Magufulification: Concept That Will Define Africa's Future and the Man Who Makes Things Happen

Magufulification: Concept That Will Define Africa's Future and the Man Who Makes Things Happen

Wednesday, 29 June 2011

Kama Nape msaliti, Wassira ni nani?

INGAWA siasa ni mchezo uliojaa uchafu, hadaa na kujilisha pepo, lazima unahitaji kutumia akili. Pamoja na uchafu wake, bado siasa ni kitu ambacho hatuwezi kuishi bila kuwa nacho.

Je, tukubali kila siasa ziwe ni chafu au tuanzisha ustaarabu na utamaduni mpya wa kuweka usafi kwenye siasa?

Tunauliza na kuandika haya kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuongeza uchafu katika siasa za nchi yetu ambazo tayari ni chafu. Kwanza tunashangaa jeuri na upogo huu vitaifikisha wapi CCM.

Kuna taarifa kuwa CCM ina mpango wa kuanza kushughulikia wanoitwa “Mapacha Watatu” ili kulipiza kisasi na kuwaokoa mafisadi waliotajwa na CCM yenyewe baada ya kupitisha uamuzi kuwa “wajivue gamba” kwa kuwatosa.

Hapa wanaotajwa kuwa Mapacha Watatu ni aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa aliyeporomoshwa na kashfa ya Richmond, Waziri na Mwanasheria Mkuu wa zamani, Andrew Chenge anayedaiwa kujiingizia mabilioni ya shilingi kwenye ununuzi wa rada na ndege ya rais na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz anayeshutumiwa kuwa nyuma ya kashfa ya Richmond na ukwapuzi wa mabilioni toka kwenye fuko la Madeni ya Nje (EPA).

Pamoja na watatu hawa kujulikana ndani na nje kwa ushiriki wao katika kashfa hizi ukiachia mbali kuwa washirika wakuu wa Rais Jakaya Kikwete. Wananchi walijitahidi kunyamaza ili waone CCM na serikali yake ingefanya nini kujiondoa kuhusishwa na watu hawa.

CCM kwa kuzidiwa na tuhuma, iliamua kuitisha vikao vyake vikuu na kutoa tamko la kuwapa siku 90 ambazo zinaisha tarehe 10 Julai. Wengi wanangoja kuona nini kitafanyika ingawa dalili zinaonyesha kuwa CCM haikufikia uamuzi huu kwa dhati zaidi ya kutafuta muda na kufanya usanii kama ada.

Katika kutafuta namna ya kufunika kombe ili mwanaharamu apite, mikakati imeishaanza ya kutaka wanaojulikana kama wasaliti chamani yaani, Spika wa zamani wa Bunge na waziri wa sasa Samuel Sitta aliyeridhia kuchunguzwa kwa Richmond na Mwenyekiti wa Kamati teule ya Bunge iliyochunguza Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, mbunge na waziri pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kwamba watoswe kwa madai ya kukisaliti chama.

Kimsingi hakuna usaliti wala kosa kichama na kisheria. Kwanza, chama chenyewe hata akikuundwa. Maana kuundwa chama kikafa bila kusajiliwa kisheria ni kwamba hakikuundwa. Hata kama wangeunda chama kikasajiliwa na kikafa wasingekuwa wametenda kosa ikizingatiwa kuwa katiba yetu iko wazi kuwa kila mtu ana haki ya kujiunga au kuunda chama chochote wakati wowote. Huu si uhuru wa CCM wala serikali bali katiba.

Kama kina Nape, Sitta na Mwakyembe watakuwa wasaliti tuwaite nani kina Stephen Wassira, Masumbuko Lamwai, Walid Kabourou, Thomas Ngawaiya, Augustine Mrema, Maalim Seif Shariff Hamad na wasaliti wengine wa wazi ambao waliowahi kukimbia chama na kurejea baada ya kusota kwa njaa kwenye upinzani au kukaa kule wakiitumikia CCM? Je, hawa wanaoitwa wasaliti na mafisadi nani wanamsumbua Mtanzania?

Tuombe Mungu wanachama wa CCM waendelee kutafutana uchawi huku wakikwepa sababu kubwa ya kuzorota na kuchukiwa kwa chama chao ambayo si nyingine bali ufisadi mitandao na ubabaishaji.

Kama wanaona waliotaka kuunda chama ni wasaliti, basi wawaone hivyo hivyo walioanzisha mitandao ndani ya chama kiasi cha kugeuka mauti yake. Waliotaka kuunda chama wana nafuu ukilinganisha na waliounda mitandao. Kwani madhara ya mitandao kwa chama na taifa yamekuwa makubwa kuliko hata hicho chama mimba ambacho hakikuzaliwa.

Kuna haja ya kuwashauri CCM waache unafiki na upofu. Bahati nzuri, tarehe 10 Julai imekaribia ambapo CCM itavuliwa nguo kutokana na mafisadi kutoachia nyadhifa zao kama ilivyowataka wafanye. Ama kweli huu utakuwa mtihani kwa CCM na Jakaya Kikwete na kufichuka kwa ubabaishaji wake.

Nani hajui kuwa mitandao iliyoundwa na Kikwete na Lowassa iliacha madhara makubwa nchini baada ya kuingiza siasa za kuchafuana na kubaguana? Kama kuna kitu kinaitafuna CCM si kingine bali matokeo na laana ya mitandao ya kuchafuana, kubaguana na kuliana njama ili kupata urais kirahisi kama ilivyotokea kwa Kikwete ambaye ameonyesha kuwa ajali za kihistoria zaidi ya kiongozi.

Nani mara hii kina Salim Ahmed Salim pamoja na uzalendo na rekodi zao zilizotukuka walibaguliwa na kuitwa Waarabu? CCM wanadhani dhambi hii itawaacha bila kuwatafuna?

Hata hivyo, CCM hawana ubavu wa kuwatimua kina Sitta kutokana na ukweli kuwa wakifanya hivyo wataumbuka zaidi. Nani mara hii kasahau jinsi walivyoficha mambo mazito yaliyomhusisha Kikwete kwenye kashfa ya Richmond? Kama Kikwete kajifanya kusahau hili akumbushwe.

Akumbushwe kuhusu waliomtangulia kama Richard Nixon wa Marekani aliyetokomea baada ya kujifanya kusahau alichopaswa kukumbuka. Hata hivyo, CCM wakitimuana na kusambaratika ndiyo neema kwa wananchi. Tuombe hili litokee ili tujikomboe.

Kitu kingine kinachofanya CCM isiwe na mpango wala ubavu wa kuwatimua akina Sitta ni ukweli kuwa licha ya kuwa wanasheria, wana funguo za mochwari ya CCM kama itajifanya kuwaita wasaliti na kutaka kuwatimua. CCM wenyewe ni wasaliti waliowasaliti wananchi kwa miongo mingi tu. Wanapata wapi mshipa wa kuwaita wenzao wasaliti wakati wao ndiyo wasaliti wakubwa?

Kama kina Sitta wataguswa, watakimbilia kwa wananchi kutaka kujua wao na mafisadi ni nani adui wa wananchi. Kama CCM hawataliona hili na kulikubali kwa kujikubali kuwa hawana ubavu wala udhu wa kuwashughulikia “wanafiki”, watakuwa wameonyesha unafiki usio kifani.

Kuna haja ya kuwahimiza CCM watimize walichoazimia wenyewe bila kulazimishwa kuvua gamba kwa kuwatimua mafisadi wanaojulikana. Je, kama CCM wataamua kuwa vipofu na vichwa ngumu kiasi hiki, wananchi nao watakubaliana na unafiki huu unaonuka kuliko kitu chochote?

Kwanini CCM wanapata muda wa kushughulikia watu wasio na hatia wakati wao ni wenye hatia?

Bado Watanzania kwa mamilioni wanashangaa inapopata muda CCM kuwashughulikia wapambanaji dhidi ya ufisadi huku ikikalia makumi ya kashfa kubwa tena zinazoendelea kuwafanya watanzania maskini kuliko wote katika ukanda huku pamoja na kuwa na “amani’ na raslimali nyingi tu!

Wengi wanajiuliza, inakuwaje viinchi vilivyokabiliwa misukosuko na vita tangu uhuru wake kama Burundi na Rwanda vinaizidi Tanzania? Wanashagaa CCM inapopata mshipa huu wakati serikali yake inakabiliwa na mauaji ya wananchi wasio na hatia huku ikitapanya pesa na mali za Watanzania!

Wengi wanashangaa kuona CCM inapata muda wa kuwaonea watu wema ili kuwalinda waovu! Hivi kina Sitta na Mstapha Mkulo aliyelidanganya taifa na Bunge kwa kuleta bajeti ya kihuni ni nani mbaya au wa kwanza mwenye kuhitaji kuadhibiwa? Je, CCM ina ubavu wa kumuadhibu yeyote?

CCM haina tofauti na mbuzi. Kwani imefungwa kwa kamba mbili, yaani mafisadi na “wasaliti.” Ikikata kamba yoyote kati ya hizi mbili bado itaendelea kuwa mbuzi tu.

Chanzo: Tanzania Daima Juni 29, 2011.

Hongera wanakijiwe kwa tuzo la kimatatizo

BAADA ya kurejesha namba kwa mtabiri aliyekuwa akitumiwa na wanasiasa kuwatisha walevi, mzee mzima nimeamua kuanza kutabiri.

Sitakuwa nikitabiri kila siku. Siwezi kufanya hivyo hadi nipate ujumbe kutoka kwa aliye juu. Msiulize juu wapi na juu ya nini wala nani.

Pia nitoe onyo. Wale waganga njaa na wasanii wa kisiasa wanaoingia kwenye madaraka makubwa kuliko uwezo wao ili wayatumie kuwaibia walevi kama ilivyo wasipoteze muda kuja kuomba niwabebe kwa kutoa utabiri wa vitisho.

Mie naaminika kwa uhakika wa utabiri wangu tofauti na tapeli yule marhuni. Sitabiri kutisha watu wala kuwafurahisha wezi wala nini bali ukweli mtupu. Isitoshe mie siendeshwi na tumbo kama wao bali nguvu za Aliye juu. Hayo leo hayanihangaishi zaidi ya hizi tuzo za kisanii na kufuru zionyeshavyo wenzetu wanavyotuona mataahira wa mataahira kulaleki!
Chanzo: Tanzania Daima Juni 29, 2011.

Utabiri wa leo ni mchaganyiko. Kwanza niliota kuwa baadhi ya wezi wenye mamlaka watakwenda Nyuyoko kupokea tuzo feki ili walipane per diem kama mlivyoshuhudia wakikenua kama vyangu. Hapa namaanisha kina Geib Bihalali na Stivi Wahasira ambao walionekana kule wakikenua kwa usanii. Eti Bongolaland imenyakua tuzo! Ama kweli watasha wamejua kututenda!

Kwa vile sasa hii ndiyo sera mpya ya jamaa zangu wasanii, tukubaliane kuwa wamenyakua tuzo. Sasa naanza kutoa utabiri. Baada ya kunyakua tuzo ya hujuma bora za jamii, Bongolaland itaanza kung’ara kuliko mataifa mengine duniani.

Najua kuna mijitu itaguna kuwa hakuna huduma bora bali bora hujuma. Hivi hii mijitu inayoguna haioni watoto wanavyokaa juu ya mawe mashuleni ili kuokoa miti? Haioni jinsi wajawazito wanavyopelekwa hospitali kwa bajaj ili kuepuka kuchafua mazingira? Anayebisha aende pale Mwanamanyala aone wanavyotendewa kwa ukalimu bila rushwa wala kuwaacha na mikasi kwenye matumbo ukiachia mbali kuokoa vichanga vingi visifie getini kwa kukosa ngawira.

Pia Muhimbili ni mfano bora ambapo madaktari waliwahudumia vyema wagonjwa hadi wakachanganyikiwa kwa furaha na kuwa vichaa kwa muda kiasi cha mmoja kumnyotoa roho mwenzake ukiachia yule aliyepasuliwa kichwa badala ya mguu akadedi kwa furaha ya huduma bora.

Hivi jamani hamuoni wajawazito wanavyoteswa, watatu kitanda kimoja ili kubana matumizi ya kununua vitanda? Kuwabanisha wajawazito kitanda kimoja kunajenga mazoea kwa watoto watakaozaliwa kujua kubana matumizi. Asiyeona hili ama ni chizi au kipofu.

Hebu nipigieni makofi kidogo kwa kufichua neema hizi. Nani hajui kuwa kupunguza vitanda kunaongeza mashangingi ya wakubwa? Je, hizo si hudama bora? Tuendelee.

Hivi hamuoni mvua ikinyesha jiji la Bongolalalandcity linavyojaa swimming pool za bure na pafyumu ya bure? Hivi hamjui kuwa wabongolalalanders wameshiba huduma za jamii na kutosheka kiasi cha kuwapenda viongozi wao hadi watawala hata nusu watawala, wake, watoto hata waramba viatu wao wakipita barabara zinafungwa ili wapite bila usumbufu?

Uzuri wanafanya hivyo bila kujali kuna mgonjwa au wanaoungua kwa jua na vikwapa kwenye madala dala. Huo ndiyo uongozi bora na huduma bora za jamii ati.

Funga kazi ni kutumia giza badala ya umeme ili kuepuka utumiaji mbaya wa nishati. TWANESKO upo mshirika hapo?

Kwanza tuzo hii itageuzwa sera na majasifu kutokana na watakaofanya hivyo ima kuishiwa sera au kujulikana wasivyo na sera wala akili. Sitawataja mnawajua. Natatibiri kuwa kesho mtasikia Bongolalaland ikinyakua tuzo ya utawala bora hasa kutokana na sera yake ya bora utawala chini ya kisingizio na ngonjera za utawala bora.

Maana duniani hakuna utawala bora kama ule unaoweza kuamrisha geshi la manjagu likanyonga walevi na hao mabwana zake wasikemee kama walivyofanya kwa kaka Moi Kibaka. Bongolalaland ina kila sifa ya kupewa tuzo ya utawala bora kutokana na utawala wake kuzingatia kujuana, mitandao, familia, ufisadi, ufisi na usanii. Rafiki yangu Njaa Kaya na Riz two mpo hapo?

Siku hizi licha ya kuficha watu unaoandamana nao kwenda kutanua, naona mshirika wako wa bedroom amegeuka ama waziri wa mambo ya ughaibuni au makamu wako.

Maana ukienda popote ukiongoea na dingi naye anaonyeshwa akiongea na maze. Siri ya mafanikio haya yote nini? Utawala na u-twawala bora. waleni walevi kama hataki kustuka.

Baada ya hapo tutegemee tuzo ya kutunza na kupamba ufisadi. Hapa kigezo cha ushindi itakuwa ni jinsi tulivyoanzisha na kushughulikia HEPA na Richmonduli ambapo kaya ilipata faida na maendeleo ya kutisha hasa kwenye medani za siasa.

Baada ya tuzo hilo hapo tegemea jingine la kuthamini wageni kuliko walevi bila kusahau ukarimu.

Tuzo itakayofuata baada ya ile ya kutunza na kupamba ufisadi ni ile ya kutunza mito hasa kule mkoani Mara ambapo juzi juzi kulikuwa na maandamano nchini Kanada ya kuunga mkono kuchanganya tindikali na maji kiasi cha kuwageuza wabongolalanders wazungu.

Nani mara hii amesahau yale maneno yaliyosikika mwekaji mmoja akimtishia mwenyekiti wa kijiji kuwa apokee mshiko baada ya kumwambia kuwa hata rahisi anahongwa itakuwa yeye.

Jamaa aliyesema hivyo nasikia anatokea kule Ukanada na anaitwa Mr Jeff. Anyway nikienda Ukanada nitaongea na bwana Harper. Maana tulisoma wote kwenye chuo kikuu cha Calgary. Hayo ni masuala binafsi tuyaache.

Tuzo zinaendelea kumiminika. Tuzo itakayofuata ni ile ya polisi kuwakomesha viherehere na kuwalinda wawekaji. Nani masahau yaliyotokea kule Tarime ambapo manjagu waliwakomesha walevi waliokuwa wakitaka kukomesha uchanganyi wa maji na zebaki wasijue ndiyo maendeleo. Njagu walinyonga sita bila taasisi za kimataifa za haki za binadamu hata kujali. Taasisi hizi huwa hazishabikii upinzani. Tuyaache.

Tuzo itakayofuata, natabiri. Itakuwa ni tuzo ya uwekezaji bora unaolenga kukuza chumi za watawala huku ukidumaza uchumi wa walevi. Leo sitaki nifumue balaa hili.

Give me some times somewhat in he future, I will try to explain this usufunctuary like rights of the walevi to benefit from their country.

So too, I surely will dwell on the whole fiasco whereby the venal rulers are stealing in the broad light day. What a heck! Sorry. Mwenembago alipanda nikaongea kitasha.

Tuzo funga kazi itakuwa ile ya watawala kutanua huku walevi wakipukutika. Please give more time for research.

Hivi yule manzi hawezi kuwa tuzo yangu tonight? Ngoja nimuwahi ili nipate tuzo ya ujogoo. See you all.

Tuesday, 28 June 2011

Mgao wasababisha vurugu Senegal somo kwa Watanzania


Wakati watanzania wakiendelea na ukondoo na kuahirisha tatizo kutokana na kuzoea kuteseka, wenzao wa Senegal wameamua kujikomboa. Juzi kulikuwa na ukatikaji wa umeme uliodumu masaa 24 katika baadhi ya sehemu. Hili kwa wasenegali wasio na mchezo na mtu lilitosha kuwatia hasira na kuingia mitaani ambako walichoma jengo la shirika la umeme la Senegal lijulikanalo kama Senelec.
Ikumbukwe. Kabla ya hapo kama siku tatu zilizopita, wasenegali hao hao walikuwa wameingia mitaani kumzuia rais wao Abdullaye Wade kutaka kubadili katiba ili aanzishe cheo cha makamu wa rais. Wanadai alilenga kuanzisha cheo hiki ili amteue mwanae Karim ambaye ni waziri katika serikali ili amrithi baadaye. Hii ni baada ya Wade kujaribu uhuni wowote bila kufanikiwa. Hata hivyo Wade aliachana na njama hii baada ya vijana kuingia mitaani na kuzusha tafrani. Je tatizo la Tanzania ni nini ambapo kuna mgao wa umeme kwa takribani miaka kumi sasa! Senegal wameweza. Sisi tutaendelea kuchezewa shere hadi lini! Hebu tufikiri pamoja. Senegal wamekosa umeme masaa 48 bila pesa yao kuibiwa kwenye ujambazi wa EPA wala wanaowalaza kizani kuingiza ujambazi wa Richmond. Je wangefanyiwa kama watanzania wa Danganyika hali ingekuwaje kwa hasira!
Kwa habari zaidi bonyeza hapa.

Thursday, 23 June 2011

Waje wamanga wasuluhishe gogoro hili

BAADA ya mkuu kuwajia juu viongozi wa kiroho na kirafi kuwa wanajihusisha na biasharaya bwimbiwi, nao walijitutumua na kumpa saa 48 atubie vinginevyo wanamuingiza motoni, nimeona nitoe darasa.

Mbona saa 48 zimepita na waramba viatu wamezidi kuwapasha nao wakanywea? Kumbe wote wasanii siyo?

Kwanza, walikosea hata kama naye alikosea. Hawakujua kuwa anawajua kama wanavyomjua? Isitoshe, angeogopa moto upi wakati amezoea kuishi huko? Heri wangemtishia kuwa watamwingiza gizani.

Maana tangu mgao wa kiza uanze hajawahi kugawiwa lau kwa siku moja.Pia viongozi wa kiroho na kirafi walikosea. Zamani waliheshimika sana. Lakini baada ya ushehe na uaskofu kuvamiwa na matapeli huku hata wale wa kweli wakikabiliwa na madai ya kulawiti, kuzini na upuuzi mwingine, hakuna anayewaheshimu tena.

Zamani ukimuona askofu au sheihe unamheshimu.

Siku hizi wamejaa wachungaji, mashehe na maaskofu bandia, tena wa kujipachika ili washibe karibu kila kona.

Mnamkumbuka yule aliyenaswa juzi kwakutaka kubaka? Pale kaya ya jirani na shehe yuko msambweni kwa kubaka vitoto vilivyokuja kusaka ilmu akavijaza haramu badala ya ilmu.

Ama kweli dunia imegeuka tambara bovu na gunia! Zama zile usingeona mpiga ramli au mganga wa kienyeji akiitwa shehe. Usingeona muota ndoto akiitwa mchungaji au askofu.

Wala usingeona mwizi au jambazi akiingia kukuu na kuitwa rai… we koma! Lakini kwa sasa hali ikoje?

Leo tutadurusu mambo mawili yanayounganishwa na uroho na roho za udini.

Kwanza ,tutaanza na ile kali ya mkuu kuwatolea uvivu wachunaji wa kondoo na mashehe na kuwa wanajihusisha na bwimbwi. Je, amekosea?

Hawa wanaoporomosha mishule ya bei mbaya kila kona kama si wauza bwimbwi njuluku walizinyaka wapi?

Muulize yule mama mwenye jina kama Tarehe.

Wengine hawauzi bwimbwi bali roho za waumini.

Wanatoza sadaka wakisema ni kwa ajili ya Sir God kumbe zao na nyumba ndogo zao.

Wapo wanaojikomba kwa wakuu kama ilivyotokea kwa shehe na mmoja aitwaye Amiss Matakataka aliyewatishia wapingaji kuwa wafuate sheria wakati yeye hafuati sheria wala sharia bali tumbo lake.

Shehe Matakataka upo hapo? Acha nikupashe. Pia usintishe kuwa utanisomea Albadir.

Ukinisomea Albadir mie nakusomea Al-geuza. Ukisoma kwenda kulia mie nasoma kwenda juu tuone. Kumbaff.

Kama ushehena haukulipi si uuze nyanya tu badala yakujikomba kwa wenye maulaji ili wakutupie makombo.

Shehena Matakataka amenikumbushe kijeshe na kimoja Kirundi kiitwacho Amiss kaa yeye kilichokuwa kikiwachonganisha watu kwa kujificha nyuma ya joho sijue wanajua habari zake.

Kitapeli hiki cha majoho eti kilikuwa kinajificha kwenye unyema wakati tukijua fika kinatokea mitaa ya Buja.

Hakuna kilichonichanganya kama maneno ya shehena Matakataka.

Alikaririwa akisema eti lisirikali kuwaonea wapingaji kwa kuigeuza Mahaka… (we koma utafungwa!)- nyumba ndogo yake kama geshi la mandata eti ni suala la kisheria.

Tangu lini shehena la taka lililokimbia shule likajua sheria kama si utapeli?

Eti Matakataka alikuwa akiwataka walevi wasifanye vitendo vya kisiasa wakati lenyewe bila hata ya chembe ya aibu lilikuwa likifanya vitendo vya kisiasa likijificha nyuma ya joho!

Ama kweli nyani haoni nonihino Lake. Fungeni madomo yenu kama hamna la kusema badala ya kujikomba.

Sasa mnayejikomba kwake ameamua kuwatolea uvivu.

Nakumbuka mashehena wengi huja juu pale wachunaji kondoo wanapomjia juu msaniiwakidai ni udini na chachi eti inataka kutawala kaya.

Nendeni skuli mkajifunze jinsi mambo ya kisasa yanavyoendeshwa na si kupayuka bila kuwa na vipaji naelimu ya kupayuka kama mimi.

Hebu tumgeukie Mkuu wa Kaya ambaye naye amejipayukia bila kujua kuwa anachowatuhumu viongozi wake wa kiroho kimo nyumbani mwake.

Kwanza namlaani yule mbea wake aliyetoa taarifa ya kipuuzi akipindisha maneno na kuwashangaa jamaa wa majoho wakati naye anapaswa kuzusha mshangao.

Hivi kweli huyu jamaa mwenye jina la yule jamaa wa Kwachaga aliyemtandika mkoloni kasomea uandishi au kanjanja aliyepewa ulaji kwa kujuana?

Mkuu alipayuka kutokana na kuwa na tabia ya kujisemea bila kufikiri.

Unakumbuka wakati wa mchakato wa akina Richmonduli alisemaje? Alijipayukia kuwa mgao wakiza ungekuwa historia baada ya muda mfupi.

Bila kuona mbali alijipayukia na mambo yaka mgeuka hadi kiza kikiageuka kansa au ukimwi. Si hilo tu. Moto ulimwakia hadi akamtoa sadaka swahiba yake ambaye tuna ngoja kuona kitakachotokea hapo Julai 10 zitakapoyoyoma siku kenda kumi zilizotolewa katika usanii wa kujivua gamba.

Mkuu wetu Kijiweni, amekuwana tabia ya kupayuka. Nani amesahau alivyopayuka miaka ya nyuma kuwa atawapeleka kwenye nchi ya nyama choma na ulabu akaishia kuwabamiza mkenge?

Bahati mbaya amemwambukiza hata kitegemezi chake Riz-One aliyetoa mpya hivi karibuni baada ya kufichuka chafu yake kuwa angewafikisha kwa Pilato waliosambaza nepi zake ugani.

Muulize atakwenda lini zaidi ya kufyata kia.
Chanzo:Tanzania Daima Juni 22, 2011.

Tuesday, 21 June 2011

HONGERA DK WILLY MUTUNGABlog hii inachukua fursa hii kumpongeza jaji mkuu wa Kenya Dk. Willy Mutunga kuchaguliwa kuwa jaji mkuu wa Kenya. Pamoja na kuwa rafiki yetu wa karibu, tunachukua fursa hii kuungana naye kwenye adhimisho hili la utumishi wa umma uliotukuka.Kwa tunaokukumbuka ukiwa Mkurungenzi mtendaji wa Kenya Human Rights Commission pale Valley Arcade Lavington kabla ya kwenda kuwa mkurugenzi wa Ford Foundation pale Kenyatta, tunajua unyenyekevu na uwazi wako. Tunaokujua kama Mutunga na si daktari wala jaji mkuu, tunajua ni aina gani ya mtu na mchapakazi Kenya imepata hasa kipindi hiki cha kuanza kutekeleza katiba mpya ya Kenya. Tunaamini mchango wako utakuwa somo na changamoto kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki zinazoendelea kutawaliwa na ubabaishaji, ukale, usanii na majaribio.
Kila la heri na Mungu akuongoze na kukufanikishia kila chema ulichodhamiria kuitendea Kenya.
Dk Mutunga, tunaamini utakuwa chemi chemi ya mageuzi na ukombozi wa Kenya kama ambavyo umekuwa siku zote.
Ni rafiki yako Nkwazi Mhango

Monday, 20 June 2011

Wanampigania Mungu au shetani je hawa si makafiri?


Police said Monday that militants kidnapped a 9-year-old girl on her way to school and forced her to wear a suicide bomb vest. The girl and police said she managed to escape her captors as they directed her to attack a paramilitary checkpoint in northwest Pakistan.

Sohana Jawed, who is in third grade, said she was abducted near her home in the northwestern city of Peshawar on Saturday and taken to Lower Dir district, a four hours' drive away, where she was found Monday.

Police in Lower Dir presented Jawed at a news conference, where she told her story dressed in her blue and white school uniform. But police in Peshawar said they haven't received a complaint of a missing girl and haven't identified a resident with her name.

Initial police reports of security incidents in Pakistan are sometimes wrong.

Militants in the country have often used young boys to carry out attacks, but the use of young girls is rare.

Jawed said during the news conference that she was grabbed by two women while on her way to school and forced into a car carrying two men.

One of the kidnappers put a handkerchief over her mouth that knocked her unconscious, Jawed said in a separate interview with a local TV station.

When she woke up and started crying, one of the women gave her cookies laced with something that again knocked her out, Jawed said. The next time she woke up she found herself in a strange home, she said.

"This morning, the women and men forced me to put on the heavy jacket and put me in the car again," said Jawed.

The suicide vest contained nearly 20 pounds (9 kilograms) of explosives and seemed to be designed to be set off remotely, Lower Dir police chief Salim Marwat told The Associated Press.

"Most likely it had to be detonated through a remote control since a minor was wearing it," he said.

The kidnappers brought her to a checkpoint run by the paramilitary Frontier Corps located about 6 miles (10 kilometres) outside Timergarah, the main town in Lower Dir district. When they got out of the car, she sprinted toward the paramilitary soldiers to show them what she was wearing, said Marwat.

"I got the chance to release my hand from the woman and run," said Jawed.

By the time the paramilitary soldiers realized what was happening, the kidnappers had escaped, said Marwat. Police have launched a search operation to find them, he said.

It's unclear why the kidnappers didn't detonate the suicide bomb vest after Jawed ran away. Marwat suggested they may have simply panicked and fled.

Asif Khan, the police chief in the area of Peshawar where Jawed said she lived and was kidnapped, Hashtnagri, said they haven't received a complaint of a missing girl and haven't identified a resident with her name.

Police in Lower Dir plan to ask Jawed additional questions after she is examined by a psychiatrist, who is helping her cope with the trauma of her ordeal.

"Police will try to get more information from her once she gets normalized," said Marwat.

Source: Internet

Saturday, 18 June 2011

Chiluba is no more


Frederick Chiluba, Zambia's first democratically elected president, has died at home at the age of 68.

Mr Chiluba was hailed as Zambia's "liberator" by his supporters when he came to office in 1991 after 27 years of single party Socialist rule.

He won praise for his economic and political reforms but was later accused of embezzlement and turning a blind eye to corruption.

The cause of his death is not known but he was known to have heart problems.

Under Mr Chiluba, Zambia was considered to be a model of African democracy and his presidency was welcomed in the West.

The former trade union leader and son of a copper miner introduced many reforms which dismantled the restrictive policies of former President Kenneth Kaunda.

But he was dogged by corruption allegations and was accused of taking an authoritarian approach to his political opponents, firing critical colleagues and jailing outspoken journalists.

He attempted to alter the constitution to allow him to run for a third term in office in 2001, but stood down after huge public protests.

Mr Chiluba was prosecuted for alleged embezzlement in 2002 but acquitted after a six-year trial.

In 2007, he was convicted of fraud by a London court and ordered to repay $58m in embezzled funds, but the ruling was never carried out by Zambia.

He spent his final years at his resident in Lusaka, confined by ill health and the confiscation of his passport by the authorities.
More on This Story

Source: BBC

Tuesday, 14 June 2011

Waumini waliwao mpo hapo?

Nigeria's pastors 'as rich as oil barons'

Nigeria's pastors run multi-million dollar businesses which rival that of oil tycoons, a Nigerian blogger who has researched the issue has told the BBC.

Mfonobong Nsehe, who blogs for Forbes business magazine, says pastors own businesses from hotels to fast-food chains.

"Preaching is big business. It's almost as profitable as the oil business," he said.

The joint wealth of five pastors was at least $200m (£121m), he said.

Mr Nsehe said the richest of them, Bishop David Oyedepo of the Living Faith World Outreach Ministry, was worth about $150m.

Bishop Oyedepo owned a publishing company, university, an elite private school, four jets and homes in London and the United States, according to Mr Nsehe.
'Private jets'

The Nigerian blogger said Bishop Oyedepo was followed on the rich list by Pastor Chris Oyakhilome of the Believers' Loveworld Ministries. He was worth between $30 and $50m.
These pastors are flamboyant. You see them with private jets and expensive cars.

"Oyakhilome's diversified interests include newspapers, magazines, a local television station, a record label, satellite TV, hotels and extensive real estate," Mr Nsehe said.

He said three of the other richest pastors were:

Temitope Joshua Matthew of the Synagogue Church Of All Nations (worth between $10m and $15m);
Matthew Ashimolowo of Kingsway International Christian Centre (worth between $6 million and $10 million) and
Chris Okotie of the Household of God Church (worth between $3 million and $10 million).

Mr Nsehe said representatives of all the clergymen, except Pastor Ashimolowo, confirmed ownership of the assets he had listed on his blog.

"These pastors are flamboyant. You see them with private jets and expensive cars. This extravagance sends out the wrong message to their followers," he told the BBC's Network Africa programme.

He said the pastors acquired their wealth from various sources, including their congregations.

"We have Nigerians who are desperate, looking for solutions to their problems. They go to church for salvation, redemption and healing and pastors sometimes take advantage of them," Mr Nsehe said.

Source BBC

Monday, 13 June 2011

Mabalozi wetu na aibu na uroho wao

The wife of a Congolese diplomat in Serbia has been detained in neighbouring Romania for alleged cigarette smuggling, prosecutors said on Monday.

Esther Pascaline Bombeto was arrested during the night soon after crossing the Serbian border.

Police found some 18,500 cigarette packages concealed in her car.

According to local media, the woman and her driver refused to leave the car or open the doors, arguing they benefited from diplomatic immunity.

The police had to break the window in order to search the vehicle bearing diplomatic licence plates.

The husband, Marc Marius Itela Elombola, second counselor of the Republic of Congo's embassy in Belgrade, has also been charged with smuggling. He is currently in Serbia.

"The authorities did what they had to, detaining a person suspected of contraband," a spokeswoman for the prosecutor's office told AFP.

"The issue of diplomatic immunity will be probably raised before the judge is called upon to deliver an arrest warrant," she added, stressing that it was not clear what the woman's diplomatic status was.

"Before the arrest we consulted the Ministry of Foreign Affairs in order to make sure we did not violate any law," prosecutor Mircea Andres, who is in charge of the investigation, told journalists.

He said that according to the Vienna Convention diplomats committing a felony in a country other than that to which they are accredited are not covered by immunity.

Andres added that the Congolese couple had been monitored for three months.

They used to cross into Romania once or twice a week, and, availing themselves of their diplomatic passports in order to avoid customs controls, smuggled large amounts of Albanian cigarettes into the country, he said.

Three Serb nationals, including Bombeto's driver, and three Romanians have also been arrested.

Source: Daily Nation.

Sunday, 12 June 2011

Meet with the "tallest" man on earthJunrey Balawing, the "World's Shortest Living Man" declared by the Guinness World Records, holds a ruler in front of his family and townmates in Sindangan, Zamboanga del Norte in southern Philippines June 12, 2011. Balawing was certified by the Guinness World Record as the shortest man in the world with standing and lying down average measurement of 23.5 inches (59.93 cm) on his 18th birthday on Sunday. The previous title holder is Khagendra Thapa Magar from Nepal who measures 26.4 inches (67.06 cm), and 2.9 inches (7.36 cm) taller.
Source: Internet

Thursday, 9 June 2011

Bunge liwe linafanyika Railway Gerezani

BAADA ya kugundua uhovyo na uchovu wa wabunge wao wa ulaji, kijiwe kimekuja na mkakati wa kuwapindua ili walevi wapate wawakilishi wenye udhu na makali. Kuna kashfa zilizolazimisha kijiwe kuanza kufikiria kulipindua bunge.

Tunataka kurejesha heshima ya bunge na lenye viwango vya kistaarabu na si kuburuzana, kushindana kuonyesha fasheni za blackberry, dhahabu, mavazi na utumbo mwingine kama vile kulala bungeni, kupayuka na kupokea taarifa za wizi bila kuufanyia kazi.

Tunataka Bunge la walevi na si wachuma ngawira. Bunge tunalotaka si la kulipana posho za vikao na kupitisha miswaada na bajeti za kipuuzi. Hatutaki Bunge la jikoni bali la walevi.

Kwanza tulaani kitendo cha mandata kumkamata kiongozi wa upingaji bungeni bwana Freedom Mboe.

Geshi letu la mandata nalo limegeuzwa jibwa la Chama Cha Mafisadi kiasi kwa kuwa tayari kuwakamta wabunge huku likiwapigia saluti mafisadi. Acheni umbwa na unepi mtafanyiwa kitu mbaya siku moja. Shauri yenu.

Nashangaa. Kama Freedom angekuwa mbunge wa Chama Cha Magamba unadhani hao mbwa wa CCM, yaani Chama Cha Magamba wangethubutu kumkamata? Sijui kwanini hii mijitu haitaki kujifunza kutoka Misr!

Kuna siku hayo madaraka viraka yatachukuliwa na kupewa wengine. Yaani mauaji ya Talime hayajatulia mnakamata kiongozi wa upingaji. Kama hao wanaowatuma hawataki upinzani si watangaze ufalme ijulikane. Hayo ya kukamatwa wa arawa nayaachia hapa. pole sana arawa babangu.

Sababu ya pili ya kijiwe kudhamiria kutwaa Bunge ni ufisadi. Baada ya kuchunguza orodha ya wabunge na mishiko ya makali (sitting allowances) wanayopata bila kufanya lolote, kijiwe kimeamua tuchukue hatua. Tuhakikishe wabunge wote mafisi, mafisadi, magamba, vinyoka vilivyorithi nafasi za wazazi wao au kuukwaa kutokana na ukoo vipigwe kibuti.

Tatu, ni ubabe. Baada ya kuona mama Kipaza Sauti au microphone or speaker kwa kimombo kutembeza ubabe akitetea mafisadi waliomsimika, tumebuni mkakati wa kuhakikisha anapigwa chini kama alivyofanyiwa Sam Sixx kutokana na usongo wake wa kuwabamiza mafisadi.

Baada ya mama huyu aitwaye Annae Mwenye Makinda achezaye Makida makida kuwa mbabe na mroho na mbinafsi kiasi cha kufunga hata njia za watu ili ajenge hekalu lake, kijiwe kimeona ni busara kuanza mikakati ya kumgaragaza chini ili afanyiwe kweli kwa kumtosa.

Pia kijiwe kimegundua kuwa wabunge wanalipwa mishiko mikubwa ikilinganishwa na uchumi wa kaya. Hivyo, tumekuja na mkakati wa kupunguza maulaji yao kwa kuchagua watu wasio na stori na pesa wala utajiri bali uzalendo na maendeleo.

Nne, kashfa ya wengi wa wabunge kuwa vihiyo wenye shahada za kughusi imetulazimisha kuunda kamati ya muda au ad hoc committee ya kurejesha kaya kwenye mstari.

Tano, baada ya kuona mapapa na mabingwa wa ufisadi na ukoo na kujuana wakipewa uenyekiti wa kamati nyeti za Bunge, tumeamua kujipanga upya kulitwaa Bunge ili liwe na watu safi na si mafisi na mafisadi na magamba na vinyoka kama Jannie Makambale Mgosi, Hussain Muinyi, Emmy Nchimvi, Wars Kawaua na dada yake Zamazaradi.

Hapa bado hujawataja wengine wenye majina ya vigogo kama Msuuuya na wengine wengi wanaojulikana kuwapandikiza vitegemezi au wake zao bungeni. Wana kijiwe na walevi si wanafiki. Wanajua hata wakuu wa mawilaya hata mikowa walipewa ukuu kutokana na majina ya baba zao au kujipendekeza hata kujihonga kwao. Bado hapa hujaongelea wana geshi waliojazana kwenye vyeo vya kisiasa wakati ni kinyume cha sheria.

Sababu nyingine ya kuchukua hatua ni ile hali ya wabunge kushindwa kuliadhibu lisirikali tokana na kushindwa kulinda mali za walevi. Wako wapi akina Kagoda, EPA, SUKITA, Meremeta, IPTL, Richmond, Dowans na wengine wengi?

Ili kuhakikisha tunafanikiwa kuikomboa kaya kutoka kwenye mikono ya mafisi na mafisadi, tutaandaa mikutano kayani kote kutaka katiba ibadilishwe haraka na sifa za wagombea ubunge zibadilishwe. Tunapendekeza mgombea awe na sifa zifuatazo ili aweze kugombea ubunge.

Mosi, awe bingwa wa kupiga masumbwi na si kupika majungu wala kughushi vyeti kama wale walivyo. Pili, ajue kupayuka kwa sauti na busara kama mzee mwenyewe na si mipasho na umbea kama mgosi Machungi na Mape Nnaye.

Tatu, asiwe mpenzi wa njuluku kama Annae Makapi au Sisalama Kikwe ambao waliotumia kukuu kufanya umachinga kwa NGO.

Nne, awe tayari kuvua nguo si magamba. Maana uchafu wa mtu huonekana kwenye nguo kuliko ngozi ambayo hufichwa na hiyo nguo. Hivyo, tutapendekeza mwenye kutaka kuonyeshwa ukweli wa usafi wake avue nguo ili abaki utupu kila mtu aone madhambi yake.

Ewassa, Chwenge na Rostitamu mpo washirika? Stop cheating yourself just like the Bunge that plays bungee with the rights of our walevi. What a—lie so to speak.

Lol! Mwenembago kaishapanda kiasi cha kuanza kuongea kwa lugha ya majini ya kwa mama! Tuendelee na sifa za wabunge watarajiwa. Lazima mwenye kuutaka ubunge awe tayari kutangaza mali zake. Awe tayari kuchukia kitu kidogo na kikubwa yaani rushua.

Pia awe tayari kuvimbishwa mishavu kwa ngumi na asione aibu badala ya kuvimbisha matumbo na mishavu kwa pesa ya ufisadi. Aweze kuonea aibu kuvimbisha mitumbo na mishavu kwa pesa ya ufisadi.

Pia anapaswa ajue kuvaa gwanda au jezi ili awe tayari kupiga karate na si misuti ya ujambazi. Kwanza nani anataka suti Bongolalaland ambako joto ni kama tuko kwenye oveni? Nani anataka suti ili kumaliza kodi za walevi kwa kulipia viyoyozi kweni vya kwenye mashangingi yenu havitoshi?

Sifa nyingine, Kuwa tayari kutoa jasho kwa kukimbia ili kufanya mazoezi ya kuwachapa wapinzani wetu badala ya kukimbiza mishiko na dogo dogoz wakati wa vikao vya Bunge.

Pia mwanamume au mwanamke atakayeutaka ubunge awe tayari kuupenda udugu na si uheshimiwa wakati wengi wa wanaoung’ang’ania uheshimiwa hawana heshima wala kuistahili kutokana na matendo yao ya kinyani nyani. Hawa ni waishiwa.

Sifa nyingine ni ya Speaker. Lazima awe amesoma sheria, awe na mke au mume na si kanunga. Pia awe na akili timamu na busara na asipendekezwe kwa jinsia yake au ushikaji na mafisadi kama ilivyokuwa huko nyuma alipopigwa buti Sam Sixx.

Asiwe mbinafsi, mlazimishi, mpenda makuu wala tunda na chaguo la mafisadi. Aingie kwa sifa na si kubebwa na jinsia au kujuana.

Naona makabrasha ya kusaini mshiko yameletwa. Acha nijiwahi kutia mkono ili niende kuutwika na kusaka vyangu waliokuja kushiriki bunge la usiku kwenye nyumba za kulala wageni.

Bunge lifanyike uwanja wa ngumi Gerezani ili tuchapane ngumi sawa sawa.

Muishimiwa spika naomba kutoa hoja.

Chanzo:Tanzania Daima

Tuesday, 7 June 2011

RENATA BENEDICTO ANATAFUTWAYaweza kuwa binafsi lakini ni kwa kuwa nahitaji msaada.
Desemba mwaka 1999 nilikuwa miongoni mwa wasafiri waliokuwa kwenye hilo basi la Tawfiq ambalo kwa bahati mbaya lilipata ajali na kuua watu wengi alfajiri ya tarehe 23. Wengi tulijeruhiwa japo wengine tulihitaji huduma zaidi kulingana na majeraha yetu. Katika safari hiyo nilikuwa nimekaa na binti mdogo ambaye baadae alijitambulisha kwangu kama Renatha Benedicto. Alikuwa kidato cha pili shule ya sekondari Kibasila, Dar. Kuwa mdogo ama mwanafunzi, si sababu ya kumsaka leo. Namsaka kwa kuwa alikuwa shujaa katika siku hiyo na ninasikitika kuwa juhudi zangu nyingi za kusaka mawasiliano naye (zikiwa ni pamoja na kutumia redio) zimeshindwa kunirejeshea mawasiliano naye.
Katika ajali hiyo, nilijeruhiwa vibaya. Nilichubuka sehemu kubwa ya uso upande wa kulia. Nilipasuka juu ya jicho, ndani ya mdomo, sehemu mbili za kidevu, michubuko ya magoti. Pia nilikatika ulimi na kunifanya nishindwe kuongea kwa siku nilipokuwa hospitali. Pia ilinitibua mgongo ambao kwa miaka 9 iliyofuata nimekuwa nikipita kwa wataalamu mbalimbali kupata matibabu. RENATHA alikuwa zaidi ya mhudumu kwangu. Alitafuta dawa, kuhakikisha natibiwa, pia alihangaika kusaka mawasiliano ya kuwajulisha walio nyumbani kuwa tukingali hai (bahati mbaya mawasiliano hayakupatikana). Alihangaika wakati wote ambao nilikuwa siwezi kusema lolote kutokana kushonwa ulimi. Alitengeneza "chakula" kilichoweza "kushuka" kunipa nguvu na kuwa msemaji wangu akitumia taarifa nilizomuandikia kwenye karatasi na passport (kwa kuwa hatukuwa tukifahamiana kwa majina). KWA HAKIKA ALIKUWA MSAADA MKUBWA KWANGU.
Baada ya likizo tuliendelea kuwasiliana na mpaka alipomaliza shule mwaka 2001 na mara ya mwisho kuonana naye alikuja kuniaga (2002) akisema anakwenda Songea kusomea ualimu. Aliahidi kuwasiliana nami baada ya kufika huko na kwa bahati mbaya nami nikahama. Baada ya hapo nikaanza pilika za maisha zilizonifikisha huku nilipo, lakini kila nikifikiria "njia" ya maisha nauona mchango mkubwa alioweka maishani mwangu na najaribu kumtafuta bila mafanikio..
Nimeona leo niweke hapa ili kama kuna anayemtambua anisaidie kurejesha mawasiliano naye.
Ni Renatha Benedicto. Alisoma Kibasila Sekondari kati ya 1998- 2001 kisha akasema anakwenda Songea TTC.
Njia rahisi ya kuwasiliana nami ni barua pepe ambayo ni
changamoto@gmail.com

Sunday, 5 June 2011

Zimbabwe policeman jailed for using Mugabe's toilet

Relatives of a policeman jailed in Zimbabwe for using a toilet reserved for President Robert Mugabe are appealing for his release.

The policeman, Alois Mabhunu, was arrested last month in the city of Bulawayo after he used a special presidential toilet at a trade fair.

A police court on Wednesday ordered his imprisonment for 10 days.

Zimbabwean human rights lawyers said there was no law forbidding people from using the president's toilet.

They said Mr Mabunhu should not have been arrested.

Mr Mugabe, 87, visited Bulawayo, the country's second city, for the opening of the annual Zimbabwe International Trade Fair on 6 May.

Mr Mabunhu was on duty when he was caught short and rushed to use the reserved toilet. He was arrested several days later.

According the Zimbabwe's Daily News paper, his charge sheet did not specify what laws he had breached or how he had compromised security.

The BBC's Thabo Kunene in Bulawayo says his relatives are angry that he was tried before a police tribunal without lawyers present.

Mr Mugabe, who has been the leader of Zimbabwe for the three decades of its independence, is currently in a power-sharing government with long-time opponent, Morgan Tsvangirai.

Source: BBC

Thursday, 2 June 2011

Kikwete aende ughaibuni, mawaziri vijijini

Kikwete akibembea na mkewe alipokuwa Jamaica


KATIKA semina elekezi ya hivi karibuni iliyofanyika mjini Dodoma, Rais Jakaya Kikwete alikaririwa akiwafokea na kuwaagiza mawaziri waende mikoani kufafanua ‘mafanikio’ ya serikali yake!

Hii si mara ya kwanza kwa Kikwete kufanya semina elekezi isiyoelekeza kitu bali kula pesa ya wananchi. Alianzia kule Ngurdoto 23 – 27 Agosti, 2006. Semina hii ilihusisha wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala wa mikoa na wilaya.

Kama kawaida yake, Kikwete alitaka aonekane anajua uongozi na kuwajali wananchi. Alitoa maelekezo yafuatayo kwa walengwa wa semina husika:
Alikaririwa na vyombo vya habari akisema: “Nendeni mkatekeleze majukumu yenu kwa kuzingatia kuwa tabia nzuri na mwenendo mwema ni sifa ya msingi ya kiongozi. Ukipungukiwa sifa hiyo unapunguza hadhi yako mbele ya jamii unayoiongoza.”

Wakati akisema haya yeye alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kufanya ziara nyingi hadi baadahi ya wabaya wake kumwita ‘Vasco da Gama wa Afrika.’
Aliendelea: “Tumieni madaraka yenu vizuri, msiyatumie kuonea, kudhulumu, kuomba au kutoa rushwa au kulipiza kisasi.”

Wakati akisema hayo alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kuwakingia kifua mafisadi akiwamo mtangulizi wake kutokana na kadhia ya kujimilikisha machimbo ya makaa ya mawe ya Kiwira. Hakupata kukanusha tuhuma hizi.

Kikwete aliendelea: “Zingatieni na kuheshimu sheria za nchi na kanuni zinazotawala utendaji wa serikali. Kama Viongozi tuwe mfano wa kuzingatia hayo. Watumieni sana makatibu tawala wa mikoa na maofisa tawala wawajulishe sheria, kanuni na taratibu.”

Katika hili, bahati mbaya hakujiangalia. Kwani ni wakati huu alikuwa akishutumiwa kumruhusu mkewe kutumia ofisi ya rais kujizolea mabilioni ya fedha kwa kuanzisha NGO yenye kutia shaka kama alivyofanya mke wa mtangulizi wake, Benjamin Mkapa.

Tuko na Kikwete bado. Aliendelea kupiga siasa: “Muwe na mahusiano mazuri na viongozi wenzenu na wananchi mnaowaongoza.”
Wakati akitoa nasaha hizi alisahau kuwa alikuwa akishutumiwa kwa kulea mitandao ya kimasilahi ndani ya chama chake iliyokuwa ikifanya nchi isitawalike kutokana na vita ya ndani kwa ndani ya kugombea ulaji.

Nukta ya tano ya Kikwete alisema, “Muwe wepesi katika kushughulikia matatizo ya wananchi. Muwe kimbilio la wananchi kwa jua na mvua. Muwape nafasi ya kuwasikiliza na kushughulikia matatizo yao.” Maskini Kikwete alisahau kuwa wakati akiwaambia watendaji wake wawe kimbilio la wananchi, yeye alikuwa kimbilio la wawekezaji huku akiwakimbia wananchi kwa kufanya ziara ambazo Profesa Lipumba aliwahi kusema hazikuwa na maslahi kwa taifa.

Katika nukta ya sita, Kikwete alikaririwa akisema: “Jengeni moyo wa kujituma, kufanya kazi bila kuchoka, na kushirikiana na wananchi.

Tufufue moyo wa kujitolea miongoni mwa mwananchi. Yapo mengi yanayoweza kufanywa na wananchi wenyewe bila kusubiri serikali. Kinachotakiwa ni uongozi ambao ni kazi yetu.”

Hapa alisahau pia alisahau kuwa alionywa kutounda serikali kubwa akadharau.

Nukta ya saba Kikwete alisema: “Simamieni halmashauri zenu vizuri.” Hivi wangepata wapi mshipa wa kusimamia halmashauri zao wakati yapo malalamiko kuwa rais hasimamii nchi vizuri?

Nukta ya nane Kikwete alisema: “Kasimamieni vizuri kilimo na hasa Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP)”

Kwanini wao wasimamie kilimo programu za kuendeleza kilimo wakati yeye alikuwa akisimamia programu za kuendekeza uwekezaji kama wa madini ambao leo hauna tija hadi kuibua migogoro kama ile ya Nyamongo?

Nukta ya tisa Kikwete alihimiza: “Hakikisheni kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anakwenda sambamba na kuwa na sekondari kila kata. Aidha maandalizi ya ujenzi wa shule za sekondari yaanze sasa ili kuweza kukabiliana na idadi ya wanafunzi watakaofuzu kuingia kidato cha kwanza mwaka 2008.”
Hapa, rais alisahahu kwamba shule alizozipigia chapuo ziliishia kuwa si shule za kata tu, bali pia shule za kata elimu na kuongeza ujinga!

Kumi Kikwete alisema: “Simamieni kikamilifu utoaji wa huduma za afya na kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ukimwi.” Hapa sina chakuongeza.

Kumi na moja Kikwete alilonga: “Simamieni kikamilifu ujenzi na utoaji wa huduma za kiuchumi katika mikoa yenu.” Wakati akisema haya, alikuwa akipuuzia malalamiko ya wananchi kutoka mikoa ya Mara, Mwanza na Shinyanga ambako wawekezaji wake walikuwa wakiwabughudhi hata kuwaua wananchi.

Kumi na mbili Kikwete alisema: “Simamieni na hakikisheni suala la hifadhi ya mazingira. Hili jambo ni la kufa na kupona.”
Binafsi najiuliza, mazingira yangehifadhiwa vipi wakati serikali ilikuwa ndiyo imezidisha mgawo na ulanguzi wa umeme, vitu vinavyowalazimisha wananchi kukata miti ili kupata mkaa kufidia pengo la umeme.

Kikwete hakungoja watendaji waende na kutekeleza aliyowatuma. Badala yake aliwamwagia matarajio yake likiwemo hili.

“Tuwe na uhusiano mzuri na vyombo vya habari. Tufanye kazi na vyombo vya habari vitusaidie kufikisha ujumbe wetu kwa watu wengi kwa urahisi na kwa wakati mmoja”. Kazi kwako msomaji kutathmini hayo.
Chanzo: Tanzania Daima Juni 1, 2011.

Tutaendelea kudanganywa na walevi hadi lini?

LEO nina hasira kuliko hata wiki jana wakati nataka kujilipua. You know what. Kwanza yale mauaji ya Tarime yamenifanya nichukie lisirikali na mandata kuliko wakati wowote katika ma-life yangu.

Pia mauaji haya yamefanya niwachukie walevi hasa wadanganyika kwa umbwa na ukondoo wao. Hivi mtauawa hadi lini wakati mkiona? Mwadhani kuna mjomba wenu atakayekuja kupambana na geshi la mambwa mwitu linaloamrishwa na mafisi kuwaueni?

Hayo ya Tarime mtajiju au kumalizana wenyewe. My concern today is showing my dismay regarding the whole bragadaccio ya kujivua gamba.

Najua viherehere wanaosoma hapa wanasema kuwa najidai kujua umombo. Mie najua lugha zote duniani isipokuwa ile ya mafisadi na matapeli wa kiroho wenye uroho.

Hivyo nikimwaga ung’eng’e uvumilie hata kama roho inakuchonyota. Hii ndiyo faida ya kwenda shule kuongeza ujinga-sorry elimu. Hata kuongeza ujinga inawezekana. Maana ukiangalia maprofwesa waliojazana serikalini wanavyofanya mambo ya kipuuzi kama Dokta Muinyi ambaye wizara yake ilifanya upuuzi kule Mbalaga akashindwa inshu ndogo tu-kuwajibika au madaktari uchwara wa kughushi kama akina Emmy Nchinvi, Mere Nyago na wengine, kuna ukweli kuwa kuna watu walikwenda shule kuongeza ujuha si ujinga.

Hawa leo sina mpango wa kuwananga. Maana tabu lao liitwalo Education for Ignorance liko mekoni likikorogwa ili nao baadaye wakorogwe na kupakuliwa wakati ukifika. Hivyo my friend Diddie Massamburi na PhD yako feki na Makorongoro Muhanga, Vickie Mwambalashwa kaa mkao wa kuliwa na kupakuliwa mambo yenu.

Leo nina hasira kama nilivyotonya hapo juu. Nina hasira sawa na wale vijana wa chama cha mafisadi wa kule AR waliotaka Mere Kitanda atimke baada ya kuzua noma kutokana na ujuha wake.

Japo wapo wanaosema kuwa wanatumwa na Ewassa ili kulikoroga, kama mbaya mbaya. Kwanini Ewassa awe fisadi pekee wakati na swahiba wake, mkewe hata mwanae ni mafisadi wa kunuka?

Kwenye ufisadi Njaa Kaya anamtoa knock out Ewassa kwa sababu Ewassa anatuhumiwa yeye na kitegemezi wake Freddie huku mama yake Regi akiwa nje ya ulingo wa unyakuzi. May be mambo yake hayajajulikani.

Ukija huku ni mess. NjaaKaya mwenyewe yumo kwenye First Eleven ya Dk. Silaha Kali, huku bi mkubwa Sisalama na Riz-One wakichukua nafasi ya juu kwenye tuhuma za ufisi.

Ziko wapi tambo za hichi kitegemezi uchwara kudai kitakwenda kwa pilato? Kimenywe kama dingi wake. Mama yake ndiyo usiseme. Anaendelea kusanya kama Anna Makapi. Jamani kuna haja ya kubadili methali zetu na kusema: walevi ndiyo waliowao na wadanganyika ndio waibiwao.

Hapa ndipo maana ya looting au tuseme lulling or bullying party yanapojitokeza. Kwa tafsiri rahisi ni kwamba chama ongelewa ima ni cha majambazi, wasanii au wanyanyasaji hata wauaji. Kama nimewaongopea msikonde bali kwenda shule na kujua bila kutegemea tafsiri yangu. Alright! Kulaleki!

Hebu niwaulize walevi tena huenda wanaweza kutia akilini. Hivi mtaendelea kuongopewa huku jua likiwaka hadi lini? Ni juzi tu mmeletewa upuuzi wa kuvua gamba na kuvaa jezi za kulindana na kuwahadaa. Mmeendelea kuwa watazamaji na waathirika huku mkiishi kwa matumaini! Hadi lini?

Kabla ya moto wa changa hili la machoni kuzimika mara Dk. Silaha akafichua kuwa kitegemezi cha mkuu wa kijiwe ni kibilionea.

Mmesikiliza na kuendelea kutoatoa mimacho kama kunguru aliyenaswa kwenye ulimbo! Nashangaa mlivyoridhia kila ujambazi. You know what? Dowanis mmeliwa tena.

Kwani walioinunua wameishapata hakikisho toka lisirikali kuwa watazalisha na kuwauzieni hapo hapo. Na kwa taarifa yenu muelewe.

Dowanis haijauzwa kitu bali Rostitamu na wenzake wamebadili mikakati yao kwa kuleta sura ya mtasha baada ya mmanga tapeli kutofua dafu. Yule alikataa kupigwa picha. Mtasha kapigwa nyingi tu.

Najiuliza, hivi Dowanis kama hawajalipwa pesa yao waliyopewa na mahakama ya kimataifa, wamepata wapi uhalali kisheria kuuza mitambo yao kama siyo usanii wa kipumbavu kwa vile wana dili na walevi na wadanganyika?

Siku hizi sisikii Rostitamu akidai amepewa Powers of Attorney na Dowanis kufanya kila kitu hata kuibia Danganyika. Amenywea baada ya kugundulika. Hata kile kitegemezi cha Mgosi Makambale Machungi ninchosikia eti kinapigiwa debe kututawala miaka 20 ijayo kimenywea!

Kweli walevi wanatukanwa kila matusi ya nguoni. Eti Jannie Makambale anaandaliwa kuwa rais! Mwe! Hii kali! Yaani harufu ya maziwa ya mama yake haijatua eti tuletewe kinyago kingine cha mpapure kama kile cha Mzee Musa kilichoingizwa majaribuni na Dellila Anae Tamaa wa Kishumundu!

Ama kweli Hassan alisema: wadanganyika ni kichwa cha mlevi mwendawazimu kujifunzia kunyoa. Mzee Ali alijua. Maana alifanya kila ufisadi na kuumba huu unaotusumbua bila kushtukiwa. Kwani unadhani NjaaKaya aliumbwa na nani kama si mzee Ali?

Loh! Nshasahau! Lengo la kuandika unabii haikuwa kushughulika na vijifisadi uchwara wala mafisadi wakubwa bali genge liitwalo Chata Cha Mafisadi. Walevi mbona siwasikii mkilishinikiza lijivua gamba kama lilivyowahadaa au ndiyo mmekubali kuliwa kama kawa ingawa huko nyuma hamkuwa hivi?

Niulize swali simpo. Ni fisadi au mafisadi wapi watawatimua mafisadi wenzao? Sitaki mseme nina wivu na rafiki yangu. Rejea ile orodha ya aibu au List of National Shame ya Dk Silaha kule Mchungwa Simba Meteke.

Nimalizie kwa kuuliza swali la kilevi. Sinema ya Loliyondo imekwisha. Je tutegemee ipi ili kuendelea kuwalewesha na kuwadanganya walevi na wadanganyika?

Au ni yale yale ya Zenj ambapo siku hizi baada ya ngunguru kufunga ndoa na ngangaru ni ulaji kama kawa?

Nimalizie na angalizo na kipuuzi. Una habari kuwa yule kijana Mapepe Tunaye anaanza kuishiwa kama Willy Mukami? Naona wameishiwa sera baada ya kujikuta wakichekwa hata na ndege na vyura kwa ujuha wao kudhani wanaweza kutumia Kiama cha Majambazi eti kulipiza kisasi kwa mafisadi wenzao.

Yote kumi. Kile kizee kiitwacho Mgosi Jose Makambale kimeishia wapi? Au kiko na Kimdunge Ngumbaru mwehu ambaye naye ametokomea.

Tokomea Makambale. Tokomea Kimdunge. Tokomea CCM. Tokomea. NjaaKaya. Tokomea tokomea tokomea mshirika wa bed. Stop! Maana nawe mpuuzi juzi ulisema nachelewa kurudi una wasi wasi na dogoz. Kumbaff nyote.

Namuona mkuu wa manjago ananijia, ngoja nichomoke maana mdomo huu sasa utaniponza!
Chanzo:Tanzania Daima Juni 1, 2011.