- Tangazo la kukanusha habari iliyochapishwa na Tanzania Daima kuhusiana na msimamo wa rais wa kuendeleza uwenzetu ni ushahidi kuwa sasa kiatu kimefika mwake. Kimsingi, Kikwete huwa haaminiki wala hajiamini. Huwa anakwenda na upepo kiasi cha kuitwa mbayuwayu. Kutoka kwa tangazo kanushi ni ushahidi kuwa hoja ina nguvu na kama Kikwete atazubaa inaweza kumuondoa yeye na genge lake kama siyo kumtoa waziri mkuu Mizengo Pinda sadaka kama ilivyotokea kwa Edward Lowassa na mawaziri wengine.
SUNDAY, APRIL 22, 2012
KANUSHO LA HABARI POTOFU KATIKA TANZANIA DAIMA AMBALO LEO LINA KICHWA CHA HABARI KISOMEKACHO "JK.ALINDA MAWAZIRI"
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Gazeti la Tanzania Daima la leo Jumapili Aprili 22, 2012 lina habari katika ukurasa wake wa mbele yenye kichwa cha habari ‘JK alinda Mawaziri’, inayodai kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.
Habari hiyo imedai kuwa Mhe. Pinda anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini, imeendelea kudai habari hiyo, “Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita”.
Tunachukua nafasi hii kuweka bayana kwamba habari katika hilo hazeti la Tanzania Daima Jumapili si za kweli, bali ni za uzushi na upotoshaji mkubwa.
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.
How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Sunday 22 April 2012
Huu ni ushahidi kuwa ukombozi unakaribia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment