Magufulification: Concept That Will Define Africa's Future and the Man Who Makes Things Happen

Magufulification: Concept That Will Define Africa's Future and the Man Who Makes Things Happen

Thursday, 28 October 2010

Chonde chonde CCM, damu mliyomwaga inatoshaCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kupitia mgombea wake wa urais na wapambe zake, waliposema kuna njama za Watanzania kumwaga damu, wengi hawakuwabana wawataje wahusika.

Wao (CCM) walilenga kuuchafua upinzani kutokana na sera kuu ya CCM kwenye kampeni zinazomalizika kwa kuchafuana. Bahati nzuri ni kwamba Mungu huwa hamfichi mnafiki. Kwa yaliyoripotiwa hivi karibuni kutendwa na mashabiki wa CCM, Mungu amewafichua. Watawambia nini watanzania waliowahadaa kwa kuwasingizia wenzao?

Kwa wanaojua mizengwe ya CCM, walijua walichokuwa wakimaanisha wakubwa hawa wa CCM. Walimaanisha tofauti na walivyosema kama kawaida yao. Rejea madai mengi dhidi ya kuondoa kero mbali na kutoa ahadi nyingi ambazo ziligeuka kuwa usanii. Walitumia mbinu ambayo wazungu huita pre-emptive method wasijue yatawarudi!

Hii imekuwa sawa na walivyowahadaa watanzania kuwa watapambana na mafisadi wakaishia kuwapamba, kuleta maendeleo wakaishia kuleta maanguko na ufisadi. Rejea hatua ya wazi ya Kikwete kusimama bila aibu kuwapigia kampeni watuhumiwa wakuu wa ufisadi wa mabilioni yaliyowaacha Watanzania maskini. Hapa hujaongelea matumizi mabaya ya fedha na raslimali za umma.

Sasa hayawi hayawi huwa! CCM imekamatwa red handed ikitekeleza kile vigogo wake walichojifanya kulaani! Kumbe danganya toto!

Mara kadhaa Kikwete amenukuliwa akisema: “Sisi ni CCM. Sisi ni chama kisichohubiri umwagaji damu. Sisi ni chama cha amani. Umwagaji damu hauna maslahi yoyote na wala tija kwa yoyote isipokuwa kwa wanasiasa wanaotaka kutumia maiti za watu kama ngazi ya kuingilia Ikulu.”

Je, kweli CCM ni chama cha amani au vurugu? Inakuwaje kama ni chama cha amani kisilaani vitisho vilivyotolewa hivi karibuni na mnadhimu mkuu wa jeshi ukiachia mbali mganga na mtabiri wake, Yahya Hussein? Inakuwaje kisizuie vikundi vyake vya kigaidi vya Green Guard kuwakata watu wasio na hatia mapanga? Amani gani ndani ya migawanyiko, vurugu, rushwa, ukosefu wa haki, ufisadi na mitandao?

Baada ya kugundua uzushi wa CCM mpinzani wao mkuu kwenye mbio hizi CHADEMA walikaririwa wakisema: “Mimi sitaki kwenda Ikulu kwa kumwaga damu ya Mtanzania yeyote. Sijatamka hata siku moja kumwaga damu. Nataka uchaguzi wa amani na utulivu. Katika mikutano yangu zaidi ya 400 niliyofanya sasa, nimehimiza watu wangu kuzingatia amani…Nyie mkipigwa shavu hili geuza jingine, msiwe chanzo cha vurugu,” alikaririwa mgombea wa CHADEMA wa uraia Dk. Willibrod Slaa akisema.

Hata hivyo kuna maswali muhimu ya kujiuliza juu ya nani yuko tayari kumwaga damu. Nani anamiliki vyombo vya dola vinavyoweza kusababisha umwagaji damu zaidi ya serikali?

Maana tuliona kenya. Watu wengi waliouawa wanasemekana waliuawa na Jeshi la Polisi kutokana na amri za wakubwa wao. Hata yale mauaji yalilitia doa jina la Tanzania ya Zanzibar, walioua ni polisi na si wanasiasa wa upinzani.

Pia ikizingatiwa kuwa taarifa zote za usalama zimo mikononi mwa serikali, inashangaza kuona serikali haiwashughulikii hawa wabaya wa taifa. Lakini nani atawashughulikia iwapo wanatekeleza amri za wenye serikali yenyewe?

Yaliyojitokeza kwenye Jimbo la Musoma na Maswa hivi karibuni ni ushahidi kuwa watuhumiwa waliokuwa wakitajwa na CCM kumbe ni CCM wenyewe. Rejea watu kadhaa wa wakazi wa Kigera Musoma kukatwa katwa mapanga na wafuasi wa CCM maarufu kama Green Guards.

Waliokumbwa na mkasa huu walitajwa kama Suleman Mwita ambaye alidai kuwa viongozi wa CCM tawini Kigera walisimamia unyama huu. Ajabu CHADEMA wanaodaiwa kumwaga damu ndiyo wamethibitisha kuwa waokozi. Maana Mwita alikaririwa akisema: “Wakati nikiokolewa na wananchi kidogo likatokea gari la mgombea wa CHADEMA, Vincent Nyerere, ambalo lilinichukua na kunipeleka polisi kupata fomu namba tatu ya polisi kisha kunipeleka hospitalini.”

Mwingine aliyeathirika na vurugu hizi ni mtoto Rahab Malima (15) ambaye kosa lake ni kuzaliwa na mama Tatu William aliyeruhusu bendera ya CHADEMA kupepea nyumbani kwake. Kosa la kupeperusha bendera ya CHADEMA limesababisha Rahab kukatwa vidole vya mkono wa kulia!

Mbali na watajwa hapo juu, wengine waliojeruhiwa ni Kapuru Charles (44) na Mapambano Malima (30) wote wakazi wa Kigera. Bahati nzuri CCM haikukanusha habari husika ukiachia mbali na nyingine kama hii iliyoripoti wana CCM kufanya mashambulizi ya umwagaji damu kule Busanda mnamo mwenzi wa tisa.

Kwanini wahusika hawakamatwi? Hili ni swali litakalokuwa likiwahangaisha wengi. Jibu wanalo Charles Kayele, Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Musoma na mgombea ubungu wa CHADEMA, Vincent Nyerere waliokaririwa wakisema kuwa vyombo vya dola vimekuwa vikifumbia macho malalamiko dhidi ya CCM.

Katibu wa CCM wa Wilaya ya Musoma Haula Kachwamba, alipotakiwa kuelezea malalamiko dhidi ya chama chake alisema hana, kwa vile suala hili lilikuwa la polisi!

Hapo juu ni tukio moja kwenye eneo moja. Yapo mengi mengine kama haya. Nani mara hii kasahau unyama uliofanyika jimboni Busanda au Hai bila kusahau vurugu na vitimbwi huko Arusha?

Inabidi umma uibane CCM iache kumwaga damu. Damu haina uchache wala wingi zaidi ya kuwa damu. Tone moja la damu ya Mtanzania ni sawa na damu ya Watanzania wote.

CCM imeisharidhia umwagaji wa damu za vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi hadi kufikia kuteua mgombea anayehusishwa na jinai hii. Hii inatosha. Inatosha. Hakuna haja ya kuvuka mpaka na kuendeleza mauaji kama ilivyotokea kwenye visa vya hapo juu.
Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 27, 2010.

Nimekuja na gea mpya kutaka kura

Baada ya kuona maji yanazidi unga huku kitumbua changu kikianza kuyoyoma, kwa vile nimetangaza dhahiri nitaingia Ikuu, nimekuja na mikakati mipya ya kukata na shoka.

Tumeweka mikakati mingi kuhakikisha tunashinda japo mambo yanakwenda ndiyo siyo kwa sasa. Tumegawana kaya mimi bi nkubwa na kitegemezi chetu na mashoga zao. Mkakati mwingine ni kuhakikisha tunachakachua ima kwa kuchukua na kuweka waa au. Kuhakikisha hili tumeishaandaa mazingira ambapo tunatumia utafiti wa kishikaji unaonifagilia ukiwaponda wenzangu ili hapo tutakapochakachua tuutumie huu utafiti wa washikaji wetu ambao tunawalipa kuhalalisha uchakachuaji wetu.Ukiwa na njuluku na wasomi wa nepi ambao wako tayari kufanya kila upuuzi wako hukwami sana.

Hii ikishindikana, tutaingia kwa fosi yaani kuwatumia vijana wa dolari kutembeza kipigo kwa wasimamiaji kula watakaokataa mshiko ili tufanye vitu vyetu. Tuna uzoefu hasa tukitumia ule uzoefu wa kule Zaainzibaa miaka iliyopita. Tulishalianzisha kwa kuwatumia washikaji zetu kwenye fosi ambao mambo yao si haba huenda kishimbo shimbo. Ingawa wengi wamestukia mkakati huu, watake wasitake hatuwezi kuondoka kwa vipande vya karatasi hata kidogo.

Mkakati mwingine ni kujifanya mnyonge na mwenye kuwajali na kuwapenda na kuwahusudu wanyonge hasa wazee na walemavu ambao nawatembezea takrima ya bajaj na magari ili kuwazuga wengine. Hamkuniona nikaa kwenye matope huku wapiga picha wangu wakinipiga picha kama hawana akili nzuri? We ngoja niukwae tuone kama mtaniona nikidhalilika hivi. Kula si mchezo lazima uwe bingwa wa sanaa hasa za maonyesho. Nani aliwahi kumnasa samaki bila kuweka chochote kwenye chambo?

Hamkuniona nikijichanganya na hata kuwapa shikamoo watoto na kutoa rushwa sorry zawadi mbali mbali ukiachia mbali kupandisha hata mshiko wa baadhi ya watumishi wa kaya? Msidhani mie njinga. Nafanya hivi ili muingie mkenge halafu tuwakomeshe. Na ikitoka hairudi. Maana sina mpango wa kugombea tena zaidi ya kuweka kibaraka wangu ili hapo baadaye alinde maovu yangu.

Kuhakikisha walevi hawastuki, nimewaagiza baadhi ya vibaraka wangu kuhakikisha wanapiga magoti kwenye michanga wakati wakiniombea kura bila kujali wana PhD za kweli au kughushi. Nataka waonekane watiifu hata kama ni wahalifu.

Mkakati mwingine ni kuhonga bajaj ili nikipata ulaji ninunue mishangingi. Kuna ndude imegunduliwa nchini Ukanada inaitwa Knight XV. Nasikia inauzwa dolari 800,000. Nikishinda lazima ninunue hizi kwa ajili yangu, mawaziri, bi mkubwa, kitegemezi na mashoga zao ili tufaidi sawa na walevi watakavyokuwa wakifaidi bajaj zetu.

Kweli walevi ndio waliwao. Unawahonga bajaj wanakupa ulaji wa kufa mtu? Unakula wewe, bi nkubwa na mashoga zake, vitegemezi na maswahiba wengine. Mwe! Najisikia kupasuka kwa furaha. Acha wanipe raha. Nikishapata raha nawapaka kuwa raha wajipe wenyewe wasingoje kupewa na wasanii kama mimi.

Mkakati mwingine ni kutumia vitisho kwa kupitia mtabiri wangu na masoja walio washikaji wangu ambao nilishawapa ulaji wakahomola kama yule Shimboka.

Mkakati mwingine ambao ndiyo mtaji wangu mkubwa ni kuwachafua wenzangu kwa kutumia waandishi vyangu. Hamkusikia wakimkandia jamaa kuwa alikwipa kidosho cha mtu wakati mie ninavyo milioni? Mkakati huu kiasi fulani haukufua dafu. Hata yule shangingi wa kinshomile Silvia Rweyependekeza aliyeubuni miaka iliyopita anaonekana kuishiwa mbinu kutokana na kumpa ulaji akageuka bomu. Akiendelea na ujuha wake mie nitamtimua nimweke shangingi jingine la kinshomile liitwalo Mihingulo Rweyependekeza. Maana naye naona anajipendekeza kiasi cha kunikuna.

Mkakati mwingine ni kutumia majuju majini na vitisho vya kishimboshimbo ili walevi wajue wasiponichagua nitavuruga amani ya kaya kwa kuwatumia watu wangu ambao wako tayari hata kuniramba manonihino nikisema. Mie ni chaguo la God, Majini masoja na hata wadudu. Mpo hapo vichaa wangu?

Inabidi walevi wajue fika kuwa amani ya kaya ni kuniacha mimi na watu wangu kula kaya kama hatuna akili nzuri. Asiyekubaliana na hili anatishia amani ya kaya ambayo kimsingi inategemea na kuniacha mie na watu wangu tukitesa kama hatuna akili nzuri hata kama ni kwa walevi kuteseka.

Wanaohoji tunavyopunyua njuluku za kaya na kuwekeza kwenye kampeni za ulaji wetu hawaitakii kaya amani.

Mkakati mwingine ni kumwaga ahadi kama sina akili nzuri. Walevi wengi, kwa kupenda vya dezo na kukosa kumbukumbu watanipa ulaji wasijue wataliwa wao. Mpaka sasa wataalamu wangu wameniambia kuwa nimeishatoa ahadi zenye thamani ya pesa ya madafu kitu kama Zillion mbili! Manijua Zillion wasomaji? Ni kiwango kikubwa cha pesa ambacho hakijawahi kuwapo duniani tangu kuumbwa kwake.

Bila kuwafunga walevi kamba hupati kula. Kwa vile walevi wanapenda sana kuahidiwa uongo na uongo haunigharimu kitu, lazima niongope kama sina akili nzuri. Kipindi hiki nitaahidi kuwapeleka walevi kumuona Mungu wakiwa hai. Mambo ya Kanani yamepitwa na wakati. Mambo yote ni kuwapeleka walevi kukutana na Bwana God ambapo watapewa ulabu kama hawana akili nzuri. Asiyeamini ukweli huu anatishia amani ya kaya na vijana wangu wa Red Brigade watamtia adabu kwa kumwaga damu yake.

Mkakati mwingine tuliobuni ni kukacha midahalo ili tusiadhirike kutokana na viherehere wengi kutaka tuende kule watuvue nguo. Sisi tunategemea ujinga wa walevi. Hivyo ijulikane kuwa walevi huwa hawana muda wa kutazama luninga. Kwanza hawana luninga na wakiwa nazo hawana umeme na wakiwa na umeme wanaangalia michezo ya kuigiza ya Nigeria na mpira wa mateke wa Uingerezani. Hata magazeti yenu ya udaku wa kisiasa hawasomi. Badala yake wanasoma yale ya udaku wa ngono na upuuzi mwingine. Unacheza na wapuuzi sorry walevi nini? Hakuna mtaji mzuri kwetu kama ujuha na ujinga. Na bila kuondoa hili wanaotaka siti yetu walie kwa sana tu.

Pamoja na mie kuwa kilaza, hata ningekuwa na ubavu nisingekubali kujitia kitanzi kushiriki upuuzi huu wa kuvuana nguo. Mlitaka niende nikaulizwe nilitekeleza nini na kushindwa nini siyo? Nimewastukia. Kaya hasa ya walevi ahitaji kuwa na mkuu mjuaji zaidi ya msanii. Ebo! Mshikwe wapi mstuke? Muambiwe nini muelewe kuwa mtaliwa ad infinitum this time around. This is cinch to happen. Kumbe ulabu umepanda hadi namwaga umombo!

Tena ngoja niwahi mechi ya Manchester nikamuage Rooney Wayne.
Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 27, 2010.

Tuesday, 26 October 2010

Kikwazo cha Tanzania si CCM bali wananchi

Kama Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia ushindi halali au wa kuiba kura au vyovyote kitarejea madarakani, watanzania watateseka zaidi ya wanavyoteseka sasa. Pia hii itawaonyesha kama watu wa ajabu na wasiojifunza hata kidogo. Na wasimlaumu mtu wala chama bali wao wenyewe.

Mwaka huu tumeshuhudia mitikisiko kuanzia ndani hadi nje ya CCM. Kulikuwapo na miparurano ya mitandao ya kugombea ulaji. Kulifuatia zoezi lililotawaliwa na rushwa la kuteua wagombea ukiachia mbali uongozi legelege na fisadi na wa kujuana. Tulishuhudia rushwa ilivyokivuruga, kukidhoofisha na kuzidi kukichafua chama huku kuenguana, kuchafuana, kuhujumiana na kutosana vikianza kuchukua nafasi ya sera.

Yote hayo juu yakichangiwa na kuishiwa sera, visheni na mikakati, kutoa ahadi hewa, ufisadi, uzembe, ubabaishaji (usanii), ukale na mawazo mgando ya baadhi ya watendaji wakuu wa CCM, ni dhahiri CCM ni hoi na hovyo. Hivyo, haina sababu ya kurejea madarakani kama watanzania watataka kusonga mbele na si nyuma. CCM irudishwe kufanya nini kilichoishinda kwa miongo yote hii?

Pamoja na udhalili na utepetevu tajwa hapo juu, watanzania wana kazi kubwa ya kujibu swali dogo lakini muhimu. Nani anaonyesha kuweza kukidhi mahitaji na matakwa yako kama mpiga kura, mwananchi hata mkazi kati ya CCM na CHADEMA? Nani ana sera zenye mashiko tofauti na usanii waliouzoea? Nani anafanana nao na kuongea lugha yao na si ya mafisadi?

Kuna kitu rahisi kinachowashinda watanzania-upembuaji kati ya pumba na mbegu. Kwa mfano, CHADEMA, wameahidi kutoa elimu na huduma nyingine za kijamii muhimu bure sawa na alivyofanya mwanzilishi wa Tanzania, Julius Nyerere. Japo hili linawezekana hasa wahusika wasipofisidi mali za umma, kuna watu, tena tunaodhani wana akili sawa sawa kumbe siyo, wanakejeli tamko hili kombozi na la kizalendo!

Ajabu wanaowacheka CHADEMA ni wale waliotoa ahadi magunia miaka mitano iliyopita wasitekeleze. Ni wale wale wanaoendelea kutoa ahadi za kuahidi kutekeleza sera zisizotekelezeka kama alivyowahi kuonya rais mstaafu Benjamin Mkapa! Na wanaendelea kutoa ahadi nyingine za uongo wa wazi kiasi cha hata kurudia zile walizotoa miaka mitano wasitekeleze! Hivi hapa kweli kunahitaji shahada za vyuo kujua muongo na mbabaishaji anayepawa kunyimwa kura ni nani?

Kwa vile watanzania wengi wamejitoa mhanga na kuishi maisha ya kujidanganya kwa kujipa matumaini kama waathirika wa ukimwi (maisha ya uongo na urushi), nao wanaogopa ukweli na kukumbatia urongo wa mchana.

Tumewaona watabiri na wahubiri njaa, wanajeshi uchwara wanaotumiwa kama nepi, waandaaji kura za maoni mapakacha, mashehe shehena na wengine wengi wakijitahidi kujipendekeza kwa walaji waliopo ili nao wapewa mabaki kiasi cha kuzidi kuwatishia na kuwahadaa watanzania. Hawa tuliodhania wanafikiri sawa sawa wameusaliti umma uwe wa wananchi au waumini na kulala kitanda kimoja na ufisadi.

Wametanguliza matumbo badala ya vichwa kiasi cha kuwa shirika moja na wanaonajisi na kuliibia taifa letu.

Watanzania wanapaswa kutambua jambo moja rahisi. Kila tapeli na jizi linalokuja linajificha nyuma ya kulinda amani ya Tanzania. Huwezi kulinda 'amani ya Tanzania' kwa kuwakingia kifua mafisadi na matapeli wengine kama wale walioghushi vyeti vya taaluma, wawekezaji wezi na mauzauza mengine. Huwezi kulinda amani ya Tanzania kwa vitisho au kukiuka haki.

Amani ni haki na si maguvu, lugha tamu za uongo, vitisho iwe vya majeshi au majini na mengine kama haya. Amani ya kweli hainyeshi toka majukwaani wala haifundishwi na wanasiasa uchwara wenye mawazo mgando na ya kijima. Amani ya Tanzania haiwezi kulindwa kwa kuzuia watu kuhoji utawala wa kujuana, uswahiba, kulipana fadhili, familia na upuuzi mwingine namna hii. Amani ya Tanzania-kama ipo kweli- inawezeshwa na watanzania ama kutokana na ujuha au uvumilivu wao. Hapa sijui ni kipi ni kipi zaidi kuhitaji utafiti na darasa zaidi.

Si kwamba watanzania hawa ni majuha au mataahira kama wanavyodhaniwa na wanaowadanganya kutaka kuwatumia kama watakengeuka. Wasipofanya hivyo watathibitisha walivyo majuha. Kinachogomba hapa ni watanzania kushindwa kuwa wakweli kwa nafsi zao. Wameridhika na ubangaizaji na udokozi na bora liende kiasi cha kuona ndiyo maisha na kutishiwa nyau na wezi kwa kutishia kupotea kwa amani.

Kwangu heri nikose hiyo 'amani' mawenge ya kugeuzwa punda au ng'ombe ili nifaidiwe na makupe. Kwangu hakuna amani baina ya kupe na ng'ombe au kuku na mwewe. Amani ya namna hii ni mauza uza tu na uongo wa mchana unaodhalilisha mwenye kuukubali na kuutumikia.

Kinachoshangaza ni ujuha wa watanzania. Inakuwa vigumu kuamini kuwa wangehofia kuwa CHADEMA inaweza kuwadanganya ikilinganishwa na CCM ambayo iliwadanganya kwa kuwaahidi mengi isitekeleze lolote huku mgombea wake akiendelea kutoa ahadi nyingine za uongo. Nani wa kuweza kuamini kati ya Wilbrod Slaa na Kikwete ambaye miaka mitano yake madarakani imekuwa balaa na hasara tupu? Slaa akidanganya hatakuwa na ujanja wala kunusurika kama Kikwete ambaye anadanganya kwa makusudi akijua hii ni awamu yake ya mwisho. Na isitoshe kama CHADEMA kitachaguliwa hakitakuwa na ubavu wa kufanya madudu kama Kikwete kwa vile kitakuwa na chama chenye nguvu kwenye upinzani yaani CCM.

Inashangaza kuoan watu wazima wanaendelea kumuamini Kikwete na sera zake zisizotekelezeka kama alivyozielezea mtangulizi wake Benjamin Mkapa ambaye akilinganishwa na Kikwete ni sawa na mlima na kichuguu!

Kinachogomba zaidi ni watu hawa hawa kulalamika wanapoendelea kutapeliwa kwa upogo wao. Leo kwa mfano nani asiyejua kuwa fedha inayoishia kwenye misamaha ya kodi, rushwa, ufisadi, kutorosha nyara, madini na pesa za kigeni ukiachia mbali kuibiwa wizarani kila mwaka inaweza kutoa huduma za jamii bure?

Nani hajui kuwa kama Tanzania itapata viongozi si watawala wenye mipango na common sense wasiofuja pesa wala kupenda ukuu na kutumiwa inaweza kujiendesha bila kuhitaji misaada ya kipuuzi itokanayo na kujidhalilisha kwa kuombaomba? Nani anathamini elimu kati ya CHADEMA na CCM iliyoendelea kuwakingia kifua vigogo wake waliotuhumiwa kughushi?

Tatizo la Tanzania si ukosefu wa mtaji wala raslimali wala CCM zaidi ya watanzania wenyewe kuwa na malengo uchwara. CCM haina ujanja kuliko KANU. Wakenya walipoamua kuipiga teke KANU 'profesa' wa siasa Daniel arap Moi aliishia kutimka. Tumepoteza mianya mingapi tokana na viongozi wetu kuwa ndumila kuwili? Nani alijua kuwa CCM ingenusurika kutimliwa na kashfa ya Richmond ukiachia mbali wanafiki waliotuaminisha kuwa wanapinga ufisadi kutojiengua kama ilivyotokea Kenya?
Chanzo: Dira ya Mtanzania Oktoba 25, 2010.

Monday, 25 October 2010

News that reduced Mugabe to nothing but a goon
Zimbabwean President Robert Mugabe’s wife, Grace has reportedly been having a secret affair with central bank governor, Gideon Gono.

South African Sunday Times newspaper reports that Grace, 41, has allegedly spent the last five years cuckolding the veteran president with Gono, her husband’s financial adviser and key politically ally.

The report says that Mugabe’s sister Sabina warned her brother before she died that he was being betrayed by two of the most important people in his personal and political life: his wife and his personal banker, a pivotal member of his regime.

The couple would meet as often as three times a month either at Grace’s dairy farm or in expensive hotels in South Africa as well as on foreign trips to Asia.

Mugabe is said to have learnt the shocking news as he sat by his dying sister’s bed in July. He is said to have left the meeting “devastated” although initially refusing to believe the allegations.

The president later consulted his most trusted bodyguard, Cain Chademana, who had sat in on the meeting with Sabina.

Kanisa linapoita wakaguzi wa hesabu!!!!!

The Roman Catholic archdiocese of St.John's, N.L., has called in auditors to look into financial irregularities.

Archbishop Martin Currie says Ernst and Young's annual external audit of financial statements found that money was missing from some accounts.

The church has directed that a comprehensive probe of all its accounts be conducted.

Currie has accepted the resignation of the archdiocese's business manager and the auditors have been directed to widen their investigation.

An assessment is also being made with a view to changing internal controls.

Currie says he wanted to inform parishioners as soon as possible and a message was sent out to parish councils on the weekend.

Friday, 22 October 2010

Je waweza kujioa? Soma kisa hiki cha kweli


TAIPEI (Reuters) - Chen Wei-yih has posed for a set of photos in a flowing white dress, enlisted a wedding planner and rented a banquet hall for a marriage celebration with 30 friends.

But there is no groom. Chen will marry herself.

Uninspired by the men she's met but facing social pressure to get married, the 30-year-old Taipei office worker will hold the reception next month in honor of just one person.

"Age thirty is a prime period for me. My work and experience are in good shape, but I haven't found a partner, so what can I do?" Chen said.

"It's not that I'm anti-marriage. I just hope that I can express a different idea within the bounds of a tradition."

Her T$50,000 ($5,675) wedding comes after online publicity that has netted 1,800 largely sympathetic comments.

"I think there will be more and more girls like this," said "divagirl," who did not elaborate.

Taiwanese women are marrying later and less often as their economic status advances, fuelling government concerns about a drop in the birth rate and its impact on productivity.

Only 40 percent of women surveyed earlier this year by the education ministry said they imagined married people could live better than singles, local media said.

"I was just hoping that more people would love themselves," said Chen, who will go on a solo honeymoon to Australia.

Chen said her mother had insisted on a groom at first but later jumped aboard the solo marriage plan.

But as Chen cannot officially register a marriage to herself, if she finds a man later she will wed again.

"If I had a steady boyfriend, I wouldn't do this," Chen said. "it would be offensive to him, anyway."

(Reporting by Ralph Jennings; editing by Elaine Lies)

Msiwaone wameacha kuvaa suti mkadhani ni wenzenu

SIKU hizi mzee mzima nimegeuka researcher au mtafiti kwa lugha isiyo ya kisomi. Natafiti kila kitu. Ila kwa kipindi hiki cha uongo na ujambazi mbuzi, nimejikita kwenye kampeni na kampani za uchafuzi wa uchaguzi. Katika utafiti wangu nimegundua mambo kadhaa ambayo walevi wanapaswa kujua na kuchukua tahadhali kabla ya kubamizwa mkenge.

Mosi, walevi wa masuti, dhahabu, na viwalo vya bei mbaya ukiachia mbali kujiona wao ni bora kuliko wengine, siku hizi wamevikimbia hadi vinalalamika makabatini. Nani avae suti? Wale walevi wa uheshimiwa siku hizi hawautaki. Ukimwita mtu mheshimiwa anakukata jicho kali.

Anafanya hivyo kutokana na kutaka kumharibia kitumbua hasa kipindi hiki cha kusia uongo ili kuutafuta uongozi.

Hamuwaoni wakijidhalilisha kwa kutoa shikamoo, kupiga magoti hata wengine kukaa chini ili waonekane ni wenzenu wakati ni watesi wenu?

Vitu vilivyoshindikana kukwepwa ni mabodigadi, ulinzi wa majini, ndege na mishangingi waitumiayo kwenda uswekeni kuwaongopea, kuwakoga na kuwatapeli walevi. Hamkumuona msanii mmoja msaidizi akitoa ubani kwenye msiba wa mlalahoi kule kwa waja leo waondoka kesho? Hizo ndizo kampani za kampeni. Kila mnafiki na mfisidi na hasidi atajifanya rafiki ilhali akiomba umpe kura yako kesho akukomeshe kwa kukuuza wewe na uzao wako.

Msiamini uzao wa nyoka hata wakijigeuza miwa. Nyoka ni nyoka hata ajitoe magamba hageuki samaki. Msifanye kosa kudhani chui akivaa ngozi ya kondoo hugeuka kondoo. Kwanini sasa na si siku zote kama kweli hawa ni wenzenu? Nani anahitaji usuhuba wa kinafiki na kiwizi? Hili pamoja na mengine ni swali kuu la kujiuliza kabla ya kuamua nani wa kumpa na nani wa kumnyima.

Msiwaone wamekimbia suti mkadhani ni wenzenu kwa vile wanavaa mavazi casual kama yenu. Mioyoni wanawaona nyinyi mabwege hakuna mfano. Baada ya kupata wanachotafuta, neno ndugu wanalotumia sasa litakufa na kuja mheshimiwa tena mbaguzi ambaye hatawa kumbatia wala kuwasalimia kama sasa ambao wengine wanafikia eti kukaa kwenye mavumbi wakati wao ni wa peponi huku wengine wakiwapigia magoti msijue chambo!

Ni samaki gani anakamatwa kwa kuonyesha ndoana tupu zaidi ya kuwekewa nyama? Je ni aibu kiasi gani mja kutenzwa kama hayawani?

Wakishapata kula hata hamtawaona tena huko madongo poromoka na mkiwafuata huko mjini mtaitiwa polisi na kukamatwa kwa kosa la kuwaghasi wakubwa na waheshimiwa hata kama wezi wa miwa.

Hamjamuona jamaa yangu mpenda suti na viatu vya bei mbaya anavyovaa malapa huku mama akivaa shanga na kukwepa midhahabu. Yote juu ya nini? Walevi waingie mkenge wadhani ni wenzao wakati siyo. Walevi stukeni hao ni wezi wanaotaka kuiba maisha yenu kwa miaka mitano ijayo.

Nichagueni mimi baba Kidume muone nitakavyoipaisha nchi kama dege la Ewassa kwenda Kanani kweli si hii ya Njaa Kaya na kundi lake la wezi.

Jamaa zangu wauza unga na gongo kwa sasa wana likizo hadi mwezi Novemba. Leo haya sitayaongelea kwa undani. Ila kabla ya kwenda kwenye mada, acha nitabiri kuwa mwakani kutakuwa na serikali ya umoja wa kitaifa kama kura zitaibiwa. Yale aliyoshangaa Tunituni kule visiwani yako mlangoni kutokana na hali niliyoiona kwenye maenga yangu ya kitabiri.

Kuna jambo lenye kusikitisha lililonichekesha na kuniacha hoi.

Nani angeamini kuwa kwenye karne hii ya sayansi na teknolojia kungekuwa na mtu au watu wangedhani pikipiki za miguu mitatu Bajaj zingekuwa kichocheo cha 'maendeleo'?

Kinachogomba si watu kutumia bajaj bali ile hali ya ahadi ya kuleta maendeleo kwa bajaj kutolewa na wale wanaoshindana na waarabu kununua mashangingi!

Katika utafiti wangu nimegundua kuwa lisirikali la kaya yetu lina zaidi ya mashangingi 6,000. Hapa hujaongeza yale ambayo wezi wakubwa wameishauziana kwa bei mchekea. Huwezi kuamini mkuu wake eti anaahidi vibajaj 400 kwa ajili ya kubebea wajawazito!

Swali ni kwanini wazaa chema wabebwe kwenye bajaj wakati wezi na mafisi na mafisadi wakizawadiwa mashangingi kwa ushangingi wao kwa uchumi wetu? Kwanini bajaj iwapo watoto wa wezi wakubwa wananunua mihekalu ya mabilioni ukiachia mbali hongo za hapa na pale kwenye kampani za uchafuzi?

Ni uchuro kiasi gani kuona mahawala wa watu fulani wakipewa vyeo simply because wamevua nonihino zao? Kwani uongo? Kwani haya hayafanyiki tena mbele ya hadhira na nyuma ya pazia?

Inashangaza ukiachia mbali kuchefua. Kwanini vinchi vidogo viwe na ambulance sisi tuwe na bajaj pamoja na utitiri wote wa madini? Kwanini tuendelee kurudishwa nyuma kwa kudanganywa tunasonga mbele. Zamani tulikuwa na ambulance za land rover. Leo tunaambiwa tutapewa bajaj tunakubali na bado tunajiona tuna akili kweli! Tutukanwe matusi gani tusituke jamani?

Mie napendekeza tuwape bajaj watawala wetu badala ya mashangingi ili waonje utamu wake kama wanaona bajaj ni dili.

Hakuna kitu kilinishangaza ukiachia mbali kunichefua na kunichukiza kama upuuzi niliousoma kwenye magazeti fulani uchwara, moja la kimombo na jingine la msimu. Vyandudoa wa maadili wanaojiita waandishi wa habari ingawa ni wahandisi wa uongo wa habari, walikuwa wakisifia kila upuuzi wa Njaa Kaya.

Nasikia wameahidiwa ukuu wa wilaya hata ubalozi! Kama ni kweli tumekwisha. Hawa wanaoongoza matumbo yao hata kwa kujivua nguo wataongoza nini yarabi?

Ajabu bado hawa hawa wanawadanganya walevi kuwa wanaweza kuondosha maovu wakati waovu ni wao! Hivi unapogawa vyeo vya umma wa walevi kwa wahalifu kama hawa kwa sababu eti walikupigia debe, kuna uovu kuliko huu? Je huku si kutumiana? Ajabu jitu linapewa sifa za uongo nalo linaamini eti limesifiwa. Huu ni ukahaba wa kimaadili hata ungepewa jina la mikakati.

Inashangaza kuona baadhi ya ofisi za umma na kiama kujaa wahalifu! Wengi tunawajua hawana hata elimu ya kutosha ukiachia mbali kughushi vyeti. Ila kwa vile kayani kwetu kughushi si kosa tena sawa na kuibia mabenki, huenda watapewa hivyo vyeo vya aibu.

Anayetoa na kupokea cheo wote ni vyangudoa. Ni vyangudoa sawa na wale watabiri na wahubiri wa uongo.

Yule kidosho mali kweli. Acha nimfukuzie nipige kampeni ya kupata …..

Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 20,2010.

Tuesday, 19 October 2010

Fikra Mbadala-Ningekuwa Kikwete nisinge.........


Fikra mbadala

Wapendwa wageni wangu, nawataarifuni kuwa kila nipatapo fursa na wahayi, nitakuwa nikiwaletea wazo mbadala kwenye uga huu.

Leo najiuliza na kutoa baadhi ya dukuduku na majibu tuelekeapo Oktoba 31.

Ningekuwa Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete nisingefanya yafuatayo;

Nisingegombea urais kwa awamu nyingine. Badala yake ningewaomba msamaha watanzania kwa kuwaangusha vibaya sana.

Nisingekubali mke wangu na mtoto wangu kuwa wasemaji wangu kwenye kampeni huku nikiwapiga teke marais na mawaziri wakuu wastaafu ambao nao wamegoma kunisaidia hasa saa hii ya kujaribiwa. Na wala nisingewaruhusu kuitumia ikulu na mamlaka yangu kusaka ngawira kama wale walionitangulia. Ningepiga marufuku NGO za wake wa wakubwa.

Nisingeruhusu upuuzi kama kutumia uhuni kama vile kutuma ujumbe mfupi kwenye simu wenye, waandishi wa habari nyemelezi na vyangudoa kuwachafua wenzangu au uzushi wa kumwaga damu wakati wamwagaji wa kweli wa damu ni chama changu.

Pia nisingejiruhusu kutegemea mafisadi kurejea ikulu. Badala yake ningewategemea watanzania ambao ningewambia fika; sina udhu wala sera kugombea tena. Ili niwafanyie nini zaidi ya kuwaingiza mkenge. Pia nisingetoa ahadi nyingine wakati za awali zilinishinda.

Kadhalika, nisingeruhusu wachumia tumbo na wapiga ramli kunizuga nikijua fika nikiporomoka watanikimbia kwa vile msosi utakuwa nao umetimka.

Nisingejidanganya na kuwadanganya watanzania kuwa nafaa wakati najua fika sifa hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi.

Ningekuwa Kikwete, ningeanza kujiandaa kustaafu na kuachia haki katika uchaguzi itawale kama alivyofanya mzee Kenneth David Kaunda wa Zambia ili umma unisamehe na kuniheshimu.
Kabla ya kutokomea ningehakikisha natoa maelezo kuhusiana na kuhusishwa kwangu kwenye list of shame ya Dk. Wilbroad Slaa.

Ningewachisha kazi Yusuf Makamba,Lawrence Masha, Salva Rweyemamu, Abdulrahman Kinana, Tambwe Hiza na wachumia tumbo wengine ambao wamegeuka kongwa.


Zaidi zaidi, ningeenda kujipumzikia na kujiuguza badala ya kujipa moyo ilhali nikijua najidanganya.

Ningefanya mambo mengi kubwa likiwa ni kuanza kutubia na kuomba msamaha kwa sana.

Kila la heri. Nategemea ushauri na mawazo mbadala. Naomba ushauri wenu ili lau nijinusuru na taifa letu. Enough is enough. Wale wanaonitegemea kula watafuta pa kula au wakale Ukonga. Time will come when this will be cinch reality. Je wewe ungekuwa Kikwete ungefanya nini?
Nkwazi

By STAFF REPORTER THE SUN October 19, 2910.

Soma habari za mjukuu shoga wa mfalme wa Saudia ambaye alimuua mwenzake huko Uingereza na kukutwa na hatia.


A GAY Saudi prince is facing life in jail today for brutally battering and strangling his servant to death.

Saud Abdulaziz bin Nasser al Saud carried out a campaign of "sadistic" abuse against his manservant.

He was today found guilty at the Old Bailey of murdering Bandar Abdulaziz in a "brutal" assault in their five-star hotel suite.

The prince was fuelled by champagne and "sex on the beach" cocktails when he bit the 32-year-old hard on both cheeks during the attack in February.

They had just returned from a Valentine's Day night out when al Saud launched the ferocious assault.

When he was arrested he at first wrongly believed he had diplomatic immunity, but his special status as a Saudi royal could not save him from British justice.

The 34-year-old, a member of one of the world's richest and most powerful dynasties, was found guilty of murder today by the jury after just one hour and 35 minutes of deliberation.

Al Saud showed no reaction as the decision was announced.

Kanada yaja na mchuma wa kisasa na salama


Aina mpya ya gari lililogunduliwa Kanada Knight XV ambalo limefanya magari maarufu kama Hummer kuonekana viduchu. Lina horse power 400 na uzito zaidi ya tani sita. Hapa chini ni vidokezo juu ya mtambo huu wa bei mbaya. Sijui watawala wetu wasiopitwa na kitu watanunua mangapi kwa kodi ya wafa njaa? Wauza unga wamelitaka sana lakini wazalishaji wamewatolea nje. Je haitakuwa busara zaidi kuwatolea nje hata watawala wetu ambao tofauti yao na wauza unga ni kwamba wauza unga hawashiriki uchaguzi?

A magnetic detector attached under the vehicle can also alert the driver when a remote-control bomb or a tracking device has been attached to the Knight XV.

And don’t worry if the bad guys shoot out your tires, the Knight XV can run flat on rims made of steel that is the same strength as that used in the wheel rims on massive passenger jets.

“No matter what happens,” says Conquest president and founder William Maizlin, “you’re in an armoured plated cocoon. You’re safe.”

A fully loaded Knight XV costs nearly US$800,000, and oddly as it sounds this armoured-clad behemoth is being built in Toronto, far from violent destinations like Iraq where its blast-proof plating just might come in handy.

One Saudi sheik was so anxious to get his hands on one that he demanded it be shipped in a week’s time. The shipping costs alone came in at $50,000

Sunday, 17 October 2010

Uwekezaji au Utumwa?Pichani mwekezaji wa kichina nchini Zambia akifaidi matunda ya utumwa ....sorry...uwekezaji. Habari za karibuni kuhusiana na utumwa huu mpya ni kwamba mameneja wa mgodi mmoja nchi Zambia waliwafyatulia risasi wafanyakazi wa mgodi walioandamana kudai maisha mazuri kazini. Watu 11 walijeruhiwa na hakuna aliyekamatwa.Waliojeruhiwa ni Simon Simwete 28, Abby Siameba 25, Virason Mwanamusiya 24, Madinda Siamubotu 27, Wisbone Simukonda 25, Boston Munakazela 21, Wallen Muntanga 28 na Humphrey Sinuka 24.
Wengine ni Brighton Sianfuno 21, Bowas Syapwaya 21, na Vincent Chengele 20. Tunawaombea wapone haraka. Pia tunaomba faraja kwa familia zao. Huu ndiyo uwekezaji ambao Benjamin Mkapa alisema utajenga uchumi wa kisasa. Kumbe alimaanisha uchumi wa kisasi! Picha kwa hisani ya Afro Spear Think Tank
Picha hii sambamba na ya juu ni mtawala wa Uganda Yoweri Museveni akifaidi uwekezaji katika siasa. Huyu ni mmojawapo wa wawezeshaji wawekezaji kuja kuchukua na kutumikisha waswahili.Rejea mauaji na vurugu zilizotokea Uganda M7 alipogawa msitu wa Mabira kwa wahindi wake.

Friday, 15 October 2010

Matokeo ya utafiti wa KEDET kuelekea uchaguzi

Dk. Longolongoson Bunner (msomi nepi na nyemelezi) akitoa matokeo ya utafiti wa uongo na kifisadi uliodhaminiwa na Chama Cha Mafisadi (CCM)BAADA ya Redet kutoa matokeo ya utafiti juu ya maoni ya walevi kuelekea uchakachuaji matokeo na kubebana, na Kijiwe kimetoka na matokeo yake chini ya asasi yake isiyo na makengeza wala upendeleo ya Kedet yaani Kijiwe Electoral and Democratic Evaluation Trust.

Wakati Redet ilihoji watu wao wasiofikia hata 3,000, Kidet imehoji walevi karibu wote kaya nzima. Katika utafiti huu walevi wameonyesha wazi kumchukia mtu mmoja aitwaye Njaa Kaya na Chama Chake Cha Maulaji.

Kidet ilitoa dondoo zifuatazo kwenye hoja zake.

Mwaka huu utamchagua nani na kwanini? Asilimia 80 ya waliohojiwa wanasema watamchagua Dokta Silaha na sababu waliyotoa ni kumlipizia kisasi Njaa Kaya kwa kuwaahidi Kanani akaishia kuwaswaga motoni huku Kanani ikijaa mafisidi na mafisi.

Pili, je serikali iliyomaliza muda wake imekidhi matarajio yako na kuna haja ya kuipa ridhaa tena?

Asilimia 90 ya waliohojiwa wametoa majibu yenye kila aina ya ukweli na kulipiza kisasi.

Tutanukuu majibu ya mmoja wa walio hojiwa aliyeandika kama ifuatavyo: “Tulitoa kura tupate maendeleo na maisha bora. Sasa tunahangaika na kuendelea katika kutoendelea huku maisha yakiwa maisha balaa badala ya maisha bora! Tumo msambweni tukilalama na kutumiwa kama wanyama wa mizigo-beasts of burdens! This should not be repeated.”

Tofauti na Redet, Kedet siyo NGO ya ulaji wala kujikomba kwa yeyote.

Chini ya wakurugenzi wa Kedet, Profesa Mpayukaji Msemambovu na Dk. Msomi Mkatatamaa, yafuatayo ndiyo matokeo ya utafiti uliohusisha walevi, vibaka, wachumia tumbo na wajigongaji-bootlickers and cheerleaders and praise singers.

Hawa tumewapata kwenye mabaa, madanguro, vijiwe vya kahawa na vya kuuzia bangi na gongo. Kwa upande wa wanasiasa na wachumia tumbo tuliwapata kwenye mikutano ya kampeni na uchakachuaji ukiachia mbali kwenye lisirikali la Njaa Kaya mwenyewe.

Wajumbe wa kamati ya Kedet walitolewa mkuku maeneo ya wazito kwa kupigiwa zegere la mwizi huku walinzi na mbwa wa getini wakitoa mpya kwa kutishia kuwanyotoa roho wadodosaji wetu.

Kidet ilizunguka Kaya nzima kwa mtaji wa pesa ya kahawa na kuibuka na yafuatayo.

Kwanza, wanakaya waliokuwa wakimmwagia ujiko Mkuu wanaonekana kubadilika vilivyo. Wanasema wazi kuwa amewaangusha na kuwasaliti. Utafiti unaonyesha kuwa kiwango cha kuungwa mkono na kuaminiwa kimeshuka kutoka asilimia 89 hadi 19.

Katika nyanja ya kukidhi matarajio na kuaminika katika ahadi zake, Mkuu ameibuka na asilimia 11. Asilimia hizi amezipata kutokana na kuweza kuunganisha nyumba zake na marafiki kwenye ulaji wake.

Ukilinganisha na asilimia nyingi alizokuwa alipoukwaa baada ya walevi kuukwaa mkenge, ni kwamba Mkuu ametoka kapa kwenye uongozi bora. Amefanikiwa kwenye uongo bora ulioweza kuwafanya wananchi wasiingie mitaani baada ya kuangusha vibaya sana.

Kwenye uwajibikaji ameambulia asilimia tano au kutoka kavu kabisa. Hata hizi asilimia tano amezizoea kutokana na kuwajibika kwa marafiki na familia yake.

Kwenye kipengee cha maendeleo, Mkuu ameendelea sana kuanguka kutokana na kuelekeza maendeleo kwenye jamaa zake na chama chake huku wanakaya wakikosa maendeleo kabisa. Kitaalamu amepata asilimia zinazotafsirika kama HOVYO. Yaani Hakuna organizasheni, visheni yeyote na open policy. Uchumi umezidi kuendelea katika kifo cha kuporomoka na kutegemea takwimu za wajanja fulani.

Kwenye eneo la mipango, Mkuu amepata alama tisa ambazo kitaalamu zinatafsiriwa kama CHOVU yaani Choka mbaya, hali holelea, ovyo, vurumai kiutawala na ufisadi.

Kutengeneza ajira, Mkuu amepata alama maarufuku kama CHOO yaani Chakavu, hasara, ovyo na omba omba.

Tahadhari. Msomaji inabidi uvumilie kupambana na maneno-terminologies ngumu kutokana na hali halisi ya mambo ambapo kwa miaka mitano mafanikio yaliyotokea ni hasi. Mfano, kumekuwa na mafanikio kwa kundi dogo la wanasiasa na wasaka ngawira wengine ambao wamefanikiwa kuzidisha utajiri wao na kukuza mazingira ya kuiibia Kaya kama vile kusaini mikataba mingine feki huku ikiundwa tume ya ulaji kwa nia ya kuwazuga wanakaya na kuwachanganya wapingaji. Rejea kutaka kunyakuliwa kwa Kabwela ambaye chama chake kimeonyesha ukomavu kwa kuliepa zengwe zima.

Mawaziri waliotia fora kummaliza jamaa ni wale walioghushi vyeti vya taaluma na wale walioendekeza ziara nje ya kaya. Hata katibu wa CCM mgosi Makambale naye amemuangusha sana bosi wake kwa kuwa kihiyo na mwongo tena mwenye kuwakejeli walevi na kujipendekeza kwa bosi ili aendelee kula.

Pia marafiki na washirika zake ambao hakukutana nao barabarani yaani Eddy Ewassa, Bazie Rambarambapesambili, Endelea Chenga, Roasttamu Kagodoka na wengine, walimwangusha chari.

Kwani walimkaba shati kuwa lazima awapigie kampeni na asivyofanya hivyo wangemwaga mtama kwenye kuku wengi. Hivyo walevi wameamua kumnyima kura ili kuona kama mafisadi wenzake hawa wataweza kumpa kura za kula za kutosha.

Pia bi mkubwa na kitegemezi chake nao wamewatisha wapiga kura. Kwani wamekuwa wakitoa matamko kama marais ukiachia mbali kutumia fedha na raslimali za umma kujenga biashara ya ukoo yaani kuusaka ulaji kwa mgongo wa kodi za walevi maskini.

Kundi jingine ni lile la vyangudoa wa kimaadili yaani wahandisi wa uongo waitwao waandishi wa habari. Kundi hili ambalo linamramba jamaa visigido limewatia kinyaa walevi kwa kuwachafua wagombea wengine na kummwagia sifa za uongo jamaa wakati likijua hana bao wala sera. Hata sura yenyewe siku hizi imeanza kuvia kutokana na uzee, mieleka, maradhi na mambo mengine ambayo ni siri.

Gesi la Watawala yaani DWTZ limemmaliza mkuu kwa kutoa vitisho kwa wapiga kura na walevi.

Mapendekezo ya Kedet

Mosi, Mkuu kutogombea. Kama angeacha mwanachama mwingine mwenye udhu na akili agombee huenda matokeo yangekuwa tofauti. Lakini hili hakulifanyia kazi.

Pili, alipaswa kutaja mali zake, mkewe na mwanae hasa tuhuma kuwa anamiliki bungalow la madafu bilioni. Pia alipaswa kuwafikisha kwa Pilato mifasadi na washirika zake wote ili wafungwe na kunyang’anywa mimali waliyokwanyua.

Tatu, chama cha maulaji kivunjwe au kurejeshwa kwa makapuku waliokianzisha wakati wa nabii Musa.

Nne elimu ya uraia itolewe hadi kwenye mabaa na madanguro huku maandamano yakiingizwa kwenye katiba.

Tano, njuluku zilizopatikana kutokana na ufisadi, mikataba, uuzaji wa magogo, uuaji wa wanyama vitalu na migodi zilizotoroshwa zirejeshwe nchini. Hapa kampuni la Deep Green wa magrini lilitia fora kwa kutoroshea njuluku nje ya nchi hasa kwenye visiwa fulani.

Sita, wanakaya wasipewe aiskrimu takrima kwenye uchaguzi wala ahadi hewa na za hovyo.

Saba kiongozi atayeunguza kwa kuongopa atiwe bakora hamsa na kushushwa jukwaani huku akizuiliwa kushiriki siasa maisha.

Saba, wabunge wazururaji wasingeruhusiwa kugombea.

Nane, ameshindwa kupata suluhu ya migogoro ya miungano kama ule wa Zenj. Muungano uvunjwe kuepuka migogoro na mitafaruko huku kiranja wa Zenj akichaguliwa na wanakijiwe wa Zenj kwa maelekezo toka Zenj siyo Idodomya.

Kitu kingine kilichobainika kwenye utafiti ni kuchoka kwa katiba ya Kaya ambayo licha ya kuwa na viraka ni ya mwaka 47. Kedet inapendekeza iandikwe mpya kwa kasi mpya, ari mpya, nguvu mpya na watu wapya.

Tisa, Kedet inapendekeza kosa la ukeketaji wa kimawazo liingizwe kwenye Penal code au kanuni ya jinai na adhabu ndogo ya miaka 50 itolewe kwa watakaotenda kosa hili.

Kedet ina mpango wa kuchapisha kitabu chenye kurasa 1000 kuelezea upya jinsi Kaya inavyoweza kurudishwa kwenye hadhi yake aliyoiacha Musa kabla ya Farao na Delila kuinajisi Kaya takatifu ya watulivu na wenye mapendo vitu vinavyoanza kutumiwa na mafisadi kuwaumiza wanakaya.

Taarifa hii imeandaliwa na Profesa emiritus Mpayukaji Msemambovu wa Kedet. P.o Box Mafichoni kwa Mfuga mbwa.
Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 13, 2010.

Thursday, 14 October 2010

Leo ni siku ya kumkumbuka Nyerere


Hivi ndivyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) alichokiasisi Marehemu baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ilivyojikuta katika 'kumuenzi' kwa kumsanifu.
Kwa wenye mapenzi na Tanzania poleni sana kwa msiba huu wa kuwa na majambazi kwenye serikali.
Katuni kwa hisani ya gazeti la Nipashe.

Monday, 11 October 2010

Miaka 11 bila Nyerere: Ni fitina, unafiki mtupu
KESHO ni Oktoba 14, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa taifa, Julius Nyerere kilichotokea Uingereza mwaka 1999.

Mwaka huu ukiwa wa 11 tangu mwasisi huyo wa taifa la Tanzania afariki, pengo lake linaonekana kila siku na kila mahali. Chini ya uongozi wake (si utawala), nchi ilijijengea heshima kubwa ndani na nje hata kama ilikuwa maskini kwa kiasi fulani.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) alichoasisi mwaka 1977, kilikuwa mfano wa kuigwa. Kiliheshimika, kupendwa na kuaminika tofauti na sasa. CCM chini ya Mwalimu haikuwa inazomewa na hakukuwa na kashfa lukuki.

Hakikuwa na vinyamkera na changudoa wa kisiasa na kimaadili kwenye ofisi na safu yake ya uongozi. Nani angeweza kuingia kwenye ofisi zilizoongozwa na mtu mwenye udhu ili kutafuta kujaza tumbo lake?

Leo ni tofauti, watuhumiwa wa ujambazi, wauzaji dawa za kulevya, wezi wa pesa katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), wenye kashfa ya rushwa ya rada na mkataba wa kifisadi wa Richmond; wanapigiwa debe nao wawe viongozi.

Yako wapi maadili aliyosisitiza Mwalimu?

Waandishi wa habari sasa wamegeuka mbwa mwitu wakiandika kila aina ya uchafu na uongo ili wazawadiwe vyeo serikalini na kwenye chama. Uko wapi uadilifu wa kitaaluma?

CCM ya Nyerere ilifanya mengi, kubwa zaidi likiwa kutoa huduma za jamii bure na kujenga jamii ya watu walio sawa bila kujali rangi, kipato wala mtu atokako. Mbona leo pengo kati ya maskini na matajiri ni kubwa?

Viongozi waliolelewa chini ya misingi ya uadilifu ya Mwalimu, sasa wamekuwa fisi wanakula bila kunawa wala kusaza raslimali za nchi. Huko ndiko kumuenzi Baba wa Taifa?

Watu wenye fikra, visheni na utashi wanasema elimu na huduma za jamii zinaweza kutolewa bure kwa jamii, lakini viongozi waliopo wanathibitisha aliyosema Horace Kolimba, kwamba hawana dira. Wameng’ang’ana kuwa haiwezekani. Kwa nini hawafunguki akili?

Mwalimu angekuwepo angewaambia viongozi hawa kuwa elimu bure inawezekana. Angekemea ulafi huu wa raslimali; angekemea mafisadi, matajiri kutawala siasa na serikali kukumbatia matajiri.

Katika kipindi cha miaka mitano serikali imetengeneza mafisadi 11; wameshiuka chama na serikali; viongozi hawafurukuti kwa sababu baadhi ya mafisadi ni viongozi wa serikali.

Mafisadi hawa wanauza viwanja, wale wanatia saini mikataba na kupewa ahsante ya asilimia 10; wengine wanakula kupitia madini na baadhi wanakulipa kwa kampuni hewa. Viongozi wakubwa kwa wadogo wanakula nchi; aibu tupu.

Watanzania watamuenzi Mwalimu kwa aibu na unafiki? Watasoma risala za utii, watasema huku wamejishika vifua kwa hisia kali, watadai wao wanafuata nyayo za Mwalimu lakini kwa uongo mwingi.

Watu wenye akili wanacheka hususan wakiona mambo yanayofanyika sasa.

Wanasema huwezi kumuenzi shujaa kama huyu kwa mipango ya kuhujumu demokrasia, kutoa ahadi za uongo na kufanya usanii.

Huwezi kumuenzi Mwalimu kwa kutegemea ushirikina na ramli; kwa wizi wa mali ya umma au ufisadi; kwa kutumia vibaya na kufuja fedha za serikali.

Huwezi kumuenzi Mwalimu kwa kukwapua raslimali za taifa alizotunza kwa ajili ya vizazi vijavyo; kwa kutoa madaraka kwa kujuana (ndugunaizeisheni).

Wenye akili wanasema huwezi kumuenzi Mwalimu kwa kuendekeza unafiki na lugha tamu wakati matendo ni mabaya; kwa kuendekeza utawala uliogeuka ulaji na kulipana fadhila.

Huwezi kumuenzi mwalimu kwa uchafuzi wa maadili na mazingira kama vile watu wa Buhemba walioachiwa mashimo na wawekezaji baada ya kuchukua madini.

Viongozi hawawezi kusema wanamuezi Mwalimu kwa kuwafukuza wachimbaji wadogo na nafasi yao kuchukuliwa na makampuni ya kigeni.

Madhara yake ni wazi kabisa: Wachimbaji wa Mererani, North Mara, Buzwagi wamegeuka vibarua katika machimbo yao na nje ya migodi.

Watu waliosoma, kufanya kazi na kumpenda Mwalimu wanajisikia vipi wanapoona urithi aliouacha unachotwa na wachache?

Mwalimu alipokuwa anahoji watu wanaokimbilia ikulu, hakuwa anamaanisha wapinzani tu bali hata wanachama wa CCM, kwamba baadhi yao hawakuwa na sifa.

Mwalimu alisimamia mchakato wa kupata viongozi safi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 Miaka minne baadaye akaaga dunia.

Tangu hapo na mambo yalianza kuharibika. Viongozi wameweka kando miiko ya uongozi na misingi ya utawala bora. Sasa ni bora liende.

Chanzo: MwanaHALISI Oktoba 13,2010.

Saturday, 9 October 2010

African elite rulers, quacks and bulimiaIt came just like any blockbuster-cum-hit. This is when it came to light that Zimbabwean tyrant, Robert Mugabe his cabinet and the whole country were duped by just an ignorant witchdoctor to believe that they can get diesel out of the stone. The media has it that Mugabe set a cabinet committee to look into this phantasmagoria.

One Rottina Mavhunga claimed to have discovered refined diesel at a mountainous area. Thus, Mavhunga would pull Zimbabwe nation out of fuel crisis. Interestingly Dr. Mugabe fully and confidently subscribed to this rubbish! I don’t want to boggle my mind asking why did the guy with all many degrees consented to this maniac in the first place. This is not the first person to take Mugabe for a ride. His wife Grace Marufu has always ruled him so as to become the president behind the curtain. And this is the replica of many African first ladies who are using their husbands to rob public coffers.

But again, Mugabe is not alone. In Tanzania, one astrologer did the same to the current president Jakaya Kikwete, when he foretold that anybody that would stand to challenge Kikwete in his party would die instantly. And this farce did work. For nobody stood against the incumbent. After this quack saw how his ‘magic’ worked, before long, he came with another prophecy when his customer president collapsed on 21 August thanks to failing health and being tired. The astrologer said that his subsidence was caused by his enemies. He, thus, promised to protect the president by providing some unseen genies to protect him. Many wondered how the head of state with all body guards could goof this much.

Like Mugabe, Kikwete is currently using public funds to run his campaigns in order to remain in power. His chief campaigners are none but his wife Salma and his son Ridhiwani. Recently, there were undisputed allegations that even the three choppers he is currently using were donated by investors who seek favours in return. Kikwete’s wife and son have been making statements just like presidents. They, too, are acclaimed at the airports by public servants and regional commissioners, who read special speeches as if they’re receiving the president himself.

On this and that of the astrologer, the opposition sought explanations as far as the stance of the government was concerned. The government replied by saying that the astrologer is entitled to freedom of expression (even by making things up!). Regarding abusing public funds by the family of the president, Kikwete’s party, Chama Cha Mapinduzi (CCM) provided forged documents to ‘prove’ that it was hiring plane for the first lady.

What’s more, the quack astrologer, to spice his bulimia, on 28 September the same astrologer who has enjoyed funding from the president, came with yet another gut-wrenching bombshell. He said that either of the two competent presidential aspirants for this year elections, namely Kikwete and his arch contender Dr. Wilbroad Slaa of CHADEMA, will die before polling day! To cut the story short, as I am writing, neither the government nor Kikwete himself has repudiated this hogwash. This means. They believe in it.

Kikwete and Mugabe are neither the first nor the last to show how uneducated they are despite attaining university degrees. In Kenya during the KANU dictatorship, one Indian Kamlesh Pattni duped president Daniel arap Moi and his professor-vice president, George Saitoti, by forming a bogus company that would make Kenya world renown gold producer without even a single mine. This move saw Kenya approaching economic demise.

There are many untold story of sorcery in Africa today. One renown is in Gambia where an ignorant tyrant, Yahya Jammeh was duped by magicians to believe that he discovered a cure for AIDS and impotency. What appalls is the fact that his doctor of medicine, Minister of Health Dr. Malick Njie stood by this stupidity. Who is educated between the duo? I don’t want to answer this. In South Africa, the current president Jacob Zuma slept with HIV-positive woman. He took a shower believing it would cure AIDS! How mad and ignorant such a punk is?

The other day news broke that a Tanzanian professor minister received kickback from the investor in minerals. You know what this kickback was? Just to pay school fees for his daughter that was admitted at a substandard college in South Africa.

From such a few episodes you can see why Africa has always lugged behind when it comes to advancement. If all that we have as rulers and policy makers are zombies and lunatics as we have seen in the above examples, especially ‘the Zimbabwean way of discovering pure diesel’, do you think we can make it out of this economic impasse especially when the same are on the helms?

To do away from this suicidal stance Africa is on thanks to having goofy rulers, we need to boot them out and overhaul our education system. If a PhD holder plus many other degrees like Mugabe can be easily cozened, what of a rural farmer?

Source: Afro Spear October 8, 2010.

Friday, 8 October 2010

Kama Sheik Yahya anaumwa ajue mojaNimepata habari kuwa shehe Yahya Hussein yule tapeli anayejiita mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati amelazwa. Ana mazoea ya kuwatabiria wenzake mabaya hasa wapinzani ili apate fadhila toka kwa Jakaya Kikwete mgombea wa Chama Cha Mapinduzi ambaye kwake ni Mungu.

Kwa vile mzee huyu mtu mzima hovyo amemsahau Mungu wa kweli na pekee na kumtukuza na kumwabudia binadamu tena mchafu, wakati umefika wa kumwambia kuwa zake zinazidi kwisha. Katika safu yangu ya Jicho la Kijiweni nilitabiri kuwa badala ya kufa wapinzani atakufa yeye. Kama anavyowaombea mabaya wapinzani, mie namwachia Mungu aamue. Naomba kila siku kile anachowambea wengine kimrjee ili awe somo kwa wachumia tumbo wengine wanaoabudia upuuzi kama vile wenye madaraka na vitu. Hata akina Kagoda na wenzake wanajidanganya. Wanatesa watu wengi wa Mungu na Mungu hafurahishwi na hili. Hata huyo baba yao fisadi mkuu ni suala la wakati akaenda njia ya Oumaru Yar'Adua kutoka na kujifanya mjanja wakati siyo kwa kuficha maradhi yake.

Wacha Mungu tuombe sana Mungu atutetee dhidi ya mafisadi hawa wanaojiona miungu.
Je kati ya utabiri wa Yahya na wangu ni upi utakuwa wa kweli? Ni suala la muda. Na hii ni namna ya Mungu kuongea na wachumia tumbo na wasaliti kama Augustine Mrema na waandishi wa habari wanaotumiwa kama nepi kuwachafua wapinzani. Inshallah Mungu yupo na analipa hapo hapo.Kesho nitatangaza vifo vya wenye picha hizo hapo juu na lini mazishi yao yatafanyika hasa yule wa kwanza hapo 31 Oktoba 2010 inshallah. Tusione aibu kuonyesha hisia zetu dhidi ya mafisadi hawa. Mbona wao wanatangaza vitisho na uovu wao bila woga wala kificho kuanzia kutumia majini hata majeshi? Lt Gen Shimbo na mbwabweka wenzako mpo?

Toni Braxton files for second bankruptcy in LA

Toni Braxton has filed for bankruptcy a second time, citing millions of dollars in debt and financial problems exacerbated by a heart condition that forced her to cancel a series of Las Vegas shows.

The filing will likely result in the six-time Grammy Award winner having to sell some of her assets to pay off debts listed in court records as ranging between $10 million and $50 million.

Her attorney, Debra Grassgreen, said in a statement the filing will allow Braxton to pay off tax debts, sell heavily indebted property in Atlanta and still care for her children.

Braxton has had high-profile health issues in recent years. In 2008 she was forced to cancel a series of Las Vegas shows after experiencing chest pains that were later diagnosed as microvascular angina. Later that year, she performed on the ABC series "Dancing with the Stars" but missed the finale while recovering from removal of a benign breast tumor.

Grassgreen said the Vegas show cancellations left Braxton, 43, saddled with debts from which she could not recover.

The singer and her company Liberty Entertainment filed for bankruptcy Sept. 30, court records show. The filing was first reported Thursday by celebrity website TMZ.

"This was a very difficult decision for Ms. Braxton," Grassgreen said. "However, after months of trying to work out an acceptable arrangement with her principal creditors, she determined that the only way to assure that she could meet her tax obligations and provide for her two small children was to commence these bankruptcy cases."

Braxton has assets worth up to $10 million, her filing states.

She previously filed for bankruptcy in 1998.

Grassgreen's statement said Braxton is currently in good health.

Known for songs such as "Un-Break My Heart" and "Breathe Again," Braxton sued Lloyd's of London, which had insured her for the Las Vegas performances in case they had to be canceled. The insurer denied her claim, stating she had a pre-existing condition, and court records show the case was dismissed on Sept. 20.

Braxton's spokeswoman Jennifer Mercer said the case was "settled to the satisfaction of all parties."

Grassgreen said the bankruptcy will not prevent Braxton from future performances.

Je haya si matumizi mabaya ya madaraka?


Hakuna kitu kibaya kinachoweza kukubalika hata kama umma utalazimishwa 'kukikubali'.

Hakuna siri kuwa wadhifa wa mkuu wa wilaya nchini unaanza kuwa kama kichaka cha wachovu, waramba viatu, washirika na maswahiba wa rais. Uteuzi wa mkuu mpya wa wilaya ya Masasi, Nape Nnauye, hauwezi kupita bila kuhojiwa.

Wengi hasa waandishi wa habari na wachumia tumbo wengine wa kisiasa sasa wako kwenye heka heka za kuupotosha umma ili wateuliwe wakuu wa wilaya na rais kama kulipa fadhila kwa usaliti wao. Na zingatia hili. Baada ya uchaguzi mtashangaa sana kuona hata wahuni wakiteuliwa kuwa wakuu wa wilaya.

Mtaona marafiki., mashoga wa mkewe, marafiki wa wanae na wapambe wa rais wakiteuliwa kwenye wadhifa huu. Mtaona watu wa hovyo wasiofaa hata kuwa mabalozi wa nyumba kumi wakiteuliwa kuwa wakuu wa wilaya. Ila ikumbukwe. Pamoja na rais kulipa fadhila, ajue hawa wateule wake wanalipwa kwa pesa yetu na si pesa yake binafsi. Pia watu hawa wanaotokana na kujikomba na si uchapakazi, wanazidi kutukwamisha kimaendeleo. Maana hata wakivurunda hakuna wa kuwagusa ikizingatiwa kuwa aliyewateua ni mungu mtu kikatiba. Hamjaona mkewe, mwanawe na wapambe zake wanavyofuja pesa yetu kumpigia kampeni?

Mchezo huu wa hatari ulianza pale rais Jakaya Kikwete alipomlipa fadhila mpiga debe wake mwandishi wa habari Salva Rweyemamu aliyemteua kuwa mkurugenzi wa tume ya mawasiliano ikulu.

Hata wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa mchezo huu ulikuwapo japo si sana kama sasa. Angalia baadhi ya waajiriwa wa Ikulu. Utakuwa wengine wana udugu na mke wa Mkapa. Huu ni ufisadi hata kama unatendwa na wakubwa.

Na hii si siri. Kuna mwandishi mmoja tena tapeli ambaye hata sijui kama aliusomea huo uandishi wa habari ambaye alikuwa mhariri wa gazeti moja dogo la kila wiki lenye makao yake maeneo ya Kariakoo. Huyu anatangaza wazi wazi kuwa lazima ateuliwe kuwa mkuu wa wilaya. Sababu? Anaendelea kazi ya kuwachafua wapinzani wa Kikwete kwa kuzua mambo akifanya kibarua hiki kichafu ili ateuliwe kuwa mkuu wa wilaya. Uzuri ni kwamba anajulikana alivyoghushi vyeti. Ila kwa vile watuhumiwa wa kughushi vyeti vya kitaaluma wenye uswahiba na Kikwete hawaguswi, huenda mpumbavu huyu akapewa ukuu wa wilaya.

Na hii ndiyo sababu ya kuwasikia wapiga debe wachovu waliorundikana ofisi ndogo makao makuu CCM Lumumba wakihanikiza kupigia debe CCM hata kwa hoja chafu na zilizokufa.

Hivyo msishangae kuona wengi wa waliokataliwa kwenye kura za mchujo wa kugombea ubunge kupitia CCM wakiteuliwa kuwa wakuu wa wilaya. Rejea tamko la Kikwete kuwaasa wavumilie watatafutiwa nafasi.

Inashangaza mkuu wa wilaya anapokuwa kada wa chama kinyume na katiba ambayo inataka mtumishi wa umma asiwe na upande. Hata awe mteule wa rais, anapaswa kuzingatia hili. Ndiyo maana mahakimu, majaji, polisi na watumishi wengine wa umma wanapaswa kuwa neutral.

Wakuu wengi wa wilaya hata mikoa wamekuwa wakilaumiwa kwa kukibeba chama chao hata kufikia kutisha na kunyanyasa wananchi ili kufanikisha malengo yao. Hebu ninukuu kauli ya hivi karibuni na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa aliyoitoa hivi karibuni jijini Arusha.

Alikaririwa akisema: “Nilisema Mbeya na sasa narudia Arusha, wakuu wa mikoa na wilaya, waache tabia ya kuzunguka vijijini na kuwatisha wananchi kuwa wakiwachagua wagombea wa vyama vya upinzani hawatapata maendeleo na kuwataka wakichague CCM, hilo halikubaliki.”

inashangaza miaka zaidi ya 50 ya uhuru bado kuna watu wanawatisha wenzao bila hata serikali kuchukua hatua. Nani atachukua hatua iwapo hawa wakoloni walioteuliwa na rais ndiyo serikali yenyewe?

Huu ni ushahidi tosha kuwa wahusika licha ya kufanya uhuni ni makada wa chama. Wanafanya kazi za chama. Lakini wanalipwa na serikali toka kodi za wananchi wote wakiwamo wanachama na wasio na wa vyama vya upinzani.

Na anayewateua makada wake kufanya kazi za chama chini ya ajira ya serikali anavunja katiba hata katiba yenyewe kama ni ya kizamani na chama kimoja. Pia huyu anapingana na kanuni za utawala bora. Yeye, wateule wake na chama chake wanaliibia taifa. Hawafai kuwa madarakani hawa. Kwani hawajiamini wala kuwa na sifa ya kuongoza ndiyo maana wanateuana kwa kujuana na si sifa za uchapakazi.

Tulimsikia rais Kikwete akiwapa moyo waliong'olewa kwenye kura za mchujo kuwa atawatafutia ajira. Je kwa kuanza kuteua watu wakati wa kampeni ni motisha kwa wale waliokuwa ima wakitaka kuhama chama au kutoshilikiana nacho kupiga kampeni wafanye hivyo kwa imani kuwa watapewa ulaji wa dezo wilayani?

Kweli hapa ndipo naona mantiki ya katiba mpya ya nchi jirani ya Kenya kuondoa vyeo vya mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa. Maana vinatumiwa na watawala wabovu kuwapa ulaji na kuwajaza serikalini marafiki zao ambao pia ni wabovu. Huu ni wizi na ufujaji wa mali na fedha za umma. Hivi tukiondoa vyeo hivi tutaokoa mabilioni mangapi ambayo yatatuwezesha hata kutoa elimu bure kama wanavyosema CHADEMA?

Tuhitimishe kwa kumtaka Kikwete kuacha kutuhujumu kwa kuwafurahisha na kuwaneemesha ima wanachama wake au marafiki zake.

Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 5, 2010.

Wednesday, 6 October 2010

Walimu au viwembe?


More than 500 teachers have been dismissed after being implicated with impregnating girls in primary schools, the Teachers Service Commission has said.

The revelation by the TSC chairman Ibrahim Hussein Wednesday also puts teachers on notice that besides losing their jobs they will also face criminal proceedings in courts after the Commission moved to involve the police.

Last year, Mr Hussein said 600 teachers had their names struck from the TSC register for impregnating their pupils.

But the chairman took issue with some parents, who have been a stumbling block in the disciplining of errant teachers by opting to settle such cases outside courts and leaving the randy teachers scot -free.

“The number of teachers who have been sacked and taken to court may appear to be small but this is an issue of concern that we would need the support of the parents and the community to bring it to an end.

“It is wrong for teachers who have been entrusted the care of the girls to turn against them and interfere with their education,” he said at the Sheikh Zayyed Welfare Centre in Mombasa during the Kenya Primary School head teachers’ association annual conference.

Mr Hussein, however, called on parents to ensure that the affected girls are allowed to go back to school after delivering so that their education is not curtailed.

He said it would be appropriate to take such girls to different schools after childbirth to avoid stigma.

At the same time, he said head teachers will be taken through special training on how to deal with such cases adding that the police have already started taking the lead in punishing the teachers.

“Nobody will be victimised but we call for cooperation in enforcing this so that the future of the girl child is secure,” he said.

Education minister Professor Sam Ongeri said despite a campaign on gender equity, some regions still discriminated girls in the provision of education.

He singled out North Eastern, Coast and Nyanza provinces where the number of girls in upper primary was very low compared to that of boys and called on head teachers to ensure there were equal opportunities for both boys and girls.

Source: Daily Nation.

Hata Ulaya Uchawi Upo

MOOSE JAW, Sask. - There will be no spirit at a Halloween fundraiser in Saskatchewan this year after complaints from religious objectors killed a planned séance.

The Moose Jaw Western Development Museum had organized a "ghost walk" as well as a presentation on talking with the dead.

That was to be followed by a demonstration.

Pastor Larry Gerow is one of the people who took offence and there were also complaints to the local member of the legislature.

The museum's board of directors says staff were fielding so many complaints, it was decided they had better things to do with their time.

David Klatt, the museum's executive director, says it's too late to put together a different fundraiser in time for Halloween. (CJME-CKOM.
Source: The Canadian Press

Kampeni za kitanda kwa kitanda ni kueneza ukimwi

JUZI nilihudhuria mkutano wa kampeni uliokuwa ukihutubiwa na bi mkubwa wa mkubwa. Jina leo silitaji atakayejitokeza kujihisi, atajiju. Japo wengi wamekuwa wakimshutumu kufanya kampeni kifamilia, mie sina ugomvi na hilo kama wataacha kutumia njuluku za Kijiwe chetu.

Hata wakitaka na mbwa na paka wao wawapigie kampeni ruksa. Ilmradi wasiguse njuluku zetu. Kwa vile nami ni mgombea na rais mtarajiwa, naamua kuwananga kwa kuninanga kuwa sina sera bali photocopy na wao ni orijino tena handsome orijino.

Hata mie ni handsome. Sema sina tabia ya kujisifia ujinga. Hayo tuyaache.

Kwenye kampeni za rais mama, nilishangaa kusikia upuuzi badala ya sera. Badala ya mtu awahamasishe walevi kwa kuwaambia atakachowafanyia, cha ziada zaidi ya kile alichokwisha wafanyia, anahanikiza upuuzi mwingine. Ni kero na machukizo hasa upuuzi huu unapotoka kwenye kinywa cha mtu anayeitwa mheshimiwa.

Basi bwana, mama mkubwa alitua kwa ndege yake kijijini kwetu na wasaidizi, walinzi yakiwamo hata yale majini wake, huku akilakiwa na viherehere wa mikoa na ngoma za kitamaduni.

Ukiona anavyotembea, kupungua mikono na kuongea, utaamini naye ni rais. Hapa bado hujaangalia utitiri wa mishangingi na mishankupe anayoandamana nayo.

Anahutubia kama rais na kulala hata Ikulu kama rais. Je, huyu si rais nyuma ya pazia? Mie nasema mapema. Si Bi mkubwa wangu wala kitegemezi changu watakaribia hata kiti changu achia mbali kutumia madaraka yangu kuwaibia walevi kijiweni. Hivyo lazima wote mnipe nifanye kweli na si kuambiwa mfanye kweli kitanda kwa kitanda. Kitanda kwa kitanda ni kueneza ukimwi na nyumba kwa nyumba ni kueneza ujambazi.

Nasikia wanasema zile ndege anazotumia Bi mkubwa, zinalipiwa na lisirikali hili kapa. Kama siyo ujambazi mbuzi, wanamlipia kama nani? Hata mkubwa hapaswi kulipiwa usawa huu. Maana ashamaliza ngwe yake. Nashangaa kumuona hata akiwapa ulaji waramba viatu wake usawa huu ambapo yeye si rahisi bali mgombezi!

Basi mama, bila chembe ya aibu, tuseme. Kutokana na kiherehere chake si alianza kumwaga matusi akidhani ni sera. Alipayuka. “Kuanzia sasa nawataka wanachama wetu wafanye kampeni nyumba kwa nyumba na kitanda kwa kitanda. Wafanye hivi bila kukoma.”

Umma wa mashabiki wake majuha ulimshangilia sana. Kwenye mti jirani, kunguru walimzomea na kuwashangaa walevi wanavyolishwa matusi na uchafu.

Kabla ya kuendelea sisi hatuna mbavu. “Wafanye bila kuchoka! Kitanda na kampeni wapi na wapi kama si kutaka kumalizana kwa ukimwi kutokana na kuhongana ngono?” Nilimsikia mkota mmoja akizoza.

Naye Mkota wa pili ambaye anaonekana anaunga mkono chakudema aliiingilia haraka. “Dokta alishasema hawa watu hawana sera zaidi ya uhuni. Lakini wadanganyika walio wengi hawataki kumwamini. Sasa mmesikia na kuona wenyewe,” alimalizia.

Siku hiyo niliandamana na Msomi Mkatatamaa. Yeye alichomekea hapo hapo. “Siku zote nimesema kuwa hawa watu licha ya kuwa na mawazo mgando, wamefilisika vichwani hamtaki kuniamini.

Hili jimama laonekana kulewa madaraka na kudhani hayana mwisho.” Alinigeukia na kuendelea. “Ngoja mzee Mpayukaji ashinde kiti tuwafungilie mbali hawa gendaeka.” Nami kwa kumwagiwa ujiko nilikenua kama Chekacheka utadhani nami ni kibopa wa kaya hii.

Tukiwa na kikao chetu ndani ya kikao, mama mkubwa aliendelea. “Nawahimiza kina mama msilale hadi kieleweke. Msichague wapinzani wana ahadi za uongo kama zetu.” Kabla ya kuendelea nilisikia mhuni mmoja aliyejichora rangi za chama cha mafisadi akisema. “ Toboa mama toboa lazima wafanye kweli na kieleweke.”

Mke wa mkubwa kusikia kasifiwa ujinga anapanua domo lake na kuongeza. “Hamjasikia kuwa mwanamke lazima awe ndoo kichwani na vidumu mikononi? Bila hiyo, hakuna raha.” Alimalizia mpuuzi huyu kujivua nguo. Kumbe anadhani wote wazaramizi? Kusum audhubillahi minaa shaitwan rajiim.

Mwingine alidakia: “Mnatukanwa na kutumiwa ajabu mnashangilia. Kweli nyinyi danganyika. Mama anaongopa huku. Baba kule. Mwana naye kadhalika wakitafuta uongozi nanyi mlivyo majuha mnazidi kuwashangilia badala ya kuwashushia mkong’oto kama aliokoswa koswa kiherehere wao kule kwa kina Kamwene.”

Tokana na uhuni aliokuwa akifanya ma mkubwa, nilipandwa hasira hadi umombo ukanitoka. Nilimgeukia Msomi na mgosi Machungi na kuzoza: “First off, I'm totally against impotent and incompetent politicos you see in power campaigning on public funds and resources.”

Msomi naye kuwaonyesha kuwa ni msomi na siyo wale vilaza wa kughushi alijibu. “Mzee you're dead right. These goons must be booted out the sooner.”. Mgosi Machungi yeye alisema: We wee make sure that the are not coming back mgosi. Kwai?” Baada ya kuona wachovu walio kuwa karibu nasi kuanza kunong'ona kuwa tunajifanya watasha tuliachana na ung'eng'e na kuondoka tukijadili hili na lile.

Mpake leo sijaelewa ni kwanini Chama Cha Mafisi kimeamua kufanya uhuni kikidhani ni sera na isiwe dharau kwa wanaoambiwa matusi haya!

Yaani mafiga matatu kama wale ndugu zangu wanaotumia matatu yaani kutoa chifu original (figa la kwanza) kutoa uchifu kwa chifu feki (figa la pili yaani daddy au mkuu) na kumalizia kugawa ‘uchifu’ kwa mtoto wa chifu feki (figa la tatu).

Tusipoangalia kuna siku kutakuwa na figa la nne yaani na mama kupewa uchifu maana wote ni walevi wa sifa na kutapeliana. Wanawatapeli walevi na walevi wanawatapeli wezi kwa kuwapa uchifu.

Siku Bi mkubwa wa mkubwa akitangazwa na akina Twa mbombo twa bakangale kuwa chifu nitacheka hadi ninyauke kama siyo kupagawa. Lakini hata hivyo hawana kosa. Kama mama amepata urahisi kutokana na mumewe kuwa rahisi atashindwa nini kupata uchifu?

Mwanzoni nilidhani mpuuzi ni bi mkubwa, kumbe na baba naye hovyo tu! Maana kila anapokwenda kuongopa kwa jina la kampeni utamsikia akihanikiza: “Tumefanya, tutafanya na tutaendelea kufanya zaidi.” Ukiuliza mmefanya nini zaidi ya ufisadi na ujambazi, utaambiwa wewe photocopy.

Heri photocopy isemayo ukweli kuliko orijino katika ufisadi. Yote hii ndugu zanguni ni uhuni, usanii, ubabaishaji na ukosefu wa sera. Ni aibu hata ukosefu wa busara. Nashauri mnichague mimi kwa vile nina sera madhubuti na adabu ya hali ya juu.

Mie nina sera si uhuni. Na isitoshe mie situmii midege ya mafisadi ambao baada ya kuniwezesha watataka wawanunue nyinyi na raslimali zenu. Nichagueni niwafunge mafisadi na kuwanyonga bila huruma. Sitegemei yule shehe mhuni ambaye natabiri atafia India hivi karibuni.

Kabla sijasahau, yule shehe wa Migomigo nasikia anatumiwa kutangaza mbinu za kutaka kuninyotoa roho. Ninyotoeni roho damu imwagike.

Du kunguru kaninyea. Wewe kunguru mwanga na mhuni kama shehe ubwabwa na bi mkubwa wa mkubwa. Khalas kweisine.
Chanzo: Tanzania Daima Septemba 6, 2010.

Monday, 4 October 2010

Hatuchukii CCM, Kikwete wala kampeni zaoKuna maswali mengi kuliko majibu kuhusiana na staili ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jakaya Kikwete ya kutumia wana familia yake kwa gharama za serikali. Pia kuna shutuma na lawama nyingi kuhusiana na mtindo wake mpya wa kuendesha kampeni zake kwa ujumla akiwatumia wakuu wa mikoa na wilaya kinyume cha sheria. Rejea waraka wa hivi karibuni uliofichuliwa na CHADEMA uliodaiwa kuwahimiza kuhakikisha CCM inashinda. Kutumia raslimali za umma kwa manufaa binafsi ni ufisadi. Ingawa hili linapotoshwa na wapambe zake, ukweli ni kwamba umma haufurahishwi na matumizi ya familia yake.

Kikwete si wa kwanza kutumia wana ukoo wake kufanya kampeni. Rais wa zamani wa Argentina Nestor Kirchner alimpigia kampeni hata kumwezesha kushinda kiti alichokiacha mkewe Cristina Elizaberth Fredinand de Kirchner. Lakini alifanya hivyo bila kificho kwa njia zinazokubalika kikatiba. Alimpigia kampeni mkewe kama mgombea (mwanasiasa) aliyeteuliwa na chama chake cha Partido Justicialista na si kama mkewe. Na isitoshe Cristina alijulikana kuwa mwanasiasa tangu akiwa mdogo na siyo kuanzia alipokuwa mke wa rais kama hawa wetu.

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, alimpigia kampeni mkewe Hilary lakini kama mwanasiasa na si mkewe. Kadhalika Hilary alianza siasa akiwa shuleni na siyo White House kama hawa wetu.

Barbara Bush aliwapigia kampeni mumewe na mwanae Gerge W Bush Sr and Jr si kama mke au mama bali mwanachama ambaye hakutumia raslimali za umma.

Juzi juzi tulimuona mke wa rais wa Marekani Barack Obama, Michelle akimpigia kampeni mumewe. Alifanya hivyo kabla ya mumewe kuwa rais na akigombea tena hawezi kutumia fedha ya umma kufanya hivyo na asiathiri matokeo yake.

Hapa ieleweke bayana. Kinachogomba kwenye kampeni za Kikwete si kampeni bali namna zinavyofanyika ukiachia mbali wafadhili wake. Kinachogomba ni kile waingereza huita nepotism yaani utawala wa kidugu.

Salma na Ridhiwani, Miraj Kikwete hata Rahma Kharoos binti Kasiga wana kila haki ya kumpigia kampeni mpendwa wao. Kinachogomba ni matumizi mabaya ya magari, fedha, ndege hata muda wa umma. Rejea kashfa ya hivi karibuni iliyofichuliwa na CHADEMA kuwa Salma alitumia ndege ya serikali. Kama nani hata kama ni kwa kukodishw ana CCM?

Salma na wanae wana kila sababu na haki ya kumpigia kampeni baba au mume lakini wafanye hivyo kwa njia sahihi. Salma kama mke ana haki ya kumpigia kampeni mumewe lakini si kama mwenyekiti wa WAMA.

Kinachogomba si wanafamilia ya Kikwete kumpigia kampeni bali kulindwa na vyombo vya dola, kupokelewa na wakuu wa mikoa na wilaya na makandokando mengine ambayo si stahili yao kikatiba. Huu ni ufisadi na ufujaji wa raslimali na fedha ya wanuka umaskini wa Tanzania. Huku ni kucheza rafu. Maana, kwa kugharimiwa na serikali, wanapoteza sifa mojawapo ya uchaguzi wa kidemokrasia na huru na haki. Tunataka uwanja sawa na fursa sawa hata kwenye vyombo vya habari.

Salma anatoa khanga na matamshi ya kukandia wapinzani kwa kutumia pesa yao kama wananchi walipa kodi wa nchi hii. Hii si haki. Huu ni mchezo mchafu hata kama unafanywa na wenye madaraka. Hii ni hatari kwa mstakabali wa taifa kama wapinzani na wapenzi wao wataamua kusema enough is enough. Hii inaweza kuzusha rabsha na mapambano baina ya wanaohujumu haki na wanaohujumiwa.

Kama Salma hawezi kuishi bila kufanya siasa au kuvunja katiba basi achague moja kati ya haya mawili. Agombee nafasi ya kisiasa hata kumshawishi mumewe amteue waziri kama alivyofanya imla wa Uganda, Yoweri Museveni aliyemteua mkewe kuwa waziri au mwanae kusimamia kikosi maalum. Pili aache kujificha kwenye NGO yenye jina zuri la Wanawake (wa Tanzania nzima bila shaka) na Maendeleo. Ajitokeze kama Salma mwanasiasa na si mwenyekiti wa NGO yenye kutia mashaka ukiachia mbali kuonekana kama matumizi mabaya ya madaraka hasa ikulu kusaka ngawira.

Imla wa Kenya, Daniel arap Moi, pamoja na uimla na ukihiyo wake, hakuwahi kuwaruhusu watoto wala mke wake kushiriki siasa ingawa aliwapa kibali cha kutumia jina lake kuibia mabenki na taasisi za Kenya. Kwa hili aliona aibu. Imla na wezi wa Congo Denis Sassou Ngwesso na yule wa Equatorial Guinea ndiyo hadi leo wana uchovu wa kuwatumia watoto wao wanaoibia serikali huku wao wakifumba macho. Hivyo sifa mojawapo za utawala wa ukoo kama tulivyoona kwenye baadhi ya mifano hapo juu ni uimla, wizi, matumizi mabaya ya mali ya umma vitu ambavyo nisingependa vimkumbe Kikwete.

Mfumo wa utawala wa kifamilia unapoanguka balaa huwa kubwa na familia husika huteketea. Maana huwa hazina uhalali zaidi ya kujificha nyuma ya madaraka ya mtu mmoja (rais). Tumeyaona kwa Saddam Hussein imla wa Iraki aliyeruhusu wanae kuwa marais wadogo wakifanya watakavyo. Wao na baba yao, utawala wao wa kizandiki ulipoangushwa wamekufa kama mbwa. Hatutaki hili kwa aliyewahi kuwa rais wetu.

Yule mwizi wa DRC zamani Zaire Joseph Desire Mobutu alipoangushwa familia yake ilisambaratika sambamba kutokana kuwa na marais wadogo wenye kutumia jina la rais kama sifa yao ya kuongozea nyuma ya pazia wakitenda kila aina ya jinai na aibu.

Imla wa Togo Gnassingbe Eyadema alipofariki madarakani aliacha balaa ambapo watoto wake wawili, rais Faure Eyadema na Kpatcha wanatishiana kutoana roho wakigombea urais wa baba yao.

Tumalize kwa kuzidi kushauri kuwa Kikwete, ili ajitendee na kututendea haki, aachane na siasa za ukoo urafiki na familia. Aachane na mambo haya kutokana na ukweli kuwa cheo ni dhamana. Hufikia mahali kikatoweka na mwenye kuwa nacho akabakia na aibu yake kama aliyatumia vibaya au heshima kama aliyatumia vizuri.
Chanzo:Dira ya Mtanzania Oktoba 4,2010.

Sunday, 3 October 2010

Tishio la jeshi linadhalilisha taifa na jeshi

Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo akitoa vitisho mbele ya waandishi wa habari
Tamko au tuseme kitisho kilichotolewa hivi karibuni na mnadhimu mkuu wa majeshi ya Tanzania Luteni Jenerali Adbulrahman Shimbo, licha ya kulidhalilisha taifa na jeshi ni ushahidi kuwa nchi yetu iko hatarini-haina jeshi bali waganga njaa wanaojikomba kwa Chama Cha Mapinduzi ili wafaidi makombo ya ufisadi.

Jeshi liache siasa kwa wanasiasa. Lifanye kazi ya ulinzi badala ile ya kufua nguo chafu za CCM. Ni aibu na hatari.
Inashangaza. Wananchi wamegwaya kiasi cha kushindwa hata kuandamana na kulaani uimla huu! Muhimu ni jeshi na CCM kutambua kuwa atakayemwaga damu ataishia kunyea debe kule The Hague kama Charles Taylor. Mambo yamebadilika siyo kama zamani ambapo jeshi lilijiona kuwa juu ya kila kitu na kufaidi bajeti kubwa za siri zilizoishia kufaidiwa na mafisadi wa kijeshi.

Hivyo wananchi wapuuzie vitisho vya jeshi na kusimama kidete kuhakikisha kura zao haziibiwi. Maana tishio la jeshi ni ushahidi wa kushindwa kwa Kikwete ambaye bila kubebwa na jeshi, tume ya uchaguzi, polisi na wezi wengine wa kura hawezi kushinda. Atashinda kwa lipi iwapo ameiuza nchi badala ya kuitawala?

Inashangaza jeshi kujichafua kwa kuridhia wizi wa kura na likawa tayari kuubariki, kuulinda na kuulazimisha kwenye mioyo ya watanzania. Hii ni kashfa sawa na EPA hata Richmond. Je kazi yake ni kuwatumikia wananchi na si wananchi kulitumikia jeshi. Licha ya kuwapo kwa utashi wetu, lipo kutulinda na mali zetu zikiwemo kura.

Je kwanini jeshi letu limefikia hapa? JWTZ yaani Jeshi la Wananchi wa Tanzania sasa ni jeshi la watawala uchwara na mafisadi.

Kwanini wanafanya hivyo? Je wamezuzuliwa na vyeo vya kukatiwa vya wakuu wa wilaya na mikoa?
Kwa njaa yake limejivua heshima ya kuwa jeshi la wananchi na kuwa Kamanyola lile jeshi habithi la Zaire lililowalinda wezi wakiongozwa na jambazi Mobutu Seseseko.

Limeikataa heshima iliyoyandisha majeshi ya Kenya, Malawi, Zambia na Benin yalipokubali mageuzi ya kweli ya kidemokrasia yachukue nafasi hata kukataa shinikizo la wachovu waliokuwa madarakani.

Letu limegeuka mbeleko ya kuubeba mzigo uitwao CCM uliojaa mafisadi. Hivi jeshi halina common sense kujua kuwa kuvunjika kwa amani hakusababishwi na wapinzani bali ukosefu wa haki?

Hebu malizia makala hii kwa kujikumbusha makufuru ya Shimbo mwanajeshi-mwanasiasa na kada wa CCM.

Alikaririwa akisema, tena baada ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari ili kuwatisha watanzania kama ifuatavyo: “Dalili zimeanza kuonekana za kutaka kuvunja sheria katika kampeni, kuchochea fujo na uvunjifu wa amani… dalili hizo sio nzuri. Pia kuna baadhi ya taasisi na mashirika yameanza kujiingiza kwenye kampeni kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuhusu upigaji kura au kutoa matamko yanayolenga kushabikia vyama vya siasa na wagombea.”

Kumbe kuwapa wananchi elimu ya uraia ili wachague vizuri ni dalili ya kuvunjika amani! Je amani kwa Jeshi ni pale kundi la mafisadi wenye madaraka wanapokula bila kubughudhiwa huku nalo likiwalinda? Kwanini halijawahi kutishia mafisadi kuwa watavuruga na kuondoa amani? Je ni kwa vile wengi wa wakubwa zake ni mafisadi?

Hebu angalia upuuzi huu wa Shimbo: “Napenda kulisisitiza hili, vyombo vya ulinzi na usalama havifungamani na upande wowote katika siasa. Kuvihusisha huko ni kutuchokoza, msituchochee wala kutuchokoza tuko kwa ajili ya kuwalinda,”

JWTZ inafungamana CCM na ushahidi ni hiki kitisho cha hivi karibuni. JWTZ imejigeuza mbwa ajikombaye kwa anayemfuga kwa malipo ya makanyagio (ukuu wa wilaya na mikoa) na upuuzi mwingine. Hili haliwezi kuwa jeshi alilolisuka mwalimu Julius Nyerere baada ya lile la kikoloni la KAR kuasi usiku wa jumamosi kuamikia jumapili 18-19 Januari 1964.

Kwa ufupi ni kwamba jeshi letu limetudhalilisha na kujidhalilisha na linapaswa kusukwa upya. Jeshi gani linalobariki wizi wa kura ukiachia mbali kutojua chanzo cha kuvunjika amani. Lijiepusha kuwa kama jeshi la polisi lililoua wananchi kule Zanzibar mwaka 2001 ukiachia mbali kuwa kinara wa rushwa na ujambazi nchini.

Jeshi la Mafisadi wa CCM halipaswi kuitwa jeshi la wananchi wa Tanzania. Haya ni matusi ya nguoni. Jeshi liache kutuchokoza na kutoa visingizio vya kitoto.


NB: Wasomaji mnaweza pia kupitia kwenye taarifa ya Human Rights Watch juu ya uvunjaji wa amani na mauaji ya Zanzibar ya mwaka 2001 vilivyofanywa na jeshi la polisi. Soma kwenye comments utaiona kwenye maoni yaliyotolewa na ndugu MBELE.

Saturday, 2 October 2010

Shehe Mpayukaji atoa kinga kwa mgombea

WIKI jana nilieleza utabiri wangu ambao si sawa na yule mpiga wa Migomigo aitwaye Shehe Ubwabwa Yaya. Mie ni mtabiri tena msomi aliyesoma somo la Nyotology, Ontology, Metaphysic na Astrology na kutoka na alama A.

Unaweza kuona jinsi ambavyo sitabirii njaa wala kutafuta kujikomba ili nipewe mabaki yatokanayo na pesa ya ufisadi.

Natoa kinga bure wala sihitaji kusafirishwa kwenda India. Hata nikiumwa nikahitaji kwenda kule nitakwenda kwa pesa yangu halali na si makombo ya mafisadi. Nitatoa kinga kwa mgombea anayeuzika na asiye shirika na mafisadi.

Hili halihitaji ruksa ya mtu wala taasisi. I mean it. This is not a calumny or con aiming at anybody. Sorry. Siku hizi nina ka-ugonjwa kama ka waheshimiwa wasio heshima kitu ambao hawamalizi sentensi bila kumwanga ung'enge uchwara ili waonekane wasomi ingawa wengi wao ni vilaza walioghushi vyeti. Hayo tuyaache. Nani atawagusa iwapo mwenzao mwenye madaraka ameamua kuwakingia kifua ili watumiane?

Hamkumsikia juzi akimuombolezea na kumwagia sifa Ewassa kwa kusema eti ni mchapakazi duniani hakuna! Wakubwa kwa kupenda kusifiana. Anyway, leo humu si mwake. Kuna siku nitawatokea kinoma ili wajue njemba nipo na bado nawapumulia kisogoni.

Kwanza nitawatajia nyota za wagombea wanaotisha kwenye kijiwe chetu, yaani Njaa Kali na Willie.

Nyota ya wa kwanza yaani Njaa Kali ni aina ya Al-dhi’b wal shaari yaani mbwa mwitu wa shari na jini wake ni infritah ambaye ni mbaya kuliko shaytan mwenyewe. Huyu jini akikupenda utapendwa. Akichukia utachukiwa hadi ujichukie.

Anapokuwa amechukia mwenye kuwa naye huanguka hovyo hovyo na kutamka maneno bila kuyamalizia. Ni jini mbaya sana ambaye anaweza kusababisha mtu kupenda ngono hata starehe. Nyota ya mama yake ni mkia yaani Al dhayl yaani asiye na faida sawa na mkia kama wenye nyota hii.

Kwa wale waliosoma khutba al Dhayl Lisan al-mizan wajikumbushe maneno: Ruwat duafa aw tukullima fihim, lam yudhkaru fi kutub al-duafa wa-al-mutakallam fihim, wanaweza kujua nimaanishacho hapa ingawa kinyume. Msiende ndani hivyo. Huko ni kwa magwiji kwenye kunga. Hivyo chukulia hiyo kama rejea tu. Kumradhi kwa kuwakoga kwa usomi wangu wa fani ya utabiri.

Jini huyu hupenda kuwafanya wenye kuwa naye kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri ukiachia mbali kuwanyima aibu. Huwafanya wachekecheke hovyo hata mahali pasipostahili kiasi cha kuonekana kama watu wa mzaha mzaha ambao ni rahisi kutumiwa na watu wengine kufikia malengo yao. Wenye jini huyu ni watu wa kuhurumiwa.

Kwani mara nyingi huwa hawajijui wala kujua wanachofanya zaidi ya kuwa watumwa hasa wa sifa za kipuuzi. Huwafanya wafanye vitu vya kipuuzi ambavyo huviona vya maana huku vya maana wakiviona vya kipuuzi.

Watu wenye jini huyu, kama ni wanaume, huwekwa mikononi na wanawake na kama ni wanawake huwa asharati hakuna mfano. Kwa wanaume huwa hawajiwezi kimapenzi yaani wako tayari hata kutembea kwa magoti ilmradi wapewe ngono hata kama ni kwa kuhatarisha usalama wao. Hawafai kuongoza hata kaya achia mbali taifa.

Wanapopata madaraka basi jua rushwa ya ngono itakuwa kubwa na kina mama hasa wenye uhusiano nao watapewa vyeo kama asante ya huduma yao.

Sasa nije kwa huyu wa pili. Huyo nyota yake ni ni Al Maisan wal Heri. Hii ni nyota nzuri sana kuwa nayo. Mtu mwenye nyota hii hupendwa na kuenziwa. Hata akifanya makosa kidogo husamehewa haraka kutokana na kuwa na vipaji vingi.

Mwenye nyota hii ni mpenzi wa watu ambaye mara nyingi yuko tayari hata kupoteza uhai wake kwa ajili yao. Si rahisi kutumiwa, kuhongwa, kudanganywa wala kugeuzwa juha iwe na wanaume au wanawake.

Jini la huyu wa pili ni Al-Nasr At-Ta'ir au tumbusi anayepaa. Huyu ni hodari wa kufanya mambo ya maana. Ni jabali hasa ambaye hata akisema kitu kinashawishi na kuaminika.

Hana mzaha katika shughuli zake. Si mkurupukaji wala mbabaishaji. Akisema kitu lazima akitolee ushahidi tena wenye kuingia akilini siyo bora ushahidi. Si rahisi kutumiwa na watu zaidi ya yeye kuwaongoza katika ufanisi. Huyu anaweza kuaminiwa hasa uongozi wa nchi hasa kama yetu iliyoko kwenye makucha ya mafisadi.

Kwa vile mpinzani wake ameaahidiwa ulinzi wa majini, japo nao ni upuuzi nami leo natangaza rasmi kuwa mgombea wangu daktari atapewa ulinzi wangu. Ulinzi wangu unajulikana na kuingia akilini. Ulinzi huu si mwingine bali kuwataka wananchi wampe kura kwa wingi awatumikie na kuwaondoa kwenye uchafu wa hawa wachovu mafisadi wasio na visheni wala utu. Mpeni kura WS mjionee mambo.

Mkimpenda mkamchagua na kumuunga mkono nani mwingine atamdhuru? Afya yake ni fit na hana ugogoro wala la kuficha. Hivyo ulinzi wangu ni kura ya ndiyo na si majini uchwara yatokanayo na njaa na kujipendekeza.

Ulinzi mwingine ni kumtangaza kila kosa hadi kila mpiga kura popote alipo amfahamu na kumkubali kuwa anaweza kutuvusha kama tutamwingiza madarakani na kumbana atimize ahadi zake anazotoa leo ili asiwe kama JK aliyeahidi pepo akaleta ghalika.

Maana wale wezi wamekuwa wakitumia ujinga na ukosefu wa habari kama jimbo lao ukiachia mbali kuwageuza wapiga kura maskini na wajinga shamba la bibi la mafisadi kujihomolea kama ambavyo wamekuwa wakifanya miaka nenda rudi.

Mwaka huu kiutaalam wa utabiri ni mwaka wa ngurumo ambazo zitasikika toka Danganyika karibu maeneo yote hadi mji wa The Hague. Hii maana yake ni kwamba wagombea wanaoshinda kwa kutegemea kuiba kura hawatafanikiwa mwaka huu kutokana na wapinzani wao kuwa makini na tayari kufa wakilinda kura zao.

Hali hii itasababisha malumbano hadi watu kunyea debe kama wataendelea na jinai hii. Kuondokana na hili ni kwa wahusika, hasa wale wezi wa kura, kuachana na jaribio hili. Maana wakati umebadilika. Kondoo wanaweza kuwatembezea kichapo hadi hata kuwaua fisi.

Na wakati wenye ndiyo huu ambapo hakitaeleweka hadi haki itendeke. Na wananchi wasiogope. Utabiri unaonyesha kuwa atakayethubutu kuiba kura atashindwa hata kufungwa. Natabiri kuwa mwaka huu Tanzania inaweza kufanya maajabu kwa kuwapiga teke wababaishaji na watesi wa taifa. Lolote lawezekana.

Wapiga kula msicheze chandimu wakati kuna chakudema. Nyinyi ni malaika na walinzi wa ukombozi. Hivyo. nitatoa ulinzi wa malaika si majini ya wale washenzi na washirikina wasiojiamini.

Natabiri kuwa kijiwe kitakomea hapa leo.

El Commandante Mwenyewe.
Chanzo: Tanzania Daima Septemba 29, 2010.