Free Thinking

I Fear Nothing But Fear Itself

The Curse for Salvation

The Curse for Salvation

Wednesday, 29 March 2017

Kumbe Tanzania imefika hapa!

            Wengi wa wapenda demokrasia, haki na usawa nchini watakuwa wameshangazwa na hata kuchukizwa na yaliyojiri hivi karibuni. Ni kuhusiana na sakata la kughushi; mbali na la uvamizi wa vituo ya Clouds.  Hii ni baada ya kuachishwa kazi kwa aliyekuwa waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye. Hata hivyo, kosa lake halikuwekwa wazi ukiachia mbali kujengeka hisia kuwa kadhia hii ilitokana na Nape kuunda tume ya kuchunguza uvamizi wa vituo tajwa hapo juu. Japo rais hapaswi kuingiliwa kwenye mamlaka yake ya uteuzi au utenguzi, kuna haja umma kujulishwa hasa, ikizingatiwa mhusika alikuwa ameshikilia madaraka ya umma. Je kweli kosa la Nape ni kuunda tume kuwachunguza wateule wasioguswa?
Japo ni haki na mamlaka ya rais kuteua na kutengua, kuna haja, wadau yaani wananchi, kujulishwa kinachoendelea jikoni; kuepuka kujengeka dhana ya udikteta, upendeleo na upatilizaji kwa wenye mawazo tofauti. Umma unapaswa kujulishwa nani wanapaswa kuguswa na nani hawapaswi kuguswa hata watende makosa makubwa kiasi gani. Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayopaswa kuendeshwa kwa haki, kanuni, sheria na usawa bila kusahau katiba inayotamka wazi kuwa watanzania wote ni sawa na wana haki sawa.
Mengine yaliyoibuka kwenye kadhia tajwa ni matumizi mabaya ya vyombo vya dola. Inakuwaje mtu mmoja, tena asiye na stahiki kisheria kutumia vyombo hivi kwa maslahi binafsi na katika mambo binafsi kama ilivyokariri taarifa ya uvamizi wa Clouds? Mbali na hili, inakuwaje, kama taifa, tunaanza kuminya na kutishia vyombo vya habari ambavyo viko kikatiba na si kwa mapenzi ya mtu hata awe na mamlaka kiasi gani? Inakuwaje; wahusika wanashindwa kujua vyombo vya habari ni sauti ya wasio na sauti au voice of voiceless dhana nyepesi kabisa kujua? Rejea namna rais alivyokaripia na kutishia vyombo vya habari kuwa kama vinadhani vina uhuru, it is not to that extent au si kwa kiwango hicho. Haya si maneno ya rais anayefuata na kulinda katiba wala kuheshimu uhuru wa kiraia.
Katika kutishia na kuonya vyombo vya habari, rais alisikika akijigamba kuwa yeye ni rais anayejiamini na ambaye utawala wake hautokani na ushauri, usaidizi wala ushirika wa mtu yeyote. Kwani alipokwenda kuchukua fomu za kugombea urais, licha ya kutoshauriwa na yeyote, alikwenda peke yake. Hii ni kweli; japo sijui kama alijipigia kura na kushinda. Isitoshe, rais wa nchi anapaswa kuwa rais wa wananchi wote bila kujali tofauti zao. Hili, hakika, ndilo ambalo rais amekuwa akilihubiri; japo anaonekana kutolitenda.  Kwa maneno ya rais, ni kwamba utawala wake ni wake binafsi. Je inawezekana taasisi kubwa na muhimu katika taifa ikadhibitiwa na mtu mmoja hata awe mjuaji kiasi gani? Urais kama, taasisi ni mkusanyiko wa vyombo vingi. Hivyo, unahitaji maelfu ya wananchi ili uweze kufanikisha malengo uliyokabidhiwa na wananchi. Hata wafalme huwa hawatawali peke yao pamoja na ufalme kuwa sawa na mali ya familia.
Japo simuonei huruma Nape kwa yaliyompata hasa ikizingatiwa alichangia kikubwa kuyaunda, nampongeza kwa kufia ukweli. Socrates (469 B.C. to 399 B.C), mwanafalsafa wa zamani wa Kigiriki aliyesifika kwa kupenda ukweli aliwahi kunena “do not be angry with me if I tell you the truth” yaani usinichukie ninapokwambia ukweli. Yesu naye alisema ‘tuitafute kweli; kwani itatuweka huru.’ Hii maana yake ni kwamba mtu anayechukia na asiyependa kweli si huru. Anahitaji uhuru hata kama ana uhuru wa kisiasa. Je hatuhitaji uhuru utokanao na kweli hata kama unawaudhi wenzetu tena wenye madaraka? Je kadhia inayomkabila mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ya kughushi vyeti vya kitaaluma na kuvamia Clouds si ukweli tunaoutaka kama jamii ili, licha ya kutendeana haki kwa usawa, utuweke huru? Nani huyu mtumwa asiyependa kujua kweli imuweke huru? Je tunaweza kushindana na kweli na kuishinda tukawa salama kama jamii na taifa? Leo tutakwenda na falsafa ya Socrates tokana na mfano bora alioacha wa kuitafuta kweli hata kwa gharama ya maisha yake kama ilivyomtokea pale aliposhitakiwa kuwa alikuwa akiwaharibu vijana kwa mafunzo yake. Baada ya kuhukumiwa kunywa sumu aina ya Hemlock au Conium maculatum, Socrate alisema “yapo maarifa ya kweli na katika kujua hili hujui kitu.”
Tukirejea kadhia zetu hapo juu, nani hajui kuwa mengi yaliyojitokeza ni ya kweli? Nani hajui kuwa tumeanza kujenga taifa la watakatifu wasiokosea, wanaojua kila kitu na taifa la wasio na haki wala maarifa ukiachia mbali stahiki na haki ya kueleza mawazo yao? Nani huyu fedhuli anaweza kufunga mawazo? Je inawezekana? Ukijua hili jua hujui na kama hujui kuwa hujui basi hujui na utajua,
Tumalizie kwa mfano wa Socrates kuwa tusiogope kusema ukweli kwa kuhofia kufukuzwa, kunyamazishwa au kutishwa. Ukweli utabaki kuwa ukweli kuwa mambo yanavyokwenda, licha ya kuwa tofauti na mategemeo yetu, sivyo ndivyo. Uhuru wetu kama wana jamii una thamani na gharama ambavyo hakuna anayeweza kuvipoka huku nasi tukiangalia. Ama! Tanzania imefikia hapa!
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.
 
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 07:57 5 comments:

Mgoshi Apendekeza Kijiwe Kihamie Koromije

Baada ya kushuhudia vimbwanga na vibwengo, visa, visasi, mikasa na makosa, kijiwe kimeamua kutia timu kwenye jiji la Koromije kule kwenye nchi ya Kusadika na Kuburuzika. Kinakwenda kule kumsaka mbaya wake aitwaye Bushit. Yote hii ni kutaka kuweka mambo sawa ili kaya iwe sawa iondokane na kubebana, kupatilizana na kuburuzana.
Akiwa amevalia kanzu yake na kofia ya tarabushi vya bei mbaya, Mgoshi Machungi leo kaja kinomi. Hata kabla ya kuamkua, Mbwamwitu anamchokoza “Mgoshi unaenda kuongeza jiko nini mbona leo umetisha hivi?”
Mgoshi anajibu “kama unaye mwai sina neno. Niko ai kamii. Si minaona niivyouamba. Isitoshe, napendeza na kuvutia kwa kia kinda na jiko au vipi jamani.si minipigie angau makofi kwa niivyojikwatua.”
Kama ada, anaamkua ‘asaamaeku jamia.” Tunajibu na anaendelea kula mic “wagoshi, hivi tinasemaje kuhusi hiki kitatange na kimbembe vinavyoeendee kwenye kaya?”
Mchunguliaji anajibu “yapo mengi yanaendelea kuanzia sanaa za kuwasaka na kuwanyaka wauza bwimbwi ambazo hata hivyo zimefunikwa na Bashiiit na Nipe Mapepe aliyetimliwa baada ya kutaka kuwagusa watakatifu hasa mwana wa pekee wa mfalme. Je unamaanisha lipi kati ya haya na mengine mengineyo?
“Mgoshi hapo umepiga kwenyewe. Ni kama uikuwa kwenye akii yangu! Kusema ue ukwei, hii kadhia ya kutishia vyombo vya umbea na kuindwa kwa Bashiiit vimenikea kiasi cha kuja na wazo kuwa tihamie huko Koomije tukakoome na kuchunguza ii tijue ukwei. Maana, inachanganya na kuudhi,” anajibu Mgoshi huku akimpa kikombe muuza kahawa ammwagie.
Mijjinga ambaye anatokea karibu na jiji la Koromije anakula mic “unadhani kuwa hata ukienda Koromije kusaka ukweli utapokelewa na kufanyiwa kazi? Mbona mkuu amesema atakufa na mtu wake na kumpatiliza yoyote atakayemgusa mwanae mpendwa? Hujitaki nini? Kamuulize Nipe Mapepe ndiyo ufanye hayo unayotaka kijiwe kifanye.”
Kapende anampoka mic na kuronga “nadhani wengi hawakumuelewa mkuu; wanamlaumu bila sababu. Kama nimemwelewa ni kwamba, hataki umbea na mambo ya kwenye mitandao. Anataka ushahidi wa kisayansi ndipo atumbue au vipi?”
Mipawa anamchomekea Kapende “nadhani hukumuelewa mkuu. Alichomaanisha ni kwamba wateule wasisemwe wala kukemea as long as yeye anawapenda na kuwakubali. Hivyo, hata tukienda kule na kuja na magunia ya ushahidi, tutazodolewa tu hasa ikizingatiwa kuwa mwenye mapenzi haoni. Mbona kwa Nipe Mapepe hakungoja kuletewa huo ushahidi wa kisayansi unaodhani ndiyo anaoutaka?”
Kanji anakatua mic “mimi ungana na veve. Kuu hapana taka hii teule guswa hata kama naua. Kuna kweli gani hapa natakiwa kama vote nasitaki yeye nasema kweli yote? Kama Kuu iko taka shahidi scientific kwanini nafukuza Pepe bila soma ripoti yake?”
Msomi anakatua mic “kimsingi, hapa Mkuu amefanikiwa kuua ndege wengi kwa jiwe moja. Kwanza, ametoa kauli za kuchanganya hata kuchanganyikiwa ikizingatiwa kuwa alifanya tofauti na anachohubiri. Pili, alitumia fursa hii kutoa vitisho kwa wote wanaodhani wanaweza kumkosoa wakati anajua kila kitu. Tatu, amethitibitisha ukweli kuwa ile sera ya kulindana ya chata lao bado ipo. Nne, amethibitisha kuwa maji yanaanza kuzidi unga kiasi cha kuchanganya. Tano, amemvua Nipe Mapepe gamba wakati akimwacha Bashiit mwenye magamba manene kibao ambayo kwa msemo wa mzee wa Vijsenti yanahitaji shoka na si kalamu. Je atamvua yule ampendaye?”
Kabla ya kuendelea, Mbwamwitu anadakia “chonde Msomi. Amvue ili iweje?”
Msomi anampuuzia na kuendelea “japo wazo la kijiwe kuhamia kufanya uchunguzi kule Koromije ni jema, je ukweli utakaopatikana utakubaliwa au kusulubiwa kama ule wa Nipe Mapepe? Je kuna masikio ya kuweza kuusikia wakati yaliyopo yameishajazwa vijiti? Nadhani hapa la kufanya ni  ima kuingia mitaani ili kujua hii kaya ni ya nani, kunyamaza au kwenda kwa pilato kumshitaki mtuhumiwa.  Vitendo vilivyotokea vimenikumbusha shujaa Chris Mtikisa. Angekuwa hai, kesi zingeishajaa mahakamani.”
Mheshimwa Bwege anakula mic “mie leo sichangii mengi. Ninachoona ni kwamba tunaanza kugeuzana mabwege kwa ubwege bwege tu wa mabwege wengine. Haiwezekani mhalifu mmoja alindwe kwa mitutu na mamlaka kaya iwe salama. Tunafanya vitu kana kwamba hatuna ubongo wa kukumbuka historia za waliopita waliowahi kulewa maulaji kiasi cha kujilisha pepo wakaishia kuumbuka. Wako wapi wababe kama Saddam Hussein au Mwamali Kaddafi? Si walipigwa teke na kutokomea wakasahaulika? Hakuna ubwege kama kukinzana na ukweli na mambo yaliyo wazi. Hivyo, mwende Koromije au msiende, haisaidii. Majibu yako hapa hapa kama tutaamua kama jamii ya wachovu wanaochukia na kuchoshwa na ubangaizaji, kubebana na kupatilizana kwa sababu binafsi.”
Sofia Lion aka Kanungaembe anakwanyua mic “siungi mkono wazo la kwenda Koromije. Kwanini mnatka kufukua makaburi ambayo mtashindwa kuyafukia? Kwanini suala hili limepewa uzito kuliko mambo mengine? Kama mmesahau makaburi kama Escrow, EPA, IptL na sasa Symbiosis ambayo juzi ilishinda kesi ya kuibia mabilioni kaya, kwanini msijisahaulishe na hili ili msiumize mioyo yenu? Sioni kama kuna haja ya kuendelea kuwapigia mbuzi gitaa zaidi ya kuacha wakati ufanye kazi yake. Naungana na Mheshimiwa Bwege. Tuache ubwege na mambo ya kibwegebwege kwenye mambo ya umma.”
“Du, da Sofi hapa umefunga nyama na kufumba!”
Kijiwe kikiwa kinapita si akapite Bashiiit! Kama siyo kuzungukwa na ndata na mitutu mbona tungemfanyia kitu mbaya!
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 07:56 No comments:

Sunday, 26 March 2017

Kwa Sasa Rais wa Tanzania ni Nani?

Image result for photos of magufuli na makonda

Tokana na mkanganyiko utokanao na upendeleo wa wazi tena wa kuvunja sheria na kulealea jinai baina ya rais John Pombe Magufuli na mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda aka Daudi Albert Bashite unashindwa kuelewa nani anatawala Tanzania kwa sasa. Hili ndilo chimbuko la swali hilo hapo juu. Je kati ya Magufuli na Makonda, nani anamtumia nani na kwanini?
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 10:38 No comments:

Kashfa ya Makonda: Inatakiwa busara si ubabe

Image result for photos of magufuli na makonda
Kauli ya rais John Magufuli kuhusiana na sakata la mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kughushi vyeti vya kitaaluma imestukua, kusikitisha, kukwaza na kushangaza wengi ukiachia mbli kumtia aibu yeye mwenyewe na mamalaka ya rais. Hata kabla ya mstuko na hasira kwisha, rais alimfukuza kazi waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alivuliwa madaraka kwa kumgusa kipenzi cha rais, jambo ambalo ni kinyume na matarajio ya watanzania na ni hatari. Kama alivyosema mwenyekiti wa Wamilki wa Vyombo vya habari Reginald Mengi, kilichotokea ni aibu kwa taifa hivyo, hakikwepi lawama. Hata hivyo, wanaomlamumu Magufuli wanafanya makosa kutokana na faida itokanayo na hatua yake ya kumkingia kifua ambayo imeonyesha sura ya rais na namna ya utendaji wake. Rais alijigamba kuwa yeye ni rais anayejiamini na watu wasipoteze muda kujadili personalities naye akaishia kujadili hizo personalities kama wale aliowalaumu. Nadani kujiamini tu bila kuaminika inaweza kuwa bure.
  Licha ya kutostahili, kauli ya Magufuli haikutegemewa kulalia upande mmoja; na ni ya kulaaniwa kwa hasira na uzito unaostahili. Je nani anamtumia nani kati ya Magufuli na Makonda? Haiwezekani, kwa mfano, mtu atuhumiwe kughushi vyeti ambalo ni kosa la jinai, halafu rais anayejipambanua kama mpambanaji dhidi ya jinai hii amkingie kifua hata kwa kuwaumiza wengine. Huku ni kijichanganya na kujipiga mtama kwa lugha ya watoto wa mjini.
 Haiwezekani Makonda huyu huyu awatukane Waheshimiwa Wabunge lakini bado rais huyu huyu amkingie kufua kusiwe na mgongano baina ya mihimili hii miwili ya dola. Sijui bunge na wabunge waliotaka kumwajibisha Makonda wanajisikiaje. Haiwezekani Makonda huyu huyu avamie kituo cha Televisheni usiku wa manane akitumia vyombo vya dola kienyeji ukiachia mbali kitendo chake kuvunja katiba bado akakingiwa kifua na rais na kusiwe na namna. Wakati rais akimkingia kifua, waziri mhusika alilaani kitendo hiki jambo ambalo ni kama serikali kupingana yenyewe. Hapa lazima kuwa na uhusiano wa wawili hawa usio wa kawaida. Ama kweli mwenye mapenzi haoni! Kama haitoshi, bunge limetuma kamati yake. Bila subira wala simile, rais anamtetea mtuhumiwa ambaye hata waziri wake ameunda tume ya kuchunguza sakata hili. Sijui kama kauli ya rais haitaathiri matokeo ya uchunguzi. Maana rais ameishaonyesha upande wake katika sakata hili. Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Bunge Peter Serukamba alikaririwa akisema kuwa Kamati ya Bunge itachunguza na kutoa ushauri kwa serikali. Sijui ushauri gani huo ambao utamshawishi Magufuli wakati alishatoa hukumu hata bila kungoja kusikia matokeo na ripoti za tume husika.
Je ni kwanini Magufuli ameamua kufa na Makonda ilhali akiwatumbua wenye makosa madogo kuliko yake? Je Magufuli anatoa mfano gani kwa taifa? Si rahisi kujibu swali hili. Wapo wanaodhani kuwa ni sababu ya ukabila. Hata hivyo, ukiangalia namna Magufuli alivyomtimua Waziri wake wa kwanza wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga, unaondoa dhana hii japo lolote linawezekana. Je ni kwanini Magufuli ameng’ang’ania Makonda pamoja na kuchafuka hivyo? Kitendo cha Magufuli ni kwamba anatumia mamlaka yake kwa upendeleo na visasi. Rejea alivyonyamazia jinai ya kuwekwa ndani kwa Mbunge wa Arusha Godbless Lema kwa miezi minne kinyume cha sheria.
Je sababu inaweza kuwa kujuana kunakotokana na mmoja kujipendekeza na kumuabudia mwenzie? Inawezekana; hasa ikizingatiwa kuwa Magufuli ni aina ya viongozi wanaopenda kuabudiwa jambo ambalo Makonda ameonyesha ubingwa kulitekeleza hata kama ni kwa kuwasaliti au kuwachongea wenzake. Kimsingi, hapa kuna usanii ambao mwisho wake unaweza kuwaumbua wote ukiachia mbali wawili hawa kugeuka maadui hasa kila mmoja atakapoujua malengo ya na ukweli wa mwenziwe. Hakuna urafiki wenye kuvunja kila kanuni unaoweza kudumu milele. Wawili wakiudumisha, waliowazunguka watauvunja. Jikumbushe urafiki wa imla wa zamani wa Libya Muamar Gaddafi na Abdullah Senussi mkuu wake wa usalama ambaye wengi walimwita blackbox ya Gaddafi kama angekuwa ndege. Pale Kenya, Nicholas Biwott alimponza Daniel arap Moi. Je uhusiano na kulindana kwao viliishia wapi? Nani hajui kuwa wapambe kama kanali Isaac Malyamungu walimpotosha Idi Amin hadi akavamia Tanzania na kupata cha mtema kuni? Wengi wanauliza. Makonda anapata wapi hiki kiburi cha kufanya atakavyo? Nadhani jibu ni rahisi. Kiburi kinapatikana ikulu.
Inashangaza kwa rais ambaye huwa mwepesi wa kutenda kuchukua muda mrefu kuongelea kashfa za mteule wake na mwana wa pekee. Rejea alivyobatilisha maagizo ya kuhama wamachinga na waoaji kutakiwa kuwa na vyeti vya kuzaliwa. Je kwanini kwa Makonda amepata kigugumizi? Kuna tusiyoyajua yanayowaunganisha wawili hawa? Hata hivyo, urafiki na kazi za umma vinapaswa kuwekwa kando. Tokana na kumkingia Makonda kwenye makosa makubwa kama haya, inaanza kujengeka dhana kuwa Magufuli ndiye anayemtuma Makonda kuyatenda anayotenda. Bila hivyo, haiwezekani akawatukana wabunge sasa anaambiwa achape kazi. Hata hivyo, Makonda ametusaidia kuona na kujua sura ya pili nay a kweli ya Magufuli ambaye kwa msimamo wake anahubiri maji na kunywa mvinyo. Sakata hili limeibua picha nyingine kuwa katika utawala wa Magufuli kuna sacred sheep; yaani wasioguswa hata watende machafu kiasi gani.
Bila kujali urafiki wao au madaraka yao, watanzania wenye kuheshimu demokrasia na katiba walaani kitendo hiki cha hovyo na kiovu. Lazima tufanye hivyo tukizingatia kuwa rais si Mungu asiyekosea. Hapa amechemsha kweli kweli. Madaraka waliyo nayo ni ya wananchi na si yao wala marafiki au wapendwa wao. Je Makonda hata Magufuli ni zaidi ya Tanzania? Sijui mkanganyiko na udhaifu huu vinajenga picha gani kwa taifa? Je tumechoka amani hadi tunafikia kupinda haki ili kuokoana na kulindana? Inahitajika busara na tafakari vya kina.
Chanzo: Tanzania Daima Jumapili leo.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 10:36 No comments:

Saturday, 25 March 2017

Mlevi kuliambia na kulikolomije taifa

Baada ya kushuhudia namna taifa letu linavyogeuzwa shamba la bibi na matapeli kila aina, nimeamua kuja na kuwapa vipande vyao bila kujali kama watachukia, kukoma au komaa. Acha niwakolomee kana kwamba natojea Kolomije kwa akina Bashite kuja kuwapasha wapashike. Hata hivyo, sitawakolomea kwa uongo, visa na visasi kama wale waliokwisha kujima wakaishia kugwajima na kugwajimkaga kiasi cha kugeueza Kolomije kuwa aina fulani ya dini ambayo siku hizi wsanaihuribiri kila wiki kana kwamba mahubiri yamekwisha. Nitakoromea kikolomije na si kitapeli. Wala sitajificha nyuma ya Bwana wala neno lake kama wale. Nawakolomea kama mlevi mwenyewe asiyechelea wala kuogopa chochote. Kwani, naona matapeli wa ndani na nje waliojificha kwenye majoho wakitaka kutuingiza mkenge mchana kweupe wakifikiri hatuna akili ya kuwastukia na upuuzi wao. Kila anayekuja ni kuliombea taifa. Kwani taifa limekufa na kuishiwa hadi kuombea na matapeli waganganjaa na wasakatonge? Wanyong’onyee na kushindwa. Pamoja na ulevi wangu, nimechoka na mikelele ya wasakatonge hawa wanaolenga kuliibia taifa kwa kujifanya wanalipenda; hivyo kuliomboea. Najua wengi hawana kazi. Basi katafuteni pengine pa kuiba lakini si taifa letu. Nimeona wengine wakitoka Nigeria hata Zambia eti wanakuja kuliombea taifa letu. Kwa upendo gani?  Kama kuombea taifa ni dili basi kaombeeni mataifa yenu. Hatuwahitaji wala maombi yenu uchwara na kitapeli. Wapi Yesu aliombea taifa? Mnapata wapi huu upuuzi wenu wanahizaya nyie?
Tofauti na wao, mimi sitaliombea taifa. Kwanza, taifa langu ni hai. Pili, hata kama ni kuliombea taifa, sitafanya matangazo wala kugeuza sala kuwa sera. Tatu, nitaliambia taifa letu kuwa liondokane na ufisadi, ubangaizaji, ukandamizaji, uombaomba na kuchapa kazi kwa bidii huku walevi wakitendeana haki.
Kila anayekuja kuomba kuomba, nenda mkaombee wazazi wenu waliozaa matapeli tena watu wazima wasio na aibu. Rais mnayelenga kutapeli ashasema “Hapa Kazi Tu”, mmeshikilia kuomba. Kwanini hamtaki kujua kuwa hakuna aishie kwa mkate tu? Tangu lini fisi akawaombea wanakondoo zaidi ya kutamani awararue? Badala ya kuliombea taifa jiombeeni muondokane na dhambi ya utapeli na uganganjaa vinavyowasumbua. Kwani mnadhani walevi hawajui kuwa mnajifanya kuliombea taifa ili muwe karibu na wenye madaraka muwatapeli? Kama kuomba mali, mbona hatukuwasikia mkiwaombea waathirika wa tetemeko Kagera? Kama kuomba mali, kwanini hatujawaona mkiombea mateja na mafisadi au ni wale wale waliolala kitanda kimoja na wezi wa Escrow bila kujali dhamana na vyeo tena vya kiroho walivyopewa? Kama waliopewa vyeo kihalali wamechafuka itakuwa nyinyi mbwa mwitu mnaotaka kuwararua wanakondoo? Mshindwe na kunyong’onyea!
Nichukue fursa hii kumshauri rahis asiwasikilize. Awape vipande na kutoa amri kwa mageshi yetu kuwashughulikia kama alivyoshangaa mijitu michafu iliyojificha nyuma ya majoho eti kwenda Central police station na kwaya na isikatwe mitama. Nampongeza kwa kusema kuwa hata migari yao iwekwe lockup na kuchomolewa mitairi yake. Mnadhani hajui mlivyochuma ukwasi kwa kuwaibia na kuwadhulumu wajinga walioshindwa kutatua matatizo yao kisayansi mkawaaminisha kwenye ushirikina na miujiza wakati ni utapeli mtupu. Kumbaff kabisa!
Kila anayekuja anajiita mtumishi wa Bwana. Mkimuona huyo Bwana mtamjua? Kama mna bwana si mwingine bali utapeli, tamaa na uongo. Hivi kweli kaya yetu inahitaji kuombewa na wanigeria au wazambia? Shame on you all!
Acha niongee na walevi. Jamani, taifa lenu halihitaji kuombewa bali kuambiwa kuwa mambo si mambo. Iko wapi katiba mpya? Kuko wapi kutekeleza sheria kwa haki na usawa? Sijibu. Kawaulize akina Godbless watakwambia namna sheria zinavyopindwa kama alivyosema jaji wa magimbi ukiachia mbali jaji Manentie. Mlevi anawekwa ndani miezi minne kinyume cha sheria hamsemi wala kuwaombea wanaotena kufuru hii kwa vile wana madaraka. Go tell it to the birds na maombi yenu uchwara. Nawaambia walevi tena kwa kinywa kipana. Waambie matapeli wafu wa kiroho wakawaombee wafu wenzao waliolala katika ufisadi na uganganjaa. Tangu lini wafu wakawaombea walio hai? Tangu lini manabii wa uongo wakaombea taifa likapata baraka zaidi ya laana ya kuendelea kuburuzana, kudanganyana, kulindana hata kuchuuzana kama ilivyo? Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi! Hivi kweli nchi ya mzee Mchonga ni ya kuombewa na wenye mizigo ya dhambi? Ama kweli paka akiondoka mapanya hujitawala! Angekuwapo simba mwenyewe mzee Mchonga mngesema mnayosema? Go to hell! Hawa matapeli wa majoho na akina Bashite wanatukwaza.
Kwa vile sijapata kalaji, acha nikitoe nikapige mma tayari kuwaza la kusema wiki ijayo. 
Chanzo: Nipashe Jumamosi leo.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 04:13 No comments:

Friday, 24 March 2017

Bashite Kachape Kazi


Mwanangu Poo Makonda, nakuita usikie
Jinsi ninavyokupenda, ya watu usisikie
Najua wanakuponda, mwanangu usijutie
Wewe mwanangu mpenzi, niliyependezwa naye

Jinsi ninavyokupenda, wewe nenda utulie,
Najua kimewapanda, acha na kiwashukie
Awaye akakuponda, rungu limuangukie
Na bastola chukua, ndata wakusindikize

Mkono nitakuunga, nenda kazi jichapie
Najua wanakung’ong’a, ya vyeti uniachie
Hakuwa wa kukufunga, mambo yote niachie
Nchi nimeshika mimi, nani wa kunichezea?

Hata kama ulighushi, wao chawauma nini?
Umefoji si uzushi, wao yawahusu nini?
Ewe mwana shika mchi, adui dunda kichwani
Hongera kwa kazi njema, kuwavamia wanywanywa

Mwanangu na usitishwe, babayo najiamini
Mzigowo unitwishe, wa kunikabili nani?
Atayejitia ubishi, nisimNape kwanini?
Hii ni himaye yetu, mwanangu tulie ule

Nasema najiamini, sitishwi na wapuuzi,
Nimeushika mpini, ole wako uniudhi,
Takupa ngeu kichwani, ukuondoke uchizi,
Wa kudhani uko huru, not to that extent

Nenda ukachape kazi, tumbue unaotaka
Na usifanye ajizi, fanya utakalotaka
Timiza yako mapenzi,  fanya roho nataka
Hata ukitaka benzi, wabane wauza bwimbwi

Atayekukatalia, msakizie miunga,

Utakayemchukia, mwambie auza unga,
Lazima kuwawakia,watishie kuwafunga,
Sema watatumbuliwa, wale wenye madaraka

Mwanangu ninakuasa, na uwe na roho ngumu,
Washilawadu kwa visa, wao ni wasaga sumu,
Ulaji ni wetu sasa, hili ndilo la muhimu,
Bashite shika mpini, wabaya wakolomije

Usimwope yeyote, tuko juu ya sheria,
Utachotaka chochote, mie nitakufanyia,
Utapokuwa popote, mie nitakutwangia
Nitapokuwa popote, shurti kukusifia.

Ewe mwanangu Daudi, maneno yangu yashike,
Wewe ongeza juhudi, ewe mwana wa Bashite
Uzidi kutahidi, ili wao niwasute
Chapa kazi we Daudi, Albert wa Bashite

Nkwingwa kajagi lulu, kubyala gawiza,
Ukitaka kaa ikulu, hili bado naliwaza,
Sitataka kukufuru, ila mambo twayaweza,
Huoni wanavyonywea, nilipomNape mtu?

Acha nende bandarini, nenda kuwaibukia,
Hata kama usanii, kama wanavyodhania,
Hukuona ule mchuma, unayo namba bandia?
Kamera zilishakula, nani atafuta picha?

Muhimu ninakwambia, usiwaamini watu,
Kama ulivyowambia, hautatishwa katu,
Bora mkwara kutia, asikuchezee mtu
Waclouds watakaovimba, uutembeze undava.

Nimekwisha kupa ndata, sasa nini kikushinde?
Nenda wapigishe kwata, ata tume waunde,
Habari nikizinyaka, natumbua tena punde,
Hii ni himaye yetu, ngosha twanga mzigo.

Wadai  una nyingi mali, wataka uwe kapuku?
Wanataka maadili,  Bashite we kula kuku
Jipigie zako dili, kutawala ndiyo huku,
Bashite chapa mzigo, na ufanye utakavyo.

Wachimvi uwapashe, wajue umoja wetu,
Lazima uwasomeshe, wajue ukuu wetu,
Wala usiwakopeshe, uwapashe kila kitu
Wewe mwana mimi baba, wote ni kitu kimoja.

Wewe umo ndani yangu, nami nimo ndani yako,
Kilicho chako ni changu, kilicho changu ni  chako,
Ufanyacho ndicho changu, huu ni wosia wako
Sisi ni kitu kimoja, kututenganisha mwiko.

Baba kampenda mwana, hadi kampa ukuu
Ni wa mfalme mwana, aliyejaa ukuu,
Atakalo litafana, autumia ukuu
Baba kampenda mwana,  katoa kondoo wote

Mwana siyo kama Yesu, yule mwana wa Josefu,
Huyu ni Dav Bashite, tena mwana mshaufu,
Amesimama kidete, kufaidi utukufu
Kondoo wamfie, siyo yeye awafie,

Baba kampenda mwana, kasulubisha kondoo,
Kwa sababu yake mwana, na wafe wote kondoo,
Mradi apone mwana, kwa gharama ya kondoo
Haya mapenzi ya baba, kwake mwanae kipenzi.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 19:17 No comments:

Wednesday, 22 March 2017

Kwanini Magufuli anawadhalilisha mawaziri wake

Image result for photos of magufuli mwakyembe, mhagama and simbachawene
            Hakuna ubishi. Rais John Magufuli ana sifa nyingi za uchapakazi japo ameanza kuonyesha sifa nyingine zinazokinzana na uongozi bora. Hivi karibuni alijiongezea sifa ya kutaka kujua na kufanya kila kitu kiasi cha kuwafanya mawaziri wake waonekane kama viranja mbele ya mkuu wa shule ukiachia mbali wengine kuabishwa. Mfano, hivi karibuni, waziri wa Sheria na Katiba, Dk Harrison Mwakyembe, alitoa amri kuwa kila atakayetaka kufunga ndoa, lazima awe na cheti cha kuzaliwa. Baada ya amri hiyo, rais John Magufuli alitoa amri ya kupingana na Mwakyembe kwa kusema “kwa hiyo, ndugu zangu Watanzania, msiwe na wasiwasi wowote. Endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti za kuzaliwa ndipo aoe au kuolewa, nitamuelekeza waziri Mwakyembe apeleke bungeni kikarekebishwe.”  Japo hoja ya rais ina mashiko, hii inatafsiriwa kuwa serikali ya Magufuli haina mfumo mzuri wa mawasiliano.  Kwanini rais hakuwasiliana na Mwakyembe kupitia taratibu za ndani ndipo akampa nafasi ya kurekebisha kifungu husika hata kukitengua? Je rais anafanya hivi kutokana na kutojua sheria au ubabe tu? Je rais haoni kama anawapa mishale wapinzani wake kuanza kumpa majina mabaya kama vile dikteta uchwara?
            Mfano, ukiangalia umri wa wanaoa kwa sasa, uwezekano wa kuwapatia vyeti ni mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa wengi wamezaliwa kwenye hospitali au zahanati. Kwa amri hii, rais amesaidia wageni kujipenyeza na kuja kuishi nchini tena wengi wakitumia visingizio vya kuoa wasichana wa kitanzania ili waendelee kuishi nchini ukiachia mbali kutoa upenyo wa watu kuoa watoto kwa kisingizio cha kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa. Serikali, kwa muda mrefu, imefanya uzembe kuwaacha watanzania wajiishie kama wanyama huku wageni wakiingia na kujazana nchini hadi wengine kufikia kupata uongozi wa juu bila stahiki. Wengine wanatumia mfumo huu uchwara na kujipata afya na elimu bure wakati si raia.
            Ajabu, kila unapofika msimu wa kampeni wanasiasa wanawaaminisha watanzania kuwawatawapeleka kwenye karne ya 21. Yaani hadi karne hii serikali haina uwezo wa kutoa hata vyeti ya kuzaliwa kwa raia wake. Hii maana yake ni kwamba Tanzania ni kama pori ambako mnyama yeyote toka mahali popote anaweza kuingia na kutoka bila kujulikana. Wenzenu nchi zilizoendelea humwandishi mtoto shule wala kufanya lolote bila cheti cha kuzaliwa. Ili kuondoa watu kuishi bila kujulikana, kila anapozaliwa mtoto, awe raia au mkazi hupewa cheti cha kuzaliwa haraka ili kuweza kutambulika na kujua idadi ya watu ambao serikali huwahudumia.
            Kuna haja ya kuibana serikali iache uzembe kama alivyokiri rais aliyekaririwa akisema “hadi sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ni chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi waishio vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.” Je nini maana ya kuwa huru iwapo watu hawawezi kuwa na haki ya kuwa na cheti cha kuzaliwa? Msisingizie hali ya wengi wa watu wetu kuishi vijijini. Inakuwaje waweze kupata simu na noti washindwe kupata hati muhimu kama cheti cha kuzaliwa?  Kama serikali ingekuwa makini na nia, watanzania wote wanaweza kupata vyeti vya kuzaliwa na vitambulisho vya uraia. Bila kufanya hivyo, ni kwamba unaruhusu wageni wafurike nchini mwako na kutishia usalama wako ukiachia mbali kutumia raslimali zako bila stahiki.
            Kimsingi, rais licha ya kuingilia mamlaka ya waziri, amemdhalilisha kwa kutengua amri yake na kupingana naye tena hadharani bila kujali kuwa naye ana mamlaka yake kisheria. Kwa wenzetu, alichofanya rais kingewasukuma baadhi ya wananchi kwenda mahakamani kupinga amri yake isiyo ya kisheria.  Hapa uko wapi utawala bora na wa sheria kama waziri hana mamlaka wala hajui mipaka ya mamlaka yake? Wapinzani wakilalamika na kuhoji mawaziri kufanya kazi bila vitendea kazi wanakamatwa na kuonekana wachochezi. Basi tutangaze kuwa Tanzania ni nchi ima isiyo ya kidemokrasia au ya kifalme.
            Magufuli amekuwa akiingilia maamuzi ya wasaidizi wake bila kufuata sheria wala kuwapa staha kwa watendaji wake. Rejea kufuta agizo la kuondoa machinga mijini lililokuwa limetolewa na waziri wa  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) George Simbachawene ukiachia mbali mawaziri wengine Nape Nnauye (Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), na Jonista Mhagama waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu). Rejea mazoea ya kutoa maamuzi hadharani na si ofisini. Imefikia mahali sasa mawaziri wanafanya kazi kwa hofu kama viranja wa shule mbele ya mwalimu mkuu. Wamegeuka sawa na watumishi wa mfalme ambao hawana ubavu wa kumpinga au kumlazimisha aheshimu maamuzi na madaraka yao. Rejea kuendelea kumkingia kifua mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda licha ya kuchafuka kwa shutuma za kughushi vyeti. Rejea kumteua mtuhumiwa wa kashfa ya Escrow waziri Sospeter Muhongo bila kutoa hata maelezo ya kufanya hivyo kama ishara kuonyesha alivyo mbabe na asiyewajibika hata kwa wale waliomchagua.
            Tumalizie kwa kuwataka mawaziri wenye udhu kujiuzulu au kwenda mahamakani pale mamlaka yao yanapoingiliwa.
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 10:37 3 comments:

Kijiwe champongeza Keinerugaba


            Leo Msomi Mkatatamaa ameingia kijiweni akiwa mwenye furaha japo si kawaida yake kuonyesha hisia zake. Anaamkua na kumpa gazeti Mchunguliaji na kusema “mmesikia yaliyomkuta daktari feki Makorongo Muhanga?”
            Kabla ya kuendelea mzee Maneno anauliza “huyo muhanga kama mnyana ana nini nasi na inawezekanaje mnyama akaitwa daktari?
            Msomi anajibu “kaka huyu si mnyama. Na kama ni mnyama basi ni mnyama wa kughushi. Mara hii mmesahau muishiwa wa Ukonga aliyejipachika udaktari wa falsafa na mwanaharakati Msematruth Keinerugaba akamuumbua yeye na wenzake alipofyatua kombola aliloliita mafisi na mafwisadi wa ilmu nchini?”
            Kapende anachomekea “Msomi nimekupata. Nilisoma kesi ya huyu jamaa aliyofungua kupinga kuumbuliwa akidai alidhalilishwa na kuvunjiwa heshima wakati ni kihiyo wa kawaida.”
            Mijjinga anampoka Kapende mic na kuronga “hata nami niliipata kuwa pilato alitupilia mbali kesi hii baada ya mlalamikaji na wakili wake kuufyata na kushindwa kuhudhuria kesi, hivyo, kumlazimisha pilato kuifutilia mbali akimbandika mzigo wa kulipa gharama zote za kesi ambazo naambia ni milioni kumi na moja na ushei.”
            Mipawa anakatua mic “hii kitu naijua sana; na ilikuwa ikinisumbua hasa zama hizi za akina Daudi Bashite ambaye anaonekana kukingiwa kifua na dokta Kanywaji asijue anajipinga, kujiuumbua na kuonyesha asivyotenda haki kwa wachovu wote.”
            Sofia Lion aka Kanungaembe ambaye amevuliwa uanachama hivi karibuni anatwaa mic “huyu jamaa na genge lake wametuonea sisi. Ngoja Mungu awaumbue. Nangoja kusikia hatua atakazomchukulia huyu dogo kiherehere Bashite. Bila shaka hapa tutajua mbichi na mbivu. Halo haloooo! Ama kweli Mungu si Mpayukaji.” Ananitazama huku akitabasamu. Mie siongezi kitu zaidi ya kutabasamu.
            Mgoshi Machungi anakula mic “tiisema kuwa wapo wasomi wengi vihiyo tikachekwa. Sasa yako wapi? Niisoma kwenye gazeti la Danganyika Daima jana kuwa Makongoo Muhanga amebanwa kuipa uchache ambao hana. Aitaka eti awe anaipa laki tano kwa mwezi akini Keineugaba aikomaa na kutaka asweke upango hadi atapike njuuku.”
            Mpemba anakatua mic “wallahi mie nshangaa hawa vihiiyo. Kama wajua huna hiyo shahada wadai unayo ili uonekane nsomi wakati maamuma ili iweje? Mie nasema lazima huyu jamaa alipe hiyo njuluku. Pia nanshauri Keinerugaba awashitaki wale wote alowataja ili wapewe adhabu kama wengine. Hili la Bashite, kama hatoshughulikiwa, wallahi mie ntaandamana hata kama watanipiga mabomu na wapige.”
            Kanji anamchomekea Mpemba “sasa veve Pemba iko tafuta sida. Kama kuba naamua kula pini veve tafanya nini lazimisha yeye atimue hii Shite?”
            Kabla ya Mpemba kuendelea, Mheshimiwa Bwege anakwanyua mic na kuronga “mie sitegemei chochote cha maana kitendeke. Ukiona bingwa wa kutumbua amenyewe jua naye ameambukizwa hayo majibu aliyosifika kutumbua. Nyie mmeshikilia Bashite pekee wakati wapo wengi. Hamjui kuwa na Bill Lukuuuvi naye anatuhumiwa kuwa kihiyo anayedai ana masters wakati ni mweupe; na hata ndege wanajua kuwa ni kihiyo aliyeghushi?”
            Msomi anarejea “nadhani kuna haja ya kuepuka woga. Tuwakabili hawa jamaa watumbuane vinginevyo kwenye uchakachuaji ujao tuamke na kuwaambia wachovu madhambi ya hawa jamaa wanaolindana huku wakilipana njuluku zetu ukiachia mbali kupeana vyeo vinono wakati sisi wenye elimu za kweli tukidoda vijiweni. Huo ukubwa wa nkoa anipe mimi uone nitakavyoleta mapinduzi.”
            Mgoshi anarejea “kwanini jamaa hataki kuwa mkwei kwa nafsi yake? Mbona mgoshi Makambae aiweza kupata vyeo vya juu pamoja na kutosoma. Si aisema ukwei na akaeeweka? Huyu Bashite namshaui aonyeshe vyeti vyake yaishe; na aendeee kuchapa mzigo.”
            Kanji anarejea na kukatua mic “mimi iko jua hii Shite iko Hiyo. Kwanini naita vatu kuwa nauza bimbi bila shahidi ya kutosha? Hapana jua kuwa kama naita mtu bila shahidi navunjia yeye heshima yake? Kweli hii iko Hiyo kweli kweli.”
            Mijjinga anamchomekea Kanji “nakubaliana na wale wanaosema kuwa hakuna la maana litakalofanyika. Hebu fikiria. Dokta Kanywaji alizuia waishiwa na mawaziri kusafiri ughaibuni lakini hapo hapo akampa ofa Bashite na bi nkubwa wake waende kutanua kwa Joji Kichaka, Ufaransa na Dubai kabla ya juzi juzi kwenda Bondeni kuweka mambo sawa. Tunamdanganya nani na kwanini? Ama kweli ukisikia Danganyika basi si nyingine bali hii. Ni aibu kwa wanene kufumbia macho uoza huku wakituhadaa kwa kuhangaika na dagaa.”
            Msomi anarejea “umenikumbusha sakata ambalo halijapoa. Je mnajua kuwa Richomonduli imefufuka upya? Juzi nilisoma kwenye jarida moja la kimataifa kuwa Symbiosis bin Richmonduli imeishataki kaya na kupewa haki ya kulipwa madafu trilioni moja kwa kukatiza mkataba wa akina Kagoda. Hii maana yake ni kwamba akina Kagoda, sawa na IpTL wanaendelea kutuimbia wakati nasi tukishuhudia bila kufanya lolote.”
            Mipawa anakatua mic “Msomi sasa huu uchokozi. Hivi hamjui kuwa dingi alisema kuwa hawezi kufukua makaburi ili asishindwe kuyafukia. Hujui kuwa symbiosis, Kagoda, IptL na madude mengine yalianzishwa na wanene waliostaafu ambao wamefanikiwa kumtisha Dokta Kanywaji asiwatumbue?”
            Kijiwe kikiwa ndiyo kinakolea si alipita Makorongo Muhanga huku akilialia. Acha tumtoe mkuku ili kumfanyia kitu mbaya aache kughushi na kujiita daktari wakati ni hamnazo!
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 10:33 No comments:

Sunday, 19 March 2017

Keinerugaba usisamehe fisadi wa elimu

Image result for photos of makongoro mahanga
                Hivi karibuni, sakata la kughushi limetawala kwenye vyombo vya habari nchini hasa baada ya kuibuka madai kuwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda, alitumia vyeti visivyo vyake kujipatia elimu ya juu; ukiachia mbali kutumia majina bandia. Mbali na hiyo, kesi iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya mwanaharakati wa haki za binadamu Msemakweli Keinerugaba kwa madai ya kumchafua Makongoro Mahanga Mahanga aliyekuwa mbunge wa Ukonga na waziri wa zamani katika serikali ya awamu ya nne ambayo iliamu kunyamazia kashfa hii iliyowahusisha vigogo wengi wakiwamo mawaziri imekoleza moto uliokuwa umeanza kuzimika. Hii ni changamoto kwa serikali ya awamu ya tano ambayo rais wake Dk John Magufuli alisema hana simile na walioghushi na wafanyakazi hewa watokanao na kadhia hii.
Kimsingi, Keinerugaba aliposema ukweli kwa kuandika kwenye kijitabu chake cha Orodha ya Mafisadi wa Elimu Tanzania alijua alichokuwa akifanya ukiachia mbali kuwa kashfa ya kughushi ni tatizo linalofahamika kitaifa japo halishughulikiwi. Keinerugaba alipodai kuwa Mahanga hakuwa na shahada ya Uzamivu Doctor of Philosophy (PhD), alionekana mzushi na kituko hadi kutishiwa kushitakiwa kama asingeomba msamaha na kufuta madai yake. Kwa vile Keinerugaba alikuwa na ana ushahidi wa alichoandika, alikataa kuomba msamaha huku akiwahimiza watuhumiwa waende mahakamani. Muda ukapita bila Mahanga kuchukua hatua zozote za kisheria kama alivyokuwa ametishia. Baada ya kuzongwa akaamua kujitoa kimasomaso na kufungua kesi ambayo ilitupiliwa na Mahakama hivi karibu; na hivyo, kuamuru Mahanga amlipe Keinerugaba gharama za kesi zipatasho shilingi milioni 11 na ushei. Mwaka 2009, Mahanga alifungua kesi ya madai namba 145/2009 dhidi ya Msemakweli ambayo ilifutwa Julai mosi, mwaka 2014 na Jaji Salvatory Bongole baada Mahanga na Wakili wake kukwepa kuhudhuria kesi mara nyingi tu.
            Baada ya maji kuzidi unga na ushahidi kuonyesha kuwa kweli Mahanga hana hiyo PhD hivyo si daktari wa falsafa, eti anamwangukia Keinerugaba!  Ili iweje? Viko wapi vitisho na majigambo wakati mhusika ni kihiyo wa kawaida tu?  Je wako Mahanga wangapi ambao serikali–kwa sababu ijuazo yenyewe–imeshindwa kuwachukulia hatua huku ikiwaandama wadogo? Kama Mahanga alikuwa akijua alikuwa anakana ukweli, kwanini aliruhusu alimtisha, kumpotezea muda na fedha Keinerugaba wakati akijua ukweli? Anajua Keinerugaba aliathirika kiasi gani kwa vitisho vyake, ukiachia mbali muda wote alipokuwa mshitakiwa? Kwani alimshirikisha au kumomba ushauri Keinerugaba alipoamua kufungua kesi husika? Ana bahati Keinerugaba hajamfungulia kesi nilizogusia hapo juu. Isitoshe, kama Mahanga angempata Keinerugaba, sidhani kama angemsamehe zaidi ya kumtumia kujifisia kuwa ana elimu ya kutosha wakati hana hata chembe.
            Keinerugaba amfungulie Mahanga kesi nyingine ya udanganyifu, kujipatia fedha bila stahiki, kujitambulisha kwa utambulisho usio wake, kujipachika sifa asizokuwa nazo. Kulidanganya na uliibia taifa, kughushi huku akiwaunganisha na wengine aliowataja wakiwamo akina Deodorus Kamala, Emannuel Nchimbi, Mary Nagu, David Matayo David, Raphael Chegeni na Victor Mwambalaswa ambao walidai wana PhD wakati hawana ukiachia mbali wengine kama William Lukuvi Hii itasaidia kutoa onyo kwa vihiyo wengi waliotamalaki nchini wakati waliogopa umande.
Pia Msemakweli aitake mahakama itamke kuwa serikali ina wajibu wa kupambana na kadhia hii na yule atakeyeshirikiana au kuwalinda waliogushi naye aunganishwe kwenye jinai hii bila kujali ukubwa wa cheo chake au taaisi yake hata kama ni serikali yenyewe. Pia mahakama iitake serikali kutangaza wazi wazi kuwa wanaojipachika vyeo vyovyote wanatenda kosa la jinai. Imefikia mahali udaktari unadhalilishwa kiasi cha wanganga wa kienyeji na matapeli wengine wa kiroho kujiita madaktari au maprofesa wakati hawajui hata maana na thamani ya udaktari wa falsafa.
Kama mahakama itatoa hukumu dhidi ya kadhia hii, naamini ukimya na kutowajibika kwa serikali dhidi ya kadhia hii vitakuwa historia. Haiwezekani mtu atuhumiwe kughushi aendelee kuwa kwenye ofisi ya umma wakati kitendo alichofanya ni jinai ya wazi. Hapa sijui wahusika wanaolindana wanamdanganya nani zaidi ya kupingana na ahadi zao za kufufua elimu na kupambana na jinai hii inayoanza kuota sugu nchini kiasi cha kuwakatisha tamaa watanzania wanaojituma kuisaka elimu kihalali.
Kwa vile imeshathibitika kuwa Mahanga hana elimu aliyodai kuwa nayo, basi alipe fidia huku akingoja kushitakiwa kwa makosa mengine yaendanayo na jinai aliyotenda. Pia tutumie fursa hii kuiasa serikali iache kulinda wahalifu hata kama wana madaraka makubwa au wako karibu na wakubwa wa serikali. Tuwataje, tuwashitaki na kuwaumbua ili umma uwajue na kuwadharau ukiachia mbali kuwaadhibu vihiyo ambao ni maadui wa elimu Tanzania.
Tumalizie kwa kumpongeza Keinerugaba kwa mchango wake adhimu na muhimu katika mapambano ya kurejesha thamani ya elimu nchini. Pia tumsisitizie kuwa hana haja ya kusamehe mtu aliyechipachika cheo asichostahiki huku akimpotezea muda na fedha mahakamani. Nadhani hili licha ya kuwa somo kwa wengine, ni cheche ya kuanza kuwasaka na kuwawajibisha matapeli na vihiyo wote wanaotumia sifa wasizokuwa nazo kihalali. Tutumie fursa hii, pia, kumpa changamoto rais Magufuli awatumbue watuhumiwa bila simile wala kupepesa macho. Kwani wanakwamisha na kulihujumu taifa letu ukiachia mbali kusababisha aibu kwa kujenga dhana ya kutoaminika kwa wasomi wetu wa kweli.
Chanzo: Tanzania Daima Jumapili leo.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 08:19 No comments:

Saturday, 18 March 2017

Mlevi aadhimisha siku ya kinamama kwa kumteua mkewe


    Image result for photos of salma kikwete    
Baada ya wana mama karibu dunia nzima kuendelea kunyonywa na mfumo dume, juzi kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake ulimwenguni, mlevi niliteua mke wangu bi mkubwa almaaruf Salama Chinga Domokubwa kuwa mjumbe wa kigwena cha walevi aka Bunge la walevi. Hii ni baada ya kugundua kuwa kumbe walevi wengine huwateua bi wakubwa wa marafiki zao kuwa wanene. Mie sikungoja nistaafu ili atakayechukua kiti changu ameteue bi nkubwa wangu. Kama mzee K M7 pale Ug, nimeamua kumpa bi nkubwa ulaji wakati nikiwa kwenye ulaji.
Tofauti na wale walioteuana na kuzusha gumzo, walevi waliridhika nauteuzi wa bi nkubwa wangu kwa vile wananiamini. Na isitoshe bi nkubwa wangu ni kapuku ambaye hana cha NGO wala kipato cha ustaafu. Tofauti nyingine ni kwamba bi nkubwa wangu amepiga shule hadi akaambiwa no more class go to your husband and cook and do other things for him. Yeye hategemei unene wangu kuteuliwa bali kisomo chake ambacho ni wanawake wachache wanacho kwenye kaya ya walevi. Hii sitafsiri ili wale walioghushi vyeti au kuogopa umande kama siyo kubashite waipate. Hapa lazima mtembee na kamusi. Mbali na hiyo, tokana na mfano uliowekwa hivi karibuni kule kwa Joji Kichaka na Trumpet, si vibaya nikaanza kupiga mahesabu ya nke wangu kugombea hata urais wa walevi.
Walevi ni viumbe poa sana kama ukiwaelewa. Wanachotaka ni wewe kuwaonyesha kuwa u mnyenyekevu na asiyejitia kujua kila jambo. Wao hata ukimteua mbwa wako kuwa mjumbe hawajali ilmradi uwape kanywaji na mapupu pale Uwanja wa hyena au vipi? Wala hawana visa na visasi kama wale wachunaji ninaowasikia wakihanikiza kupambana na wabaya wao wakimsingizia God utadhani wanamtumikia kweli. Hata hivyo, walevi si kama wadanganyika wala wabongolalalanders. Hakuna kitu wasichokubali kama kuwaburuza au kuwatisha. Kwa mfano, ukimweka lupango mwakilishi wao, hawangoji kipaza sauti anchomoe. Watakutokea wenyewe na utamwachia bila kungoja mapilato wenye adabu, heshima na udhu kumchomoa baada ya wewe kuchemsha kama nilivyoshuhudia hivi karibuni.  Ukitaka maulaji yao yakushinde jifanye imla. Ukitaka kukosana na walevi wadhulumu au kuwakingia kifua waliowadhulumu au kuvunja sheria zao. Watakutokea na michupa ima wakutie ngeu au utoke mkuku kama mbwa aliyefumwa akiiba nyama kama si paka aliyeiba maziwa. Kama ukifanikiwa kuwaburuza walevi ujue zako zesha. Kwani, watakulia pini hadi msimu mwingine wa uchakachuaji wakupige chini. Pamoja na ulevi wao, walevi wana sifa nyingine. Wana kumbukumbu kama tembo. Unaweza kuwaudhi ukajishaua na kujifanya wewe muungu mlevi kwa wakakushiti. Ila siku ya siku ikifika, utaona visasi vyao.
Turejee kwenye uteuzi wa bi nkubwa wangu. Guess what. Mwaka jana niliteua wajumbe wengine wa dezo. Kwa sheria za kilevi, lazima uteue angalau asilimia ya akina mama kwenye kila uteuzi. Kwenye uteuzi ule nilijitia ubabe na kuteua vidume wengi kuliko akina mama. Acha akina mama waanze kunung’unika. Si walikwenda kwa bi nkubwa ambaye wananchukulia kama shoga yao na kumpa onyo kuwa asipoteua mwanamama kutimiza matakwa ya sheria za walevi asahau ukuu mhula ujao. Kuona hivyo, si nikaamua kumteua bi nkubwa wangu ingawa yeye ni tofauti na hao mashoga zake hasa ikizingatiwa anatoka kwenye ukoo ule ule wa wanene wa walevi kama wale wa kule Idodomya.  Baada ya baadhi ya walevi na wavuta bangi kuanza kulalamika kwanini nimemteua bi nkubwa wangu, sikunyamaza zaidi ya kuwapa kanywaji na kesi kuishia hapo. Wengine walizidisha unywanywa. Kuwakata ngebe niliwaambia kuwa bi nkubwa wangu ni bonge ya supu yaani ni msupu au mzuri kwa wale wasiojua Kiswahili cha walevi.
Kimsingi, waliokuwa wakinitia taabu ni akina mama. Kwa vile wanaweza kudanganyana na kuwekana sawa, nilishangaa kuona walivyoridhika na mimi kumteua bi nkubwa wangu utadhani atawawakilisha makapuku waliokuwa wakinibana niteue ili kuleta uwiano wa kijinsia kwa mujibu wa katiba ya walevi. Sasa kwa vile nshamteua bi nkubwa. Next time, nanteua kitegemezi chetu kiitwacho Riziki ili kaya yangu yote iwemo njengoni. Isitoshe kama kitegemezi kitakuwa na mama yake njengoni, wale vishoka wanaosifika kunyemelea vya wenzao wataogopa kwa vile kipo. Hii nayo dili hasa usawa huu ambapo nasumbuliwa na malazi ambayo ni siri kuwaambia walevi hata kama wanayajua. Isitoshe mimi kwa cheo changu kama dingi wa kaya ya walevi si mjumbe wa kigwena chetu. Hivyo, sirahisi kuwapo kule kuhami mali zangu zisiliwe na vishoka, mafisi na vispring chickens vya kirume kama alivyofanyiwa nzee Madiba alipokuwa lupango. Hayo tuyaache. Kwanini tusiagane?
Chanzo: Nipashe Jumamosi leo.


Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 07:15 No comments:
Newer Posts Older Posts Home
Subscribe to: Posts (Atom)

Cordially and unlimitedly welcome to this blog.


Writing and reading are two different processes but which share the same goal-to educate, communicate and entertain.
It is my pleasure to have you as the guest of this tablet.
I, thus, warmly and always, welcome you to share ideas.
Importantly and eminently, shall there be anything amiss or you think can advance this blog, please donate it.
Allow me to humbly and kindly welcome you once again.
Nkwazi N Mhango- A Man And a Half

When wisdom brings no profit, to be wise is to suffer. Not all thoughts are good and constructive. Others are even worse than bullets. The good thinkers are the ones that think constructively for the manumission of all bin-Adams regardless their diversity. Mwl. Nkwazi N Mhango,
Canada.


The Curse of Salvation

The Curse of Salvation

Gen Z and Internet Revolution

Gen Z and Internet Revolution

I Cry for Ambazonia and Darfur

I Cry for Ambazonia and Darfur

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do.

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do.

Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Yoo-hoo, Africa Is Yowling

Yoo-hoo, Africa Is Yowling

The Story of Stories

The Story of Stories

The Chant of Savant

The Chant of Savant

AFRICA’S CONTEMPORARY FOOD INSECURITY Self-inflicted Wounds through Modern Veni Vidi Vici and Land G

AFRICA’S CONTEMPORARY FOOD INSECURITY Self-inflicted Wounds through Modern Veni Vidi Vici and Land G

AFRICA MUST DEAL WITH BLATS FOR ITS TRUE DECOLONISATION

AFRICA MUST DEAL WITH BLATS FOR ITS TRUE DECOLONISATION

Epistle to Afrophobic South Africa

Epistle to Afrophobic South Africa

Magufulification

Magufulification

BORN NUDE

BORN NUDE

Total Pageviews

Heko Rais Magufuli

Heko Rais Magufuli

DECOLONISING EDUCATION

DECOLONISING EDUCATION

Kudos President Magufuli

Kudos President Magufuli

JOKEY HORSE-JOCKEY NORTH-SOUTH RAPPORT Diagnostic-cum-Prognostic-Academic Perspectives on Who Truly

JOKEY HORSE-JOCKEY NORTH-SOUTH RAPPORT Diagnostic-cum-Prognostic-Academic Perspectives on Who Truly

The Family Friend of Animals

The Family Friend of Animals
Children's Book

Matembezi Mbuga ya Wanyama

Matembezi Mbuga ya Wanyama
Kitabu cha Watoto

Our Heritage

Our Heritage
Children's Book

How Africa Developed Europe:Deconstructing the His-story of Africa, Excavating Untold Truth...

How Africa Developed Europe:Deconstructing the His-story of Africa, Excavating Untold Truth...

Africa's Dependency Syndrome: Can Africa Turn Things around for the Better?

Africa's Dependency Syndrome: Can Africa Turn Things around for the Better?

'Is It Global War on Terror' or Global War on Terra Africana?

'Is It Global War on Terror' or Global War on Terra Africana?

Perpetual Search

Perpetual Search

Africa's Best and Worst Presidents

Africa's Best and Worst Presidents

Psalm of the Oppressed

Psalm of the Oppressed
Psalm of the Oppressed

AFRICA REUNITE or PERISH

AFRICA REUNITE or PERISH
A new approach towards empowering Africa

BORN WITH VOICE

BORN WITH VOICE

Soul on Sale

Soul on Sale

Soul on Sale

Nyuma ya Pazia

Nyuma ya Pazia

We are one

We are one

SAA YA UKOMBOZI

SAA YA UKOMBOZI

Feel at home

You are always welcome to this epistle again and again time after time, ad infinitum.


Most read Posts

  • Sarkozy’s Take on African Fat Cats a Welcome Move
    At last the chicken are coming home to roost! French authorities made a groundbreaking decision by culling three most corrupt African presid...
  • Napanga kuanza kuuza mitumba na si maneno
    Ingawa mimi si mtumba, napanga kuuza mitumba. Nimechoshwa na jamii ya mitumba. Kila kitu mitumba. Mitumba, mitumba mitupu. Siasa za mitumba...
  • Better or Bitter Life for all?
    When I deeply muse on how an arrogant and brutal cabal of hoity toity (Coverted Con Men (CCM)) is tirelessly hoodwinking and dividing the ho...
  • Africa's Becoming more Despotic and Nepotistic
    "King of Kings" Gaddaffi The seven-day 40th anniversary of Libya strongman’s autocratic rule and charade elections in Gabon where...
  • Kuna siku tutataifisha haya mahekalu haki ya nani
    Taarifa kuwa waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige alinunua nyumba kwa zaidi ya shilingi bilioni moja licha ya kuwastua wananchi na...
  • Nyangumi mdogo akutwa amekufa ufukweni BC
    Hii ni picha iliyotolewa ya Nyangumi aina ya Humpback ambaye alikumbwa na maji na kutupwa kwenye ufukwe wa bahari ya Pasifiki kwenye eneo l...
  • Kikwete, Charity Begins at Home!
    President Jakaya Kikwete Pea...
  • Kweli binadamu si chochote wala lolote, wamkumbuka huyu?
    Walioko madarakani mkiabudiwa kama miungu au sanamu kumbukeni vijana hawa hata baba zao  ambao maiti zao zinaoza jangwani. Ungewaambia...
  • Pinda kulia hakutoshi, awajibike
    INGAWA kilio cha Waziri Mkuu, Mizengo Peter Kayanza Pinda, kinaonekana kuyeyusha hasira za Watanzania kwa muda, kuna haja ya kudodosa zaidi....
  • Hawa si wachungaji bali ni fisi na mbwa mwitu
    KUMEZUKA mtindo mchafu na wa rejareja wa baadhi ya wachumia tumbo na matapeli kumtania hata kumtumia Mwenyezi Mungu kufanya utapeli na ujamb...

Followers

Blog Archive

  • ►  2025 (26)
    • ►  May (2)
    • ►  April (4)
    • ►  March (6)
    • ►  February (8)
    • ►  January (6)
  • ►  2024 (92)
    • ►  December (7)
    • ►  November (4)
    • ►  October (11)
    • ►  September (9)
    • ►  August (7)
    • ►  July (9)
    • ►  June (9)
    • ►  May (8)
    • ►  April (7)
    • ►  March (6)
    • ►  February (7)
    • ►  January (8)
  • ►  2023 (118)
    • ►  December (10)
    • ►  November (10)
    • ►  October (9)
    • ►  September (2)
    • ►  August (4)
    • ►  July (6)
    • ►  June (9)
    • ►  May (8)
    • ►  April (18)
    • ►  March (13)
    • ►  February (9)
    • ►  January (20)
  • ►  2022 (208)
    • ►  December (14)
    • ►  November (14)
    • ►  October (20)
    • ►  September (20)
    • ►  August (12)
    • ►  July (25)
    • ►  June (22)
    • ►  May (18)
    • ►  April (13)
    • ►  March (18)
    • ►  February (18)
    • ►  January (14)
  • ►  2021 (323)
    • ►  December (23)
    • ►  November (34)
    • ►  October (26)
    • ►  September (13)
    • ►  August (19)
    • ►  July (21)
    • ►  June (29)
    • ►  May (25)
    • ►  April (23)
    • ►  March (43)
    • ►  February (29)
    • ►  January (38)
  • ►  2020 (290)
    • ►  December (33)
    • ►  November (37)
    • ►  October (28)
    • ►  September (35)
    • ►  August (31)
    • ►  July (26)
    • ►  June (17)
    • ►  May (21)
    • ►  April (18)
    • ►  March (15)
    • ►  February (17)
    • ►  January (12)
  • ►  2019 (160)
    • ►  December (8)
    • ►  November (7)
    • ►  October (12)
    • ►  September (9)
    • ►  August (27)
    • ►  July (18)
    • ►  June (18)
    • ►  May (11)
    • ►  April (11)
    • ►  March (9)
    • ►  February (16)
    • ►  January (14)
  • ►  2018 (162)
    • ►  December (12)
    • ►  November (6)
    • ►  October (13)
    • ►  September (10)
    • ►  August (20)
    • ►  July (9)
    • ►  June (14)
    • ►  May (9)
    • ►  April (16)
    • ►  March (21)
    • ►  February (17)
    • ►  January (15)
  • ▼  2017 (306)
    • ►  December (20)
    • ►  November (23)
    • ►  October (20)
    • ►  September (26)
    • ►  August (31)
    • ►  July (31)
    • ►  June (34)
    • ►  May (26)
    • ►  April (24)
    • ▼  March (20)
      • Kumbe Tanzania imefika hapa!
      • Mgoshi Apendekeza Kijiwe Kihamie Koromije
      • Kwa Sasa Rais wa Tanzania ni Nani?
      • Kashfa ya Makonda: Inatakiwa busara si ubabe
      • Mlevi kuliambia na kulikolomije taifa
      • Bashite Kachape Kazi
      • Kwanini Magufuli anawadhalilisha mawaziri wake
      • Kijiwe champongeza Keinerugaba
      • Keinerugaba usisamehe fisadi wa elimu
      • Mlevi aadhimisha siku ya kinamama kwa kumteua mkewe
      • Mahakama isijirahisi hadi kuingiliwa na kunajisiwa
      • Kijiwe chawapa shavu CCM kuvuana magamba
      • Serikali isipoteze muda kuwafunga wakosoaji
      • Breaking News!!!! Kimenuka CCM washikana uchawi na...
      • Barua ya wazi kwa Makondakonda and Gwajimmy
      • Trump Giving Terrorists a Field Day
      • Waandishi wa habari hamjamtendea haki Janet Magufuli
      • Kijiwe chastukia matapeli wa maombi
      • First lady kuwa mbunge ni demotion au promotion?
      • Neema Muita Wa-mura: Wanene wote waige moyo wa Mugful
    • ►  February (28)
    • ►  January (23)
  • ►  2016 (269)
    • ►  December (22)
    • ►  November (21)
    • ►  October (22)
    • ►  September (15)
    • ►  August (12)
    • ►  July (27)
    • ►  June (24)
    • ►  May (23)
    • ►  April (29)
    • ►  March (26)
    • ►  February (27)
    • ►  January (21)
  • ►  2015 (399)
    • ►  December (34)
    • ►  November (24)
    • ►  October (22)
    • ►  September (34)
    • ►  August (29)
    • ►  July (37)
    • ►  June (22)
    • ►  May (32)
    • ►  April (35)
    • ►  March (46)
    • ►  February (47)
    • ►  January (37)
  • ►  2014 (502)
    • ►  December (47)
    • ►  November (49)
    • ►  October (47)
    • ►  September (37)
    • ►  August (40)
    • ►  July (42)
    • ►  June (30)
    • ►  May (35)
    • ►  April (47)
    • ►  March (44)
    • ►  February (39)
    • ►  January (45)
  • ►  2013 (399)
    • ►  December (37)
    • ►  November (27)
    • ►  October (31)
    • ►  September (26)
    • ►  August (33)
    • ►  July (39)
    • ►  June (28)
    • ►  May (40)
    • ►  April (44)
    • ►  March (39)
    • ►  February (26)
    • ►  January (29)
  • ►  2012 (597)
    • ►  December (27)
    • ►  November (26)
    • ►  October (27)
    • ►  September (30)
    • ►  August (47)
    • ►  July (94)
    • ►  June (86)
    • ►  May (119)
    • ►  April (83)
    • ►  March (23)
    • ►  February (17)
    • ►  January (18)
  • ►  2011 (261)
    • ►  December (20)
    • ►  November (19)
    • ►  October (20)
    • ►  September (21)
    • ►  August (27)
    • ►  July (12)
    • ►  June (15)
    • ►  May (20)
    • ►  April (27)
    • ►  March (32)
    • ►  February (24)
    • ►  January (24)
  • ►  2010 (205)
    • ►  December (25)
    • ►  November (23)
    • ►  October (23)
    • ►  September (23)
    • ►  August (17)
    • ►  July (13)
    • ►  June (12)
    • ►  May (10)
    • ►  April (18)
    • ►  March (9)
    • ►  February (16)
    • ►  January (16)
  • ►  2009 (163)
    • ►  December (19)
    • ►  November (14)
    • ►  October (11)
    • ►  September (6)
    • ►  August (12)
    • ►  July (9)
    • ►  June (11)
    • ►  May (20)
    • ►  April (22)
    • ►  March (14)
    • ►  February (12)
    • ►  January (13)
  • ►  2008 (191)
    • ►  December (12)
    • ►  November (11)
    • ►  October (14)
    • ►  September (15)
    • ►  August (16)
    • ►  July (23)
    • ►  June (10)
    • ►  May (19)
    • ►  April (16)
    • ►  March (19)
    • ►  February (17)
    • ►  January (19)
  • ►  2007 (33)
    • ►  December (13)
    • ►  November (20)

About Me

My photo
View my complete profile

Travel theme. Powered by Blogger.