The Chant of Savant

Sunday 13 May 2012

Utumwa mwingie wa hiari! Mangungo wapya

Habari kuwa wabunge wa Marekani wana mpango wa kuisemea Tanzania ni maudhi. Ajabu balozi wetu huko anajisifu amefanya jambo la maana. Je kazi ya wabunge wa Marekani ni kuisemea Tanzania au Marekani? Kazi ya serikali ya Tanzania ni nini kama inasemewa na wabunge wa Marekani? Heri balozi Mwanaidi Sinare Majaar angehangaika na kusafisha jina lake kutokana na kuhusishwa kwenye wizi wa EPA badala ya kuzidi kufanya madudu. Kimsingi,kilichofanywa na balozi ni kuuza uhuru wa nchi. Huu waweza kuwa ushahidi kuwa mhusika hajui hata kazi aliyopewa kama balozi. Je ni yale yale ya kutumiwa vigezo vya kujuana na upuuzi mwingine?  Utumwa mwingine ni wa hiari. Heri hata akina Mangungo wa Msovero hawakuwa wasomi kama hawa madaktari wetu ambao udaktari wao unatia shaka.

No comments: