na umuhimu za kujitambulisha alizofanya Kikwete mwaka 2006; hata huko aliandamana na walaji.

Endelea kujiuliza: Ziara hizo ziliteketeza mabilioni mangapi ya shilingi za mlipa kodi? Kwanini kujitambulisha nje ya nchi kana kwamba ndizo zilikupigia kura? Mbona hatuwaoni marais wa nchi nyingine wakija kwetu kujitambulisha?

Hebu jionee baadhi ya ziara: Rwanda, Uganda, Kenya, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Botswana, Namibia, Afrika Kusini.

Nijuavyo, rais yeyote akichaguliwa hutambulishwa na vyombo vya habari duniani. Na kama ana wasiwasi sana na kujulikana kwake, basi anaweza kuwaagiza mabalozi wake walioko nchi husika kufanya kazi hiyo.

Sikumbuki kuona marais wapya kama Ian Khama (Botswana), Rupiah Banda (Zambia), Bingu wa Mutharika (Malawi) au Jacob Zuma (Afrika Kusini) wakija kujitambulisha Tanzania. Kwanini iwe big deal kwa rais wetu kujitambulisha kwao?

Haya ni masuala ambayo wapinzani wanapaswa kukumbusha wapiga kura kuonyesha Kikwete asivyofaa kuchaguliwa tena. Hana uchungu na nchi hata kidogo.

Tuchukue kuwa kila ziara rais alitumia Sh. 500,000,000. Ina maana kujitambulisha kumelihujumu taifa si chini ya Sh. 5 bilioni.

Nimefanya makadirio kwa kurejea maneno ya waziri mkuu wa zamani Fredrick Sumaye alipofanya ziara Marekani na kutumia Sh. 500 milioni alizosema zilikuwa kidogo.

Je, fedha hii ingesomesha vijana wangapi vyuoni, kutibia wagonjwa au kujenga shule ngapi ukiachia mbali kujenga kilometa kadhaa za barabara?

Je, kwa uzembe na israfu hii, kwa kipindi kizima cha urais, rais atakuwa amepoteza fedha kiasi gani ambazo zingeweza kutukwamua kimaendeleo?

Hapa hujaongelea mawaziri wake wanaoweza kufuatwa na mashangingi kila waendapo ili kujishaua.

Hebu angalia hili. Rais anatumia fedha za walipa kodi maskini kwenda kushangilia timu ya Real Madrid nchini Hispania. Ilikuwa 15 Septemba 2006.

Je, hii ndiyo njia ya kujali mateso wanayopata Watanzania? Kuna haja ya mabadiliko.
Chanzo; MwanaHALISI Januari 6, 2010.

Wednesday 6 January 2010

Reclaiming Mau Forest Not Enough

Moi to be compensated


When I read that Kenya’s former president Daniel arap Moi and his cronies will be paid over Kshs 2,000,000,000 as compensation of “their” parcels of land (They grabbed) retaken by the government in Mau water tower, I felt like crying. I asked myself: Who bewitched African rulers and the badly affected hoi polloi?

The value of the land, including tea bushes, is placed at between KShs150, 000 and KSh300, 000 per acre. What is unclear is why the Kenya government is willing to pay such hefty money to land grabbers. Is it because some of the grabbers have influence in the current regime? Guess what. In this open rip-off, former president Moi is taking almost a billion shillings!

To rub salt in a wound, the said yokels are not zapped from criss-crossing the country gulling victims (to rally behind them) with their pancake theory that forests do not make rains instead rains make forests! What a farce! What an abuse to their own intelligence! How can an educated person say such things when the whole world is concerned about environmental health? To such people, the future is in their stomach. Their egos supersede the nation!

As this scandal rocks Kenya, a similar saga is unfolding in the neighbouring Tanzania as villagers in Tanga region accuse former president Benjamin Mkapa for exploiting them (while in power) and grabbing thousands of acres of land after retiring. These two episodes rejuvenate fresh memories of 2007’s carnage when Ugandan strongman Yoweri Museveni attempted to offer Mabira forest to his friends and partners.

Rulers in East Africa have created a very bad legacy with land and economies. Soon, the East African Community will become a cropper thanks to Tanzania’s land-related fears. And indeed, being the only country with a big chunk of land in the union, Tanzania seems to stay put to see to it that her land is not used to nourish bad-land policies in other countries especially Kenya.

For long, Kenya, sadly, under Jomo Kenyatta, Moi and presently Mwai Kibaki has been

gang raped. Now that Kenya has taken very bold steps to reclaim the Mau forest, it needs to do more. Many Kenyans are landless as few settlers and former rulers sit on big tracts of land grabbed from the public thanks to their abuse of power. The dynasty of the founder of Kenya, Kenyatta is believed to sit on the land the size of Nyanza province!

As Kenyan authorities reclaim the Mau forest in order to conserve and rejuvenate this water tower, they also ought to reclaim other land parcels stolen from the public by both past and sitting regimes. Without land, the victims will perish even if they have stable supply of water.

If top shots were able to grab thousands of acres on one area such as Mau Forest, what of other fertile areas of Kenya? Was Mau the only area they grabbed? Which other areas were grabbed?

Kenya is 582,650 sq km with a population of over 30 million. Density is 2 settlers per sq. km, while in the rich and fertile western region, population density goes up to 120 settlers per sq. km. This can nicely show you what is going on in Kenya. Why should white settlers own bigger land than Kenyans whilst it is openly known that they grabbed the same?

Given that all land owned by who’s who and white settlers in Kenya was grabbed, it won’t amount to breaking law shall the authorities or the people of Kenya reclaim it. They know who grabbed their land when and how much. It is time that landless Kenyans must stand up and reclaim their God-given land. Why is Tanzania able to assure every citizen of the ownership of land whilst Kenya can’t?

Without land, nobody can truly belong to the country he calls his. And without this sense of belonging, the affected person will never care about the same. This is why it is easier to recruit rebels in Africa where economies are abused by, and only benefit, the ruling cabal. Even animals in our national parks are comparably better and boast of belonging and owning the forest they are found in. They’re even more protected than our people thanks to attracting tourists. The other day I was asking why rhinos in Tanzania are more protected than perishing albinos. The authorities did and have nary bothered to ponder on this question!

Kenyan antelopes, wildebeest and warthogs have more land to live and enjoy than Kenyans. Go to Kitengera just in the outskirts of Nairobi. You will find that many an antelope has thousands of acres for grazing whilst a Kenyan does not have even an acre! No joke. This is a real situation. Animals in Africa are more protected than Africans. Even donors are offering more generously when it comes to animals.

Kenyans should see to it that taxpayer’s money does not reward land grabbers.Instead of contemplating to redress criminals however big and honorable, the government should bring them to book. Mau forest must remain a water tower and those saying they have invested in it must be charged for investing on restricted area they obtained illegally.
Source: The African Executive Magazine Dec. 6, 2009.

Mpayukaji avunja baraza la mawaziri

KATIKA kuufunga mwaka, mzee mzima natoa zawadi ya mwaka mpya nikiwa nimejipanga upya. Niliwahaahidi wanakijiwe kuwa nilikuwa nikijipanga kujibu mapigo si hoja. Sasa najibu kwa vitendo. Na hii si kwa ajili ya kampeni.

Najua wakosoaji watasema narudia utapeli wangu kuwafunga wadanganyika wa kijiwe changu kamba ili niwabamize mkenge kwa mara nyingine. Msiwasikilize hao. Mie bado ni chaguo la Sir God.

Hata hivyo, ni vizuri kuelewa. Raha lazima mjipe wenyewe baada ya hapo. Mpo wadanganyika wangu?

Baada ya wanakijiwe kulalamika sana kuwa nawakingia kifua mafisadi na vihiyo, sasa navunja mwiko kwa kukata kamba zangu za raha jipe mwenyewe. Sasa raha nawapa mimi.

Kutokana na muda kuzidi kunipa kichogo na uchaguzi mkuu wa kijiwe kuwa mlangoni huku nikiwa nimeishiwa na kamba za kuwafungia, mzee mzima nimeamua kuwapa raha kwa kuvunja baraza la mawaziri na kulisuka upya.

Nimelazimika kufanya hivyo ingawa roho inauma kutokana na washikaji zangu kutupwa nje na kuwa mzigo mwingine nyuma ya pazia. Hata hivyo, washikaji msikonde. Mie bado ni wenu nanyi ni wangu.

Nikishawabamiza kenge hawa makenge nitawakumbuka na kuwapa ulaji tena. Nitavunja baraza na kuwarudisha baada ya kupata ulaji. Mtakuwa nje ya ulaji kwa mwaka mmoja ingawa katika siasa lolote laweza kutokea. Tusameheane. Wadanganyika wamenijia juu sana.

Katika kuvunja baraza la mawaziri kuna mambo mengi nimezingatia. Nitaunda baraza dogo ili kuokoa pesa ya wanakijiwe wangu ili wavutiwe nami wanipe ulaji baadaye niwaache solemba. Nitazingatia elimu safi, umri, ukoo, dini, mtu atokako na ushikaji kwa mbali hasa ile mitandao. Hata kuzurura mwaka huu sifanyi.

Wizara ya wanawake na watoto imepiga panga. MAWAWA ya mke wangu inatosha. Shughuli zilizokuwa zikifanywa na wizara hii zitapelekwa kwenye ofisi ya MAWAWA, bi mkubwa atakuwa waziri asiye rasmi.

Wizara ya vijana na michezo nayo inakwenda na maji; sitaki mchezo siku hizi. Nimefuta Wizara za Kilimo na kuanzisha ya umachinga, ushirikiano wa Afrika Mashariki kutokana na washirika wa nchi zisizo na ardhi wala demokrasia kutaka tuungane ili watuibie ardhi na kutorosha madini yetu.

Mkuu wa mkoa wa Bongo, Bill Mukuvi, naye nimemtupa nje kutokana na kuwa kihiyo tena aliyeghushi.

Wizara mambo ya nchi za nje na uhusiano wa kimataifa nitaichukua mimi na naibu wangu atakuwa bi mkubwa mama watoto wangu ambaye atakuwa waziri asiye rasmi. Pia ieleweke, kwa muda nilioruka naye ameonyesha uzoefu mkubwa kutulia kwenye pipa na kupiga picha uwanja wa ndege ukiachia mbali kuwa bingwa wa kubembea na kunipigia kampeni kinamna.

Wizara ya Fedha, Uchumi, Mipango na Biashara nitaibadilisha kuwa ya EPA, kushughulika na ufisadi na umachinga.

Waziri atakayeisimamia nitamtaja baadaye baada ya kushauriana na bi mkubwa kuona atatusaidiaje kuepa Ma-EPA.

Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia nimeiunganisha na ya ulinzi na kumpa mtoto wa aliyenitengeneza.

Hivyo daktari Hu-Sen atakuwa waziri mpya wa wizara hii mpya wakati tukimuandaa kuchukua kijiwe cha Zaainzibaa.

Wizara ya Elimu, Utamaduni, Michezo na Ubunifu itafutwa. Wasomi tunao wa kutosha na isitoshe wanaopaswa kusoma ni watoto wetu watosoma ughaibuni. Kama huna pesa uliye tu lazima mwanao aende kwenye kilimo first. Wawe wabunifu ili iweje?

Wabuni jinsi ya kuingilia ulaji wetu siyo na kuleta utamaduni mfu wa kutukosoa na kutuzomea ukiachia mbali kututupia mawe kama kule kwa kina Malafyale?

Wizara killimo, ushirika, mifugo, ardhi na maji viwanda, uchuuzi, masoko, ushirika na ujasiriamali nazo nazifuta. Maana uzoefu umeonyesha ujasiriamali siku hizi haulipi isitoshe nifanyao mimi na bi mkubwa unatosha.

Wizara ya sheria, katiba na haki za binadamu nayo naifuta kutokana na waziri wake kuwa na uogonjwa wa kupayuka. Na isitoshe kila mwanakijiwe anapata haki yake na si lazima wajue sheria. Maana wanaweza kunigeuzia kibao na kunifunga hawa.

Sambamba na wizara hii, ninamfukuza kazi katibu wa chama changu cha Ulaji, Ufisadi na Ubangaizaji mgosi Joe Makambale Machungi na Mkurugenzi wa Tume ya Mawasiliano ya ofisi yangu, Silvia Rweyenshomile (mshiriki mkuu wa unepi). Hawa wamekuwa wapayukaji badala ya watendaji.

Wizara ya Nishati, barabara na uchukuzi kwa sasa aihitajiki kutokana na kujenga bara bara za kutosha na kuwezesha watu kukimbilia mijini. Kama ni kuhitaji nishati, tunayo ya kutosha kiasi cha kuachana na mgao wa umeme.

Wizara ya kazi, ajira na maendeleo imefutwa kwa sababu ajira kwa sasa zinafuata ukoo wa mtu. Hivyo haihitajiki wizara.

Nitangaze rasmi kuwa mawaziri wafuatao nawapiga panga kutokana na kuhusishwa kwenye tuhuma za kughushi, kupayuka hovyo na upuuzi mwingine. Wafuatao hawamo tena kwenye ulaji wangu: Makorongo Muhanga, Meli Nyagu, Imanu Mpimbi, Dad Matoya Dad, na Diodomus Kamirioni.

Pia mawaziri wafuatao nimewalamba wino mwekundu baada ya ama kuchukua wizara zao au kutoridhishwa na utendaji wao. Nao ni Mwalimu Ijumaa wa Kupuyanga, Mwl. Ijumaanne Majembe, Stevie Wahasira, Shemeji Hawanaghasia na Ben Maembe.

Mama Sofii Mpayukaji Yanga nisamehe sana. Imebidi nikupige kibuti kutokana na kuzoza hovyo huku ukijenga mazingira ya mimi kustukiwa na hata wabaya wangu kupata la kusema.

Domo lako chafu limekuponza mshirika wangu. Wewe na mgosi Makambale Machungi siwezi kuwavumilia kutokana na kuharisha kwa midomo badala ya nonihino. Tusaheane. Wa kuuza nyanya mkauze hata wa kufanya uchangudoa mwingine ruksa mradi msiguse kitumbua changu.

Mawaziri wengine mshikaji ambao nimemlamba panga ni Joka Mkunjika na Joni Chilisosiyagati.

Kwanza nyinyi licha ya kutofanya lolote zaidi ya kelele za chura, hamkubaliki majimboni mwenu. Hivyo hamuwezi kuleta ushindi mwakani. Lazima niwapumzishe mwende kwenye vijiwe vya kahawa mkapayukie huko.

Haki ya mama, mwaka ujao baada ya uchaguzi ni wa kurejesha imani kwa kijiwe. Nitafikisha mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi wa kahawa na kashata bila kusahau wauza bwibwi kijiweni.

Sitakuwa na mchezo na mtu. Mwaka ujao ni wa kutimiza ahadi zote bila kubakiza hata chembe. Ni mwaka wa kuwapeleka walevi peponi. Maana wamechoka. Kidumu chama cha ulaji.

Onyo; mtu atakayejitia kiherehere kutaka kusimama nami kugombea ulaji atakolimbwa. Amini si kamba za shehe Ubwabwa. Sikumtuma kunifagilia. Njaa nyingine bwana! Angejua ya kesho si angetabiri kuwa kipindi kile shehe mkuu angemtimua. Mbona hakujitabilia. Upuuzi upuuzi mtupu.

Basi nipigieni makofi kidogo maana nimewapa raha ya milele.

Naona ndata wanakuja wasije wakanikata mitama kwa kumpasha bosi wao. Acha nikitoe na mapema.
Chanzo: Tanzania Daima Januari 6, 2009.