The Chant of Savant

Monday 21 May 2012

Rais anapopewa kichapo cha mwizi!

Junta supporters in Bamako (21/05)
Habari tulizo nazo ni kwamba rais wa muda  nchini Mali, Diancounda Traore, pichani  amelazwa baada ya kupata kipigo toka kwa wananchi wenye hasira wanaopinga uteuzi wake. Mali iliingia kwenye mtafaruku baada ya rais wa zamani Amadou Toumani Toure kupinduliwa na  Kapteni Amadou Haya Sanogo ambaye alirejesha madarakani kwa umma baada ya wiki tatu za kukaa madarakani. Baada ya hapo spika wa bunge wa wakati ule aliapishwa kuwa rais wa muda. Hajakaa hata miezi miwili ashapewa kipigo n waandamanaji! Je haya ni mageuzi katika Afrika au tunaelekea kuwa bara lenye vurugu na hasira baada ya wananchi kuchoshwa na wanasiasa? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: