How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Saturday 28 February 2015

Picha ya mwezi: Senior na Junior wanapochonga

Hapa ni mimi na Junior tukichonga. Si haba sasa bwana mdogo anaikimbilia miaka mitatu. Anaonekana kuzimilki nyayo za Senior kuliko hata kaka yake Nkuzi.

PCCB and cops are corrupt through and through!

  ... , PCCBs boss Edward Hosea and ex-President Benjamin William Mkapa
          I’d not believe my eyes when I read Afrobarometer’s findings-cum-bombshell that Prevention and Condoning Corruption Bureau (PCCB) is among the most corrupt govt agents in the hunk I thought kanywaji and bangi had claimed my eyes. I’d to read over and over again. As an alkie I’d to worry.
           I was wrong. My eyes are doing spiffy. Let me share what made me freak out as I read the Newspaper. The sentence that sent my heart racing noted, “Police ranked the highest corrupt public office with a score of 50 per cent of the respondents followed by TRA officials and local government agents at 37 per cent while judges and magistrates came third with 36 per cent.”  The other day I told sozzlers that these folks were corrupt through and through but they didn’t believe me. I knew this from the beginning due to the fact that most of PCCB officials are my buddies who live in citadels and drive oil guzzlers of the same value and price to those of MPs or ministers. Where did they get the dosh if it isn’t by the way of soliciting kickbacks?  Another way of looking at how filthy rich PCCB folks are is look at their tummies. Some have bigger bellies than even the MPs and other eaters. They’re more pregnant than business cops. Even the lassies they elope with are not those vinuka jasho of Ohio and Kinondoni. They’re employed in reputable offices and others are even wedded ladies.
          The other day one banker told me that if you want to compare rich public workers  pick from the departments of Finance (TrA and Central Bank), Harbour, Airport, Energy and Minerals, Investment, Trade,  Home affairs (cops, and immigration that vends our passes)  and Tourism (whose officials are known for promoting tourism through touring the world), to mention but a few.
          Another nugget, my friend working with intelligence gave me is that some of PCCB honchos have some accounts abroad. So, dispatched to investigate vigogo such as Mzee wa Vijisenti or Rugemalayer of hela ya ugolo they end up asking for bung and stash it in their accounts abroad. This is why all big pinches have nary worried or being arrested even after the media made a lot of noises about their crimes. Who’ll arrest or investigate whom if all are in the same game of robbing paupers and boozers?
          The other day I heard their god complaining that they’ve kiherehere like school girls he once hollered at saying their kiherehere makes them arrest and prosecute without making thorough investigation. He missed a point big time. Kiherehere isn’t the reason for PCCB folks to lose cases. It is mshiko they receive that makes them frame their cases wrongly. It seems the boss forgot his cronies in investment contracts who break the law in entering them to enable thieves –posing as investors – rob our hunk wantonly like IpTL does.
          Let’s think together. What do you expect when the chicken eats its own eggs? What do you expect when a thief’s assigned to guard the shop or a bank? This is Bongo guys. You can’t know who’s who in this game of deceit known as public service or government.
          Afrobarometer has opened my eyes that PCC is the top most corrupt agent in the hunk. Now you can see why corruption’s become the order of the day wantonly. You’re dispatching a thief to arrest another while they’re all in the same game. Akili au matope? Though Afrobarometer exonerated the office of the president which is nary legally audited, PCCB being under it is another nugget why they all are the same.
          The shibboleth or kiherehere of putting PCCB under the office of president makes it difficult for it to operate freely. Thus, use the opportunity to make private dosh out of corrupt and unscrupulous movers and shakers in the hunk. For PCCB to up the ante so as to be accepted and trusted by seething boozers, it’d free itself from the office of the biggie. I know Mr Biggie’ll gloat saying he’s been right all along for imprisoning PCCB in his office for reasons only known to him and friends. Again, after he packs and jumps, what next? Yes. He’s been right given that none of his consigliore’s ever been roasted by PCCB. What else’d he does he want? If he can keep PCCB in a seam zone and keep his foothold on it, then what else?
          Again, the major question to be asked after all this mess, shame is: What’d be done to finesse, attune and fine-tune PCCB so that it can work for boozers? This is important. For the hunk now is in a logjam after being taken over by fisadis. Wait. The other day I read one weekly alleging that in the offshore-dosh-stashing scandal involves even the biggest of the heads of two former regimes. I’m still waiting to hear what PCCB has to say about this new and damning revelation. Wana ubavu if they failed even to investigate illegal grabbing of Kiwila Coal Mine? When a dog turns against its puppies – mind you – things are not well. Who’ll take on the dogs that eat their puppies if the watchdog itself does the same?
Source: Guardian Feb., 29, 2015. 

Hii imekaaje nayo?

John Komba afariki

 
Habari tulizopata ni kwamba Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM) John Damian Komba hatunaye tena.  Atakumbukwa kwa nyimbo zake na kuuchapa usingizi mjengoni  ukiachia tishio la kwenda porini kama Katiba mpya ingepita.

Afrika mke wa rais ni rais pia hata kama nyuma ya pazia

Kinana akimaliza S.Sudan akasuluhishe Somalia

Mratibu wa kampeni wa rais Kikwete, Abdulrahaman Kinana akiagana na rais Salva Mayardit wa Sudan ya Kusini baada ya kusimamia mazungumzo ya amani mjini Juba juzi.

Mnaua elimu wasomi wametosha eeh!

Kaya yetu inasifika duniani kuwa ya wasomi. Rais wetu ni profesa. Wengi wa mawaziri na wabunge ni madaktari wasiotibu.Usiniulize kama wameghushi au la. Kaya ina wasomi kila tabaka.Wapo wa ukweli, wa kughushi, kubaingaiza,kuungauga hata feki, kujipachika vyeo vya kisomi. 
Yote ni matokeo ya marehemu Mwalimu Mchonga kutoa elimu ya bure. Je alifanya hivi kwa vile alikuwa ticha? Ngurumbili ni viumbe wa ajabu na tatanishi. Wakikosa wanalaumu, wakipata wanakufuru. 
Baada ya “watalaumu” wetu wa ‘taalauma’ kugundua kuwa kaya ina wasomi kiasi cha kazi kuadimika, wengine kushinda baa, kula msosi mzito wa viroba na kuvuta mibangi kama mimi, wamekuja na ubunifu wa hali ya juu. 
Wameamua kuanza kujaza ujinga kisera ili kupunguza tatizo la kuwa na wasomi wengi wafanyao kaya isilike wala kutawalika kiulani. Hivyo, wamekuja na mbinu ya kutukuza ujinga na kulaani usomi. Wameruhusu watu –tena wazito –waghushi taaluma huku wengine wakizawadiwa vyeo vizito vizito kitaaluma bila kujua hata mlango wa darasa la kusomea vyeo hivyo ulipo! 
Kutokana na kuwa na wasomi wengi –tena wanaoongea Kiswa-Kinge hata mjengoni –wataalamu wamekuja na gia ya kuwakata kilimilimi. Wanapendekeza Kiswaa kiwe lugha ya kufundishia kunzia vidudu hata vyoo vikuu. Upo hapo mshirika? Tuache utani. Hiki kinachoitwa sera mpya ya ilimu si chochote wala lolote bali mauti ya vizazi vijavyo. 
Hivi, uliposoma wakati wa mzee Mchonga –tena bure –ukasoma vitabu kibao kuanzia Adili na Nduguze, Kusadikika, Hamkani si Shwari Tena, Mfanyabiashara wa Venice, African Child, Things Fall Apart, No Longer at Ease, The Great Ponds, The River Between, New life in Kyierefaso na Songs of Lawino ukaamua watoto wetu wasome kitabu kimoja unamaanisha nini kama si kuwajaza ujinga? Let’s face it folks. 
Juzi nilisikia daktari mmoja feki akisema kuwa kwa kufundisha kwa Kiswaa wanagezi wataelewa sana tofauti na sasa ambapo kimombo eti kinawafanya wasiambulie kitu. Uongo. Mnaua ilimu kwa kusingizia lugha? Basi kafundishe kwa Kimakonde au Kisambaa au Kitumbuka muone balaa lake. Hakuna cha lugha wala nini bali sanaa na kukosa ubunifu. Wekezeni kwenye ilimu. 
Wape maticha motisha na marupurupu mnayopotezea kwa wanasiasa muone kama haitapaa. 
Sikubaliani na upuuzi wa kusoma kitabu kimoja. Hata hizo dini, pamoja na kuwa na kitabu kimoja kimoja, ndanimwe kuna vitabu vingi.Hamjui kuwa kutumia kitabu kimoja ni kuua vipaji vya wanafunzi ukiachia mbali kuwamaliza watunzi na wachapishaji? 
Naona hili limefanyika ili wavivu fulani wanaoandika vitabu vya hovyo wapate soko. Kama si hivyo mbona vitabu vyangu havifundishwi maskulini wakati ni vya kisomi na vimekwenda shule ile mbaya.Tena, vingine vimechapishwa nje kuonyesha vilivyo bomba. Hata hivyo, nani atatumia vitabu vyangu wakati vinawasuta? 
Watu wameendekeza usanii na ufisadi hadi kwenye ilimu.Huu ni ushahidi wa kutoona mbali na kushindwa vibaya sana.Vijana siku hizi hawana motisha wa kusoma kwa vile hakuna ajira ukiachia mbali kuhalalishwa kwa usanii,uhalifu na mazabe mengine.Kwa sasa vijana wanatamani kuwa wasanii wawe wa kweli au kisiasa, au ikizidi ikapungua, majambazi ili waukate kama mafisadi na majambazi wakubwa wa kalamu wanaowaona wakiwaongoza njia ya kuelekea kwenye utwahuti. Huwezi kubariki jinai ukategemea watu wawe na motisha wa kufanya kazi kwa bidii au kusoma. 
Wahangaike na kusoma ili iweje wakati mtu ananyaka silaha ya SmG usiku mmoja na kuamka tajiri na hakuna anayemhoji? Rejesheni sheria ya maadili na kuondokana na madili muone kama ilmu haitapaa.Wahangaishwe na kusoma ili iweje iwapo ajira nyingi zinaangalia udugu na rushwa badala ya elimu? Mara hii mmesahau skandali ya uhamishaji ndani ya Wizara ya Mambo ya Uani ya Nchi, ambapo waajiriwa wote walikuwa ‘dugu’ za mabosi wa idara siyo? 
Nenda bandarini, uhamiaji, viwanja vya ndege, undata, TrA, mizani, mipakani, Benki Kubwa aka Belly of Tembo (BoT) iliyojaa watoto wa vigogo ambao wamefoji midigilii na kwingineko kwenye njuluku ya chapchap. Sijui ile kashfa ya BoT kujaa watoto wa vigogo iliishia wapi? Nani anakumbuka iwapo walevi na wachovu wana sifa kuu ya kusahau kirahisi wanaposahauliswa kwa movies mbali mbali?  
Nani anaongelea tena escrow au kurejesha mshiko kutoka Uswisi? Kila kitu kimesahaulika. Mambo shwari kwa wenyewe kula kaya.
Tukirejea kwenye ilimu wakubwa wana shida gani iwapo wanapeleka vitegemezi vyao ughaibuni kupata elimu ya nguvu ili waje vitawale walevi?   Tena wanafanya hivyo kwa kutumia mshiko wa walevi na wachovu waupatao toka kwenye kodi. Nani anajali iwapo wenye kaya wana namna ya kuwajaza ujinga walevi ili waendelee kuwaibia? Ndiyo maana hata hawakuona aibu kuja na mauzauza haya wakayaita nyenzo ya maendeleo bila kufafanua kuwa maendeleo yenyewe ni ya kwenda nyuma au shimoni. 
 Mara hii mmesahau tambo za mgosi Jose Makambale kuwa mwanae amesoma, tena, ughaibuni. Hivyo, angepewa uwaziri na kweli akaupata kiasi cha kutaka hata urahisi? Unadhani angekuwa amesomea kwenye shule za “shule za kata elimu” angekuwa na ubavu wa kumwaga nyodo hadharani asihofie wachovu wangemtolea uvivu? Alisema akijua wengi wa walengwa ni hamnazo wasioweza kumstukia na kuzuia jinai yake.  
Unafikiri  tambo hizi angemtolea mzee Mchonga mwanae angapata huo uwaziri?  Thubutu. Nani anajali iwapo mambo yamebadilika kiasi cha makaburi ya watakatifu kusafishwa na wenye dhambi?  
 Kwa vile wanaopaswa kufaidi kaya wanahisi wasomi wametosha, lazima waongeze ujinga ili kutawala kiulani. Mara hii mmesahau maneno ya mzee Mchonga aliposema kuwa wajinga hutawaliwa kirahisi kuliko wasomi. Hata hivyo, mzee hakuwa na mtima nyongo.  
Aliendelea kutoa elimu ya bure kwa kila kitegemezi bila kujali mbari wala kipato. 
 Matokeo yake wale waliofaidi elimu hii wameisahau na kuanza kufanyia majaribio vichwa vya vitegemezi vyetu. Mwenzenu hawanipati nitahamishia changu baa lau kifyatuke kama mimi na kunena:Ueni elimu wasomi wametosha. 
Mtajijuu.
Chanzo: Nipashe Feb., 28, 2015.

Thursday 26 February 2015

Sijui Kikwete analipwa kwa nini na lipi wakati ni mzururaji?

unnamed
Kikwete akiweka shada la maua kwenye makaburi wa wendazake marais wa zamani wa Zambia Levy Mwanawasa na Fredrick Chiluba mjini Lusaka.
Juzi alikuwa nchini Kenya kwenye mkutano wa wakuuw a EAC. Kabla ya hapo alikuwa Davos. Nadhani muda anaokaa ikulu na Tanzania ni mdogo kuliko anaokaa kwenye ndege. Hakika Kikwete ataingia kwenye vitabu vya historia kama rais wa hovyo, dhaifu, fisadi na mzuraraji aliyewahi kutokea katika historia ya Tanzania. Laiti tungemwelewa baba wa taifa Marehemu Mwl Julius Nyerere tusingechagua hasara na sanaa kukaa ikulu kwa miaka kumi.

Tuesday 24 February 2015

Mnaua elimu na kusingizia lugha!

Taarifa za hivi karibuni kuwa Tanzania imeanzisha mpango mpya wa elimu ambapo elimu ya awali itakwenda hadi kidato cha nne, kama ingekuwa siyo siasa ni ya kufurahisha. Pamoja na kujivuvumua huku, wengi wanajiuliza: Hiyo fedha itatoka wapi –na kama itapatikana –hiyo elimu itakuwa elimu bora au bora elimu?
Hakuna kitu kilichowaacha hoi wengi kama pendekezo kuwa Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia kwa ngazi zote. Mojawapo ya kipengele cha sera mpya ya elimu kinasema, “Lugha ya Taifa ya Kiswahili itatumika kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote za elimu na mafunzo na Serikali itaweka utaratibu wa kuwezesha matumizi ya lugha hii kuwa endelevu na yenye ufanisi katika kuwapatia walengwa elimu na mafunzo yenye tija kitaifa na kimataifa.” Huwezi kuwa na tija kimataifa kwa kufundisha lugha ambayo hata kama ni ya kimataifa, haijapanuka ikilinganishwa na lugha pana ya kimataifa inayoondolewa na kuweka Kiswahili. Hii ni siasa na hata mantiki ya kufanya hivyo ni haba sana.
          Kimsingi, kinachofanyika ni kusingizia lugha kwa mafanikio haba jambo ambalo linaonyesha upofu wa wahusika kuhusiana na chanzo cha matatizo ya elimu nchini. Nadhani kama watanzania wangekuwa makini wasingehitaji kutapatapa kutafuta namna ya kuendeleza elimu. Wana marejeo ambayo ni wakati wa awamu ya kwanza ambapo elimu ilisifika kimataifa na kujenga kizazi cha kisomi kikilinganishwa na cha sasa. Hivyo, badala ya kuhangaika warejee huko watapata jibu la kutosha.
Mfano kipengele kimojawapo cha sera mpya ya elimu kinasomeka, “Serikali itatoa na kusimamia matumizi ya kitabu kimoja cha kiada kwa kila somo katika elimu msingi ili kufanikisha upimaji wa matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji unaofanana katika ngazi mbalimbali za elimu.’’ Huu ni upuuzi mtupu. Kwanini wahusika wasirejee namna ya ufundishaji wakati wa awamu ya kwanza ambapo idadi ya vitabu vilivyotumika katika somo ilitegemea aina ya somo na kiwango cha elimu. Huwezi, kwa mfano ukafundisha Kiswahili darasa la tano hadi saba kwa kutumia kitabu kimoja ukasema umeelimisha wanafunzi. Wanafunzi wanataka kuanza kuzoea kutumia na kusoma vitabu vingi ili wanapokwenda mbele wawe na uzoefu. Hapa Kanada mtoto wa darasa la tano anasoma vitabu vingi kuliko mtu wa kidato cha kwanza Tanzania.
 Kama wahusika wanaogopa kuwa wanafunzi hawatasoma, wajiulize zama za awamu ya kwanza watu walisomaje na kufundishwa kwa vitabu vingi? Kulikuwa na motisha katika elimu. Mwalimu Julius Nyerere alikuwa msomi na mtunzi wa vitabu. Alishiriki na kutoa mihadhara chuoni mara kwa mara. Nyerere hakutungiwa vitabu bali alijitungia mwenyewe. Je kwa sasa hali ikoje? Viongozi wanatungiwa vitabu utadhani ni maiti au mataahira au vichanga wasioweza kuandika vitabu vyao? Mbona rais Yoweveri Museveni ameandika kitabu?
Chini ya Nyerere Elimu ilikuwa ndiyo ufunguo na si jinai   kama ilivyo sasa baada ya kuzika sheria ya maadili ya utumishi wa umma.
Nadhani tatizo kubwa la elimu yetu ukiachia mbali walimu kutolipwa vizuri, ni kutowajibishwa kwa wale wanaovuruga elimu. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, amevurunda na si mara moja wala mbili lakini hakuwajibishwa hadi kusema kuwa hawezi kujiuzulu utadhani ofisi ni mali ya mama yake. Unajiuliza mantiki ya mtu huyu huyu aliyevuruda kwa muda mrefu kuja na kitu kipya tofauti na ukale ule ule tuliouzoea toka kwake.
 Tusisitize kuwa walimu hawana maslahi ya kutosha, wanakabiliwa na mazingira magumu ya kazi, ukosefu wa huduma muhimu kama nyumba kwa walimu, vitendea kazi kama vile vitabu na mbao vya kutosha ukiachia mbali kutokuwapo motisha. Imefikia mahali eti walimu wanaishi madarasani au vyooni. Hivi kweli hawa wanaweza kuwa na motisha wa kufanya kazi au bora liende? Zamani kazi ya ualimu ilikuwa ni kazi yenye kusakwa na kuheshimiwa sana. Lakini baada ya kuingia sera za siasa za wizi na kutowajibika ambapo watu wachache wanaweza kutumia nafasi zao au jinai kujitajirisha na wasishughulikiwe, hakuna anayetaka kazi ya ualimu tena. Wito wa ualimu umekufa baada ya siasa za kuabudia vitu kukubalika nchini hasa chini ya mazingira ya sasa ambapo ufisadi na uuzaji midarati na ujambazi vinalipa kuliko kazi.
Wanafunzi nao hawana motisha wa kusoma kwa vile kuna njia za mkato –hata kama ni haramu –za kupata ukwasi kirahisi na haraka.  Vijana wengi sasa wanafikiri kuimba rap ili kuukata kuliko kusoma. Hapa unategemea nini?
Viongozi nao hawaongozi kwa mfano. Tunaona viongozi wetu kwenye matamasha ya miziki, semina lakini si kwenye shule au vyuo wakitoa au kushiriki mihadhara kama zamani. Mfano mzuri ni kwamba rais Jakaya Kikwete amekuwa mwepesi wa kuhudhuria misiba, kusafiri je, kukutana na wazee wa Dar es salaam hata makocha wa timu za mpira wa miguu kuliko kutembelea vyuo na kutoa au kushiriki mihadhara. Je hapa motisha kwa vijana utapatikana wapi?
          Nafasi haitoshi. Tatizo la elimu ya Tanzania si jingine bali siasa chafu za kujihudumia zinazosimamiwa na watu wasio na visheni wala uwezo wa kutosha wa kuona mbali zaidi ya usawa wa pua zao na matumbo yap. Hivvyo, kuiboresha hakuwezi kufanywa kwa kuongeza vidato bali kubadili mfumo mzima wa hovyo wa kisiasa unaotupatia viongozi wabovu na wachovu. Kuhusu lugha, hata mkifundisha kwa lugha za makabila yenu, bila kubadili mfumo wa kifisadi na kiherehere yote ni bure.
Chanzo: Tanzania Daima Feb., 25, 2015.
 

Kanji apanga kupeleka toto yake Bombei


          Baada ya waswahili kuanza kuingiza uswahili hata kwenye elimu, Kanji anapanga kuregesha watoto wake Bombay ili wakapate elimu safi warejee huku watawale na kuhomola.
          Si kawaida ya Kanji kuanzisha mjadala. Leo anavunja mwiko huu kwa kuwa wa kwanza kuanzisha jadala.
          Baada ya kupiga kahawa yake anakwanyua mic na kuchonga, “Zee iko sikia hii vatu leta herehere sema eti sasa Sahili tumika sule yote hata Univesiti?”
          Mpemba anadandia, “Kwani kuna ubaya gani kuongeza ujinga juu ya ujinga? Waongelea huu usanii wa juzi wa kuharamisha kimombo kwenda Kiswahili? Kiherehere kitupu kama cha bwana kiherehere mwenyewe anayewashitaki wengine kuwa na kiherehere wakati yeye bingwa.”
          “Kumbe dugu yangu veve jua kuwa sasa ongeza jinga juu jinga. Ukiongeza jinga juu ya jinga napata jinga kuba.” Anacheka na kuendelea, “Veve napanga nini toto yako au vaacha hapa iwe jinga sana?” Kanji anauliza huku akicheka.
          Mpemba anamjibu kwa swali, “Yakhe kwani wewe wapangani na hao watoto wako?”
          Kanji anajibu, “Mimi iko peleka toto vote Bombei. Mimi ona si zuri acha toto haribiva hapa na jinga jinga kuba. Yeye peleka toto yake soma nje nadanganya sisi zani sisi jinga siyo?”
           Msomi aliyekuwa akisikiliza anaamua kutia timu. Anakula mic, “Kanji leo umenifurahisha sana. Naona unaanza kufaidi elimu inayotolewa bure hapa kijiweni. Ni kweli kama ulivyosema ukiongeza ujinga juu ya ujinga unapata ujinga ule ule kama hawa wanavyotaka kuendelea kwageuza wachovu majuha. Hivi kweli kwa ulimwengu wa utandawazi unaweza kufikiri kutumia lugha ndogo kama Kiswahili kufundishia hadi Chuo au choo?”
          Mijjinga anaamua kutuacha hoi.  Anakula mic, “Nilishawaambia mnichague mimi muone elimu yenu itakavyopaa. Sina mchezo na mtu akila kitu kidogo namshushia nyundo kubwa na mambo mswano au vipi? Akighushi mtu natupa lupango bila kumwangalia usoni kama hawa wanaolindana kinyaninyani. Jamani nipeni angalau ubunge muone jimboni kwangu Kisesa.”
          “Nyie mnawashangaa hawa wasanii kupendekeza vitu vya ajabu na kisanii! Wao wanashida gani iwapo wanatumia kodi zenu kupeleka vitegemezi vyao nje vikasome elimu ya maana na kutema umombo kama ndugu yangu Msomi? Hamumuoni mtoto wa mgosi Makambale anavyotaka kugombea urahisi kwa vile amesoma ughaibuni?” Anauliza Mijjinga huku akibofya kisimu chake.
          Leo Kapende kaja na tablet yake. Naona yuko bize nayo kiasi cha kutoshiriki maongezi kama kawaida yake. Si  unajua tena Wachovu akipata kitu kipya lazima awakonge wenzake kinamna.
          Mipawa anaamua kula mic, “Tusipoamka na kuondoa hawa wasanii tutaendelea kuliwa tukijiona. Lazima hawa jamaa wawe wamechanganyikiwa au huenda wanataka kuanzisha shule za English Media na Vyuo vya English Media ili waendelee kupata uchache baada ya kukitoa. Maana haiingii hata akilini.” Mgosi Machungi asivyopenda neno hili, anaamua kula mic haraka haraka, “Kwanza sikuabiani nawe kuwe tinaliwe. Ila nakubaiana nawe mgosi kuwa hawa mafisadi wana ajenda za siri. Kwanza huu ni ujinga sina mfano. Napendekeza titunge sheia ya kuzuia mwanakaya yoyote kupeeka kitegemezi chake kusoma ughaibuni ii tuone kama hawataonja joto ya jiwe.”
          Sofia Lion aka Kanungaembe anaamua kula mic, “Hivi nyie mfanyiwe nini chema ndiyo mshukuru? Hamjui kuwa Kimombo kilikuwa kikifelisha watoto wetu wengi? Sasa mtaona watakavyofaulu hadi muanze kulalamika kuwa wanafaulu sana kiasi cha nyinyi kuonekana hamkuwa na akili shuleni.”
          “Sofi angalia lugha hiyo tusikosane bure,” Mzee Maneno anamtahadharisha Sofi baada ya kuona anavuka mipaka.
          “Acheni uvivu wa kufikiri. Kwani hicho Kimakonde mmeelezewa kitakavyofanya wasomi washinde au mnakariri maneno yao kama kasuku? Nadhani kianchofanyika hapa ni kutapatapa. Bila kuwekeza kwenye elimu hata mkifundisha kwa lugha ya malaika mtafelisha. Njuluku mnaiba na akina escrow na kuwekeza kiduchu kwenye elimu halafu mnategemea mfanye vizuri siyo?” Kapende anaamua kujibu hoja ya Sofi.
          Msomi anarejea, “Kapende umeongea utadhani umesoma mawazo yangu. Niongezee hapo. Hivi unategemea ufaulu uongezeke bila kuongeza marupurupu na mishahara ya wala chaki? Mishahara yenyewe mnawakopa huku wengine wakiishi vyooni. Hivi mwalimu anayelala chooni anaweza kuwa na akili ya kufundisha wenzake kweli? Maprofesa wamevamia siasa mnategemea Vyuoni wasifelishane? Rushwa hadi za ngoni zimeshika kani mnategemea nini? Usanii umegeuka dili ya kuukatia huku mihadarati na ujambazi na ufisadi ukipanda chati mnategemea kuwe na motisha hasa kwa watoto kusoma kweli?”
          Anachukua leso yake na kujifuta jasho na kuendelea, “Kwanini hawataki kuangalia ukweli machoni? Nadhani sababu ya kutofanya vizuri ukiachia mbali bajeti kidogo na kusahaulika kwa sekta ya elimu ni kutamalaki kwa jinai kama vile kughushi vyeti, ufisadi, ujambazi wa kalamu na wa silaha, viongozi kutokaa maofisini wakashikilia kuzurura wakifuja njuluku ambayo ingepelekwa kwenye elimu. Hivi unategemea nini kama wakubwa wenyewe ni vilaza na vihiyo watupu? Hebu angalia viongozi wa kwa akina Joji Kichaka wanavyoandika vitabu. Hapa ukiondoa gweiji Mchonga nani amewahi kuandika kitabu zaidi ya wengine kuandikiwa utadhani maiti au kuokoteza hotuba?”
          Mbwamwitu anaamua kumchomekea, “Hili la maprofwedha kuvamia siasa limenikumbusha maprofedheha kama Anna Kajuamlo Tiba, Saucepie Muongo, J4 Majembe, Jimmy Kapuyanga na madaktari uchwara kama Shchool Kawa-dog wanaoendelea kuvurunda utadhani hawakwenda shule.”
          Kijiwe kikiwa kinanoga si akapita muuza vitabu akiuza kamusi za kimombo!
Chanzo: Tanzania Daima Feb., 24, 2015.

Kupambana na ufisadi,Takukuru na wimbo wa jogoo

      
    Jogoo ni ndege mbabe afugwaye tena wa kuhurumiwa. Anasifika kwa kuwanyanyasa majike na vifaranga huku naye akinyanyaswa na aliyemfuga. Pia ndege huyu shaufu lakini dhaifu husifika kwa kupenda kuimba. Hata hivyo, ana kasoro moja kuu, huimba wimbo ule ule kila uchao miaka nenda miaka rudi. Ni ndege asiye na ubunifu wala kumbukumbu wala asiyejali alama za nyakati. Kwani hufikia mahali akachinjwa hata baada ya kushuhudia wageni wakija nyumbani akijua fika lazima atatolewa kafara kwao. Ya jogoo tuyaache.
 Hivi karibu Tume ya Kupambana na Kudhibiti Rushwa (TAKUKURU) ilijivuvumua kwa kusema eti itawashughulikia watuhimiwa wakuu wa wizi wa escrow ambao umezamisha mabilioni ya fedha za umma huku ukiwagusa na kuwaondoa vigogo wengi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mkurugenzi wa Takukuru Dk Edward Hosea alikaririwa na vyombo vya habari hivi karibuni akisema, “Tunawachunguza wote, hatuwezi kufanya kazi harakaharaka kama zimamoto, tunakwenda hatua kwa hatua, uchunguzi ukikamilika wote watakaopatikana na hatia watapelekwa mahakamani.” Kuchunguza ni jambo moja na kuja na matokeo tarajiwa ni jambo jingine. Kwa wanaokumbuka jinsi Takukuru hii hii ilivyotaka kumsafisha waziri mkuu za zamani aliyetimka kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa, hawana imani nayo tena. Kwani licha ya kuwa idara nyeti lakini dhaifu, Takukuru imegeuka shahidi wa jinai nyingi nchini hasa zinazohusisha wizi wa fedha nyingi za umma. Rejea kwa Takukuru kushindwa kuwakamata majambazi wa wizi mwingine wa mabilioni wa EPA, RITES, Meremeta, Mwananchi Gold, orodha inachosha. Je ni kitu gani Takukuru watafanya tofauti na walivyozoea?
Wapo wanaoona kama hakuna jipya na kauli ya Takukuru ni ya kujivuvumua na ya kisiasa zaidi ya kitaaluma.  Takukuru wanaweza kujipiga kifua na kuapa kwa miungu yote kuwa watashughulikia kashfa ya escrow ili kujenga picha kuwa serikali inafanya kazi na inapambana na ufisadi.kimsingi, tamko hili laweza kuwa la kisiasa hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu. Timming ya Takukuru ni nzuri hasa ikilenga kuwaingiza mkenge wananchi hasa wapiga kura kuihukumu vizuri serikali yao. Kesho kesho utawasikia viongozi wa CCM wakijisifu kuwa wanapambana na ufisadi na wanaweza hata kunukuu au kunasibisha maneno yao na ya mkurugenzi wa Takukuru. Baada ya uchaguzi? Kila kitu kitafutikwa chini ya busati kama ilivyotokea kwa Kagoda na wizi mwingine na tunaendelea na business as usual.
Takukuru wamefanya nini kuwachunguza na hata kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wezi katika serikali za mitaa ambao wanasifika kuzamisha fedha nyingi kila mwaka kuanzia kulipa mishahara hewa na kupandisha gharama za miradi? Takukuru imefanya nini kupambana na majangili wa kimfumo waliosafirisha wanyama wetu tena hai nje?
Tokana na historia ya utendaji tata na wa shaka ya Takukukru, wengi wanadhani hiki kinachoitwa kuchunguza wezi wa escrow ni wimbo ule ule wa jogoo. Kuna maswali mengi ya msingi ya kuulilza: Hadi wanafikia hapo walipo Takukuru mlikuwa wapi kama siyo kutumika na kuwatumikia mafisadi waliowateua. Fanyeni kama mwendesha mashtaka wa Argentina ambaye hata kama aliuawa ilikutwa hati ya kutaka kumkamata rais wa nchi bila kujali ukubwa wa cheo chake. Umma umechoshwa na Takukuru kuonekana kama nyumba ndogo ya CCM na mafisadi. Rejea CCM ilivyohusishwa na wizi wa EPA na hakuna kigogo hata mmoja aliyehata hojiwa. Rejea expose ya mwanasheria Michael Bhyndika Sanze aliyesimamia wizi huo aliyekiri baadaye. Takukuru ilishindwa hata kumhoji na kuchukua maelezo Sanze, pamoja na kukiri kushiriki kikamilifu kwenye wizi wa EPA.
Hata hivyo, wangewezaje kuchunguza wizi wa EPA wakati uliwahusisha wale wale waliowateua wakuu wa Takukuru? Hata maafisa wengi wa Takukuru ni mafisadi wenye utajiri wa kutisha utokanao na rushwa. Takukuru walishindwa hata kuchunguza ajira ya Salva Rweyemamu aliyewahi kupewa kazi ya kuisafisha Richmond ukiachia mbali ajira yake kuonyesha mazingira yote ya rushwa hasa kutumika kuwachafua wagombea wa urais walioonekana tishio kwa mtu wake mwaka 2005.  
Ukitaka kuonyesha madudu ya Takukuru utajaza msahafu hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania inaweza kuwa mojawapo ya nchi inayoongoza kwa kuwa na kashfa nyingi za wizi wa fedha za umma huku wezi wanaoufanya huu wizi wakiendelea kuwa watu wa heshima mitaani. Wako wapi wezi waliotajwa wazi wazi wa kampuni ya Kagoda iliyotumika kwenye uhamishaji wa fedha za EPA? Si leo tunaambiwa ni miongoni mwa mabilionea waliozalishwa na taifa hili linaloabudia mibaka huku likiwachoma moto vibaka.
Tumalizie kwa kuwashauri Takukuru waachane na wimbo wa jogoo. Badala yake wafanye kazi kama wanavyopaswa au wajinyamazie kama hawana la kusema kuliko kuendelea kutupotezea muda. Wananchi wasingetaka kusikia tambo bali kuwaona wahusika wakiburuzwa mahakamani hasa kutokana na ukweli kuwa kutimliwa kwa baadhi ya watendaji wa serikali ni ushahidi tosha kuwa jinai ilitendeka na walioitenda wanafahamika kwa sura na hata majina yao. Wahenga walisema: Ada ya mja kunena muungwana ni kitendo. Tendeni basi badala ya kuimba wimbo ule ule na kufanya mambo yale yale kwa namna ile ile mkitegemea matokea tofauti. Huu waingereza huuita wehu.
Chanzo: Dira.

Monday 23 February 2015

Siku mfalme Kikwete akiondoka Prince Riz atakuwa mgeni wa nani?


Siku hizi kujikomba kwa Kikwete imekuwa fasheni au tuseme njia ya kujihakikishia kuendelea kwenye ulaji. Hapa Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Tuvako Manongi na  naibu wake Ramadhani Mwinyi wakipiga picha na mwana wa mfalme aliyekwenda kuwakagua jijini New York hivi karibuni.

TAKUKURU inapopambana na rushwa kwa kuishiriki

 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupamba na Kushiriki Rushwa (TAKUKURU) nchini Dk Edward Hosea

          Taarifa ya Afrobarometer, taasisi inayotathimini viwango vya rushwa nchini kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  ni moja ya taasisi kumi zilizotajwa kuongoza katika kuomba na kupokea rushwa zinasikitisha na kuondoa maana nzima ya uwepo wa taasisi hii. Kabla ya kufichuliwa, wengi tuliiamini na kuiasa ipambane na ufisadi mbali mbali tusijue kuwa nayo imo!
          Wengi walidhani kuwa TAKUKURU ilipaswa kujikita kwenye kupambana na kuzuia rushwa. Kumbe si hivyo, inashiriki vilivyo jinai iliyoanzishwa kupambana nayo. Huu ni ushahidi wa mfumo mbovu wa kifisadi uliotamalaki kuozoeleka, na kwa kiasi fulani, kuanza kukubaliwa na wakubwa tokana na kutamalaki. Inashangaza maafisa wa TAKUKURU wanalipwa kwa kazi gani iwapo ni washiriki wazuri wa rushwa. Kwa mujibu wa Afrobarometer,iliyoshirikiana na Repoa kwenye utafiti huu, TAKUKURU inashika namba ya pili baada ya polisi kwa kudai na kupokea rushwa nchini. Taarifa ya Afrobarometer  inabainisha, “Utafiti umebaini kuwa polisi ni vinara wa rushwa kwa asilimia 50, wakifuatiwa na maofisa wa TRA (37), Majaji na Mahakimu (36), Takukuru (29), Maofisa wa serikali za mitaa (25), watumishi wa umma (25), wabunge (22) na rais na maofisa wa Ikulu (14). Alisema pamoja na ongezeko hilo, wananchi hawaridhiki na juhudi za serikali katika kushughulikia rushwa.” Kwa kushika nafasi ya pili ni kwamba TAKUKURU imekiuka malengo ya uwepo wake ukiachia mbali kuchangia vilivyo katika kuongezeka kwa jinai inayopaswa kupambana nayo na kuizuia. Hii maana yake ni kwamba tumewapa wezi kulinda benki au duka. Je tutegemee nini? Je nini kifanyike kuondokana na kadhia hii?
          Kimsingi, mfumo wa sasa unaifanya TAKUKURU kuwa chombo cha kula rushwa badala ya kupambana nayo. Inaipamba rushwa badala ya kuizuia. Kitendo cha kuiweka TAKUKURU chini ya ofisi ya rais kinazusha shaka juu ya uhuru wake katika utendaji wake. Tujalie kuwa rais au jamaa zake wanatuhumiwa kupokea rushwa, unategemea iwashughulikie wakati inapokea amri toka kwa rais mwenyewe? Nadhani hii ndiyo maana marafiki wengi wa wakubwa wanaotuhumiwa wazi wazi kwa rushwa hawakamatwi wala kuchunguzwa. Tumeyaona na tunayajua. Wako wapi watuhumiwa wakuu wa wizi wa mabilioni ya fedha za umma chini ya kashfa ya escrow? Ilifikia hata kuwawajibisha baadhi ya mawaziri ilikuwa ni mbinde baada ya rais kuonyesha wazi kutokuwa na nia wala utashi wa kuwashughulikia hadi umma ulipokuja juu kiasi cha hali kutovumilika ndipo wakaachia ngazi. Rejea kuendelea kulipwa kwa marupurupu ya kustaafu kwa waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyeachia ngazi tokana na kubainika kuwa nyuma ya kashfa ya Richmond mwaka 2008 ambapo alidai bayana kuwa alikuwa akiripoti kwa rais kila hatua iliyokuwa ikichukuliwa. Hii maana yake ni kwamba rais alikuwa akijua na alishiriki.
          TAKURURU imeonyesha – tena tangu zamani – ilivyo chombo cha kula rushwa pale ilipotaka kumsafisha Lowassa bila mafanikio baada ya umma kuja juu hasa bunge la Jamhuri ya Muungano kuunda tume iliyomng’oa madarakani. Kwa wanaokumbuka maneno ya rais wakati akikubali Lowassa kuachia ngazi, wanajua kilichokuwa kikiendelea angalau kwa ushahidi wa kimazingira.
          Watanzania wanajua kuwa TAKUKURU imekuwa ikiwakamata dagaa huku mapapa ikila nao meza moja ili kujionyesha kuwa inafanya kazi.  Imekuwa ikikamata makarani, mahakimu wa ngazi za chini, walimu, manesi na wafanyakazi wadogo wadogo huku ikiendelea kuwafumbia macho mapapa. Uliza ni majaji wangapi wamekamatwa kwa kula rushwa. Hata hawa waliotajwa wazi wazi kupokea fedha toka kwa mtuhumiwa mkuu wa escrow bado wako kazini huku serikali ikikaa kimya kutaka mambo yapoe waendelee na mchezo kama kawaida. Namna hii hatuwezi kuishinda vita dhidi ya rushwa, na kushindwa huku ni maafa kwa uchumi wa taifa letu. Mfano mwingine wa karibuni ni kutajwa kuwa baadhi ya vigogo wameficha mabilioni ya shilingi kwenye mabenki ya Uswisi na kwingineko ughaibuni. Pamoja na serikali ya Uswisi kuahidi kutoa ushirikiano, hakuna aliyejihangaisha kutafuta huu usaidizi ili kuwabaini na kuwashughulikia waliotorosha hii pesa na kuirejesha. Nani amkamate nani iwapo kambale wote wana sharubu? Mifano ni mingi tu.
          Mbali na kuiondoa TAKUKURU chini ya ofisi ya rais, inapaswa kufumuliwa na kusukwa upya chini ya utaratibu mpya ambao utawachuja na kuwachunguza maafisi wake. Hapa ndipo haja ya kurejesha sheria ya maadili unapoonekana. Kwani kwa sasa katika Tanzania mtu yeyote anaweza kulala maskini akaamuka tajiri na asishughulikiwe wala kuhojiwa alivyopata huu utajiri wa ghafla bin vu. Watu wanashiriki vitendo vya jinai kuanzia kula rushwa, kuuza mihadarati, ujambazi na wizi wa mabilioni ya umma bila wasi wasi kutokana na sababu kuu mbili yaani kutokuwapo sheria inayowabana na kuwataka wataje mali zao na kueleza walivyozipata. Pili ni ile hali ya taasisi husika kuwa kinara wa rushwa ambayo kimsingi, ni mama wa jinai zote. Jambazi mkubwa anakamatwa anatoa rushwa na kuendelea na mchezo kama kawaida. Mla rushwa anabanwa anatoa chochote na mchezo wa “tua tugawane” unaendelea.
          Kwa sasa, kwa mfano, kuna haja ya kuwachunguza maafisa na watumishi waote wa taasisi zilizotajwa kuongoza katika rushwa ili kujua wana ukwasi kiasi gani na wameupata vipi. Si ajabu ukakuta maafisa wengi wa TAKUKURU ni matajiri wa kutupwa kwa vile wanatumia nafasi zao kujineemesha kwa kupokea rushwa waliyoapa na kuajiriwa kupambana nayo. Hawa wanapaswa kuchuguzwa kwanza na kuamriwa wataje mali zao na jinsi walivyozipata. Hata hivyo, hili linakuwa gumu kidogo hasa ikizingatiwa kuwa hao wakubwa waaopaswa kuamrisha uchunguzi huu wameshika na kigugumizi wanapotakiwa kutaja mali zao. Kuna haja ya kuwa na tume huru ya kukagua taasisi nyingine za serikali kuhusiana na utendaji wake kwa kushirikiana na ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) ambayo imefichua uoza mwingi bila kushughulikiwa.
Chanzo: Dira.

Hii nayo imekaaje?




Inaonekana rais Jakaya Kikwete anazidi kuendelea kufungwa mdomo. Maana haongelei lolote kuhusiana na matatizo ya nchi kama vile kuletwa kwa upuuzi unaoitwa sera mpya ya elimu ambayo ni mauti kwa taifa letu. Inaonekana jamaa kachoka akingoja amalize ngwe yake na kutokomea atokomeako.

Sunday 22 February 2015

UDA rip-off: Who’d we believe?

Picture
          By the look of things, Usafiri Dar si-Salama aka UDA is under a cloud after being grabbed dubiously in a deal that keeps on backfiring. There have been many exchanges of fires between those who portend to own UDA after “buying” it and those who say they’ve nary sold anything. Recently, Dar Mayor, Diddie Masaburi was quoted as saying, “It’s not true that we have sold all our shares to Simon Group. I’m ready to step down if anyone will prove beyond any reasonable doubt that all UDA shares have been sold to Simon Group.” Masaburi isn't a freak to swear by all gods without being sure of what he’s saying. If he were jesting or threatening, UDA would have tasked him to prove his point. Or they’d have sued for redress. Again, they kept mom to show that what Masaburi said is true, and only the truth. Keeping mum on Masaburi’s assertion’s all hallmarks of truth. Instead of refuting the claims, Shimoni Group has made all-out efforts to make us believe it bought UDA while it actually grabbed it thanks to Masaburi’s revelation. Again, who’d we believe?
           Another bigwig who weighed is none other than Joni Mnyika the Heshihmiwa for Ubungo who's quoted as saying, “The government itself and CAG have admitted that procedures were not followed, and as we speak the Simon Group still runs the UDA, why is the government allowing this investor to continue managing UDA?” what a nice and provocative question! Did they answer? Will they answer? Wait. Maybe, just maybe, they’ll answer when Jesus comes again to show who grabbed UDA and who offered it after being induced with dosh. Again, given this is Bongolalaland aka shamba la bibi, those grabbers may get away with murder as boozers stay side and look as if this property isn't theirs.
Those two quotes above can tell you where the truth stands. You don’t need to be a rocket scientist to see this. Again, those behind this crime-cum-scandal still think that Bongolalalanders are mere dum-dum they can take for ride by robbing them wantonly.  If boozers and Bongolalalanders are going enjoying their slumber, they’re indeed finished! Amkeni mwaliwa folks. For how long will you endure such malingering behaviour as if you’re tabula lasa? We need to be vigilant to see to it that UDA amoral dealings are brought to the agora so that we can decide if deception and horse trading are not involved in this murky thing.
          Looking at two quotations from an MP and a mayor, I see red, and wish all boozers would see it in the same light so as to –after being provoked – they can unflinchingly decide to claim back their property. How do we allow rip-offs and swindlers, filches and stinking gang honchos to rob us wantonly this way? According to the words of two heshimiwas, UDA is still boozers’ property. This conning Shimoni Group needs to be kicked out of our property. Again, looking at how meanders have been cut for long, there seems to be a top dog behind this phoney company.  We’d not allow such swindlers hiding behind spineless companies and name to take us shimoni as they name indicate.
          The other day I heard one humanoid employed by UDA saying that those who oppose this crime don’t like wazawa.  Wazawa unawajua or you simply use the word uzawa to fill your thankless tummy? The mistake such goons make is reading boozers’ minds.  How can we love wazawa more than we love ourselves? Even those who defend UdA are doing so not for the love of it but the love of their personal interests. Again, those they dupe (their employers such as UDA) think that they’re doing their job while they’re but duping them the way they want to dupe boozers. Who cares if the thief is mzawa or mgeni? A crook is a crook regardless of his genealogy. I don’t pay any hoot once my dosh is stolen in my house. If the robber is my son or neighbour’s one, I just treat them the same. To me, Chavda is as evil as Rugemalayer is. Seth SingEscrow is as evil as Mzee wa Vijisenti is. A criminal is a criminal. So, those depending on uzawa to seek our mercy should find another way to please their masters. Who cares if the skyjacker’s mzawa or  mgeni?
          Folks, given that my sacred duty is telling you where things are going awry, mine ends up here as I wait to see what’ll your reaction be. Again, whom are we waiting while everything is on the agora that our firm has been grabbed? As for wazawa and Shimoni Group, go tell it to the birds. According to the two big wheels quoted above, UdA is still ours. Whatever Shimoni Group say to justify their crime won’t hold any water up till they prove those big guns wrong.

Hosta luego gente!
Source: Guardian Feb., 22, 2015.

Saturday 21 February 2015

'Njooni niwatungie vitabu niwasifu mshinde kiulaini'


Mwenzenu leo nina furaha ajuaye ni Mungu na bi mkubwa wangu ambaye kama mpango huu utajipa lazima ajinome kama hana akili nzuri au vipi? Nina dili bab kubwa. Naona yule anatoa mimacho akidhani dili hii ni escrow au kupiga njuluku kwenye uchakachakachuaji wa katiba mpya. Ungejua mimi si fisadi wala jambazi wa kutumia kalamu, usingefikia hitimisho hili. Hata hivyo, si makosa yako. Makosa ni ya mfumo unaotengeneza ngurumbili wanaoamini kuwa kufanikiwa lazima kuwa kupitia wizi na ufisadi badala ya kuchangamkia  ntchito.
          Basi mwenzeni ni mbunifu wa kupigiwa mfano. Na karibuni nitaukata bila kuwaibia wachovu wala walevi kama wale. Nina mpango wa kuanzisha kampuni ya kuwatungia vitabu vya sifa wagombea urahisi hata ubuge kayani. Sichagui chama wala itikadi. Ni pochi yako tu. Huna haja ya kwenda Bagamoyo au Sumbawanga kuroga.  
          Najua kaya yetu imetwaliwa na kutawaliwa na mazingira ya mazingara karibu katika kila kitu. Wengi wa wachovu na wavivu wa kujituma na kufikiri hufikiri kuwa mja hawezi kufanikiwa bila kufanya ushirikina. Njoo kwangu nikuwezeshe uukwae hata kama utanisahau. Muhimu ni kukatiana mapema kabla ya kuingia kwenye mjengo au jumba la ulaji almaaruf ikulu. Inashangaza kuona jitu zima na akili yake eti linakwenda kwa mganga njaa kihiyo kutafuta dawa ya kushinda mtihani wakati mganganjaa mwenyewe hata hajui kusoma na kuandika na kama amesoma hajavuta madarasa. Wengine eti wanakwenda kutafuta utajiri kwa wezi wanaowatoza fedha huku wao wakiwa wananuka umaskini. Wangekuwa wanajua dawa ya utajiri si wangejitajirisha wao kwanza kabla ya kuwatajirisha wengine. Wanawapa dawa ya utajiri au ujinga na ufukara? Mtaishia kuwamaliza zeruzeru na vikongwe na kufia gerezani msitajirike msipobadilika.
          Kwa wale wanaoamini katika ushirikina mmekishwa. Mtatapeliwa na kuliwa bure muishie kulalamika bila sababu wakati kiboko ya ushindi nipo naita kwa wenye mshiko waje tushikishane na mambo yaende bien au vipi? Au mnataka nitangaze neema hii kwenye magazeti na runinga ndiyo mjue nafanya kweli? Njoo nikutungie kitabu watu wakusome na kukupenda hata kama wabongo si wasomaji wa vitabu. Hata ukiamua kujihoji na kujijibu wewe njoo unipe uchache wangu ubandike jina langu kuwa mimi ndiye nilikuhoji hata kama ukweli ni kwamba ulijihoji na kujijibu kama wale ninaoanza kuwastukia.
          Njoo unikodishe nikuandikie makala za kuimba sifa zako na kukumwagia sifa kemkem ili watu wakupende na kukupa kura ya kula. Nitakutungia hata zaburi na mashairi, ngonjera na tenzi kuhakikisha kila mtu anakupenda na kukupa ulaji. Nitaipamba na kurembesha sura yako hata kama ina namna hadi kila mtu akukubali kuwa wewe ni handsome and flamboyant. Hivyo, akupe ulaji. Nitakupamba kuwa wewe ni chaguo la Mungu, watu, miti, wadudu hata wanyama.  Kazi hii ninayopanga kufanya imeishafanyiwa majaribio na magwiji kama vile Silvia Rweyempendeza. Mara hii mmesahau akina Rweyependekeza waliopewa ulaji ikuu na ukuu wa wilaya siyo?
          Mie sihitaji kazi zenu wala kulipwa fadhila zaidi ya kunikatia mshiko wangu kila mtu anakwenda zake kivyake. Ukipata au kupatikana tusilaumiane ati. Nitakutungia vitabu na mashairi na nyimbo vinavyoingia akilini ili hata ukidondoka angalau uwe na cha kujisomea. Mie siyo kama wale kasuku mfano Bangendagenda aliyeandika upuuzi kibao akijigonga kwa Njaa Kaya akitegemea kupewa ubalozi akaishia kuvishwa mkenge aliotaka kumtwisha msanii mkuu. Mie naandika vitu vilivyokwenda chuo vyenye kuwavuta hata nyoka watoke pangoni. Naandika nyimbo ambazo hata nyuki na nyoka wakizikia wanafurahi na kuweka mbali sumu na ukali wao. Njoo kwangu niwapeni ulaji, urahisi hata ukubwa wa kila aina. Mimi ni kiboko wa Bagamoyo na Sumbawanga. Huna haja ya kunyotoa roho za mazeruzeru wala kutembea uchi au kubakwa na waganga ndiyo upate huo ulaji. We njoo kwangu nitayamaliza matatizo yako.
           Tuache utani. Hakika huu ni wakati wa kukwapuana. Mwanasiasa anawakwapua wapiga kura na wachovu
 Mwanasiasa naye anakwapuliwa na wauza maneno. Unamkwapua huyu naye anamkwapua yule mradi mkwapuano ngoma droo au vipi? Hii ndiyo Bongo kaya ya wasanii.
          Uhitaji kuwa na kijana kama hawa wanaotumia ujana wao kama silaha dhidi ya vikongwe. Mie nitakuweka mkorogo wa kimaandishi na wachovu watakuzimii. Nitasema wewe ni kijana wa miaka 99. Hapa lazima nipandishe na kubadilisha namna ya kuangalia umri wa mtu. Kwa vile kuna imani kuwa maisha huanzia miaka 50, hivyo ukiwa na miaka 99 utakuwa sawa na mtu mwenye miaka 40 na ushei. Hujawa kijana hapa? Ili kuwatibulia ulaji hawa vijana wanaojiletaleta wakati hawana uzoefu zaidi ya uchu na uroho wa madaraka, nitawaita vichanga ambavyo vinapaswa kuwa kwenye shule za vidudu kisiasa na si kwenye ulingo au vipi? Wale wenye mvi nitabadilisha maana ya mvi na kuziita busara hata kama ni mafisi na mafisadi who cares kama nitapata mshiko wangu?
          Eneo jingine nyeti linalohangaisha watu hadi wakaghushi na wengine kupata shahada kwa kuvua nonihino. Elimu, elimu, elimu. Uhitaji kuwa na PhD na makandokando mengine. Hata kama wewe ni kihiyo au mgonjwa hata wa miwaya wewe niachie mimi nitajua jinsi ya kukujenga. Hata kama u fisadi au kibaraka wao wewe niachie mimi.
          Kama wewe ni kibabu nitakupamba uonekane kijana hata kwa kubadili maana ya ujana kama ilivyokuwa mwaka 2005. Mara hii mmesahau jinsi vibabu vilivyoitwa vijana!
Chanzo: Nipashe Feb., 21, 2015.