Niseme wazi. Leo, sifyatui yeyote bali kufyatuka na kujifyatua baada ya kugundua kuwa kila fyatu, hata yule anayewafyatua wenzake, kuna siku atafyatuliwa. Ni suala la muda tu au kujisaulisha kama siyo ulimbukeni, upofu, hata uzwazwa kama siyo kujifyatua ufahamu wakati kila kitu kiko wazi. Kama daktari wa falsafa mwenye magudulia na maguni ya PhD, juzi nilikuwa nasome kitabu kiitwacha the Nature of Nature kilichoandikwa na professa emeritus Nkwazi Mhango Nkuzi. Niligundua kuwa kumbe kila kitu kina marejeo tena kwa usawa. Hata ufyatue vipi, ipo siku isojina utafyatuliwa uonje ladha ya adha za wale uwafyatuao. Hivyo basi, kuanzia leo, sina hamu wala haja tena ya kuslowlow au kunchimvi fyatu yoyote hata aniudhi kiasi gani. Nifanye hivyo kwanini wakati najua yapo marejeo?
Katika kusoma kitabu hiki, Professa anaeleza kuwa ufyatuzi uko wa aina mbili, yaani ule wa uhai na vitu vya umma wa mafyatu kama vile mali na njuluku. Mfano, ukiua, utauawa au kufiwa. Ukiiiba utaibiwa. Ukidhulumu kadhalika. Ukifurahia mateso ya fyatu mwenzio, kuna siku wengine watafurahia na kushangilia yako. Wenye nguvu leo hawakuwa nazo jana na kesho zitawatoka kama zilivyokuja. Mashujaa watakufa sawa na woga. Wagonjwa na wazima wote hufa. Kila kitu hufa isipokuwa dunia. Kwa ufupi, ni kwamba ukifyatua wenzio jua.
Hakika, utafyatuliwa saa nyingine vibaya kuliko hao uliowafyatua. Yawezekana wale watakaokufyatua siyo wale uliowafyatua. Wapo wanaofyatuliwa na wale waliowafyatua au ndugu zao. Wengine hufyatuliwa na Mungu ili kutoa somo kwa wengine wanaopanga kuwafyatua wenzao wasijue nao watafyatuliwa. Kisichoepukika ni kwamba utafyatuliwa tu kwa njia moja au nyingine ili inapofika zamu yako ya kufyatuliwauonje adha na uchungu wa kufyatuwa wengine.
Baada ya kugundua ukweli huu kwenye the Nature of Nature, nimeacha kujifyatua, kuwafyatua wengine, na kujifanya au kujisahaulisha kuwa siwezi kufyatuliwa wakati nafyatuliwa kama niliowafyatua. Juzi, nilipata msiba mkubwa wa swahaba yangu mkubwa aitwaye Nonihino rafiki yake rafiki yangu Mgoshi Machungi kule Mashindei. Huwa sina tabia ya kulia au kuogopa kufyatuliwa wengine tena wasio na hatia au wema kuliko mimi.
Katika kudurusu somo la kufyatua na kufyatuliwa, nililia sana baada ya kufyatuliwa rafiki yangu mchivichimvi aliyefyatuliwa polepole hadi kutoweka ghafla bila kuacha hata chembe ya alama. Baada ya hili kutokea, nililia hadi kuishiwa nguvu mpaka Mgoshi Machungi akafyatuka na kugwaya asijue siku moja atafyatuliwa kama ambavyo amekuwa akijifyatua na kuwafyatua wabaya wake. Japo Mgoshi alinionea huruma, nilimsikitikia kwa vile zamu yangu ilikuwa imefika na kupita. Ni wangapi huliona hili kama nilivyoliona? Kwa kufyatuliwa swahiba wangu, nilionja joto ya jiwe. Hivyo, nimeamua kufanya kitubio kwa Sir God na wale niliwafyatua iwe kwa njuluku hata uhai.
Kwa vile kufyatuliwa ni lazima, hata uwe mfyatuzi namna gani, siku moja usioyijua utafyatuliwa sawa na wale uliowafyatua. Utalia, kuchukia, kuogopa, na kuomboleza kama walivyofanya wale uliowafyatua au ndugu zao. Tuache kufyatuana. Duniani tunapita tu. Wabaya wangu walifurahi swahiba yangu alipofyatuliwa kwenda kwa aliyemfyatua. Wengine walisherehekea na kujiridhisha kuwa haki ambayo sikuitenda ilikuwa imefanyika. Hata kama nashukiwa kuwa na roho mbaya, kwanini mafyatu wanafyatuka na kuwa na roho mbaya hivi hadi kusherehekea msiba wangu.
Wakati roho ikiniuma na kuzongwa na machungu na majonzi, nikiwa nimefyatuliwa na mshangao na woga, nilimuuliza Mgoshi Machungi kwanini mafyatu wamefyatuka hivi hasa pale walipofyatuka wakagoma kunisamehe na badala yake wananishitikia kwa Sir God anifyatue kama alivyonifyatua. Kusikia hivyo, Mgoshi alifyatuka na kunifyatulia ukweli kuwa maisha ni kula na kulipa na huu ulikuwa ndo wakati wangu wa kulipa kwa kufyatuliwa. Alisema kuwa ukimfyatua au kuwafyatua wengine, nawe una siku yako ya kulipa kwa kufyatuliwa iwe wewe au yule umpendaye kama ilivyotokea kwa swahiba wangu mkubwa na wa pekee.

Kwa vile sasa nimelijua hili, nimeamua kutubu. Katika kufanya hivyo, nawaomba wote niliwafyatua kwa roho mbaya na uzwazwa wangu wanisamehe. Wafikie mahali waseme imetosha kama nisemavyo kuwa, kuanzia leo, sitajifyatua, kufyatuliwa na kuwafyatua wengine au kupenda na kushabikia ufyatuzi kama njia ya kumaliza matatizo na tofauti zetu. Najua wengi wanaonea wivu ulaji na unene vyangu.
Kuanzia sasa, najua ni vya muda. Najua fika kuwa ukiishi kwa upanga, utakufa kwa upanga. Ukiishi kwa kuwafyatua wengine, nawe utafyatuliwa. Mwenzenu nimefyatuliwa hadi nikaanza kuchukia na kuogopa ufyatuzi hasa utokanao na roho mbaya, ukatili, uroho, na uzwazwa. Mie ni nani hadi nijifyatue na kujifanya hayanihushu wakati yalishanisibu nilipofyatuliwa kwa kufyatuliwa swahiba wangu kipenzi Nonihino?
Kufyatua ni kutamu ila kufyatuliwa usikie. Naamini kule Mashindei akina Mgoshi Machungi na Jitu wameipata.
Chanzo: Mwananchi J'tano leo.