The Chant of Savant

Sunday 20 May 2012

Ubaguzi ni ugonjwa mbaya sana


  • President Obama (AP Photo/Carolyn Kaster); Ken Bennett (AP Photo/Ross D. Franklin, File)
  • Taarifa kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa jimbo la Arizona,Ken Bennett ametaka kuona nakala ya cheti cha kuzaliwa cha rais Barack Obama ni upuuzi usio kifani. Inawezekanaje kuwa na wasi wasi wa Obama wakati ameishakuwa rais wa Marekani kwa mhula mmoja? Je Obama angekuwa mweupe angeulizwa upuuzi huu? Je huu ni ubaguzi au kutafuta umaarufu? Je hizi ndizo kampeni za Mitt Romney ambaye Bennet ni mwenyekiti mwenza wa kampeni yake? Je Wamarekani ni wajinga na wapumbavu kiasi hiki hadi kulishwa uchafu kama huu? Je angekuwa Bush angemtakisha kitu kama hicho? Mbona haoji dini ya Romney ya Moron? Kweli ubaguzi ni gonjwa baya sana tena linalopofusha. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: