How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Friday, 20 February 2015
Mtesi wa Ulimboka anapozawadiwa ubalozi Kanada!
Rais Jakaya Kikwete ataingia kwenye vitabu vya historia kama rais wa hovyo ambaye Tanzania haijawahi, na saa nyingine, hatawahi kupata. Hivi karibuni alimteua afisa usalama aliyetuhumiwa kumtesa Dk Steven Ulimboka, Jack Mugendi Zoka kuwa balozi nchini Kanada.Ni aibu namna gani kwa mhalifu kama huyu kupewa ubalozi? Kama haitoshi, juzi kamteua Paulo Makonda kuwa mkuu wa wilaya wakati anafahamika alivyomfanyia fujo jaji Joseph Warioba. Kama haitoshi aliongezea na uteuzi wa mtangazaji Shaaban Kisu wa TBC na afisa mwandamizi wa zamani wa jeshi la polisi Zelote Stephen kuwa wakuu wa wilaya licha ya manung'uniko mengi toka kwa wananchi kuhusiana na kutokuwa na sifa wala udhu kwa wateule hawa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
4 comments:
Kitu cha mwisho nilichosikia kuhusu kesi ya Dr. Ulimboka ni kuwa polisi walikuwa wamemkamata m-Kenya fulani kwamba ndiye mhusika. Tangu pale sijasikia tena kesi iliendeleaje. Naona ni kitendawili. Na sijui hatima ya ule mgomo wa madaktari, mgomo ambao madhumuni yake yalivyokuwa yanaelezwa na madaktari wenyewe yalikuwa yanapotoshwa kwa makusudi na serikali ya CCM.
Hakuna Mtuhumiwa katika magwiji ya uahalifu wenye title ya Mh...
Kaka Mbele, taarifa nilizo nazo ni kwamba yule mkenya alikuwa framed na baadaye aliachiwa kutokana na kukosekana ushahidi. Walimtumia ili kuepuka aibu. Huenda walimkatia chochote kitu kuficha uoza wao. Madaktari walisambaratishwa na kusalitiana kiasi cha kumtoa sadaka Dk Ulimboka. CCM imeonyesha wazi ilivyo Chama Cha Mafia kinachoburuza taifa letu kipendavyo. Taarifa nilizo nazo nik wamba kijana Magoba aliyefichua uoza kwenye mradi wa JKT amefanyiwa unyama kama aliofanyiwa Ulimboka na Kibanda. Ni nchi ya hovyo baaada ya kutawaliwa na wapuuzi na vilaza wapenda sifa wakati hawana hizo sifa. Unakuwa na jitu linalodanganywa kirahisi na kupewa udaktari na uprofesa feki linashangilia unategemea nini? Tuombe rais ajaye awe mtu mwenye maono na si huu upuuzi uliopo.
Anon, nimependa title yako ya mh yaani mhalifu.

Post a Comment