The Chant of Savant

Saturday 31 December 2011

Heri ya Mwaka Mpya 2012



Wapendwa mashabiki, wasomaji na wageni wa blog hii, tunachukua fursa hii kuwatakieni heri ya Mwaka Mpya 2012. Tunaamini mwaka 2012 utakuwa ni mwaka wa kurekebisha makosa pale tulipokosea na kuongeza bidii pale tulipofanikiwa. Kumaliza mwaka si jambo lililo chini ya uwezo wetu. Ni neema na baraka za Mwenyezi Mungu aliyetujalia kuumaliza mwaka 2011, pamoja na mazonge yake, na kuuona mwaka 2012.

Hata kama kuvuka toka mwaka kwenda mwingine ni suala la kubadili namba na tarakimu, bado kuna haja ya kujiwekea malengo binafsi kama watu binafsi na taifa na kuwa tayari kuyafanikisha. Kimsingi, mwaka 2011, kwa taifa la Tanzania ulikuwa mwaka mgumu. Kwani, licha ya serikali yetu kuendelea kulegalega na kufanya madudu,watanzania wameweza kupambana na kufanya kila walichojaliwa kufanya. Mwaka 2011 ulishuhudia kuongezeka kwa ufisadi hata utapeli. Rejea chama tawala na serikali yake kushindwa kukuza uchumi na kupambana na ufisadi. Rejea kuibuka kwa matapeli wengi wa kidini na kiroho kubwa likiwa ni babu wa Loliondo aliyehadaa ulimwengu kuwa ana dawa ya kutibu kila kitu wakati si kweli bali utapeli wa kitoto. Mwaka 2011 ulishuhudia mauaji ya kinyama yakitekelezwa na polisi huku serikali ikikaa kimya. Rejea mauaji ya Arusha na mengine mengi.
Tukio la mwisho wa mwaka la mafuriko jijini Dar es salaam haliwezi kupita bila kuongelewa. Ingawa waathirika walijitakia kuishi mabondeni kwa kisingizio cha umaskini na ukosefu wa umakini kwa serikali, bado ni pigo kwa taifa kutokana na kupoteza watu wasio na hatia hasa watoto ambao hawana uwezo wa kujipangia wapi wazaliwe au kulelewa.

Kwa upande wa Afrika, mwaka 2011 ulikuwa mwaka wa mapinduzi na kujikomboa hasa kwa wenzetu wa Maghreb ambapo tawala chafu na kandamizi nchini Tunisia Misri na Libya zilianguka huku baadhi ya watawala wakifungasha virago kwenda kuishi ugeni, wengine kufunguliwa mashtaka na wengine kuawa kinyama kama wezi wa kuku kama ilivyototeka kwa Muammar Gaddafi imla wa zamani wa Libya.

Kimataifa mwaka 2011 ulikuwa na mambo mchanganyiko kubwa likiwa ni kuzorota kwa uchumi wa Ulaya ambapo nchi za Ugiriki na Hispania ziliokolewa na mataifa mengine ya Ulaya. Kingine cha mno ni kusakwa na kuawa kwa Osama bin Laden kiongozi wa Al Qaida aliyelingaisha taifa la Marekani kwa muda mrefu hapo Mei 2, 2011.

Si rahisi kuvinjari matukio yote ya 2011. Hivyo, kwa ufupi tumalizie kwa kuwatakieni heri ya Mwaka Mpya 2012.

Friday 30 December 2011

Je taifa linahitaji kuambiwa au kuombewa?




Kuna mchezo wa ajabu umeanza hivi karibuni ambapo wajanja fulani huaandaa eti mkesha wa kuombea taifa. Hivi kweli inahitaji kuombewa au kuambiwa ukwelinaviogozi wa dini na wale wote wenye udhu kusisitiza uwajibikaji na ku-deliver. Kwanini watu wengi wanatumia njia ya utapeli ya kujifanya wanalipenda taifa hili wakati wanakwepa ukweli? Tatizo la Tanzania si mikosi wala nini bali ufisadi, ukosefu wa maadili na uongozi wenye visheni. Yeyote anayetaka kujificha nyuma ya Mungu anajindanganya na kudanganya na kupoteza muda. Hivi kupambana na ufisadi kweli kunahitaji miujiza au utashi? Mjengwa, najua unachukia ufisadi na umekwenda shule, kama siyo kutoa nafasi kwa kila mtu kutoa mawazo yake, kweli namda kama hii ingeona jua la leo? Hawa kwanini hawasemi kuwa ni wasanii wanaotumia mateso ya jamii kujiweka karibu na watawala? Nawashauri wasome kitabu changu cha Saa Ya Ukombozi.

Tuesday 27 December 2011

Xenophobia: Will it Feed Hungry South Africans?

Are Africans being saved against themselves? Photo courtesy

Recently, a Tanzanian residing in Johannesburg received a very spooky letter ordering him and nationals of Ethiopia, Kenya, Somalia and Tanzania to leave South Africa or risk being killed by the South African Black Association (SABA). The letter alleged that the mentioned people were the source of all sufferings and miseries for black South Africans, such as disease, poverty and failure.

The letter shows how blind and ignorant some South Africans have become. Instead of looking at the real enemy, they are trying to create fake one as it was recently evidenced in Libya when the rebels were fighting to topple Muammar Gaddafi. They branded any colleague from South of Sahara a mercenary! How sick is this? Some targeted every dark skinned person little knowing Libya has over one-third of the same people.

I agree with SABA that black people in South Africa still lag behind economically. However, this is not because of other Africans living there but systemic rot left behind by the apartheid regime. Those conversant with Conflict Resolution Studies are aware how South Africa’s reconciliation under South African Truth Commission (TRC) that was chaired by Archbishop Desmond Tutu, did reconcile the country politically but not economically.

Julius Malema, former president of African National Congress (ANC) Youth wing once wanted President Jacob Zuma to nationalise South Africa's rich mines and seize white-owned land. The real step is to change the system.

Despite the fact that I do not subscribe to racially inspired ideas, if we face it, the wealth in the hands of white South Africans is totally incomparable to the little money refugees make in South Africa. Anybody who asserts that African refugees rake big money and are therefore the cause of miseries for black South Africans must be out of his mind. Even if you compare the wealth South African Indians own to peanuts African refugees make in South Africa, you’ll find allegations that there are obstacles, are but baseless and ridiculous. It is like comparing an apple and a higgs boson. It is easier to predict that after South African xenophobics are done with refugees, they will turn against, Indians and whites before they turn to each other (zulu, thembu xhosa and what not) till the last person. Once they are done with refugees from neighboring countries and found that their problems are still the same and even bigger according to time, they will turn against their colleagues. If this succeeds, the same perpetrators of xeonophobic atrocities will end up becoming refugees for the second time after tearing their country apart. This time, they will nary get warm welcome as the one they were accorded when they were fighting apartheid.

It is sad to find Africans crossing discriminating against each other as it happened in Libya and once in South Africa itself. It is sad too that the same African refugees who are threatened hail from countries that sacrificed a lot to see to it that South Africa attains independence. What an irony!

Though the letter in point may be ignored or regarded as mere desperation, if one looks back at what transpired on 23 May 2008 in Johannesburg, the authorities need to take steps before SABA wreaks havoc. In 2008 at least 42 people were killed, 23 of whom were Mozambican nationals. More than 17,000 people were displaced and more than 400 suspects arrested. What is important here is not to hate each other but to embark on dialogue with all efforts focused on the real enemy-economic entropy. This does not need someone to be astrophysist or a guru in mathematic to comprehend. South Africans affiliated with SABA are shying away from the real issue and creating a bigger problem. Economic poverty is less tormenting than the mental poverty SABA is displaying.

All refugees threated must report the incident to the authorities and their embassies. Wherever there is smoke, there is fire. Ironically, the rainbow nation does not look like the rainbow itself. Is it because the rainbow does not have the black colour in its colours? Is it because desperation and ignorance have been allowed to be the modus operandi of destitute South Africans? Indeed, they need to be helped out of this malady-xenophobia. It is important to note that hate begets hate.
Source: The African Executive Magazine Dec. 28, 2011.

Helikopta za uokozi hatuna, za kuchungulia waathirika zipo

MWENZENU nina uchungu sana kutokana na mazonge yaliyomkuta mwenzetu mwanakijiwe maarufu mzee mheshimiwa Mgosi Machungi Makambale ambaye ni rafiki mkubwa wa mwenyekiti na rais wa kijiwe alhaji Mpayukaji Msemahovyo mjukukuu wa mtume Waambie yamemfika makubwa.

Si alikumba na zahama ya mafuriko yaliyofurisha jiji la Bandar Salaam ambayo imegeuka Bandar furika kutokana na miundo mbinu ya kishikaji na sheria zinazofuata kura badala ya sheria. Kwa sasa kama siyo kufukuzia riziki hapa kijiweni, Mgosi alipaswa kufikiria kurejea kwao ima Vuga Mashindei au Mtibwa.

Nakumbuka, siku hiyo ambapo mafuriko yalifurisha jiji la Bongo, nilikuwa nimetoka kukutana Mgosi kijiweni.

Tulikuwa tumejadili zahama iliyokuwa imemkuta mchumia tumbo Kafulia na kuandaa mikakati ya kutumia kanuni hizi za chama kuwatia adabu wote wanaoleta mdomo kutaka kuingilia ulaji wetu kijiweni.

Nadhani kwa yaliyomkuta Kafulia baada ya kufulia na kufuliwa, akina Edhard Ruwasha, Sam Sixx, Endelea Chenga na wengine wanaotaka kupimana msuli nami watashika adabu na kutulia kama watoto wazuri kabla hawajanyolewa bila maji.

Mie sitajali kuwa watatoboa siri zangu wala nini. Nitawavua uwanachama. Ingawa alichofanyiwa Kafulia ni kitu mbaya, ni somo kwa jamaa wa magamba wanaoshindwa kuvuana magamba.

Na kama siyo ushikaji na ushirika wa mkuu, Chama Cha Magamba ni hodari wa kutumia karata hizi na zana za maangamizi ya wajivuni na mafisadi. Mambo ya Kafulia na alivyofulia tuyaache.

Baada ya kupokea taarifa toka radioni baada ya mitandao hii ya kishikaji ambapo wawekezaji wanakula na wakubwa na kuweka mimashine mibovu kugoma, niliamua kutumia radio kupata habari kuhusiana na nakama hii. Nilianza kupata wasi wasi na jamaa zangu waliokuwa nje ya nyumba zao kutokana na mibarabara yetu inayojengwa na washirika na washikaji wa mafisadi kubomoka hovyo kutokana na kutokidhi viwango.

Kwanza nilianza kumlaumu Machungi kwa kupanga mabondeni ilhali akijua matokeo yake hata kama kodi alidhani ni nafuu asijue mafuriko yataifanya iwe aghali. Baada ya kufikiri kwa muda mrefu niliachana na lawama baada ya kugundua kuwa na lisirikali lililowanyamazia wakajenga na kuwapa umeme huku likikusanya kodi ya pango nalo ni la kulaumiwa.

Baada ya kuona lawama zangu hazisaidii, niliamua kuomba lau dua ili Mgosi Machungi na mshirika wake wa bedroom, kuku, paka hata panya wapone. Maana sikuwa na jinsi ya kumsaidia wakati ule hasa ikizingatiwa kuwa wagawaji wa kiza walikuwa wamepata sababu ya kuendelea kutukatia umeme.

Nikiwa natafuta jinsi ya kuondoa ngoa niliyokuwa nimeipata kutokana na wenye madaraka kuyatumia vibaya nilijisuta na kuachana na lawama. Maana nilisikia sauti ndani yangu ikisema: Kama si kukiibia kijiwe na kujenga hekalu lako Msa… sorry sana. Sitaji maana majambazi na wachawi wanaweza kunivamia na kuninyotoa roho bure. This is a national top secret after Kagoda and Dowans… nawe si ungekuwa kwenye msambwe kama Mgosi Machungi?

Hivyo niliachana na lawama na kuanza kupanga mikakati ya kutumia janga hili kupata ulaji. Maana kwa kaya za wezi na mafisadi, kila kinachotokea hatukiangalii kwa kuzuia kisitokee huko baadaye wala kujifunza bali kutafuta jinsi ya kuwashawishi wafadhili wamwage mipesa nasi tujifaidie. Upo hapo mshirika? Mezea basi.

Kutesa kwa zamu. Huna haja ya kuwa na nkungukwa. Siku yako ikifika utatesa. Au siyo?

Najua wasomaji walioathirika na mafuriko kwa sasa wananiona kama nawachuria na kuwakoga. Hapana ila bado niseme. Siwezi kuogopa kuuona ukweli hata kama mchungu. You know what?

Hivi unapojenga bondeni kwa kusingizia umaskini unategemea nini hasa usawa huu ambapo kwa mfano hakuna helikopta za kuokoa isipokuwa za kuwachungulia waathirika? Unajenga ukitegemea nini iwapo kuna polisi wengi wa kutwanga watu virungu na wanajeshi wa kuonyesha gwaride lakini si wa uokozi? Shauri yako! Use your bloody brain madala ya kufikiri kwa makario. Hayo ni mambo ya Masumburi, si mimi

Najua masahibu ya umaskini hasa kwa wale wasio na nafasi ya kula bure na kuhomola kama mimi na wapambe zangu.

Najua wengi wajiuliza mantiki ya kuwa Meya hasa yule anayetumia ‘makalio kufikiri’ ambaye siku zote anafukuzia ulaji badala ya kutoa huduma na kutimiza majukumu yake.

Anayesema hivi si mimi. Maana baada ya mitandao feki kurejea angani na kupata fursa ya kuwasiliana na mgosi Machungi kitu cha kwanza nilichosikia ilikuwa ni lawama.

Alisema, “Meya hatikumuona, mbunge hatikumuona. Kwani makosa ya kuishi bondeni yetu peke yetu. Shi ni wao waliotufumbia macho tukaendeea kuishi Jangwani?”

Aliendelea, najua sasa mibaka inaandaa mipango ya kuvuna misaada huku vibaka nao wakitihangaisha kana kwamba hakuna siikai.”
Ingawa sikupenda lugha ya matusi kwa watu wakubwa kama mimi, malalamiko ya Mgosi yalinifumbua macho kuanzisha mfuko wa kuchangia waathirika wa mafuriko ili mimi na bi mkubwa wangu na watu wetu tuvune fweza.

Maana kufa kufaana ati. Hivyo, wewe unayesoma unabii changia mfuko wa wahanga wa mafuriko kupitia akaunti AA 1277890005JK777 TZ000 iliyofunguliwa kwenye benki ya Bank of Tufaane. Onyo, mchango wako unapaswa kuanzia madafu laki moja ili kuonyesha uchungu kwa kaya yako.

Hebu tuache mambo ya ulaji. Mgosi amepoteza magodoro mawili, simu mbili za kiganja, kuku wanne na mkataba wa upangaji huko apangako Luhanga mwisho. Ni mali nyingi hizi hasa kwa mlalanjaa kama Mgosi.

Hata hivyo, tunamshukuru Mungu Mgosi amebaki na pa kushika kwa kubakiwa na mshirika wake wa bedroom bi mkubwa mama Kidume. Magodoro yamekwenda, hata mshirika wa bedroom kama siyo kunasa kwenye mti na Mgosi kuyapiga maji na kumnyofoa, lololo tungekuwa tunaongea mengine! Mgosi angekuwa sasa analiasa kisambaaa, tate nane tate nage kaita mgima mgima sijui angelalia nini yarabi!

Mgosi ana hasira na watawala walioruhusu waroho wachache kujenga nyumba mabondeni na kupangisha wakati wao hawaishi huko. Ingawa alifarijiwa na mkuu pamoja na walaji wenzake kuja kumjulia hali, bado hajawasamehe kwa kupinda sheria kutokana na masilahi yao ya kisiasa ya kutafuta kura ya kula kwa watu wa mabondeni.

Tumalizie kwa kuwapa pole waathirika
wa mafuriko hata kama walijitakia. Sorry walilazimishishwa na ukapa.Chanzo: Tanzania Daima Desemba 28, 2011.

Monday 26 December 2011

Petroli, dizeli yauzwa kwa Sh10,000 kwa lita na nchi bado inakalika

Juddy Ngonyani,Sumbawanga

BAADHI ya wamiliki na madereva wa vyombo vya usafiri vinavyotumia mafuta katika Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, wameuomba uongozi wa Serikali mkoani humo kuingilia kati tatizo la upatikanaji wa nishati hiyo ikiwa ni pamoja na kujua bei halali wanayopaswa kuuziwa.

Wakizungumza na gazeti hilo kwa nyakati tofauti baadhi ya wamiliki na madereva walisema kuna tatizo la kukosekana kwa mafuta katika vituo mbalimbali vya mji wa Sumbawanga.Waliolalamikia tatizo hilo ni pamoja na Issa Lubega, Justin Mballa, Chacha Mwita na Zacharia Nsangazila.

Wamesema kwa sasa mafuta a petroli na dizeli yanauzwa kwa bei ya kati ya Sh6,000 na Sh10,000 kwa lita moja na kwamba yanauzwa na wachuuzi ambao inaaminika kuwa wanayapata katika vituo vya mafuta.

Waliiomba Serikali kuingilia kati tatizo hilo na kuhakikisha kuwa bei zinashuka hadi kufikia kati ya Sh3,000 na Sh5000 kwa lita.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya aliwataka watumiaji wa nishati hiyo kuwa na moyo wa subira wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiendelea na uchunguzi kuhusu tatizo hilo.

Manyanya pia aliwaasa wafanyabishara ya mafuta kuwa wakweli kwa wateja wao, ili kuepuka malalamiko na usumbufu.
Chanzo: Mwananchi Desemba 26, 2011.

Saturday 24 December 2011

Nawatakia heri ya X-mas na Mwaka Mpya 2012


Ingawa huku tuna X-mas wanayoita Green one kwa sababu ya kutokuwapo theluji, kwa waswahili kama mimi tunashangilia. Maana hakuna cha kusafisha njia ziingiazo na kutoka majumbani mwetu wala baridi ya kukera ukiachia mbali utelezi.
Tunachukua fursa hii kuwatakia Noel njema na heri ya Mwaka mpya 2012.

Friday 23 December 2011

vituko vya viongozi wetu na maafa yake! mafuriko siasa mafuriko siasa!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Bi. Monica Luis, Mkazi wa Jangwani aliyeathirika na mafuriko ya Mvua kubwa iliyonyesha jijini kuanzia majuzi, wakati makamu alipotembelea katika Kambi ya Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika wa mafuriko hayo. Picha toka Mjengwa Blog.

Watawala wetu wakishapata hugeuka miungu kiasi cha kuogopa hata kuwakaribia wapiga kura yaani waliowapa huo utukufu. Huyo juu eti anaongea na mhanga wa mafuriko! Hivi kwa umbali huo mrefu kweli wawili hawa wanaweza kuongea lugha moja tena wakaelewana? Huu ni udhalilishaji tosha ambao wananchi wanapaswa kuuona na kuufanyia kazi kwa kukinyima kura Chama Cha Mapinduzi.

Habari zilizolipotiwa ni kwamba wakazi wa mabondeni wameapa kutohama makazi yao kama alivyoagiza rais Jakaya Kikwete. Kwani wao kilichotokea wanaona ni kama ajali tu. Hivyo wataendelea kukaa mabondeni. Je serikali itaufyata kwa kuogopa kupoteza wapiga kura? Je serikali, kama ilivyojiingiza kwenye matatizo, itaendelea kuwaandalia makazi mapya kana kwamba makazi wanayoishi ni halali? Je hawa wakazi wa mabondeni wamejua udhaifu wa serikali kujiingiza kwenye tatizo ambalo si lake? Je wakazi wa mabondeni wanajua jinsi serikali isiyoaminika? Je serikali kuahidi kuwatafutia maeneo mapya ni halali zaidi ya kuunga mkono vitendo vya kuvunja sheria? Kesho tutasikia wamachinga wanaofanya biashara kwenye barabara na maeneo ya wazi nao wakitaka wapewe maduka!

Kimsingi tatizo la mafuriko ni matokeo ya utawala wa kubabaisha na kujuana na utokanao na rushwa, kuchafuana na wizi wa kura.

Wednesday 21 December 2011

Tubadili jeshi la polisi kabla ya kutupeleka kuzimu

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la kuwabambikizia kesi waandishi wa habari hasa wale wanaolikosoa jeshi la polisi au kufichua ufisadi na maovu mengine katika jamii ili ima kuwatisha au kuwanyamazisha au kuwasumbua. Jeshi tulilodhani ni letu, taratibu limegeuka kuwa lao na mlinzi na muhimili wa uovu, uonevu, ufisadi hata rushwa.

Mwaka huu tumeshuhudia waandishi wa habari wawili wa gazeti moja wakibambikiziwa kesi zisizo na kichwa wala miguu. Kabla ya hapo, mwandishi mwingine wa habari wa runinga alibambikiziwa kesi kabla ya mahakama kutomkuta na hatia na jeshi la polisi kuishia kuaibika kimya kimya.

Leo tutajaribu kurudusu hali halisi ya jeshi letu la polisi na nini kifanyike ili kulifanya liwe la wananachi badala ya kuendeshwa na kikundi kidogo cha watu kinachojificha nyuma ya madaraka ambayo nayo pia ni ya wananchi. Kwa mtu anayejua ni kiasi gani jeshi la polisi limechafuka na kupoteza imani kwa wananchi, anashangaa mantiki ya kuwepo kwake. Anashangaa hata hao wakubwa zake wanalipwa kwa lipi iwapo wanashindwa kujenga nidhamu na jeshi la kisasa hasa karne ya 21 ambayo imeshuhudia kuanguka kwa utawala mchafu na wa kikale katika nchi mbali mbali ambapo polisi na vyombo vingine vya dola vilikuwa vikitumiwa na kundi dogo la walevi wa madaraka kuwanyanyasa wananchi huku likishindwa kutambua kuwa kama si kodi za wananchi, hakuna cha jeshi la polisi wala watawala vinavyoweza kuishi.

Historia ya jeshi letu tangu kuingia mfumo wa vyama vingi ni chafu na yenye kukera. Tangu 1992 Tanzania ilipolazimishwa kuingia mfumo wa vyama vingi, chama tawala na jeshi la polisi hawakubadilika. Waliendelea na mawazo mgando ya wakati wa utawala wa chama kimoja. Nani mara hii kasahau mwaka 2000 wakati inspekta jenerali wa polisi wa wakati huo aliyestaafu na kuzamishwa na kashfa ya kutembea na mfanyakazi wake wa ndani, Omar Mahita, alipowaambia wanachama wa chama cha wananchi kuwa kama wao ni ngangari yeye na jeshi lake ni ngunguri? Ajabu Mahita alipojigeuza mwanasiasa kinyume na sheria na kanuni za utumishi wa umma, hakuna aliyekuwa na busara wala ujasiri kumuonya hata kumshauri aache kuvunja sheria. Nani angemuonya wakati aliokuwa akiwakingia kifua ni chama tawala? Nani angemkamata iwapo yeye ndiye alikuwa mkuu wa jeshi la polisi?

Baada ya Mahita kujisahau na kujichafua kiasi hicho, wengi walidhani watawala wangejifunza kufikiri na kukomesha mchezo huo. Lakini wapi! Nani mara hii kasahau mauaji ya Arusha ya Januari 5 ambapo watu watatu waliuawa mmojawapo akiwa raia wa Kenya? Mauaji ya watu wasio na hatia hayakuishia kwenye maandamano ya kisiasa. Nani mara hii kasahau mauaji ya jana ya raia asiye na hatia wilayani Kasulu mnamo Agosti 8 ambapo askari polisi walimuua kinyama Festo Andrea tena kwa kumuingiza vijiti kwenye sehemu za siri mbele ya baba yake marehemu? Mauaji ya raia wasio na hatia nchini ni mengi. Nani mara hii kasahau polisi walivyommiminia risasi raia ambaye walikataa kutaja jina huko Runzewe wilayani Bukombe mwezi huo huo wa Agosti alipouawa Andrea? Nani mara hii kasahau mauaji ya raia huko Ubaruku Mbeya wakati wananchi wakipinga kuingia kwenye eneo lao kwa lori lenye uzito zaidi ya unaoruhusiwa ambapo mtu mmoja aliuawa? Mifano hiyo ni tone kwenye bahari ya mauaji ya kinyama yanayofanywa na jeshi la polisi wale wale tunaowalipa mishahara kwa kodi zetu.

Ukiachia mbali mauaji na kushiriki siasa kwa kubeba chama tawala, polisi wetu wanasifika kwa rushwa kiasi cha kuwa taasisi inayoongoza nchini katika rushwa. Kuhusu hili Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) ilitoa taarifa kuwa jeshi la polisi linaongoza kwa rushwa mwaka huu. Taarifa ilisema, “ Inonesha kuwa asilimia 62.7 ya wananchi hao hawana imani na jeshi hilo kwa kuwa halizingatii maadili, huku asilimia 44.6 wakisema kuwa maofisa wa polisi ndiyo vinara wa kupokea rushwa, asilimia 55 walisema kuna uhusiano mzuri kati ya jeshi la polisi na wao katika kuwakatama wahalifu,” Taarifa hii haina utata. Ni ukweli usiopingika kuwa askari wetu licha ya kuwa wauaji ni wala rushwa wakubwa. Kama ingeundwa tume ya kuchunguza mali zao, wao na wafanyakazi wa mamlaka ya mapato na uhamiaji, wanaongoza kwa kuwa matajiri.

Ukiachia mbali kula rushwa, polisi wetu wana sifa moja kubwa chafu ambayo ni kuwabambikizia watu kesi ili ima watoe rushwa au wawakomoe. Ukienda kila mkoa hiki ndicho kilio cha wananchi. Wananchi wanajiuliza. Kama kweli polisi wetu wangetumia akili ya kawaida biashara ya mihadarati, ujambazi ambao umegundulika kuwa unafanywa na baadhi ya polisi ama kwa kukodisha bunduki au kusindikiza mizigo ya wizi, ufisadi, rushwa na madhambi mengine yasingetamalaki kiasi cha kumlazimisha rais kuunda tume.

Ajabu, waandishi wa habari tunapofichua uchafu kama huu tunaandamwa kwa kubambikiziwa kesi ili kututisha, kutunyamazisha hata kutusumbua kama ilivyotokea hivi karibuni kwa waandishi wa habari wa gazeti hili Mhariri mtendaji Absalom Kibanda na mwandishi Samson Mwigamba. Jamani, kwanini polisi hawataki kukubali ukweli kuwa tatizo si wakosoaji bali wao wenyewe? Kilicho wazi ni kwamba waandishi wa habari ni kama nyuki. Ukiua mmoja wanaibuka wengine wengi. Tunatoa taarifa kwa serikali na jeshi lake la polisi kuacha uonevu, ufisadi, rushwa, ubabaishaji na mauaji ya raia wasio na hatia. Madaraka yana mwisho. Hata hao polisi wanaotumika kama nepi kuna siku watastaafu na kuonja adha ambayo wananchi wenzao wanaonja. Nchi hii ni yetu sote kwa sawa.

Tusidanganywe na madaraka ambayo siku zote hulevya. Wako wapi akina Muammar Gaddafi na wapambe wao? Inatisha kuona tunaposherehekea miaka 50 ya uhuru, bado kuna taasisi tena za umma zinatenda madudu ambayo hata mkoloni hakutenda! Nchi huru lazima iwe na jeshi huru lenye kujua na kutenda haki, kulinda wananchi na si watawala, kuwajibika na kuelimika na siyo jeshi la maguvu na unyanyasaji kama tulivyoonyesha hapo juu. Kama watabishia hili tutakuja na ushahidi mwingine zaidi. Je wahusika wanataka tuanze kuwaripoti Human Rights Watch ndipo wajue wanafanya madudu?
Tumalizie kwa kushauri: tubadili jeshi la polisi kabla ya kutupeleka kuzimu.
Chanzo: Tanzania Daima Desemba 21, 2011.

Kijiwe chagawa nishani kama njugu

JUZI kijiweni kwetu kulikuwa na shughuli bab kubwa. Dk, profesa, Al Haj, Mwalimu, Field mashall, shehe, ulamaa,maulana, Man and a half, askofu, Mpayukaji mkuu wa kijiwe niliamua kutoa nishani kwa washirika zangu kwa uvumilivu na kufumba macho niendelee kuhomola na kina Mbwa Mwitu.

Mtu wa kwanza kupewa nishani alikuwa ni mgosi Machungi kwa ikiwa ni shukrani yangu kwa kujikomba vilivyo na kuhakikisha mzee mzima siguswi hata ninapofanya mazabe. Amehakikisha anawanyamazisha vidomodomo wanaotaka kugusa ulaji wangu. Machungi ambaye wanakijiwe humtania kuwa ni spika wa kijiwe al maarufu Baba Makidamakida kutokana na lugha yake ya kucheza makidamakida. Mgosi alichukua nafasi ya msomi Sam Sixx Mkatatamaa. Kupewa nishaku kulizua utata ni kwanini alipewa nishani huku nikimnyima Sam Sixx.

Watu wengine wagonjwa kweli kweli. Wakiniona nachekacheka wanadhani kicheko changu na tabasamu ni vya kweli. Kwa taarifa ya msionijua, mimi ni bingwa wa kulipiza visasi hasa kwa viherehere wanaotishia ulaji wangu.

Juzi niliwaambia jinsi Eddie alivyoniadhiri kwenye sakata la kuvuana gamba kijiweni. Adhabu yake ya kwanza kama utangulizi ni kumnyima nishani ili baadaye nimtoe nishai. Anadhani nilishindwa kumpa nishani kama ningeamua?

Najua ananilaumu kwa sasa bila kujua kuwa anapaswa alaumu domo lake na woga wake. Hata kama kwenye kashfa ya Richmonduli ya wizi wa pesa ya mkaa kwa kumpa gabacholi tenda ya upendeleo wakati ni tapeli tulikuwa wote kwanini asije nyumbani tukayamaliza badala ya kwenda kunianika? Hopeless kabisa.

Halafu mpuuzi huyu eti ana mpango wa kutaka kurithi nafasi yangu nitakapoachia ukanda wa kuibia kijiwe!

Aliyefuata kwa kupewa nishani ni loh! Nimesahau jina lake! Anyways, majina ya waliopata nishani si muhimu zaidi ya wale walionyimwa. Maana waliopewa hawalalamiki ingawa wanalalamikiwa.

Aliyenyimwa nishani si Eddie Ewassa tu bali hata brother Johhnnie Sam Mali-sera ambaye kijiweni hujulikana kama mzee Maneno kutokana na maneno yake ya kufyatua na lafudhi yake ya ki-Idodomya.

Huyu bwana nilimnyima nishani kutokana, kwanza, kutaka kushindana nami kwenye uchaguzi wangu wa kwanza wa kuwa mkuu wa kijiwe miaka kama nane sita iliyopita.

Pia mke wake bi mkubwa Hana Mali-sera ana tabia ya kunikosoa kosoa hasa akimuunga mkono Sam Sixx na wenzake wanaposhambulia utawala wangu kijiweni. Huyu mama ametokea kuwa mwiba kiasi cha kunifanya nikose usingizi. Hata hivyo kwa kumnyima mshirika wake wa bedroom nishani, nadhani message sent. Atachagua kusuka au kunyoa.

Ukiachia mbali niliowanyima nishani kutokana na kuwalipizia visasi na kuwapa taarifa kuwa mie siye yule wamtaniaye, kuna wengine niliwasahau kiasi cha kujisikia vibaya ingawa hapo baadaye nitawapa nishani.

Hawa ni Endelea Chenga na Rosti Tamu Laazizi ambao nitawapa nishani kutokana na kufanikisha mikakati yangu ya kuukwaa ukuu. Pia ndugu yangu Petero Nonyi wa Noni naye nitamkumbuka kipindi hiki. Hivyo, nawataarifu wasikate tamaa.

Kipindi hiki nikiwapa nishani nitahakikisha na mshirika wangu wa bedroom mama Kidume Riziki anapata pamoja na kidume chenyewe Riziki. Hawa watapata nishani kutokana na kufanikisha ulaji kwenye familia yetu hasa mke wangu mpendwa mwalimu Salima ambaye pia ni rais wa wanawake wote kijiweni chini ya chata lake la MAWAWA, yaani Wake za Wakubwa na Maulaji.

Rizi nitampa kutokana na kufanikisha kuwagawanya vijana kijiweni pale wanapotaka kuingilia ulaji wa mshua. Ikumbukwe kuwa yeye pia ni rais wa vijana kama ambavyo Halfa ni rais wa chipukizi.

Pia nitahakikisha nasuka mpango na vyuo vikuu vya kule Ulaya nilikosomea kuhakikisha naye anapewa shahada ya Udaktari tena wa Uchumi na Sheria.

Pia napanga kutoa nishani kwa mgambo wa kijiwe al maarufu Polishi wa kijiwe. Hawa wamefanikiwa kuwatia adabu wote wanaopinga ulaji wangu. Wamekuwa wakifanya kazi kubwa hasa kuwapiga wanywa kahawa wanaotaka kuanzisha mada za kunipinga au kuandamana kwa midomo kupinga maulaji yangu.

Nisiwachoshe na zoezi la kutoa nishani. Baada ya kuhitimisha zoezi hili niliteua wawakilishi wa wanywa kahawa kwenye vijiwe marafiki huko nje ya nchi.

Pale kwenye kijiwe cha River Road Nairobi nilimteua shoga wa mke wangu, Batinda Kwaherini kuwawakilisha walevi na wanywa kahawa pale Nairobi.

Pia nimemteua daktari mwenye shahada kwenye kuzuia jinai ya kughushi (PhD in faking) Dolorous Kamaliza kuwa mwakilishi wetu kwenye kijiwe cha kahawa cha Udachini ambako nasikia kahawa inanywewa sana.

Sikuishia hapo, kwa mamlaka niliyopewa na kijiwe, nimemteua bwana Phil Zilipendwa Mammie kuwa mwakilishi wetu kwenye kijiwe cha kwa akina Huaa Guo Feng ambako nako kutokana na baridi nasikia kahawa inanyweka vilivyo.

Kimsingi hawa washirika wangu nilitaka kuwapa nishani. Lakini baada ya kusikia minong’ono kuwa kama wanakijiwe waliwapiga teke wanapewa nishani za nini.

Kwa hasira niliamua kuwaudhi hawa waliowapiga teke kwa kuwapa ulaji mkubwa tu. Waende kule waniwakilishe na si wanakijiwe wambea wasio na shukrani hata ukiwapa takrima wakakuchagua bado wanataka eti uwakomboe wakati hukuchaguliwa kuwakomboa bali kurejesha takrima yako.

Leo sitasema mengi kutokana na kuwahi kwenda kupanda pipa kwenda kutanua na bi mkubwa baada ya kujihakikishia kuwa tumeshinda zoezi la kuvuliwa magamba. Najua hapa wasomaji wameishaanza kutoa mimacho wakidhani nimechanganyikiwa kupanda pipa wakati hata nauli ya dala dala yenywe ni mbango.

Ninaposema kupanda pipa namaanisha kupata lift kwenye shangingi la fisadi fulani ambaye anataka kunitumia kumsafisha. Upo hapo mshirika?

Kabla sijasahau. You know what? Msianze kuchanganyikiwa kwa maulaji niliyoelezea pale juu mkadhani nimewatosa baadhi ya washirika zangu wa karibu.

Kwa ufupi huo hapo juu ni mhutasari wa mipango yangu ya mambo nitakayofanya siku nikigombea urais nikaupata. Hivyo, msihangaike kwenda kwa vigagula bure kuniroga. Pia muelewe kuwa haya yaliyoandikwa yaliandikwa nikiwa kitandani naota.
Chanzo: Tanzania Daima Desemba 21, 2011.

Sunday 18 December 2011

Kafulila asipoacha tamaa na papara atafulia kila aendako


Ingawa kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini NCCR-Mageuzi, David Kafulila si haki, kulitarajiwa kutokana na tabia ya mhusika. Kafulila alipoingia kwenye siasa za upinzani alijiwekea malengo makubwa kupita uwezo wake. Kwa wanaokumbuka kilichomtoa CHADEMA, watakubaliana nasi kuwa Kafulila hajatulia.

Bahati mbaya sana kwa Kafulila, anataka kufikia malengo yake kwa njia ya mkato ambayo ni kuanzisha vurugu zisizo na sababu kwenye vyama. Wapo wanaomuona kama mganga njaa na mtu mwenye tamaa. Wengine wanamuona kama Uvuruge wa kawaida wakati wengine wakimshuku kuwa pandikizi la CCM. Yote yawezekana. Je Kafulila atarejea CHADEMA? Je CHADEMA, kwa alivyowachafua, watakuwa dhalili kiasi hiki kumpokea? Je Kafulila yuko tayari kuramba matapishi yake ili angalau apate nyenzo ya kurejea kwenye ulaji? Je Kafulila ni mwanasiasa makini au mleta fujo na mtafuta riziki kwa mgongo wa kisiasa? Je Kafulila atarejesha kiti chake? Je atakwenda CCM?

Kimsingi, pamoja na Kafulila kufukuzwa na mtu mchafu kuliko yeye yaani James Mbatia ambaye anasemekana kuwa pandikizi na kuwadi wa CCM, anapaswa kujiulaumu kwa kutaka kuukata mkono uliokuwa ukimlisha yaani chama. Na hapa ndipo anapoteza umakini na upambanaji aliokuwa akivishwa wakati si mpambanaji kitu. Kama kweli alilia asamehewe na Mbatia tena mbele za watu, basi hana lolote zaidi ya kubangaiza. Kama alikuwa akiamini alichokuwa akisimamia na kupigania, hakupaswa kulialia kama kichanga. Hata hivyo, kutimuliwa kwa Kafulila kuna somo kuwa CHADEMA ni chama makini. Kwani wao hawakumtimua zaidi ya kumvua uongozi kwa faida yake na chama. Bahati mbaya Kafulila hili hakulipata akaamua kufunga virago kumkimbia mjusi na kumkumbatia mamba. Ama kweli wahenga walinena kuwa ngoma ya watoto haikeshi.

Kafulila anapaswa akae ajifue na atulie kama kweli ana ajenda ya maana na yenye mashiko katika siasa zaidi ya kutafuta uheshimiwa ili kuhomola. Wenye akili tieni akilini siasa si lelemama wala nyenzo rahisi ya kutafutia neema miongoni mwa mafisi na mapapa kama ilivyotokea kwa Kafulila. Yetu macho kuona nini kitafuata.

Thursday 15 December 2011

Rais mwingine atupwa jela ni Chirac (Bulldozier)


Mwezi Desemba unaingia kwenye kumbukumbu kama mwaka wa uwajibishaji. Mwaka 2011, kadhalika unaingia kwenye vitabu vya historia kuwa mwaka wa mapinduzi. Siku chache baada ya rais wa zamani wa Israel Moshe Katsav kutupwa gerezani kwa ubakaji, mwenzake wa Ufaransa Jacques Rene Chirac amepewa kifungo cha nje kutokana na kupatika na hatia ya matumizi mabaya ya fedha za umma. Ulaya na mashariki ya kati wamefungua pazia. Je wezi wetu watanusurika iwapo rais wa taifa fadhili kama Ufaransa anaweza kuhukumiwa kifungo. Kwa habari zaidi, BONYEZA HAPA.

Wednesday 14 December 2011

Omar Bashir Traps Kenya in Political Cubism

Bashir in Kenya for constitution promulgation Photo courtesy
The wrangles evidenced recently between Kenya’s Judiciary and the Executive over the ruling that Sudanese strongman, Omar Bashir, be apprehended shall he visit Kenya, left many analysts flabbergasted. One judge, Nicholas Ombija, made a historical ruling when he ordered the Minister for Internal Security to see to it that should Bashir set foot on Kenyan soil, he must be apprehended and handed over to The Hague.

We used to read about such rulings made by European judges, famous ones being those that were made by Spanish Judge Fernando Andreu, and French judge Jean-Louis Bruguière, who in April 2008 and November 2006 respectively, indicted Rwandan President, Paul Kagame. When these two judges indicted Kagame, many people wrongly thought that this was a venue for only European judges. Now that Ombija has opened the Pandora’s Box for our bigwigs, who will be safe?

According to Kenya’s Minister for Foreign Affairs, it is difficult for the Kenya government to abide by the ruling of its own court. What a dangerous stance! The Minister holds that Kenya will abide by the AU position that opposes the indictment of Bashir.

How can a free country endanger its freedom for the sake of an individual who is not its citizen? Legally and logically, the constitution of Kenya is above that of AU. Whatever Kenyans do, Kenya comes first. Why is Kenya upholding AU’s non-binding decision whilst it violates the Rome Statutes that it signed voluntarily? Why does Kenya want to abuse its own new constitution before even it marks a year? Why doesn’t Kenya do like Uganda that distanced itself when Bashir was invited to a conference in Kampala?

It is shocking and sad to note that Kenya’s Minister for Foreign Affairs who was dispatched to Khartoum to mend fences, does not realise that the AU has lost its legitimacy by supporting illegitimate regimes, even when they have committed atrocities against their people. If anything, though the government in Nairobi is still flexing its muscles, the dent… deep and humongous one… has already been made.

Will the Kenya government taint its image in defence of a dictator? Will Kibaki uphold the constitution and serve the Kenyans that voted for him or trample over it and serve the Sudanese strong man? For what reasons and gains?

Kenya’s Executive arm is waging a losing battle, thanks to the fact that the judge made his decision based on the provisions of the new constitution. Therefore, whoever advises the Executive should be wise to underscore the fact that, under the new constitution, nobody is above the law. If the Executive is still thinking that it is operating in the past when the president was above the law and the Executive above judiciary, they need to be told that things have long changed.

Kibaki spoiled the party at the promulgation of new constitution by inviting Bashir. Will he add salt to injury? Thanks to the euphoria Kenyans were in, he got away with it. Will he get away with it again? The answer is nope. Logically, it doesn’t make sense for Kibaki to dent his image by siding with a dictator indicted for committing genocide against his own people.

Dr. Willy Mutunga, the Chief Justice has already weighed in heavily and categorically so to speak. Responding to rants that the executive were not thinking about complying with the ruling, Mutunga was quoted as thus: “The Judiciary and its officers shall not be intimidated to bend the law.” To make his message clear, Mutunga added that Kenya must choose between anarchy and the rule of the law. Suppose the executive stick on their guns, will the judiciary allow itself to be cowered or stiff its neck and therefore create a crisis especially at this time Kenya is at war with Al-Shabaab?

Kenya has nothing to lose by dumping Bashir. Kenya is a major economic and political player in South Sudan. Shall it keep on thinking it can serve two masters namely Bashir and South Sudan? It should not wonder when South Sudan decided to part ways with it. The French sages say:“les amis des mes sont mes amis.” That is, the friends of my friends are my friends. What of the enemies of my friends? Doing Bashir’s laundry will leave Kenya messy and stinky.

Source: The African Executive Magazine Dec. 14, 2011.

BARUA YA WAZI KWA KIKWETE NA LOWASSA


Waheshimiwa, salamu zenu,
Nitangulize samahani kuwasumbua kutokana na shughuli na yaliyowakuta hivi karibuni hasa kwenye zoezi zima la “kujivua gamba” ambalo hata hivyo halikuvuka zaidi ya kutuna. Maana watani wenu wanasema kuwa badala ya kulivua gamba mmevishana gamba kiasi cha kuchanganyana na kuuchanga nya umma. Wengi hawakuamini kuwa marafiki ambao hawakukutana barabarani wangevuana nguo badala ya gamba kama ambavyo vyombo vya habari vilikuwa vimetangaza.

Haya si maneno yangu; ni ya wengi ninaosikia mitaani, majumbani, kwenye vituo vya daladala, baa hata vijiweni wakisema kuwa kuvuana gamba kumbe kumeishia kwenye kuvuana nguo! Wengi wanasema kuwa hawashangai. Kwani walilitegemea hilo kutokana na kutoka matamshi yanayogongana hasa ikizingatiwa kuwa kila mtu aliweka wasemaji wake kwa chati.

Pia nichukue fursa hii adimu kuwapa pole kwa mfarakano wa mawazo unaoanza kujionyesha kati yenu. Najua hapa wasiojua siri ya siasa kuwa ni mchezo mchafu ambapo hakuna adui au rafiki wa kudumu bali maslahi ya kudumu wamehanikiza kushangaa hili.

Hata hivyo, jambo moja ni dhahiri. Mmetoka mbali na bado mwendako ni mbali hasa legacies zenu hapo baadaye. Good wine needs no bush walisema wazungu. Nanyi mlikuwa mvinyo mzuri kabla ya kuchacha na kuchakachuka kiasi cha kuanza kustukiana. Je tatizo ni nini? Je hamna wasaa wa kukutana kutokana kuwa bize au mnawaongopa wambea wasifichue njama zenu?

Hakuna shaka. Nyinyi ni marafiki na washirika wa muda mrefu mna mengi mliyoshirikiana yawe mazuri mabaya ya wazi na ya kificho. Nakumbuka maneno ya Lowassa kuwa urafiki wenu si wa kukutana barabarani bali mahali fulani tena kupanga mikakati ya kutimiza malengo yenu kwa gharama yoyote bila kujali nani anapinga au kuunga mkono mipango yenu. Hivyo, urafiki huu hauwezi kuvunjwa na wambea au vyombo vya habari wala kuvishana magamba ingawa mnayo tangu enzi za mwalimu. Je nini kimewasibu kiasi cha kuruhusu wambea wa kisiasa wawatenganishe haraka na rahisi vipi? Je ni arobaini ya mwizi au kutimia usemi kuwa kila kilicho na mwanzo sharti kiwa na mwisho? What is the problem?

Kuna maswali ambayo leo ningependa niulize kwa utii na taadhima. Kwanza, kama kumbe hamna ukaribu na siri kiasi hiki, Bwana Kikwete, ni kwanini ulimteua kuwa waziri mkuu wakatiukijua kuwa akizidiwa anaweza kukugeuzia kibao kama alivyofanya hivi karibuni kule Dodoma tena mbele ya vikao ambayo kila jicho la watanzania lilikuwa pale?

Pili, kama jamaa mwenyewe ni gamba kiasi hiki ni kwanini ulimpigia kampeni wakati ukijua kuwa wakati ukifika utamtosa? Una habari kuwa kama asingekung’ang’ania angekuwa historia? Je umekubali kurejesha majeshi au unafanya kile wazungu husema: retreat in order to advance? Je umefanya hivyo baada ya kuona ni zigo zito lisilobebeka au tuseme nanga shingoni mwako? Je alimaanisha nini aliposema kuwa aliachia ulaji kuokoa chama na serikali yake?

Barua hii ni ya watu wawili. Hivyo, tutakuwa tukiuliza mmoja baada ya mwingine. Sasa ni zamu ya bwana Lowassa. Je Bwana Lowassa una uhakika njia uliyotumia ni salama kwako na kwa rafiki yako au ni yale ya kama mbaya mbaya acha wote tukose? Wapo wanaosema kuwa jamaa yako na rafiki yako ni bingwa wa kuvizia na kulipiza visasi kama ilivyotokea kwa akina Samuel Sitta, je umejiandaaje kama hii ni kweli ingawa sisi tunaona kama umbea wa kawaida tu? Je akiamua kutumia shutuma za marehemu baba wa taifa huoni patachimbika bila jembe kutokana ukweli kuwa jamaa anakubalika ingawa alishaondoka zamani?

Nilisahau kusema mapema kuwa mie ni shabiki wenu nyote wawili kufa. Hivyo, siandiki haya ili mniwekee alama ya X halafu mnitumie mifedha kama vyangudoa wa kimaadili na madili wanavyofanya. Nauliza kutokana na mapenzi yangu kwenu hasa nikizingatia kuwa tangu mwaka 1995 nawajua kama mapacha ingawa upacha wenu wakati mwingine hubadilika hasa mnaposhutumiana na kutaka kutoana magamba kabla ya kuvisha hayo magamba.

Bwana Lowassa, je ni kwali kuwa una ndoto ya urais? Je unadhani rafiki yako tena wa chumbani Jakaya anaweza kukusaidia tena iwapo watu wanakusakama na hawakemei ukiachia mbali ukweli kuwa aliwateua wao kwa kazi hiyo maalumu?

Kuna swali jingine ambalo wengi kwenye mabaa na cite kama ile ya Makongoro wamekuwa wakijiuliza: “Kwanini umemgeuka sasa na si wakati wa kushutumiwa na si wakati ule ulipoambiwa upime na kuamua mwenyewe? Halafu kuna swali moja nilitaka kusahau. Nasikia wakikuita waziri mkuu mstaafu, je ni kweli kuwa ulistaafu au uliachia ngazi? Je wanafanya hivyo ili kuepuka umma kujua kuwa ukustaafu halafu kuhoji kama ukustaafu kwanini unalipwa kama mstaafu wakati wewe si mstaafu?

Nimalize kwa kuwauliza wote wawili kama mlivyotajwa hapo juu, je mnaona kuwa mipango yenu ya kukaa madarakani kweli inawezekana hasa wakati huu ambapo mnamalizana wenyewe kwa wenyewe? Je ukweli ni upi, nyote ni Richmonduli au kuna mmoja anampakazia au kumtumia mwenzie? Juzi nilisikia umoja wa vijana ukikoroma kuwa wazee ndiyo wanakwamisha chama chenu. Je nyie bado ni vijana au mmezeeka baada ya 1995?

Nimalizie waraka huu kuzidi kuwahakikishia kuwa nitaendelea kuwaunga mkono katika mabaya na mazuri. Ila naomba kitu kimoja: msome alama za nyakati na mawazo ya watanzania hasa kipindi hiki ambapo wamechoka na usanii. Kwa heshima na taadhima nahitimisha nikiwatakia mapambano mema yak u-survive. Maana tulipofikia hakuna cha rafiki wala nini bali kunusuru sura hata ziwe nzuri au mbaya kiasi gani. Nawatakia mapambano kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya na matokeo mapya.

Chanzo: Tanzania Daima Desemba 14, 2011.

Kijiwe toka Abidjan na The Hague kwa Ocampi

Ninapoandika niko mjini the The Hague Uholanzi nikila mikuku. Ila huku ni winter baridi usiambiwe. Tunavaa mikoti mirefu hata glovu mikononi ili kuepuka baridi kutuuma kama wasemavyo wazungu. The cold bites wanasema.

Nisiwacheleweshe mkaanza kusonya na kutukana gazeti utadhani ni mimi. Baada ya Lwisi Mreno Ocampi kutaka rais wa zamani wa Cote di Vwaa, Profesa Laurent Gba-gboy aletwe hapa The Hague, kwa vile nami ni mwanasheria mwenzake tuliyesoma pamoja na kufundisha pamoja pale Harvard, alinipa mwaliko kuja kushuhudia kimbembe.

Kilichotusikitisha mimi na Ocampi ni ile hali ya kugundua kuwa kumbe Gbad- boy in profesa mwenzetu tena wa historia ila asiyejua kuisoma hiyo historia anayofundisha! Tulishangaa sana kugundua kuwa kumbe na mkewe Simone ni daktari lakini asiye na busara wala visheni ya kumshauri mumewe vizuri. Naye kwa ujuha wake alijifanya rais kwa vile mumewe alikuwa rais asijue madaraka hutoka kwa watu na si mali ya aliye naye. Maskini Simone hakujua kuwa madaraka ni kama koti! Hata kale ka msemo kuwa cheo ni dhamana hakakuwa na nafasi kwenye ubongo wake mfinyu kama panya.

Tulipoingia kwenye korokoroni au cell ya Gbad-boy alimofungiwa kama fisi tunduni, tulimkuta Gbad-boy ametoa mimacho kama panya aliyenaswa na mtego. Ingawa alivaa suti, hakuwa sopu sopu kama tulivyozoea kumuona alipokuwa madarakani akipambwa na kupambika. Suti ilikuwa inampwaya na ndevu zake hazikuwa zimenyolewa vizuri. Kwa ujumla alikuwa shagrabagra. Kwa wanaokumbuka picha nzima ya siku aliponyakwa, wanakumbuka mkewe Simone alivyokuwa kachoka na kuzeeka tofauti na kimwana first lady tuliyezoea kumuona baada ya kuupara kwa vipodozi na vikodozi kama wafanyavyo wajilishaji pepo wetu madarakani. Usingeamini kuwa kiumbe huyu aliwahi kuitwa mtukufu rais. Alikuwa amekonda na kuchakaa haraka huku akionyesha wazi kuchanganyikiwa akiishi kwenye kale na si leo. Maana nilipomuuliza kwa kifaransa: comment allez vous monsieur le president? Alijibu kwa kutabasamu akidhani kuwa bado yu rais na kusema: “Waliniogopa hadi kunileta huku kwa kunihadaa kuwa walikuwa wakinipeleka Abdjan kukutana na wanasheria wangu.” Ce tres mauvais alisema kwa kifaransa chake cha hovyo.

Nilipiga swali jingine la kuuliza alipo mkewe. Alizidi kuchanganyikiwa asijue la kujibu. Ma femme? Yaani mke wangu, aliuliza? Baada ya kuona hili swali halina faida kwa wasomaji, nilibadilisha kibao na kumuuliza ni kwanini hakusoma alama za nyakati. Hili alilijibu vizuri. Kwani alikiri kuwa wapambe na waramba viatu wake walimchuuza na kumtumia asijue walikuwa na lao. Alisema: “Kaka Mpayukaji uliniambia ulipopita kwangu ukitokea Misri na Tunisia. Bado nakumbuka ushauri wako jadidi kuwa madaraka ni tunda la msimu hivyo nisiyachukulie kama urithi. Nakumbuka sana mon frère.”

Aliendelea: “Naomba ukitoka hapa uwambie wote wanaoringia na kutumia madaraka vibaya wajue kuna mwisho. Tena waonye wawaonye wake zao wasipende kutumia madaraka yao kama mali ya familia wakiiba na kunyanyasa watu kana kwamba hakuna mwisho. Wakumbuke sana walipokuwa bado hawajaingia madarakani ili wasifanye kama tulivyofanya.”

Nilimuuliza kama ameishaonana na Chaz Teila. Alijibu kuwa yeye si mtu huru sawa na Teila hivyo kuonana si rahisi ingawa wamefungwa kwenye mahabusu jirani. Wakati akiendelea kuongea Ocampi alinionyesha sero iliyondaliwa kwa ajili ya Omari Bishkir wa Sudani atakapotiwa mbaroni. Hawa jamaa kweli wanajua kukomoana. Maana hiyo sero unayoambiwa ni chumba kimoja kidogo, kitanda kidogo, choo ndogo na meza ndogo kwishnei. Huwezi kuamini kuwa rais aliyewahi kujinoma kwenye ikulu ya mamia ya vyumba angeishi kwenye tundu kama bundi. Badala ya kulindwa na ma-body guards, sasa Gbad-boy analindwa na askari magereza tena wanoko kama nini? Ule wakati wa kubebewa kila kitu kuanzia kalamu hata kitabu umepita. Gazeti lenyewe analipata likiwa limechelewa na maafisa magereza wanamchagulia asome nini na si kama zamani ambapo alikuwa na washauri wa mambo ya kipuuzi kama avae au kusoma nini na kwa wakati gani.

Baada ya kuongea na Gbad-boy nilishika pipa kwenda zangu Abidjan kuomba kibali cha kumhoji Simone Gbad-boy. Baada ya kukubaliwa kwa sharti la kutotaja aliposhikiliwa, nilipanda chopa na kwenda kumfanyia mahojiano mama huyu aliyedanganywa kwa kuitwa Hillary Clinton wa Tropiki yaani Hillary Clinton des tropiques.

Hivyo, nilipofika kwenye jela ambalo siwezi kutaja, nilimkuta bibi kizee tofauti na kwini niliyezoea kumuona kwenye runinga na magazeti aking’aa kama taa. Mvi zilikuwa zinashindana kujitokeza huku uso wa Simone ukijaa kunyanzi.kwanza nilishangaa. Kumbe hawa jamaa wenye madaraka wanatuhadaa! Kumbe sura za kuvutia tuonazao si zao bali mikorogo ya kawaida! Sikuamini macho yangu kuwa yule niliyekuwa nimepelekwa kumuona ni shemeji first lady Simone Bbad-boy daktari wa lugha na historia kusema ukweli.

Sikuongea mengi na first lady huyu wa zamani kutokana na kuonekana alivyokuwa amepigika, hivyo nilimuuliza swali moja tu. “Una ushauri gani kwa ma-first ladies wengine wa Kiswahili?” Alitabasamu kwa shida na kujibu, “Wambie: madaraka yana mwisho na unaweza kuwa mbaya.” Nilimuuliza swali jingine kuhusu alivyokuwa akimtukana rafiki Barry Obby rais wa kwa Joji Kichaka akisema shame on you alimaanisha nini? Hakujibu. Nilimtolea picha yake akiwa amevaa matenge yaliyoshonwa mshono wa mwanamke nyonga. Aliziba uso wake kwa aibu na akaanza kulia kwa kwikwi na ukawa mwisho wa mahojiano yangu na Simone.

Kwa wanaojua vimbwanga vya wakubwa, huyu mama alikuwa na mamlaka kuliko hata rais wakati wa utawala wa mumewe. Alikuwa na biashara karibu kila kona kupitia NGO yake ya FPI. Aliiba kweli kweli. Lakini swali lililobakia, atakulaje hizo alizokwapua wakati yeye na mumewe wataozea gerezani huku mtoto wao mmoja akihukumiwa naye kwenda jela kwa kutumia madaraka ya dingi yake kama yake. Je wapo wangapi kama hawa huko vijiweni? Don’t quote me please when you name names.

Chanzo: Tanzania Daima Desemba 14, 2011.

Monday 12 December 2011

Kwetu wanapeana na kulilia nishani Chinua anazikataa!


Katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, rais Jakaya Kikwete aliwatunukia watu mbali mbali wakiwamo wanaofaa na wasiofaa nishani, nchini Nigeria gwiji wa fasihi Chinua Achebe amekataa nishani kama hiyo.

Wakati kwetu watu wanahoji kwanini kwa mfano Spika wa bunge la sasa Anna Makinda amepewa nishani wakati hafai, nchini Nigeria mambo ni tofauti. Achebe alikataa nishani ya Commander of the Federal Republic award-nishani ya rais kwa madai kuwa mhusika hajashughulikia mambo muhimu ambayo Achebe ameataka yatekelezwe ambayo ni kupambana na ufisadi, umaskini na vurugu havijashughulikiwa. Achebe alitoa changamoto mwaka 2004 alipokataa nishani kama hii. Je ni nani ana ubavu wa kukataa nishani Tanzania ambapo nishani, shahada za kupewa na kughushi, kujuana katika ulaji na udugu ni madhambi yaliyohalalishwa. Waulize waliotoa na waliopokea nishani kama kuna mwenye udhu na ubavu wa kuhoji kama Achebe. Je Kikwete aliyeingia madarakani kupitia wizi wa EPA na Richmond ana udhu wa kuweza kutoa nishani yenye kuweza kuitwa nishani na kuheshimika? Kama anao basi anaweza kutoa nishani si kwa maana ya nishani bali kituko.

Kwa Achebe kitu muhimu si nishani bali matendo. Kwake rais mharifu ni mharifu sawa na kibaka. Tieni akilini na mtafakuri kwa kina. Je waliopewa nishani wamepewa nishani na mamlaka yenye udhu au wamepewa dharau na aibu? Inashangaza ni kwanini Rostam Aziz na Andrew Chenge hawakupewa nishani hizi zenye maana kinyume na tunavyoelezwa. Aibu ni kwamba marehemu Mwalimu Julius Nyerere amepewa nishani hii chafu na mikono michafu iliyoitoa! Kweli simba akifariki ngozi yake yaweza kugugunwa na panya. Imetokea tena Tanzania.Kwa habari zaidi, BONYEZA HAPA

Saturday 10 December 2011

Havuliwi mtu nguo wala gamba hapa

Let me sing ye a song Lord
Let me glofy ye Lord
Kumbaya
Oh Lord Kumbaya
Let me sing ye a song Lord
Let me show ye’re that great Lord
Greater than any one in the world
The world is thy Lord
Everything is thine Lord
Oh lord my Lord
Kumbaya
Kumbaya

Nisameheni jamani. Nimekumbuka zama zile nafundisha chuo kikuu cha Havard ambapo niliwafundisha watu kama Joji Kichaka (alikuwa kibonde sana), Toni Big Liar (alikuwa kipanga huyu), na wengine mashuhuri. Hayo tuyaache.

Anyway, jana nilikunywa ulabu toka Uingereza nikiwa najipongeza kunusurika kuvuliwa gamba na nguo ukiachia mbali kuchomwa moto. Hivyo, kila saa naongea kiingereza. Najua wambea weshaanza kusema mashauzi na kujipa ujiko. Kwani kosa? Raha jipe mwenyewe na gamba uvae mwenyewe. Wanadhani naongea broken kama jamaa wa mjengoni. No, believe ye me. Nimepiga shule hadi nikakuta kibao kisemacho no more class, go home and drink coffee, dude.

Kwa taarifa yenu niko serious. Hebu tuwe serious kidogo. Kwa haya mauzauza yaliyotokea juzi kwenye kijiwe ambapo mwenyekiti nilivishwa gamba na Ewassa mbwamwitu sijui kama wanywa kahawa wangekuwa na common sense wasingenyotoa roho tena kwa kunichoma moto au kunitia madole kama Kashafi kule Libiya.

Najua kina mzee Machungi wakisoma hapa wataanza kuapa kwa miungu ya kisambaa wakijua wataninyotoa roho. Hapa utasikia miungu ya Zumbe Kimwei, Shekuza, Shehoza, Sheshatani na mazaga zaga mengine.

Wajua walevi walikuwa wamepania kumvua gamba Mbwamwitu. Kilichomsaidia si alinitaja kuwa ule wizi wa pesa ya makaa al maaruf Richmonduli uliasisiwa nami kupata pesa ya kuwahonga wanichague. Nilipoona jamaa kataka kumwanga mboga baada ya kutaka kummwagia ugali, ikabidi nimlinde ili wote tunusurike japo roho inauma.

Jamaa alinichefua na kunichafua sina mfano. Hata hivyo, nilistuka japo sikuongopa kutokana na kujua wapinzani wangu nao njaa tupu. Kosa walilofanya ni kutojua kuwa kambale wote wana sharubu. Laiti wangejua hili wasingepoteza imani na muda kudhani mwenyekiti - gamba nene na kuu- ningemvua gamba mwenzangu. Walipoteza muda mwingi kumtafuta mchawi wakati mchawi anayewamaliza ni mimi. Walitaka kumsaka na kumchoma moto mwizi wasijue mwizi mwenyewe ni mimi niliyeshika kibiriti!

Kuondoa udhia, kabla ya kufanya kigwena chetu kilichofanyika Idodomya muhula huu, nilimtwangia simu Mbwamwitu na kupanga jinsi ya kuwatosa vidomodomo kina Mchunguliaji, maarufu Mapepe Ninaye na shoga yake Joni Chill. Tuliamua kuwa ili kuwakomesha wasichezee ulaji wetu tena, tuwageuzie kibao. Ili wasijue, tulikubaliana niue hoja ya kujivua gamba japo Mbwamwitu aliamua kunigeuzie kibao. Hata kama ni noma, sina mpango wa kugombea tena uenyekiti wa kijiwe.

Kwa vile tunawajua walevi walivyopigika kiasi cha kuwa majuha, wangekubaliana na sanaa zetu bila kikwazo. Na kweli ndivyo ilivyotokea. Hata hivyo Mbwamwitu ameniumbua. Bahati nzuri, hata wale wapinzani wetu kijiweni, hawakukusikika wakitoa lau karipio na tamko la kulaani zaidi ya kuufyata. Isitoshe, tofauti ya vyama vyetu ni majina maana chama changu cha Nyama Ugali na Maharagwe (UNM), hakina tofauti na Chama cha wapinzani wangu kijiweni cha MT yaani Misheni Town au Mshiko Tosha.

Vyama vyote ni vya ulaji. Na isitoshe wote ni wanachama wangu sema hupiga kelele njaa ikizidi. Ukiwamwagia kahawa na kashata wanaachia kila kitu na unajifaidia.

Wanywa kahawa ni watu wa ajabu sana. Juzi ungewasikia wakihanikiza kuwa mie mwenyekiti wa kijiwe mzee mzima Mpayukaji wa Msemahovyo wa Waambie wa Watieakilini eti ningewatosa washikaji zangu wawili yaani Mbwamwitu al-maarufu Ewassa na Mkwapuaji maarufu Endelea Chenga, ungedhani walikuwa na hoja.

Nakumbuka majina mengi yalitajwa kuwa nyuma ya msukumo wa kuwavua gamba jamaa zangu. Nilisikia majina kama Msomimkatatamaa maarufu Sam Sixx na mengine makubwa kijiweni. Walichonga we wasijue mie mwenyekiti ni bingwa wa sanaa kuliko hata Njaa Kaya.

Msianze kuchanganyikiwa bure na kuchanganyana kusema maneno ya nabii Mpayukaji ya kinabii sana kiasi cha kujaa mafumbo na lugha za kitume. Siku hizi kijiweni tunavuana gamba kama chama twawala chenye magamba mazito na manene.

Acha niwamegee mikakati yetu ya kuhakikisha havuliwa mtu nguo wala gamba. Kwanza, ili kuwapata walevi, tuliazimia kwenye vikao vyetu vya siri kuwa lazima tutengeneze adui ambaye atawachanganya kiasi cha kutotushughulikia. Adui tuliyemtengeneza ni kudai kuwa kijiwe chetu kinakabiliwa na upinzani mkubwa toka kwa wanywanywa wetu.

Hivyo, badala ya kushughulikia ufisi, tulikuja na sanaa ya kudai mshikamano. Na hili lilipita bila kupingwa. Maana kama walevi wangejua tulivyokuwa tunawachezea mahepe, baada ya kugundua kuwa kumbe mimi mwenyekiti ndiye gamba kuu, wangeazimia kunitimua tena kwa kunivua gamba na nguo na kunizomea hata kunichoma moto kama kibaka.

Mana kwa niliyowafanyia sina tofauti na kibaka. Walivyo wa hovyo, hata Mbwamwitu aliposema kuwa nilikuwa nyuma ya ujambazi wa Richmonduli, hawakutaka kujua zaidi zaidi ya kutoa toa mimacho kama kunguru aliyenaswa na mtego! Hawa kweli wazima?

Leo stori ni fupi sana. Kigwena chetu kiliisha kwa kuwafunga kamba walevi kuwa tutavuana magamba kupitia utaratibu wa kijiwe. Hakuna kitu kama hicho. Sana sana tutalipana pesa zaidi ya kahawa kujiandaa kumtawaza Mbwamwitu Ewassa kuwa mwenyekiti wa kijiwe baada ya mie kuachia ngazi hapo baadaye. Hivyo, kwa taarifa yenu ni kwamba walevi mtaendelea kuliwa na sisi wale wale.

Kwa vile mimi ni bonge ya mjanja, ngoja nimtwangie Mbwamwitu simu aje tuzidi kukamata manywaji tukijipongeza kwa kuwaingiza walevi mkengeni kwa mara nyingine.

Sappy tearjecker may be a creep or spooky drama; it all depends on you guys. What a tug-along that this thing is! Mizengwe sure.

Kina Mapepe Ninaye, Sam Sixx, Braza Joni Chill na mashambenga wote mkome. Sisi chata la Mizengwe nambari wani ati! Kulaleki ninasepa! Mungu ibariki Danganyika wazidi kudanganyika. Kafu mshirika upo hapo? Nasema havuliwi mtu gamba wala nguo.
Chanzo: Tanzania Daima Desemba 7, 2011.

Thursday 8 December 2011

Wanaopenda kupeleka watoto kusoma Kenya na Uganda mmeliwa na soma hapa

Utafiti uliofanyika hivi karibuni umeonyesha kuwa mfumo wa elimu wa Tanzania si mbaya kama wengi wetu wanavyoamini. Katika utafiti uliofanywa kwenye nchi za Afrika Mashariki na Kusini umegundua kuwa Mauritius inaongoza na kufuatiwa na Kenya kwenye Hisabati lakini inazidiwa kwenye kusoma na nchi za Tanzania, Seychelles, Mauritius na Swaziland mtawalia kwenye sanaa za usomaji.
Hivyo, wale wanaofuja watoto na pesa zao kuwapeleka watoto wao Kenya na Uganda wajue wameliwa haswa. Katika utafiti huu nchi za Zambia, Malawi, Namibia, Lesotho na Uganda mtawalia, zimeonyesha kufanya vibaya katika nyanja zote.
Hivyo, tunaweza kuhitimisha tukiwashauri wenye imani mfu kuwa elimu yetu ni mbaya na inazidiwa na ile ya Kenya na Uganda kufikiri upya.
Tuliwahi kuandika kuwa wakenya wengi hupeleka watoto wao Uganda huku watanzania wakipeleka kote Kenya na Uganda. Sasa wahusika mnataka nini zaidi? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

Wednesday 7 December 2011

Breaking News Rais aanza kutumikia kifungo gerezani





Rais wa zamani wa Israel Moshe Katsav (66) ameanza kutumikia kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kubaka. Katsav alifikishwa kwenye gereza la Maasiyahu jana kuanza kutumikia adhabu yake hiyo. Kwa habari zaidi, BONYEZA HAPA.

Monday 5 December 2011

Muuza gongo avishwa gamba Lake

Wenzenu baada ya kuona wenzetu kule Idodomya wakidanganyana na kuudanganya umma kuwa wanaweza kufua nguo zao na kuosha miili yao watakata na harufu iwatoke, sisi wanywa gongo tuliamua kufanya kweli.

Kutokana na kuonekana kama hatuna akili kutokana na ulevi, muuza gongo wetu mama Betty na Mumewe Baba Jaki wamekuwa wakuibia pesa kila uchao. Mtu akishapiga kanywaji na kukamatika wao wanapiga sachi. Yesu! Utamsikia mama Betty akijisemea utadhani ana dini. Kweli siku za mwizi arobaini. Ikifika ya arobaini na moja ananaswa kama alivyonaswa baba Jaki hivi karibuni pale walevi tulipoamua kumvisha gamba.

Ingawa tunawashuku wauza gongo kuwa wezi wetu, tulijua fika mlevi mwenzetu aitwaye Edhard Ruwasha alikuwa ndiye mshirika mkuu wa baba Jaki. Maana, licha ya kuwa marafiki wa muda mrefu, wote wanasifika kuwa na tabia ya udokozi. Hivyo, basi, kumkamata baba Jaki, tulitishia kumchoma moto Edhard baada ya kugundua wizi mkubwa wa pombe zetu. Purukushani iliyofumka pale usiambiwe. Sikujua kuwa walevi kuna kipindi wanakuwa na akili kuliko hata walokole. Maana jeuri waliyo nayo si kutokana na gongo tu bali hata aina ya maisha wanayoishi.

Edhard akiwa hana hili wala lile, si Mzee Jongomeza akalianzisha. Alianza kwa kusema, “Jamani, mmesikia Chama Cha Magamba na Makobe (CCMM).” Hii ni CCMM. Tafadhali msiichanganye na kile chama tawala tusije kutoana macho bure. Najua ukikitaja kila mandata yatavamia kambi yetu na kuvuruga kila kitu.

Aliendelea, “Nasi hapa tuna magamba lazima leo yavuliwe piga ua.”
Mlevi Kambwiriri aliungana na wazo la Mzee Jongomeza. Alisema, “Mwanangu umenena hapa. Maana nasi hapa kambini tuna magamba manene kama ya CCMM. Lazima leo yavuliwa na kuchomwa moto ili tuanze kula vyetu kwa usalama na raha zetu.”

Kwa ufupi ni kwamba, baada ya kusikia Chama Cha Makobe au Magamba kuja na mkakati wa kisanii wa kuvishana magamba na kuvuana nguo kwa kisingizio cha kuvua gamba, nasi walevi tuliona hii ndiyo nafasi adimu ya kuvuana magamba kwenye manywaji yetu. Tulipania wadokozi wote wa mapupu na utumbo pale mezani wapewe vipande vyao bila kumsaza baba Jaki anayetumalizia vyetu akishirikiana na Ruwasha.

Tulipoanza kupiga zegere si baba Jaki kajiingiza akijifanya mtu mwema kutaka mhusika achomwe moto asijue naye ni mmoja wapo. Baada ya Ruwasha kuona anaweza kuwashwa akaamua kumwaga mtama. Alisikika akisema, “Jamani mnanionea na mtaninyotoa roho bure. Mei huwa natumwa na baba Jaki mwenye mali zake. Mie kweli ni kibaka lakini mipango yote ya kuwachomolea vijisimu na fedha hufanywa na baba Jaki mwenyewe.”

Alimgeukia baba Jaki na kusema, “Baba Jaki, kweli tunafanyiana hivi ndugu yangu wakati vyote nichomoavyo huvichukua wewe na kuishia kunipa gongo kidogo?”
Baba Jaki anainama chini akitafuta jinsi ya kujitetea.

Kabla ya kujibu, Ruwasha anaendelea, “Baba Jaki hujui kama siyo mimi kutunza siri zako ungeishakufa zamani? Kumbuka mwaka jana ilipoibiwa simu ya mlevi wa kizungu ya bei mbaya walevi walikushuku na kama si mie kuuchuna unadhani ungekuwa hapo zaidi ya kaburini?”

Wote tulipigwa butwaa kwa ufunuo wa Ruwasha ambaye mara zote alipotuhumiwa alikuwa akikaa kimya tusijue ana mengi. Nakumbuka kipindi kile ilipoibiwa simu ya bei mbaya ya mtasha, Ruwasha alipigwa nusu kufa. Nakumbuka walevi walisema kuwa alipokea kipigo chote hicho na kuhimili ili kumlinda baba Jaki ambaye kumlipa fidia alikuwa akimpa mapupu kila alipokuja kupata kanywaji. Kutokana na tabia ya Ruwasha kumlinda baba Jaki, walevi walifikia kutoa hitimisho kuwa hata baba Jaki akiamua kumchukua mke wa Ruwasha asingemfanya kitu.

Sasa juzi Ruwasha alipoamua kuzoboka mbona wengi tulipigwa na kihoro si kawaida ingawa tulijua baba Jaki ni kibaka lakini hatukutegemea Ruwasha amvishe gamba lake kirahisi na haraka hivi hasa ikichukuliwa kuwa Ruwasha siku zote alikuwa akionekana mdumizi wa kawaida.

Wakati kimbembe kikiendelea, si baba Jaki akataka kutuingiza mkenge, aliamua kuweka muziki wa Katitu ili midundo yake ituchanganye tusimdunde.

Hiyo haikufua dafu. Kwani mlevi Mgigisi aliamua kuanza kumtwisha baba Jaki mandoo na mitama kama hana akili nzuri. Jamaa alimkwida na kuanza kumtembezea kichapo si kawaida. Mkewe mama Betty kuona hali imechafuka, alikusanya pesa aliyokuwa keshapata na kuishia mitini huku akiacha mmewe anapigwa kama kibaka. Na kama si busara za mzee Mburuma, basi baba Jaki angekuwa maiti. Maana walevi walishaamua kumtia moto baada ya kumvisha gunia ambalo lilichukua nafasi ya gamba.

Kama si baba Jaki kuapa na kuahidi kuwa hatarudia na ataendelea kutupa gongo bure walevi, angekuwa marehemu au mwendazake kwa lugha za kimambasa. Amshukuru Mungu kuwa walevi wakiona gongo akili zao huruka kichwani na kubakia wapwakiaji wa kawaida kama ilivyotokea. Hata hivyo, kwa adhabu na kipigo alichopata baba Jaki, nadhani wote wenye tabia kama yake popote walipo wamepata somo. Hata kama wapo wenye tabia chafu kama zake wanaoendelea kupeta kutokana na waathirika wao kuwa majuha, arobaini yao ikifika watachapwa vilivyo. Kipopo chawangoja. Kunusurika kipigo na kuvishwa gamba na gunia ni kuachana na ujanja wa kizamani wa mbuni kumuona adui akafutika kichwa ubawani akidhani na adui atakuwa juha kama yeye. Je wako wangapi wanaowafanyia walevi wao vitu kama hivi? Naona yule anasoma na kusonya kutokana na chama chake kuwa na tabia kama hiyo. Hapa dawa si kusonya au kumchukia mlevi bure. Dawa ni kutia akili na kujua watu wanabadilika. Mwenye masikio na asikie na mwenye akili na atie akilini mapema kabla hajavishwa gamba na kutwishwa mindoo huku akikatwa mtama. Tena wengine ni waheshimiwa. Yakiwakuta haya watakufa kwa ugonjwa wa moyo kama baba Jaki ambaye tangu aumbuliwe anaonekana mwenye mawazo mengi. Hata zile bashasha zake zimetoweka na nafasi yake imechukuliwa na aibu.

Kwa vile nimechonga sana, ngoja nikapate lau chupa moja nizimue akili.

Chanzo: Dira Desemba 5, 2011.

Saturday 3 December 2011

Picha za karne kwa Blog hii


Laiti walioko kwenye foleni ya kumfuata Gbagbo wangeangalia picha hii mara kwa mara na kutafakari mara kwa mara. Ni upuuzi kiasi gani kufikiri kama Gbagbo aliyetawaliwa na mkewe asijue anapotoshwa. Nyerere aliwahi kuonya juu ya marais kutawaliwa na wake zao. Yuko wapi mr Clean Ben Mkapa aliyeishia kuwa mr Filth?

Naye mwendazake Muammar Gaddafi alipoambiwa ya Misri na Tunisia yaja alicheka sana na kusema, "Hii ni Libya." Alimaanisha haya hayawezi kumkuta asijue yatamkuta tena baada ya muda mfupi na kwa namna ya kutia aibu na kusikitisha. Tieni akilini wakati tukimaliza mwaka huu.

Wednesday 30 November 2011

Lowassa kajivua gamba, kamvika mwenye gamba

HAKUNA ubishi kuwa Rais Jakaya Kikwete alipokuja na dhana ya kujivua gamba, alilenga kutua mizigo ambayo imemwia mizito tangu alipoingia madarakani.
Kwa mawazo yake, alidhani mizigo hiyo ni swahiba wake, Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge. Lakini kwa kadiri Rais Kikwete alivyoutega mtego wake, umemnasa hata kabla wale aliowalenga hawajanaswa.

Wakati Kikwete akiandaa mtego alisahau kitu kimoja. Alisahau kuwa alioutega kwenye njia moja hiyo hiyo ambayo alitaka kupitia kurejea salama nyumbani.

Je, angeleaje nyumbani kupitia njia hiyo hiyo asiutegeu mtego au asinaswe nao? Sasa si siri.

Lowassa amemvisha gamba Rais Kikwete kiasi cha kushindwa kuelewa gamba ni nani na nani si gamba. Ingawa Lowassa amejitetea kuhusiana na Richmond, bado hawezi kukwepa kunaswa na mtego wa marehemu baba wa taifa.

Kwa wanaofuatilia hali ya mambo na jeuri ya akina Richmond hadi walipojibadili jina na kuitwa Dowans, wamepata siri ya jeuri yao. Kwa maneno ya Lowassa, hakuna shaka yoyote Richmond-Dowans ni Kikwete.

Hebu tunukuu baadhi ya maneno yake. “Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri, kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?”

Je, Rais Kikwete aliingilia mchakato mzima bila faida binafsi? Je, anayevunja kanuni na kuvuruga utawala wa sheria anafaa kuendelea kuongoza nchi ambayo kimsingi anaikwamishwa kwa sababu zake binafsi?

Hapa hakuna shaka kuwa kitendo cha Rais Kikwete kumzuia Lowassa kuvunja mkataba kililenga kulinda masilahi fulani ya rais ambayo hata hivyo hayatajwi kwenye utetezi huu jadidi wa Lowassa.

Je, tujiulize swali moja, kwanini utetezi huu haukutolewa mapema? Jibu analitoa Lowassa kuonyesha kuwa la Rais Kikwete na Lowassa ni moja.

Anasema, “Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na si wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?”

Kwa jinsi Lowassa alivyoyapanga maneno yake, kwanza anataka aonewe huruma kama mbuzi wa shughuli tuseme alitolewa kafara.

Pili, anataka kumkumbusha Kikwete kuwa asingejitoa kuubeba msalaba wake naye Rais Kikwete kwa pamoja wote wangekuwa msalabani.

Pia ni taarifa kwa Rais Kikwete wakati wake naye kubeba msalaba wa Lowassa ni huu. Na kweli, Lowassa amefanikiwa kuzima harakati na shinikizo la kuvuliwa nyadhifa zake na kuadhirika.

Laiti Rostam Aziz asingefanya papara, naye angegoma. Maana mgomo na ushawishi na siri vya Lowassa havikumwokoa peke yake bali hata mwenzake Chenge.

Kimsingi, hoja ya Lowassa ina mashiko kuwa magamba ndani ya CCM si mawili wala matatu bali wote. Hali inakuwa mbaya zaidi gamba kuu linapokuwa rais na mwenyekiti wa CCM ambaye kwa kiasi fulani anaweza kuonekana mnafiki kuanzisha harakati hii bila kujua kuwa naye ni sehemu ya gamba tena nene kuliko yote.

Kimsingi, Lowassa amefanikiwa kuvua gamba lake na kumvisha mwenye gamba. Tumesema. Lakini hatukusikilizwa.

Kitu kingine ambacho Lowassa amefanya ni kuthibitisha ukweli wa madai ya Dk. Willibrod Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA aliyetoa orodha ya mafisadi kule Mwembe Yanga ikiongozwa na Rais Kikwete mwenyewe.

Rais Kikwete alijitahidi kutojibu tuhuma za Dk. Slaa akidhani zitajifia na kuwang’ang’ania wenzake, asijue ikifika siku ya kifo kila mtu atapambana kuokoa nafsi yake kama alivyofanya Lowassa.

Hivyo tuhitimishe kwa kusema kuwa mchawi aliyekuwa akitafutwa na CCM kumbe ni mwenyekiti wao! Je, Rais Kikwete ameelewa amedhalilika kiasi gani kwa kuwahadaa watu wake kuwa anaweza kupambana na ufisadi wakati yeye pia ni kati ya watuhumiwa wa ufisadi huo huo?

Tumalizie kwa maneno mengine ya Lowassa. Anasema, “Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo.”

Kauli hii ina ujumbe mahususi kuwa Rais Kikwete asijisahau. Pili, ni kumkumbusha kuwa, licha ya kuchafuka kiasi cha kutotamanika, bado ana rungu la urais ambalo anaweza kutumia kumwokoa Lowassa ili aweze kuendelea na mbio zake za kuusaka urais mwaka 2015.

Ukweli huu umo kwenye maneno haya ya Lowassa, “Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 walipoleta tuhuma za mtizamo wa umma dhidi yako, ulisema kwamba kuwa rais ni mipango ya Mungu.”

Wengi wanangojea kuona kitu gani kingine atafanya Kikwete kuepuka aibu hii. Pia hapa ndipo siri ya kuenguliwa kwa spika wa zamani na Waziri wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta inapojulikana.

Maana, kimsingi, Bunge ilipaswa likae na kuangalia kashfa ya Richmond upya pamoja na ukweli kuwa rais na Lowassa (waziri) mkuu licha ya kulidanganya Bunge na taifa, walificha ukweli kwa faida zao binafsi.

Hakika, huu ni mtihani mwingine kwa Spika wa sasa Anne Makinda na tuhuma kuwa alipachikwa pale kufua nguo chafu za serikali. Ajabu ya maajabu, bado magamba haya yanawafuatafuata kina Sitta kutaka kuwaadhibu pale ambapo wanapaswa kuadhibiwa wao.

Je, wabunge wetu nao watakubali kugeuzwa nepi za vigogo Ikulu? Pia kuna haja ya kuangalia upya hata haya malipo ya Dowans bin Richmond. Maana kutokana na shutuma hizi mpya ni kwamba anayelipwa ni mwenzetu na watu wake na ndiyo maana hataki kutetea wananchi dhidi ya ujambazi huu wa mchana.

Hakika Kikwete naye tuseme ni gamba. Anapaswa kujiwajibisha au kuwajibishwa mara moja kutokana na tuhuma hizo.

Hapa ndipo upinzani unapopaswa kuachana na majadiliano na kuingia mitaani ili haki itendeke - kieleweke. Kazi kwetu.

Chanzo: Tanzania Daima Nov. 30, 2011.

Mwenye Richmond kafunuliwa



BAADA ya kuomboleza kifo cha rafiki, kipenzi na ndugu yangu Ya Mlamali bin Mohammad bin Abdussalaamu bin Humahidi bin Abu Minyaaaar bin Humahid bin Nairal al Fusso Kashafi, sasa umefika wakati wa kusoma hitma yake.

Hivyo wiki hii wanywa kahawa watakunywa kahawa na kula kashata bure ili kumkumbuka mwenzetu.

Hata hivyo katika kumkumbuka ndugu yetu huyu, nitatumia fursa hii kujirekebisha na kurekebisha baadhi ya mambo kuhusiana na ninavyotawala kijiwe. Hivyo, huu utakuwa ni wakati mkubwa wa kutafakari mustakabali wa kijiwe.

Katika kufanya tafakuri jadidi nitafanya baadhi mambo ambayo nataka kila mwanakijiwe ajue.

Mosi, nitakomesha kuendesha kijiwe kama mali ya familia au shamba la bibi. Mke wangu na kitegemezi changu na walamba viatu wote kijiweni nimeishawaambia kuwa nitawavua magamba.

Mie sitaogopa kama wale wanyama wenye magamba wanaoogopa kuvuana magamba. Niseme wazi. Hata gamba liwe nene kiasi gani nitalivua bila woga wala kuzungusha.

Hakuna cha gamba kugomea kiunoni wala urafiki wa chumbani wala barabarani kama wale. Maana nimejifunza kuwa kutawala kwa kutumia ukoo, kujuana, udini, uanachama na kulipana fadhila hauna tija na kama tija ipo si nyingine bali mauti tena ya aibu kama yaliyomkuta rafiki yangu Kashafi ya kuuawa kama kibaka mwizi wa kuku wakati alikuwa mtu mkubwa tu.

Nimeamua vitegemezi vyangu vijitafutie kama nilivyojitafutia badala ya kuniganda mgongoni kama kupe. Mbona vitegemezi vya mzee Mchonga vimejitafutia na vinaheshimika? Hakuna haja ya ukupe bila sababu tena kwa mgongo wa wanywa kahawa.

Hata bi mkubwa nimempa wazi kuwa ukupe mwisho. Niko tayari hata kumtaliki kama hatataka kubadilika na kuachana na ukupe. Mbona bi mkubwa Mary Mchonga anaishi tena kwa heshima? Kwani yeye ni nani aishi kama kupe wakati kupe mwenyewe anategemea damu ya ng’ombe. Bila ng’ombe kupe hana damu. Ng’ombe akiamua kukanyaga na kumsagasaga kupe hana wa kumzuia.

Kitu kingine ambacho nataka kieleweki ni kwamba nitawapuuzia waramba viatu wangu ambao wengi ni vibaka tu wanaonitumia. Maana likibumburuka na siku yangu ikitimia hawatabeba msalaba wangu nami zaidi ya kunigeuka kama akina Jibirili walivyomgeuka Kashafi na sasa kuula wakati wao hao hao ndiyo waliokuwa wakimtukuza na kumwambia uongo asijue walikuwa wakimchuuza.

Hapa kina Ewassa wangu na Endelea Chenga nasema mlie na mliwe tu. Lazima niwavua magamba bila kuoneana aibu. Nitatumia staili ya kumuua nyani bila kuwaangalia usoni ili nisiwasamehe. Nasema muelewe. Mie si mwoga wala msanii. Nitafanya kweli potelea mbali liwalo na liwe-lazima magamba yavuliwe hata kama ni kwa kuchana ngozi ya mtu.

Na katika hili sitaitisha vikao vya woga na upotezaji pesa za umma wa wanywa kahawa. Nitaamka kama chizi nakwenda kijiweni na kutangaza kuwa fulani na fulani na fulani na fulani nimewatimua uanachama wa kijiwe. Finish. Nisikie mtu akifanya fyoko atajua kama kahawa ni mma au maji.

Kitu kingine ambacho nimejifunza toka kwa Kashafi ni kuishi kwa kujilisha pepo na kupuuzia ukweli nisijue hautanipuuzia wala kunisamehe. Avumaye baharini papa nimegundua.

Nikiendelea kujilisha pepo wakati wanywa kahawa wakizidi kuishi kwa upepo kama magurudumu ya gari na baiskeli wataninyotoa roho siku moja tena kama kibaka. Aku! Singoji yanikute kama Kashafi mie.

Kitu kingine ninachoapa kuachana nacho ni usanii na ubabe. Hauna tija zaidi ya kuwafundisha wanywa kahawa ubabe halafu wanigeuzie kibao kama alivyofanyiwa Kashafi.

Kitu kingine ambacho nimejifunza toka kwa Kashafi na ninakitafakari kwenye hitma yake ni ukweli kuwa kila chenye mwanzo shurti kiwe na mwisho. Isitoshe, nimegundua kuwa unaweza kuwafanya watawaliwa mafala nao wakazuga kwa kujifanya mafala kumbe wanapanga kukunyotoa roho tena kinoma kama walivyomfanyia swahiba na ndugu yangu Kashafi.

Singoji yanifike. Heri nionekane mwoga nipone kuliko kujifanya jabali na mbabe nikaishia kunyotolewa roho nikimwaga michozi kama kichanga kama alivyofanya Kashafi.

Juzi nilimsikia mwanae akiongea habari za ki-al-Qaida akisema eti alijeruhiwa na makafiri na si wapendwa wake wa Libya! Kweli za mwizi zikifika-utasikia kila kitu.

Anadhani Walibya ni mafala wa zama zile za dingi wake. Too late dear, those guys are going to send you to the gallows just soon son. Zamu yenu ya kutesa kwishnei bwana mdogo Sefu al Islaaaam.

Kitu kingine nilichojifunza ni kwamba ngurumbili hawatabiriki wala kuaminika. Ni makosa kuwatabiri na kuwaamini kiasi cha kuwafanyia utakavyo ukidhani ni wanyama kumbe wanadeku kila kitu na kukuchora na kukusanifu hasa siku wakikupata.

Kuwa muwazi na mdemokrasia Kung’atuka kama mzee Mchonga ili nising’ang’anie na kuishia kunyotolewa roho kama kibaka.

Tumalizie na kutoa somo kuwa katika hitma hii tumejifunza kuwa kumbe Richmonduli wapo wawili.

Mzee mzima hatimaye amefichuliwa kuwa ndiye kila kitu na kama ni kuvuana magamba basi avuliwe yeye kwanza.

Maana ushahidi wote umemwingiza na kumbana vilivyo. Kwa vile jamaa ni bingwa wa sanaa na wadanganyika ni wapenzi wa sanaa huenda atanusurika. Ila hali ilivyo, enough is enough.

Haiingii akilini kama watanusurika badala ya kukashafiwa tena kwa aibu zaidi ya Kashafi.

Acha niishie nijiandae kwenda Tahrir Square kudai Njaa Kaya na Ewassa na hata Makidamakida wao wawajibishwe kwa kutiwa kitanzini na kuzomewa kuliko hata Kashafi.

Nasikia ving’ora vyake. Acha nianze kuzomea. Hilo, hilo, gamba kuuu, kubwa.

Chanzo:Tanzania Daima Nov. 30, 2011.

Tuesday 29 November 2011

Siku kanisa lilipomuasi bwana na kudondokea mfukoni


Edward Lowassa mtuhumiwa mkuu wa ufisadi chamani mwake, amebadili mbinu ya kuusaka urais. Ameamua kuwatumia viongozi waroho na vipofu wa kidini walioishiwa roho mtakatifu na kujaa roho mtakakitu.
Kama kondoo, wanaswagwa kwenda wasikojua isipokuwa matumbo yao. Bahati mbaya sana, mbwamwitu hawa wanataka na kuwaburuza kondoo huko kwa mafisi? Je anachofanya Lowassa si udini wa wazi wazi? Mbona hatumuoni akichangia misikiti? Je makanisa yamefilisika kiakili na kiuchumi kiasi cha kujengwa kwa kutegemea pesa chafu? Tunaipeleka wapi jamii iwapo wanaodhaniwa kuwa viongozi wa kiroho wamegeuka kuwa viongozi wa uroho? Kesho Kikwete akianza kumwaga pesa misikitini maaskofu waanze kumshambulia wakati wako kitanda kimoja na udini na ufisadi vinavyonuka hakuna mfano?

Monday 28 November 2011

Mlevi akata rufaa kwa papa



Barua kwa mheshimiwa sana papa Benedicto wa 16,
Kwanza nakusalimia kwa jina la Yesu. Naamini hujambo pamoja na watu wako hapo Vatikano. Wenzako huku Uwanja wa Fisi na Bongo kwa ujumla hatuna hali hata hivyo gongo tunapata ingawa polisi wanatusumbua kwa kututoa upepo. Mambo yamezidi kutubana kama mikanda huku wanaotwambia tufunge mikanda wakifungua hata zipu. Wanaitana magamba, mafisi, mafisiahadi na majina mengine ya ajabu ajabu.

Kabla ya kukueleza kilichonisibu na kunisukuma kukuandikia waraka huu, ngoja kwanza nikueleze kuwa mie ni msomi lakini asiye na kazi wala hali bali kujinywea gongo lau nipunguze mateso na mawazo.

Mheshimiwa papa nisamehe. Ngoja kwanza nielezee uzoefu wangu na hali ilivyo kwangu kama kielelezo cha walio wengi katika kiza na mateso yasiyomithalika.

Baada ya kuzisahau na kuzishit shahada zangu nilizopata baada ya kuzisotea siyo kupewa wala kughushi toka chuo kikuu cha Harvard, makufuru yaliyofanywa na kanisa kuu la Kirumi la Mwanza yalinifanya nizikumbuke. Kumbe kila shari ina heri na kila heri yaweza kuwa na shari. Wajua nini? Si nilikuta panya wameishaanza kuzinyea. Kumbe ningechelewa wangeweza hata kutafuna shahada zangu na kuzitumia kutengenezea viota vya kuzaliwa panya wengine. Huu nao ni ufisadi wa mapanya so to speak.

Nasisitiza kuwa sikughushi shahada zangu. Nilizihenyekea kula Harvard na aliyenilipia karo na pesa ya kutanua bia wakati ule na kuotesha kirimba tumbo tena majuu si mwingine ni mzee Mchonga mwenyewe na awamu yake ya kwanza ya kila kitu kwa watanzania. Wakati huo Bongo ilikuwa bongo kweli na siyo Danga ya Nyika kama ilivyo sasa.

Je mheshimiwa sorry ndugu papa unajua kuwa huku Danganyana ya Danganyika kanisa lako limeingia kwenye kashfa ya ajabu? Kashfa yenyewe ni kuanza kuwasafisha mafisadi pale wanapotoa pesa. Kinachoendelea hakina tofauti na kile alichokuwa akikifanya muuza mibaraka wa zama za kiza wa kanisa lako kule Ujerumani aitwaye Johann Tetzel ambaye alisema kuwa kadri sarafu idondokavyo kwenye kishubaka cha kukusanyia pesa mwenye roho ya mwenye dhambi hutoka motoni na kuingia peponi. Nadhani unamkumbuka tapeli huyu ambaye makufuru yake yalichochea watu kama Martin Luther, Menno Simmons, Conrad Grebel, Wycliffe John, Melchior Hoffman, John Hut, Balthazar Hubmeier na wengine kuasi kanisa lako na kuunda madhehebu yaliyogeuka tishio baadaye. Anyways, huko kwenye mambo ya radicals and reformation leo siendi nisije nikakuudhi kama hawa walitenda makufuru huku Mwanza.

Ndugu katika Kristo mheshimiwa Papa,
Kwa niaba ya wanywa kahawa wa Danganyika nakuandika mtukutu sorry mtukufu kuwa hekalu la kanisa lako la Kirumi katika jimbo kuu la Mwanza liligeuzwa kuwa pango la wezi pale lilipomkaribisha Eddie Ewassa ambaye huku huitwa gamba kuu namba mbili eti kulichangishia pesa ya kujenga kanisa jingine. Wajua kanisa lako limeuzwa kwa bei gani? Huwezi kuamini lakini ndiyo ukweli-madafu milioni 200. Najua hujui madafu ambayo si kama Lira. Dola moja ni madafu 1900 kwa bei za kilanguzi ambazo zimeanza kuhalalishwa kutokana na wakubwa kuchota pesa za kigeni zilipo na kuzipitisha mlango wa nyuma kuchuma faida.

Ndugu Papa,
Machukizo haya makuu yaliasisiwa na kufanywa na askofu Rulanchi akisaidiana na wadogo zake katika jimbo lake. Baada ya kufanya makufuru hayo, huwezi kuamini eti alifunga safari kwenda kwenye nchi ya voodoo ulipokuwa kukutana nawe wakati huko nyuma aliacha amechafua hekalu! Najua alipofika huko hakukueleza ukweli. Maana hakujua jinsi umma wa walevi ambavyo ungechukulia haya makufuru ya hekalu la bwana kuchangiwa na wezi huku kanisa lako likiwekwa mifukoni mwa watu wezi waroho na wachafu ambao Rulanchi aliwamwagia sifa ambazo hata hajawahi kukumwagia wewe. Hakuna aliyetegemea kuwa vipande thelathini kama vile alivyopewa Yuda kumsaliti Bwana Yesu vingeweza kutumika tena kipindi hiki cha maendeleo makubwa na utajiri wa kutisha wa kanisa lako tukufu. Inashangaza na kukatisha tamaa hadi wanywa kahawa wameamua kukuandikia waraka. Hii ni baada ya kugundua kuwa mamlaka husika huku zimo kitanda kimoja na mafisi wawalao watu ambao sasa wamejipenyeza kwenye hekalu la Bwana.

Huku Uwanja wa Fisi kwenye kijiwe chetu cha kula gongo nasikia maneno machafu yakipita kila mtaa. Wapo wanaosema eti roho mtakatifu siku hizi amepinduliwa na roho mtakakitu. Wengine wanasema kuwa hekalu la Bwana kwa sasa ni halali kuwa pango la wezi ili mradi watoe mshiko. Wapo wanaosema etiuna mpango wa kuanzisha utaratibu wa ubinafsishaji wa Kanisa ili kuongeza mtaji wa kwendea mbinguni. Hali inatisha. Kama wewe au mdogo wake Porikapu Peng’o hamtamchukulia hatua huyu Rulanchi, msichanganye kujikuta mkivuna magugu badala ya mpunga kwenye shamba la Bwana.

Kwa ufupi habari nilizo nazo ni kwamba kuna waamini wa kanisa lako wengi wanaopanga kujiengua na kujiunga na madhehebu mengine na wengine kujinyonga kama hutamwajibisha Rulanchi na genge lake la mafisadi wa kiroho wanaotumia uroho kama roho mtakatifu wakati ni roho mtakachafu.

Nimalizie kwa kukushauri kuwu umwajibisha yeyote mwenye kuvaa ngozi ya kondoo ili kuwahadaa kondoo wa Bwana. Wengi wanashangaa ni dini gani inayoweza kulala kitanda kimoja na mafisadi? Ningeshauri Vatikano isikubali kurejeshwa kwenye enzi za akina Paul Mackincus yule habithi wa kimarekani aliyechafua benki ya Mungu (Banco Ambrosiano) kwa kushikiana na mafia, “Uomini di fiducia”kama akina Licio Gelli, Michele Sindona, Umberto Ortolani, Roberto Calvi na majambazi wengine waliomuua papa John Paul I (Albino Luciano). Kaka papa, nakuomba usiruhusu akina Edwardo Roberto Calvi Ewassa na Andrea Michele Sindano Chenga wa Danganyika waliteke kanisa.

Kwa vile tulivyoheshimiana na Albino Luciani, nguvu zimeniishia na siwezi kuendelea.

Wabanikiwe walioliuza kanisa kwa mafisadi huku waliolinunua wakilaaniwa milele na milele aaamini.

Chanzo: Dira Novemba, 2011.

Thursday 24 November 2011

Siku Lowassa alipomvisha gamba mwenyewe (Kikwete)




Hakuna ubishi kuwa rais Jakaya Kikwete alipokuja na dhana ya kujivua gamba, alilenga kutua mizigo ambayo imemwia mizito tangu alipoingia madarakani. Mojawapo ya mizigo hiyo ni Edward Lowassa na Andrew Chenge ambaye alimrithi toka kwa mtangulizi wake. Lakini kwa kadri Kikwete alivyoutege mtego wake, umemnasa hata kabla wanyama aliwalenga hawajatia guu mtegoni.

Wakati Kikwete akiandaa mtego alisahau kitu kimoja. Alisahau kuwa aliutega kwenye njia moja hiyo hiyo ambayo alitaka kupitia kurejea salama nyumbani . je angereaje nyumbani kupitia njia hiyo hiyo asiutegeu mtego au asinaswe nao? Sasa siyo siri. Lowassa amemvisha gamba Kikwete kiasi cha kushindwa kuelewa gamba ni nani na nani si gamba. Ingawa Lowassa amejitetea kuhusiana na Richmond, bado hawezi kukwepa kunaswa na mtego wa marehemu baba wa taifa.

Kwa wanaofuatilia hali ya mambo na jeuri ya akina Richmond hadi walipojibadili jina na kuitwa Dowans, wamepata siri ya jeuri yao. Kwa maneno ya Lowassa, hakuna shaka yoyote Richmond-Dowans ni Kikwete. Hebu tunukuu baadhi ya maneno yake. “Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?” Je Kikwete aliingilia mchakato mzima bila faida binafsi? Je rais anayevunja kanuni na kuvuruga utawala wa sheria anafaa kuendelea kuongoza nchi ambayo kimsingi anaikwamishwa kwa tamaa zake?



Hapa hakuna shaka kuwa kitendo cha Kikwete kumzuia Lowassa kuvunja mkataba kililenga kulinda maslahi fulani ya rais ambayo hata hivyo hayatajwi kwenye utetezi huu jadidi wa Lowassa. Je tujiulize swali moja, kwanini utetezi huu haukutolewa mapema? Jibu analitoa Lowassa kuonyesha kuwa la Kikwete na Lowassa ni moja. Anasema, “Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,”

Kwa jinsi Lowassa alivyoyapanga maneno yake, kwanza anataka aonewe huruma kama mbuzi wa shughuli tuseme kafara. Pili anataka kumkumbusha Kikwete kuwa asingejitoa kuubeba msalaba wake Kikwete wote wangekuwa msambweni. Pia ni taarifa kwa Kikwete kuwa wakati wake naye kubeba msalaba wa Lowassa ni huu. Na kweli, Lowassa amefanikiwa kuzima harakati na shinikizo la kuvuliwa nyadhifa zake na kuadhirika. Laiti Rostam Aziz asingefanya papara, naye angegoma. Maana mgomo na ushawishi na siri vya Lowassa havikumwokoa peke yake bali hata mwenzake Chenge.

Kimsingi, hoja ya Lowassa ina mashiko kuwa magamba ndani ya CCM si mawili wala matatu bali wote. Hali inakuwa mbaya zaidi gamba kuu linapokuwa rais na mwenyekiti wa CCM ambaye kwa kiasi fulani anaweza kuonekana mnafiki kuanzisha harakati hii bila kujua kuwa naye ni sehemu ya gamba tena nenen kuliko yote.

Kimsingi, Lowassa amefanikiwa kuvua gamba lake na kumvisha mwenye gamba. Tumesema. Lakini hatukusikilizwa.

Kitu kingine ambacho Lowassa amefanya ni kuthibitisha ukweli wa madai ya Dk Wilibrod Slaa katibu mkuu wa CHADEMA aliyetoa orodha ya mafisadi kule Mwembe Yanga ikiongozwa na Kikwete mwenyewe. Kikwete alijitahidi kutojibu tuhuma za Slaa akidhani zitajifia na kuwang’ang’ania wenzake asijue ikifika siku ya kifo kila mtu hpambana kuokoa nafsi yake kama alivyofanya Lowassa.

Hivyo tuhitimishe kwa kusema kuwa mchawi aliyekuwa akitafutwa na CCM kumbe ni mwenyekiti wao! Je ni kudhalilika kiasi gani kwa Mwenyekiti wa chama tawala na rais wa nchi kuwahadaa watu wake kuwa anaweza kupambana na ufisadi wakati yeye ndiye fisadi nambari wani?

Tumalizie kwa maneno mengine ya Lowassa. Anasema, “Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo”.

Kauli hii ina ujumbe mahususi kuwa Kikwete asijisahau. Pili ni kumkumbusha kuwa, licha ya kuchafuka kiasi cha kutotamanika, bado ana rungu la urais ambalo anaweza kutumia kumwokoa Lowassa ili aweze kuendelea na mbio zake za kuusaka urais hapo 2015. Ukweli huu umo kwenye maneno haya ya Lowassa, “ Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 walipoleta tuhuma za mtizamo wa umma dhidi yako, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,”

Wengi wanangojea kuona ni usanii gani mwingine atafanya Kikwete kuepuka aibu hii. Pia hapa ndipo siri ya kuenguliwa kwa spika wa zamani Samuel Sitta inapojulikana. Maana, kimsingi, Bunge ilipaswa likae na kuangalia kashfa ya Richmond upya pamoja na ukweli kuwa rais na Lowassa (waziri) mkuu licha ya kulidanganya bunge na taifa, walificha ukweli kwa faida zao binafsi. Hakika, huu ni mtihani mwingine kwa spika wa sasa Anna Makinda na tuhuma kuwa alipachikwa pale kufua nguo chafu za serikali. Ajabu ya maajabu, bado magamba haya yanawafuatafuata akina Sitta kutaka kuwaadhibu pale ambapo wanapaswa kuadhibiwa wao. Je wabunge wetu nao watakubali kugeuzwa nepi za rais na watu wake? Pia kuna haja ya kuangalia upya hata haya malipo ya Dowans bin Richmond. Maana kutokana na shutuma hizi mpya ni kwamba anayelipwa ni Kikwete na watu wake na ndiyo maana hataki kutetea wananchi dhidi ya ujambazi huu wa mchana.

Hakika Kikwete naye ni bomu au tuseme gamba. Anapaswa kujiwajibisha au kuwajibishwa mara moja kutokana na mateso taifa linayopata kutokana na tamaa zake. Hapa ndipo upinzani unapopaswa kuachana na majadiliano na kuingia mitaani ili haki itendeke-kieleweke. Kazi kwetu.