How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Thursday, 26 April 2012

Kuna siku tutataifisha haya mahekalu haki ya nani


Taarifa kuwa waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige alinunua nyumba kwa zaidi ya shilingi bilioni moja licha ya kuwastua wananchi na kuwachukiza, ni pigo kwa tambo za rais Jakaya Kikwete kuwa atawaletea maisha bora kwa watanzania wakati kumbe watanzania wenye aliomaanisha ni akina Maige na wateule wake! Ila amini msiamini kuna siku haya majumba tutayataifisha pale wahusika wakishindwa kutuambia walikopata hayo mabilioni ndani ya muda mfupi.  Kama nyumba ya Bwana Maige ni ya mabilioni hiyo akaunti yake ina matrilioni mangapi? Hapa hatujaona yale mahekalu yaliyoporomoshwa baada ya Benjamin Mkapa na wenzake kuiba nyumba zetu.
 Hivi hawa watu ni wazima kiakili au vichaa wasiosoma hata alama za nyakati? Huu ni ujambazi wa mchana kwa kijana mdogo aliyechaguliwa juzi kuwa mbunge kuweza kuwa na ukwasi kiasi hiki. Je hawa siyo wale wanaopata pesa tokana na kuuza wanyama wetu hata kuuza madawa ya kulevya? Anayebisha ajitokeze atwambie amepataje hayo mabilioni. Je rais Jakaya Kikwete anayewafumbia macho ana maslahi gani na jinai hii? Kweli chanzo cha umaskini wa watanzania si mapenzi ya Mungu bali ya mwandamu na mwanadamu mwenyewe mmojawapo ni Kikwete!Image Detail
Nyumba ya waziri Ezekiel Maige inayodaiwa kununuliwa kwa dola 700,000 huko kwa walio nazo.

No comments: