Epistle to Afrophobic South Africa

Epistle to Afrophobic South Africa

Thursday, 31 May 2012

Hii kitu imekaaje?

Vintage ChinaVintage China
Wachina wanaendelea kuja kwa kasi ya ajabu karibu katika kila kitu. Taratibu ustaarabu wa kichina unarejea kwenye chati. Kwa wale waliokua wakati wa serikali ya kijamaa ya Mwl Julius Nyerere watakubuka zile sinema tulikuwa tukiletewa toka uchina zama zile. Kweli ya kale dhahabu.

Is it too much or too mooch?


(Thinkstock)

When I read the story that dandelion can be a good source of vitamins, I just went hyperbolic thinking that science is now screwing us.  Um. Real? Perhaps. May. I just retorted.  Again when I realized how dandelion or the teeth of lion disturbs me to lawn mow now and then, I found it a good idea to munch these wild grasses. Now that we can garner vitamins from dandelions, what is left for us to start picking the stuff instead of  mowing it? For more info, just CLICK hither.

Waziri mkuu anapotumiwa viungo vya binadamu


Waziri mkuu wa Kanada Stephen Harper wa chama cha wahafidhina amefanyiwa kitu ambacho hakijawahi kufanywa kwa kiongozi wa taifa hili. Ametumiwa viungo vya mtu kwa njia ya posta.  Katika vifurushi  viwili vilivyokuwa na anwani ya ofisi yake, kulikutwa miguu miwili ya binadamu. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Hii sasa kaya ya madudu


BAADA ya kupata shahada zetu za udaktari, wana kijiwe tumeanza kuwa wachambuzi wa karibu kila jambo kuanzia majumbani mwetu hadi kijiweni.
Baada ya kuona jamaa zetu kule kwenye visiwa wameanzisha harakati za uangusho ili kuangusha kilicho halali, sisi tumeanzisha harakati za kuwaamsha walevi kuangusha kilicho haramu. Nadhani tunaelewana.
Leo uwanja ni wa Dk. Profesa Msomi Mkatataamaa ambaye tangu sasa tunamuita mpphilosophe. Mimi naitwa Guru of Philosophy au Abu Hekima kwa Kiarabu au baba wa maarifa kwa Kimakonde.
Kama nilivyogusia, kikao cha leo kitawaudhi wengi kutokana na Dk. Profesa M-philosophe kuahidi kuonyesha usomi wake katika kuchambua madudu ya kaya hii ambayo imeanza kugeuka kaya ya madudu.
Bila kupoteza muda anakohoa kidogo na kukwanyua mic, “Waheshimiwa madaktari na maprofesa wa kaya hii, nina furaha kubwa kuwapa mhadhara juu ya dhana nzima niliyojenga juu ya kaya yetu ambayo kusema ukweli imegeuka ya madudu.”
anainua kombe lake na kupiga tama na kuendelea, “Kwa sisi tuliosoma historia ya ukombozi kuanzia zama zile za Uamsho au Enlightment kwa lugha ya kikameruni, tunakumbuka jinsi mageuzi tunayofaidi leo yalivyoanzishwa na magwiji kama François-Marie Arouet de Voltaire, Lorenzo De Medici ambaye alisifika kuwa mtu wa kwanza kuwa tajiri duniani, John Locke, Sir Isaac Newton, Leonardo Da Vinci, Jean Jacques Rosseau, Montesqui, Thomas Hobbes na wengine wengi ambao nikiamua kuwataja tutakesha kabla ya kusikia ninachopanga kusema.”
Kabla ya kuendelea Dk. Maneno anachomekea: “Huyo Luhizo Medichi ndiyo nani tena? Nimependa jina lake maana ni kama la Kizigua.” Watu hawana mbavu.
Dk. Profesa Msomi Mphilosophe anajibu: “Wala huyu jamaa siyo Luhizo wala si mzigua bali muitaliano aliyeanzisha mageuzi ya biashara kwa kuchuma pesa nyingi na kudhamini vikao vingi vya kupinga kanisa la Kirumi na serikali kutokana na uchakavu wake hasa ufisadi kama huu mnaoona leo. Kwa ufupi ni kwamba jamaa huyu na wenzake walikuwa wakikutana kwenye vijiwe kama sisi. Tofauti ni kwamba wao waliviita vijiwe vyao salon.”
Kabla ya kuendelea Dk. Mgosi Machungi anakwanyua mic. “Mgoshi, mie sikueewi hasa unaposema eti Uhizo si Mzigua.”
Msomi Mphilosophe anamkosoa Dk. Mgosi Machungi: “Sijakana kuwa Luhizo si Mzigua. nilichosema ni kwamba De Medici si Mzigua bali mtaliana. Hata hivyo hilo si tatizo. nitakupa mfano mwingine, hivi nikisema kuwa Rostitamu si fisadi tutakubaliana? Nikisema jamaa huyu mtaalamu wa madudu anayemwendesha Njaa Kaya ni bingwa madudu anayesukumwa na kukosa uzalendo kutokana kutokuwa raia wa kaya hii nitakosea?”
Anakunywa kahawa na kuendelea: “Kwa taarifa yako Dk. Mgosi kuna wengi nimewasaza ambao wangekuchanganya kiasi cha kuona kuwa ni Wasambaa. Niwape mfano, kuna magwiji kama Ulrich Zwingli, Barthasar Hubmaier, Conrad Grebbe, Martin Luther, John Kalvin na wengine wengi. Kwa vile leo mada yangu ni madudu ya kaya, naona niwape fursa nanyi mtoe mawazo yenu kuhusiana na huu uoza na madudu ambayo waziri mmoja Nshomile alisema aliyekuta kwenye idara ya Mali ya Siri.”
“Ahaa kumbe! Kumbe ulikuwa unaelekea huko! Sasa nimekupata,” alisema Dk. Mipawa na kuendelea: “Mwenzenu nimeogopa ingawa nimefurahi kujua siri ya utajiri wa jamaa zangu wanaofanya kazi kule Mali ya Siri kama msukuma mwenzangu Heze Maige. kwa taarifa yenu ni kwamba kaya inaliwa mchana kweupe?”
Anavuta kipisi chake cha sigara kali na kumpasia Dk. Mbwa Mwitu na kuendelea, “Jamaa kwa kuchukua mabibi utadhani Liumba! Jamaa wana jeuri ya pesa usiambiwe. kwa sasa wana uwezo hata wa kuwanunua wakubwa na kuendelea kupeta kinamna. Nyie ngoje muone. Baada ya wezi wa miwa kumtimua unadhani atasota kama wengi wanavyodhani? Atateuliwa ubalozi kama yule Daktari Ladi Komba wa kwa M7 au daktari feki Nshomile Kamalae,”
Kabla ya kuendelea, Dk. Mchunguliaje anachomekea: “Kwanini asiende nje kuula na kuhakikisha wale wanyama aliowasafirisha wanazaliana na kuzuia watalii kuja kwetu? Kwa taarifa yenu, kama alivyosema mpayukaji mmoja kuwa biashara ya bwimbwi inafanywa na wakubwa, ukweli ni kwamba Maige hakusafirisha wanyama peke yake. Huu ni mtandao. Habari hizi nilipewa na jamaa yangu anayefanya kazi usalama wa taifa.”
Naona kila mtu anamuangalia mwenzake kuona jinsi ya kumeza kirungu hiki.
Dk. Mpemba naye hataki kujivunga anakwanyua mic: “Yakhe mie nshashuhudia kitoto kichanga tena cha Jana kiniofanya kazi pale Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kikinunua viwanja na upuuzi mwingine karibu kula mahali. Nasikia eti hawa mafisadi wadogo wala na wakubwa na wakubwa wana kula na wakubwa hadi mkubwa.”
Dk. Mpemba umeniacha hoi anasema, Dk. Kidevu. “Yaani unataka kuniambia kuwa na mkubwa yumo kwenye dili hili? Kweli kama alivyosema Dk. Profesa Mphilisophe hii kaya ya madudu. hapa hujagusia watoto wao na wake zao ambao nao wamegeuka wakubwa nyuma ya pazia.”
Dk. Mpemba anaendelea: “Yakhe nimesikia kuwawana akaunti nje ya nchi na waendapo huko kuongeza pesa waenda na machangudoa wengi kama njugu. Nakumbuka, kimada wa kijana anayesimamia meta ya mafuta kule kwa akina waja leo warudi nasikia ana pesa kiasi cha kumnunulia gari kila mwanamke anayetembea naye. Hivyo kaya yetu si masikini bali haya hawa wadudu wanainyevuanyevua.”
Watu hawana mbavu. Tukiwa tunacheka Dk. Mbwa Mwitu anauliza: “Ami hebu njuze, wainyevuanyevua kaya wapi?” Anauliza kwa lafudhi ya Kipemba.
Dk. Mpemba hajali anajibu: “Wainyevua kote. hebu nenda pale banki kuu, uwanja wa ndege, Uhamiaji, mbuga za wanyama, bandari, Madini, Viwanda, Elimu, Mitaani, Polisi, Mamlaka ya Mapato ambayo yageuka sasa Mamlaka ya Mapoteo na kwingineko kwingi uone. Watu waiba kana kwamba kaya hii ya vichaa au haina mwenye Wallahi.”
Tukiwa tunaendelea kutongoa falsafa si likapita jina la kijana mmoja mdogo anayefanya kazi TRA. Gari lenyewe ni aina ya Buggarti. Kila mtu anashangaa kiasi cha inzi kujaa kwenye kahawa zetu.
Kama imekugusa tusameheane.
Acha nijikate nikatafute unga wa bibi mkubwa.
Chanzo: Tanzania Daima Mei 30, 2012.

Wednesday, 30 May 2012

Kwa hili nampongeza Sitta hata wakenya wampondeKenya na nchi nyingine za Jumuia ya Afrika Masharika hawana raha na Samuel Sitta na Tanzania kwa ujumla. Hii ni baada ya kuwawekea ngumu kuingiza suala la ardhi kwenye jumuia. Taarifa toka kwenye vyombo vya habari zimeonyesha chuki kiasi cha kuanza kutafuta pa kushika kuiadhiri Tanzania ionekane kama mnafiki. Maana kichwa cha habari kinasema kuwa Tanzania inahubiri maji na kunywa mvinyo. Tulishaonya kuwa hakuna mantiki ya kuwa na muungno wa Afrika Mashariki wakati nchi zote isipokuwa Tanzania hazina ardhi na zina idadi kubwa ya watu. Chukulia mfano Kenya ambayo ni chini ya nusu ya Tanzania ina idadi ya watu sawa na Tanzania. Kama ni kuungana heri tuungane na Msumbuji na Zambia lakini si nchi zisizo na raslimali wala ardhi. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Taylor Kufia gerezani

Charles Taylor in court on 30 May 2012
Hatimaye Mahamaka ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) imetoa hukumu ya kufungwa jela miaka 50 kwa aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor. Kwa umri wake maana yake ni kwamba atafia gerezani. Kwa mujibu wa Shirika la habari la Uingereza BBC, Taylor hakuonyesha kujutia vitendo vyake vilivyosababisha upotevu wa maisha ya watu wengi nchini Sierra Leone na Liberia. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Tuesday, 29 May 2012

Pamoja na vita bado Ivory Coast wanatuzidi!

Rais Jakaya Kikwete  akiwa na mgeni wake rais wa Ivory Coast Allasane Ouatara (pichani).

Kwa mtu anayejua hali ngumu ya vita na kutokuelewana liliyopitia taifa la Ivory Coast anashangaa kuona bado wana ndege ya maana kuliko sisi ambao tumekuwa na amani miaka yote. Ningekuwa rais Kikwete hapa bila shaka ningeona aibu hata roho kuniuma na kulifufua  Air Tanzania badala ya kuacha wezi wachache walimalize. Ni bahati mbaya kuwa viongozi wetu wamekosa roho ya kujisuta hasa wanapoendekeza ufisadi na uomba omba wakati mali wanayo lakini wanaikalia na kuigawa kwa wawekezaji na matepeli wachache kwa hongo ndogo ndogo.

Kuna wanaodhani kuwa kuishi na VVU ni afadhali kuliko CCM. Wanaamini kuwa
VVU humuathiri mtu mmoja wakati CCM imeathiri mamilioni ya watanzania. 
Hivyo hatari ya VVU ni ndogo ikilinganishwa na ya CCM. 
Isitoshe, kupamba na VVU ni rahisi kwani havina polisi wala pesa bali umakini wa mhusika.
 CCM ina majeshi, Usalama wa taifa, polisi, makanjanja na zana nyingine nyingi za maangamizi. 
Hivyo. aliyebuni hilo tamko wanamuona kama hajakosea.

Muungano ukivunjika Visiwani patatosha?


Kumekuwapo na ushabiki hasa kutoka Visiwani kuvunja Muungano wakidai wanataka wawe huru kana kwamba hawako huru. Je kinachotakiwa ni uhuru au kikundi cha watu fulani kuwatumia watu wa kawaida wasiojua agenda zake za siri kufanikisha kuvuruga nchi na kutwaa madaraka? Je tatizo la Zanzibar ni Muungano au kuangalia mambo vibaya? Wengi tunajiliza: Ni kwanini harakati za kudai kuvunja Muungano zimekuja sambamba na madai ya kujitenga na Kenya kwa kundi la kigaidi liitwalo MRC au Mombasa Republic Council? Wakati tukitafakari maswali haya tujaribu kujiuliza swali moja kuu. Je Muugano ukivunjika visiwa vya Zanzibar na Pemba vitatosha kubeba idadi ya watu wa Visiwani waliozaliwa na kujazana bara? Je tutegemee Comoro nyingine ambayo itahitaji pesa na majeshi yetu kwenda kulinda amani? Think Twice.

Monday, 28 May 2012

Maafa yanayoikabili Mombasa somo kwa Dar


Hali ya mji wa Mombasa nchini Kenya (pichani) si shwari hasa kutokana na hasira za mama dunia. Taarifa zilizopo ni kwamba mji wa Momba unaweza kuzama kutokana na baadhi ya visima vya maji ya kunywa kuanza kuzama. Wataalamu wa mazingira wanaonya kuwa hii imesababishwa na kuchimbwa visima vingi na kujengwa majengo marefu karibu na fukwe. Kinachoendelea Mombasa ingawa hakijajitokeza Dar es Salaam, ukweli ni kwamba muda si mrefu kitatokea. Hii ikiongozewa na serikali ya Tanzania kutotoa huduma za maji kiasi cha kuwekeza kwenye visima vya kuchimba hovyo hovyo, ukubwa wa jiji la Dar na majengo mengi yanayojengwa kihohela. Kwa habari zaidi kuhusu Mombasa BONYEZA hapa.

Hata bila kuiba viongozi wanaweza kustaafia pazuri

Picture taken on January 28, 2011 of former South African president Nelson Mandela's house in Qunu. AFP PHOTO / ALEXANDER JOEHii ni nyumba ya Mzee Nelson Mandela rais wa kwanza wa Afrika Kusini iliyopo kijijini mwake Qunu Transkei. Mandela hana nyumba moja tu. Anayo nyumba nyingine kwenye eneo la watu matajiri  la Houghton mjini J'burg. Hili ni fundisho kwa viongozi wezi kama Bingu wa Mutharika aliyeiba na kuwekeza kwenye hekalu kuwa uongozi uliotukuka hutuzwa na taifa kama inavyoonekana kwa Madiba.

Nelson Mandela's childhood home
Hii ni nyumba ya kwanza ya Madiba huko Soweto kabla ya kuanza harakati za ukombozi.

Nelson Mandela
Hii ndiyo nyumba ya Houghton J'burg

'Misaada' toka kwa wahindi hadi lini?

Spika wa Bunge Anna Makinda akipokea msaada toka kwa mkrugenzi wa GF Truck & Equipment Ltd, Imrani Karmali huku huku mwenyekiti wa kampuni hiyo Mehboob Karmali akifaidi kupigwa picha na spika.
Ni aibu kwa nchi yetu kuendelea kuwa tegemezi. Yaani tumefikia pabaya kiasi cha hata watu tuliowakaribisha wakiwa maskini kututumia kwa kisingizio cha misaada! Hawa ndugu wa Karmali wanalipa kodi vilivyo au ndiyo hivyo wanajikaribisha kwa wakubwa ili kupitisha mambo yao? Inashangaza kuona nchi yenye raslimali lukuki kuendelea kuwa Matonya. Ingawa kinachoonekana hapa ni msaada kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Njombe, ukweli ni kwamba ni zaidi ya hicho. Kesho utasikia akina Karmali hawaguswi na yeyote hata wafanya madudu gani.  Huku ni kuuz anchi na kuwekwa mfukoni. Kwanini nchi iwasamehe hao hao kodi za mabilioni ya fedha lakini iendelee kuwaomba eti waisaidie? Akili mbovu bila shaka na za kifisadi. Shame on you viongozi wetu!

Macho yangu au mwenge ukiwaka inatoka picha ya ndege?

Utazame mwenge huu na mwali unaotoa uangalie ni picha ya nini? Hata kama ni bahati mbaya, inavuta hisia kuona mwali ukionekena kama alama ya ndege. Japo sisi si wapenzi wala mashabiki wa mbio za mwenge kwa vile zinapoteza muda na pesa, hili limetuvuta na kuona tujadili na wengine.

Kigoda amerudi Urafiki kuibinafsisha au kuihujumu?

Taarifa kuwa waziri wa Viwanda na Biashara Abdallah Kigoda (Pichani) ametembelea kiwanda cha nguo cha Urafiki zinatia kichefuchefu. Hii ni kutokana na ukweli kuwa akina Kigoda na Benjuamin Mkapa kutaka kukibinafsisha lakini baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere akakinusuru. Aibu. Bahati mbaya wanasiasa nyemelezi huwa hawana kumbukumbu. Shame on you Kigoda!

Sunday, 27 May 2012

Unamkumbuka Jane Goodall na alivyofaidika na nyani wetu?


 • Jane Goodall akifanya utafiti wake wa manyani huko Gombe Kigoma ambao ulimpatia umaarufu dunia nzima. Je sisi kama nchi tunafaidikaje na utafiti huu?
  Behavioural observation

Je Museveni kurithiwa na mkewe?

Janet Museveni has emerged as the preferred successor to the president, with the full backing of her husband, who is also chairman of the ruling National Resistance Movement.
Habari zilizotoka ni kwamba rais wa Uganda Yoweri Museveni ameunga mkono nia ya mkewe kutaka kugombea urais. Hii ilitokana na hivi karibuni Museveni kuhojiwa na  NTV Uganda na kusema kuwa hatakuwa madarakani atakapofikisha miaka 75 ya kustaafu. Hivyo hii ilifungulia majadiliano na tetesi za ni  nani atamrithi Museveni huku ikisemekana kuwa NRM ingependa Museveni arithiwe na mkewe. Je mwanae aliyeandaliwa kwa muda mrefu atakubali? Je wanganda watakubali tena kuwekwa kinyumba na Museveni? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Waswahili kwa kuigiza na utumwa wa kiakili!

The leader of Boko Haram Abubakar Shekau
Huyo hapo juu ni kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Boko Haram cha Nigeria, Abubakar Shekau akiwa na bunduki zake. Ukiangalia gaidi huyu uchwara anavyojiweka utaona moja kwa moja kuwa anamuigiza Osama bin Laden asijue kuwa mwisho wake si mzuri. Kijana huyu amejiingiza kwenye utumwa wa kiakili na kuhatarisha maisha yake akidai anapigania Mungu na dini. Tangu lini Mungu mwenye nguvu kuliko yeyote na vyovyote chini ya ardhi akawa dhaifu kiasi cha kupiganiwa na kiumbe dhaifu kama huyu na wenzake wenye mawazo mfu kama yake? Waafrika kwa kupenda kuigiza upuuzi, hakuna mfano. Watu wanashindwa kuigiza vitu vya maana ambavyo vingewakomboa wao na jamii zao wanaigiza upuuzi! Kwa habari zaidi BONYEZA hapa na HAPA ambapo limbukeni wa kiswahili eti wanataka kuanzisha serikali ya kiislamu kule Mali.

Kumbe Zanzibar tatizo si muungano bali udini?Baada ya polisi wa kupambana na ghasia kutunishiana mikono na kundi la JUMIKI au Jumuia ya Uamsho na  Mihadhara ya Kiislamu kanisa la Tanzania Assembly of God (TAG) la mtaa wa Kariakoo Zanzibar limechomwa usiku wa kuamkia leo. Je hii ni bahati mbaya au kuna ushirika wa kundi hili linaloanza kutishia amani ya nchi? Tunaambiwa watu wasiojulikana wamechoma kanisa hili. Je kweli waliochoma hawajulikani wakati dalili zote zinaelekea kwa JUMIKI? Kuna haja ya serikali kuwa serious na kundi hili ambalo lina kila alama za kigaidi. Hata Al Shabaab ilianza hivi. Maana bado kuna wendawazimu wanaodhani nchi inaweza kutawaliwa kidini. Hii si karne ya saba na kumi na nne.Je tatizo la Zanzibar ni muungano au udini?

Utumwa mwingine karne ya 212

Ingawa kila chombo cha habari kina uhuru wa kuwa na sera yake, vyombo vyote vya habari huunganishwa na kanuni moja kuu, kuandika ukweli kama ulivyo. Inashangaza gazeti linaloendeshwa kwa kodi ya watanzania kuanza kuandika upuuzi na uzushi ambao hata ndege pamoja na udogo wa ubongo wake, hawezi kuuuamini. Huku ni kuchezea akili za watu hasa wasomaji na waandishi pia. Wanafanya hivi ili wapate kitumbua chao na kuwaridhisha wakubwa wao wapumbavu kama wao. Namna hii taaluma ya uandishi wa habari inaanza kugeuka uchangudoa wa kiakili.

Saturday, 26 May 2012

Lugha wabunge watiana mgeu, ufisadi itakuwaje? • Fight in Ukraine's parliament over language bill

Ngumi na hata kutoa na damu vilitokea kwenye bunge la Ukraine baada ya kuzuka mzozo juu ya matumizi ya lugha ya kirusi. Wabunge wa Ukraine wanaonekana kuwa na hasira hasa wanapoona maslahi ya taifa yakichezewa au kutaka kuhatarishwa. Je wangekuwa Tanzania siju ingekuwaje?

Zanzibar: Huu ni uamsho au uangusho?


Hali visiwani Zanzibar si shwari. Taarifa tulizopata ni kwamba kumekuwa makabiliano baina ya polisi wa kutuliza ghasia FFU na kikundi cha kihuni kinachojiita Kikundi cha Uamsho. Je hawa wanaojiita Kikundi cha Uamsho wanaotaka muungano uvunjwe wametumwa na nani? Je ni yale yale ya kuigiza yale ya wenzao wa Mombasa Republic Council huko Kenya wanaodai kujitenga ili washirikiane vizuri na mabwana zao wa kiarabu? Leo wazanzibari wanakataa muungano wakidai wajitenge wawe huru. Je na Pemba wakidai kujitenga na Zanzibar huru mambo yatakuwaje? Mbona wenzetu wanashindwa kujifunza toka Comoro? Serikali ya muungano inapaswa kuingilia na kuhakikisha kikundi hiki kinashughulikiwa kwa njia stahiki yaani, kuruhusu wananchi kuujadili muungano. Je ni kwanini serikalil ya Muungano imekuwa kimya kwenye tatizo la muungano au ni ile hali ya serikali husika kushindwa karibu katika kila kitu? Je hiki kikundi kinachoanza kutumia mabavu cha Uamsho kinachofanya ni uamsho au Uangusho?

Kumbe 2015 ni kiama cha CCM!

Angalia umati wa wananchi na wageni waliohudhuria mkutano wa CHADEMA Jangwani Dar es Salaam leo. Kweli watanzania wameichoka CCM na ufisadi wake. Kwa sura ninazoona hapa FFU hawana ubavu wa kufyatua mabomu ya machozi. Nimaanishacho ni  kwamba kuwepo wa wazungu ni changamoto kwa FFU na CCM. Kila la heri CHADEMA. Muhimu jihadharini na nyemelezi kama John Buda Shibuda na Jaffar Sabodo.

Friday, 25 May 2012

Walijua gereza zuri kuliko yote duniani?

 •  Picha ya kiswa lilimojengwa gereza la Bastoy na picha nyingi ni mfungwa akiwa amejipumzisha
 • Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN, Bastoy nchini  Norway ndilo gereza bora kuliko yote duniani. Gereza hili ambalo limejengwa kisiwani lina kila kitu kuanzia makazi mazuri sehemu za burdani na makandokando mengine ambayo kwa nchi maskini yanafaidiwa na watawala na matajiri lakini si watu wa kawaida wala wafungwa. Hivyo basi, kwa mtu maskini kama mtanzania akifungwa kule ataomba Mungu muda wa kifungo chake usiishe. Kwa habari zaidi za gereza hili BONYEZA hapa.

Je Kikwete naye anauza au kunufaika na unga?


Kuna imani kuwa viongozi wetu wa juu wanashiriki au kushirikiana na wauza unga. Ndiyo maana wahusika hawakamatwi kwa vile wanaopaswa kuwakamata ndiyo wale wale wanufaika na jinai hii. Rais aliwahi kutuahidi kuwa angewashughulikia wauza unga na alisema kuwa orodha yao alikuwa nayo. Miaka inazidi kuyoyoma. Je rais atatimiza lini ahadi yake? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Thursday, 24 May 2012

Karume alihudhuria mkutano wa marais wastaafu wa Afrika kama nani?


 1. Amani Karume anaonekana akiwa na marais wastaafu. Je kisheria Karume ni rais mstaafu anayepaswa kupewa hadhi sawa na waliowahi kuwa wakuu wa nchi yaani heads of State? Je walioandaa mkutano huu hawakuliona hili au ni yale yale mambo ya kiafrika kujiendea kiushikaji na kienyeji? 
   Marais wastaafu Afrika waliohudhuria mkutano wao Afrika Kusini ukiongozwa na Balozi wa zamani nchini Tanzania Bwana Charles. Mwinyi (Tanzania), Mkapa (Tanzania na Karume  (? Thabo Mbeki (Afrika Kusini), Obasanjo (Nigeria), Banda (Zambia), Pedro (Cape Verde), Soglo  (Bernin).  Hata hivyo Ketumile Masire (Botswana), Joachim Chissano (Msumbiji), Alpha Konare (Mali), Bakili Muluzi (Malawi), Pasteur Bizimungu (Rwanda) na Abdulaye Wade (Senegal) hawakuhudhuria mkutano huu.
Nigerian novelist Chinua Achebe chats with former South African President Nelson Mandela at a Steve Biko memorial ceremony in Cape Town in 2002. Biko, a leader of the Black Consciousness movement, died after being beaten by members of Apartheid’s police force. Photo/AFP
Magwiji hayo mawili kwenye picha ni kielelezo cha Afrika ingawa katika nyanja mbili tofauti. Ni nadra kukutanisha vichwa kama hivi pamoja. Ingawa hii picha ni ya mwaka 2002, imenivutia kiasi kuona ni vyema kuitundika hapa. Chinua Achebe na Nelson Mandela ni mbegu za nadra kuwa nazo pamoja. Wamekosekana Ngugi wa Thiong'o na marehemu  Mwalimu Julius Nyerere.

Mapenzi au kichaa


Kumetokea malalamiko kuhusiana na kampuni moja ya kimarekeni kutaka kuuza damu ya rais wa zamani wa nchi hiyo Ronald Reagan. Taarifa zalizotolewa na vyombo vya habari ni kwamba kampuni  ilikuwa ikitaka $ 12,000 kama bei ya kuuza damu ya rais huyo. Kampuni hii imetumia mtandao kutangaza biashara hii.Wengi wanajiuliza:Je watakaokuwa tayari kununua damu ya rais huyo wana mapenzi naye au kichaa? Je tamaa ya pesa inayotufikisha hapa si tutakuja kuuza hata mama zetu? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Tanzania nchi ya 'madudu'

Taarifa zinazoendelea kupamba kurasa nyingi za vyombo vya habari ni uoza wa ajabu uliogundulika katika idara mbali mbali zikiongozwa na Maliasili na Utalii. Ukiachia mbali waziri wake aliyetimuliwa, Hezekiel Maige, tunasikia na vigogo wa mikoa ni matajiri wa kutupwa.
Bahati mbaya sana tatizo siyo Maliasili na Utalii bali nchi nzima. Ukienda TRA madudu.
Nenda Uhamiaji, madudu, Mambo ya Ndani, Madudu, Ikulu Madudu. Kweli Tanzania ni nchi ya madudu. Maana hakuna mwenye nafuu kuanzia watawala hadi watawaliwa. Kwanini tunashindwa kuwawajibisha watawala mafisadi? Simpo, tunatamani kushika nafasi zao nasi tukafanya ufisadi.

Wednesday, 23 May 2012

Huu mwaka wa Makamba family

Kwa wanaokumbuka tambo za Yusuf Makamba (Mpayukaji) katibu mkuu wa zamani wa CCM kuwa lazima mtoto wake awe waziri, wataamini kuwa Makamba ana hisa kwenye serikali ya Jakaya Kikwete. Ingawa Kikwete aliwahi kukanusha kuwa serikali yake si ya ubia, kitendo cha kumteua junya Januari Makamba kuwa waziri ili kutimiza utabiri wa baba yake ni ushahidi tosha. Makamba family haiishii kwenye siasa tu bali hutumia siasa hadi kwenye uwekezaji ambapo Makamba pia yupo. Binti yake Mwamvita  (pichani)  ssi haba. Ukitaka kujua nimaanishacho, nenda Benki Kuu uone ni watoto wangapi wa vigogo wameajiriwa kule. Kama hiyo haitoshi, angalia orodha ya wakuu wa wilaya wapya uone ni watoto wa vigogo au jamaa zao wangapi wameukwaa. Hiyo ndiyo Tanzania iliyosalia baada ya mafisi na mafisadi kula kitu na kubakisha mifupa na ngozi. Hakika huu ni mwaka wa familia za vigogo ikiwemo ya Makamba.

Sanago afanya mapinduzi tena

Photo/FILE Mali junta leader Captain Amadou Sanogo speaks at the Kati Military camp, in a suburb of Bamako, on March 22, 2012.
Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi wa Mali Kapteni Amadou Haya Sanogo mara hii ameingia na staili mpya ya mapinduzi kwa kuwatumia wanaoitwa wafuasi wake. Juzi rais wa mpito Diancounde Toure alipigwa na hao wafuasi wa Sanogo. Kama Vladimir Putin wa Urusi, Sanogo amenogewa madaraka kiasi cha kutumia mbinu za kinyani kurejea madarakani. Kichekesho ni kwamba eti wafuasi wake wamemteua kuwa kiongozi wa mpito. Wanafanya hivyo kama nani kama siyo kutumiwa? Baadaye watalizwa na wataanza kulalamika. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Wapenda sifa ni rahisi kuhongwa upuuzi mdogo mdogo


Waziri wa  Mambo ya Ndani 'Dk' Emanuel Nchimbi akivishwa shada la maua na kiongozi msaidizi wa dhehebu la dini ya kihindi ya Shri Swamirayan hivi karibuni. Nchimbi (mkristo) alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya uzinduzi wa msikiti. Mkristo na kuzindua msikiti wapi na wapi? Tukubaliane, jamaa hawa wanawaalika watawala wetu mafisadi ili kuwa karibu nao na kufanya mambo yao yaende. Ni Tanzania pekee ambapo jamii  ya wageni inaweza kumilki uchumi na watawala. Kesho utasikia mhindi fulani haguswi hata akiingiza magendo au mihadarati ukiachia mbali wahamiaji haramu toka kwao.

Ngurdoto ilipohamia Dodoma


Ingawa tukisema kuwa rais Jakaya Kikwete ni mgumu kujifunza tunaonekana kumsakama, ukweli ni kwamba ni mgumu wa kujifunza. Kwa wanaokumbuka madudu yaliyotokea wakati wa semina elekezi ya Ngurdoto, wanashangaa ni kwanini anarudia upuuzi ule ule. Uliza imetumika pesa kiasi gani kwenye semina ya wakuu wa wilaya na mikoa inayoendelea huko Dodoma? Ni mabilioni ya shilingi. Kuwasafirisha, kuwalipa perdiem, kuwalaza na mambo mengine si bure. Huyu rais ametumwa kutumaliza nini?

Africa Must Revise its Educational Syllabi
Those that went to school in the 70s and 80s still remember the words such as ‘explorers,’ ‘missionaries’ and ‘merchants’ bringing civilization to Africa. History teachers made their students believe that Africa was discovered and civilized by a white man.
Ironically, in Tanzania where I went for my primary school, I still remember how David Livingstone, Henry Morton Stanley, Columbus, Mungo Park and Vasco Da Gama were revered to the extent that some families named their children after them. It is sad that learners at their foundation level were taught to revere such people. On becoming adults, they will nary know the reasons of most of the problems they are facing.
Consider Christopher Columbus for example, who sailed with the quest of reaching India. Instead, he landed in West Indies in the modern Haiti where he caused a lot of problems. Columbus’ aim was to buy gold at a cheap price and bring it back to the king of Spain who sponsored his mission. On arriving he forced the indigenous people to get him gold. After noticing that the country he thought was India happened to be Haiti and there was neither gold nor spice or silk, he captured 15, after killing many more and sailed with them back to Europe to prove that he had been to a foreign land. What was the difference between Columbus and modern day pirates? Africa goofs by idolizing criminals.
The following excerpts from a song by Burning Spear in the Hail H.I.M. Album Lyrics expose who Columbus really was

I and I old I know
I and I old I say
I and I reconsider
I and I see upfully that
Christopher Columbus is a damn blasted liar
Christopher Columbus is a damn blasted liar
Yes Jah
He's saying that, he is the first one
Who discover Jamaica
I and I say that,
What about the Arawak Indians and the few Black man
Who were around here, before him
The Indians couldn't hang on no longer
Here comes first Black man and woman and children,
In a Jam Down Land ya
A whole heap of mix up and mix up
A whole heap a ben up, ben up,
We have fi straighten out,
Christopher Columbus is a damn blasted liar
Christopher Columbus is a damn blasted liar
Yes Jah
In Tanzania, there are many mementos and commemorations for say Livingstone. In Malawi, one whole region is called Livingstonia in honor of the man who ushered colonialism in. can people who do not know their true history emancipate themselves? This is a crucial question that can give us the answer as to why man African rulers go to western countries cup in hand begging. This can tell us why many African rulers whose countries sit on vast amounts of resources still live by begging and acquiring unnecessary loans.
At independence, most African countries were at par with countries such as Singapore, Malaysia and South Korea. Interestingly, the same are now begging from the countries they were at par with! Why? Simple, they don’t know their true history especially the legacy of the icons they commemorate instead of agitating that the countries that sponsored them return the wealth they looted. Countries like Spain, Belgium, France and Britain are richer today not just because they have resources: they robbed other countries.
Although I am not a fun of china, I would argue that if African countries play their card nicely, China is likely to bring the balance of trade that Europe has always denied African countries. Shall African countries bargain smartly with China as opposed to the West, chances are that International Trade is likely to embark on fair trade by eliminating all strings that the West has attached on business with Africa. This was evident recently in Sudan. When western countries shied away from developing its petroleum infrastructure, it went to China and made a deal so as to not only survive but also make its ruler Omar Bashir evade the long arm of ICC.
Looking at the naivety of African rulers, one would think that they are not normal mentally. The fact is, they were taught wrong history and they are using the same knowledge to keep on watering colonialism and exploitation. This wrong history has made Africans dependent, incompetent and devoid of self-awareness.
Africa needs to revisit its syllabi and revise its history with a view of discovering itself and removing distortions. If you read for example the true history of the coast of east Africa, you will find that cities like Kilwa, Sofala, Mogadishu,Lamu and others were more civilized by the whole Europe put together at that time.
Source: The African Executive Magazine May 23, 2012.

Kuanzia leo ndata bila cheti hanikamati


LEO wanywa kahawa wamejilawa kweli kweli kutokana na kuwapo tukio muhimu kwa kijiwe. Kusema ukweli leo ni siku muhimu na ya kukumbukwa kwani ni siku ya kutunukiwa udaktari kwa wanakijiwe uliotolewa na chuo kimoja nchini, jina kapuni.
Samahani kwa kuficha jina la chuo kilichotunikia kijiwe kizima PhD ni kutokana na kuogopa wapenda udaktari wasifurike kule kughushi. Ila msomaji ujue kuwa chuo hiki ni genuine na tuliopewa hatujajikomba wala kuhonga tupewa shahada hii inayopagawisha wabongoalalalanders na wadanganyika hasa wenye nazo na madaraka.
Kutokana na kupewa shahada za udaktari, madaktari wapya leo watajadili aibu ya ndata na wasoja kughushi vyeti vya taaluma kama wale mawaziri wa Njaa Kaya ambao ameamua kufa nao kutokana na huduma safi ya kuibia kaya wanayompa. Hayo tuyaache. Leo ni sisi na ndata na ndata nasi kutokana na wanavyotuhangaisha kwa kutukamata tukiwa tunarejea toka kijiweni ukiachia mbali kuingilia mada zetu kila mara hasa tunapogusa wezi wenye madaraka.
Kama kawa Dk. Mgosi Machungi analianzisha. “Wagosi, mie sieewi hii kaya inapeekwa wapi?”
Kabla ya kumaliza Dk Mchunguliaji anadandia, “Kwani hujui kuwa inapelekwa jehanamu au nalo hili uliongoja kulijua ulipopewe shahada kuu?”
Dk. Mgosi Machungi hakupenda alivyojibiwa kwa kuonyeshwa kama hajaenda shule. anakula mic kwa hasira, “Daktai Mchunguliaji tiheshimiane nisijepiga mtu zongo bure. Nauiza swai ya maana wewe unaanga nkungukwa!”
Dk. Mchunguliaji anaomba radhi na kikao kinaendelea ambapo pia anakatua mic, “Madaktari watukufu wasomi wa kaya na kijiwe hiki, kwanza nawapongezeni kwa kupewa zana zetu za ulaji hasa huko nje ambako kila mtu anapagawishwa na udaktari. Hata hivyo udaktari tuliopewa si wa kutibu watu. Hivyo jihadharini msijeletewa wagonjwa mkaaibika.”
Kabla ya kuendelea Dk. Mipawa anakula mic, “Mie nikiletewa mgonjwa namtibu. Kwani kazi? Si unamuandikia karatasi kwenda kununua dawa kwenye duka la madawa na anakulipa pesa ya kumuona daktari.”
Kijiwe hakina mbavu kutokana na Dk Mipawa anavyoonyesha makali yake.
Tukiwa tunaangua kicheko si Dk. Mbwa Mwitu aliingia akiwa na gazeti la Tanzania Daima. Anasema bila hata kutuamkua, “Jamani waheshimiwa,” Kabla ya kuendelea, Dk Eng. Maneno anadakia na kusema, “Sisi si waheshimiwa tena bali madaktari. Omba radhi uendelee kutupa ulilo nalo moyoni.”
Dk Mbwa Mwitu anaomba radhi na kusema, “Wenzangu nisameheni. mwajua kuwa cheo hiki bado ni kipya hivyo nilisahau. Nisameheni.” Anaendelea, huku akiwa anabwaga gazeti mezani huku kila mtu akiligombea asome kwanza. “Mmeona huu upuuzi unaofanywa na lisirikali na makuwadi wake? Eti ndata 4,000 na masoja 2,000 wamepatikana na kashfa ya kughushi!”
Dk. Kidevu hangoji hata aendelee, anakatua mic, “Unashangaa la ndata kughushi wakati mawaziri wameghushi na hakuna anayewashughulikia. Usishangae siku moja ukiambiwa hata Njaa Kaya alighushi kutokana na elimu na matendo yake kuwa mazabe matupu.”
Dk. Mpemba hajivungi, anakatua mic, “Siye Pemba tushazoea haya mambo. Mwankumbuka yule komandoo alokuwa akitutesa?” Anakatua kashata na kuendelea, “Yu aitwa daktari wakati hata hicho cheti cha fomu foo hana!”
Hatuna mbavu tokana na Mpemba anavyokamua lafudhi ya Kipemba. Wakati tukiendelea kucheka, Dk. Eng. Maneno anakamua mic, “Yule jamaa laana tupu. nasikia siku hizi hasikii kabisa.”
Dk Mpemba anaramba tena mic, “Kweli hasikii tena. hata wale walokuwa wakintumia weshankimbia yu ahangaika kama ndege alonaswa ntegoni. Hizo laana wallahi. Hata hawa waloghushi huku wakikamata wenzao watajalaaniwa wallahi.”
Nami Profesa Dk. Mpayukaji naingilia kati baada ya kukaa muda mrefu. Nakula mic, “Hapa laana siyo hawa wanaoghushi basi mfumo na wale wanaowafuga. Kweli kaya imegeuka kaya ya matapeli. Usishangae siku moja kusikia Dk. Koplo Mwita. Dk. Sajenti Chacha. Dk. Afande Ulaji na Dk. Mgambo wa Jiji, Dk. Mpigadebe na Dk. Masaburi, Dk. Mamantilie na kadhalika.”
Watu hatuna mbavu tena. Profesa Dk. Msomi Mkatatamaa anavaa jezi na kuingia uwanjani. Maana kabla mimi na yeye hatujaongea kijiwe huwa kinahisi kama hakujafanyika kitu.
Anakula mic huku akijifuta mdomo baada ya kunywa kahawa yake, “Wapendwa madaktari na wana taaluma wa kweli, kwanza nawapongeza kwa kupata nondo hii muhimu inayowavua nguo watu wengi wenye majina yao.”
Kabla ya kuendelea anajaribu kufukuza moshi wa sigara kali unaovurumishwa na Dk. Kidevu ambaye ametoka kubomu kipisi kwa Dk. Mbwa Mwitu.
Profesa Dk. Msomi anaendelea, “Hapa tusilaumu watu binfsi bali jamii hasa kaya nzima. Kama alivyosema profesa Dk Mpayukaji mwenzangu kuwa tatizo hapa ni mfumo, pia tatizo ni wana jamii wenyewe wanaokubali kuliwa na kuchakachuliwa kila uchao.”
Kabla ya kuendelea, Dk. Mgosi Machungi anamkatisha, “Profesa Daktai Msomi tiombe radhi kwa kusema eti tinaliwa na kuchakachuiwa. Sema wao wanachakachuana isipokuwa sisi wazee wa kijiwe. Vinginevyo unatitukana wote.”
Profesa Dk Msomi anaendelea, “Na iwe hivyo Dk. Mgosi. Sisi hatuwezi kuchakachuliwa wala kuliwa. Hamuoni tulivyopata shahada hizi nzito bila umaarufu wowote wala kutembeza pesa. Sisi ndiyo hazina ya ubongo ya kaya nzima hata rahisi anajua hili. Hivyo, ninachomaanisha ni kwamba kama wanakaya wataendelea kuvumilia uchafu ambapo mtu mchafu anamkamata mtu msafi, watakuja kufanyiwa kitu mbaya siku moja wasilalamike.”
Anavuta kombe lake na kupiga tama mbili na kuendelea, “Kimsingi kaya yetu imeingiliwa na mchezo mchafu ambapo wakubwa wamewageuza wanakaya punda wa kubeba upuuzi wao. Kuanzia leo sitaruhusu polisi anikamate au kunihoji bila kuonyesha vyeti vyake. Nina mpango wa kumwandikia rahisi na spika wa Bunge barua waitishe bunge na kutunga sheria inayomtaka kila askari kuwa na vyeti vyake kila anapokuwa.”
Kabla ya kuendelea Dk Mipawa anaingilia kati, “Kaka hilo halitasaidia. utajuaje kama vyeti watakavyokuwa navyo havijakachuliwa? Watu wanachakachua kura washindwe vyeti? Wanachakachua hata noti zetu tena mle mle banki, washindwe vyeti?”
Profesa Dk. Msomi anaonekana kukubaliana na hoja ya Dk. Mipawa. Anauliza kwa mshangao, “Sasa tufanyeje?”
Dk. Mipawa anajibu haraka, “Tufanye kama Uchina. Tukimshika mtu na cheti cha kughushi, au akifanya ufisadi tunanyongelea mbali.”
Dk. Eng. Maneno anaingilia, “Sasa hapa kaka umegusa pabaya. Utanyongwa wewe. Kambale wote wana ndevu. Naona ndata wanakuja na mikwara yao. Acha tuwazomee kwa kughushi vyeti.
Chanzo: Tanzania Daima Mei 23, 2012.

Tuesday, 22 May 2012

Watawala wetu watasemaje kuendekeza U-ekelege?


Mosquito

Taarifa zilitolewa hivi karibuni kuhusiana na mapambano dhidi ya gonjwa hatari la Malaria ni kwamba nchi nyingi za Afrika Kusini mwa Sahara na Asia zimekuwa zikitumia dawa feki kupambana na Malaria. Wengi wanajiuliza: Kama siyo ufisadi wa makusudi, inakuwaje nchi yenye kila asasi na zana za usalama inaingia mkenge hivi? Je watawala wetu wanatufanyia biashara kwa faida zao huku wakijua wanachofanya? Ama kweli Mangungo wa leo ni wabaya kuliko Mangungo mwenyewe! Ingawa watawala wetu hawatuuzi tena utumwani, wanachofanya ni zaidi ya utumwa maana utumwa ulimwachia mtu uhai na nafasi ya kuasi hata kujikomboa kuliko vifo hivi vya makusudi. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Ni mabazazi wangapi wanakumbuka kisa cha Gaddafi?


 • Hivi ni watawala wangapi wa kiafrika wanakumbuka na kuhofia yaliyompata Muamar Gaddafi hata Saddam Hussein? Kipigo cha rais wa muda wa Mali kimenikumbusha wahanga hawa. Naomba radhi kwa wasomaji wangu kutokana na picha hizi kutisha. Lakini zinasaidia kukumbuka kutokana na utishaji wake.

Unyama hadi kwa malaika!

Kwa mzazi yeyote picha hii inatisha. kusikitisha na kuchosha. Lakini ndiyo ukweli yanatokea hapa hapa duniani. Sijui tunaelekea wapi. Wakati wengine wanakesha wakiomba watoto, wengine wanawanyanyasa kama huyo hapo.